KINGAZI BLOG: 09/03/16

HABARI KARIBU YAKO ZAIDI.

Breaking News
Loading...

Saturday 3 September 2016

ALIYEAMUA KUMUUZA MKEWE ANUNUE iPHONE 6

Mwanafunzi wa Chuo kikuu kimoja cha China ambaye jina lake halikutambulika kwa haraka ameamua kufanya ‘uchizi’ ili mradi tu aipate pesa ya kununua aina mpya ya iPhone iliyoingia sokoni, iPhone6.
Kijana huyo wa alionekana akiwa nje ya chuo kikuu cha Songijiang akiwa na bango kubwa lililoandikwa kwa kichina na kutafsiriwa ‘Girlfriend Sharing’.
 Katika tangazo hilo kijana huyo anaeleza kuwa yuko tayari kumkodisha mpenzi wake kwa mtu yeyote atakayeweza kutoa pesa ili jamaa apate kiasi cha kutosha kuinunua iPhone 6 yenye screen kubwa.
Picha ya kijana huyo imesambaa kwa kasi katika mtandao wa kijamii unaotumiwa na wachina uitwao ‘Weibo’ ambao ni kama Twitter.
Tangazo hilo limeambatana na picha za mpenzi wake na amewatoa hofu wateja wanaosita kuingia nae mkataba kuwa hata mpenzi wake ameridhia na yuko tayari kudate na mtu yeyote atakaejitokeza.
Muda wa kuwa na msichana huyo baada ya kumkodi umebainishwa kutokana na malipo yatakayofanywa na mteja. Viwango ni vya saa 1 (10 yuan), siku 1 (50 yuan) au mwezi mmoja (500 yuan).
Hata hivyo, wapenzi hawa sio wa kwanza kujiweka sokoni ili wapate bidhaa ya kampuni ya Apple. Mwaka jana katika uzinduzi wa iPhone 5, wanandoa wa Shaghai waliwaweka sokoni watoto wao watatu ili wapate pesa ya kununua computer na simu za iphones lakini walikamatwa na kufunguliwa mashitaka.
Lakini pia kijana mdogo wa Hunan alijitolea kuuza figo lake ili apate pesa ya kununua iPad na iPhone.
Siyo hayo tu, hivi karibuni mwanaume mmoja wa Saudi Arabia ametaka kupewa iPhone 6 kama mahari ya dada yake hata kabla aina hiyo ya simu haijazinduliwa Bahrain.

Daktari Apatikana na Video ya Watu Wakishiriki Ngono na Nyoka


UINGEREZA: Daktari mmoja nchini Uingereza amepatikana na hatia ya kuwa na video za ngono, ikiwemo moja ya mwanamume akishiriki ngono na nyoka.

Cyprian Okoro, 55, kutoka Kusini Magharibi mwa London alipatikana na makosa matano ya kuwa na video za ngono ya kuchukiza zaidi pamoja na picha moja ya utupu ya mtoto.


Kwenye moja ya video hizo, kulikuwa na wanawake wakishiriki ngono na mbwa na nyingine ya mwanamke akifanya ngono na farasi.

Mshtakiwa, ambaye anatoka Cameron Place, Streatham, amekanusha mashtaka hayo na amepewa dhamana lakini atahukumiwa tarehe 30 Septemba.


Lakini, baada ya kutafakari kuhusu kesi yake kwa chini ya siku moja, baraza la wazee wa mahakama lilimpata na hatia kuhusia na mashtaka yote ila lile la watu ksuhiriki ngono na mbwa.

Mahakama iliambiwa kwamba Okoro alikuwa na picha na video hizo kwenye simu yake baada ya kuzipokea kupitia WhatsApp.

Ni mara ya pili kwa Okoro kupatikana na hatia wakati mnamo mwaka 2014, alihukumiwa kifungo cha nje cha miezi 18 baada ya mwanamke kuwasilisha tuhuma za unyanyasaji wa kingono dhidi yake.

Okoro alihitimu kama daktari Lagos, Nigeria, mwaka 1986.

TCU Yatangaza Kuanza Udahili Awamu ya PILI Kwa Wanafunzi wanaojiunga Vyuo Vikuu Ambao Wamekosa Nafasi Kwenye Awamu ya Kwanza

Tunapenda kuutangazia Umma kuwa tulifunga mfumo wa pamoja wa udahili tarehe 31/08/2016 saa sita usiku ili kuchakata maombi ya waombaji waliofanikiwa kuomba udahili kwa mwaka wa masomo 2016/2017.

Hata hivyo kutokana na wengine kushindwa kufanikiwa kutokana na sababu mbali mbali, Tume inatangaza kuwa itafungua maombi kwa awamu ya pili kuanzia tarehe 12 hadi 23 Septemba 2016 ili kuruhusu makundi yafuatayo kuomba udahili.
Waombaji watakaokuwa wamekosa nafasi kwenye awamu ya kwanzaWaombaji wa kidato cha Sita walioshindwa kuomba katika awamu ya kwanzaWaombaji wenye vigezo vya Stashahada ambao walishindwa kuomba kutokana na matokeo yao kuchelewa kufika NACTE kwa wakati,Waombaji ambao wamemaliza mitihani ya “Cambridge” mwaka 2016 na matokeo yao yameshatoka,Waombaji waliofaulu mitihani ya RPL,Waliokuwa wanafunzi wa vyuo vikuu watakao kuwa na uthibitisho toka vyuo vyao vya awali.

Baada ya hapo Tume haitaruhusu tena maombi ili kuruhusu taratibu zingine za kiudahili kuendelea kwa ngazi ya Bodi ya Mikopo na vyuoni.

Asanteni
Imetolewa na 
Prof. Eleuther Mwageni
 Kaimu Katibu Mtendaji
Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania 
02 Septemba 2016

MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI KWENYE HABARI ZA KITAIFA NA UDAKU NA MICHEZO



Bodi ya Mikopo Kuwapa mkopo kwa Waombaji wote mwaka huu.


BODI ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imesema wale wote walioomba mkopo mwaka huu na kukidhi vigezo watapewa.

Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB, Abdul-Razaq Badru alisema hayo juzi mjini hapa wakati wa hafla ya kukabidhi vyeti kwa watu watano waliorejesha mkopo wa elimu ya juu kwa mkupuo na kwa hiari.

Badru alisema idadi ya walioomba mkopo mwaka huu ni wanafunzi 88,000 ambao bodi itahakikisha wale wote waliokidhi vigezo, wanapatiwa fedha kwa ajili ya elimu ya juu.

Mkurugenzi huyo ambaye amehimiza walionufaika na mikopo kulipa madeni yao, alisema mwaka jana, wanafunzi waliokopeshwa ni 55,000.

Kuhusu waliopewa vyeti ikiwa ni hatua ya kuwatambua, ni pamoja na mfanyakazi wa VETA Shinyanga, Richard Jafu aliyerejesha kwa mkupuo Sh 14,749,950 na Francis Mwilafi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo aliyelipa Sh 15,115,200.

Wengine ni Mbunge wa Vwawa, Japhet Hasunga aliyerejesha Sh 255,000; Profesa Peter Msoffe ambaye ni Naibu Makamu Mkuu wa Chuo cha Dodoma (UDOM) aliyerejesha Sh 1,430,749.

Mwingine ni Mbunge wa Biharamulo, Oscar Mukasa ambaye kiasi alichorejesha hakikutajwa ingawa mkurugenzi mtendaji wa HESLB, alisema amerejesha kiasi kikubwa kwa mkupuo.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti, wadau hao walisisitiza umuhimu wa wanufaika wa mikopo kuirejesha kwa hiari ili kuiwezesha bodi hiyo kukopesha wanafunzi wengine.

Mbunge wa Biharamulo, Mukasa alishauri bodi hiyo kuangalia uwezekano wa kurekebisha vigezo kwa lengo la kuwawezesha wanafunzi watokao maeneo ya pembezoni kunufaika na mikopo hiyo ya elimu. Kwa upande wake, Mbunge wa Vwawa, Hasunga alisisitiza wabunge wanaodaiwa warejeshe mkopo kwa mkupuo.

HIZI HAPA SIFA PEKEE ZA MWANAMKE WA KUMUOA NA KUDUMU NAYE KATIKA MAISHA

Wanaume wengi wanapofikia hatua ya kuoa si kwamba wanakurupuka tu na kuoa mwanamke yeyote mwenye sura nzuri, bali huchukua muda wao mwingi kuchunguza mambo mengi juu ya wake ambao wanadhani kwamba wanaweza kuwa pamoja kwa kipindi chote cha maisha. Wanawake wengi wanajisahau na kudhani kwamba kitu kinachowezakuwafanya wakapata wachumba niuzuri hivyo kupoteza muda wao kujichubua na kujiremba ili wawavutie wanaume bila kujua kwamba kuolewa ni zaidi ya uzuri. Hali sasa hivi imebadilika ni tofauti na kipindi cha nyuma ambapo ukiwa na sura nzuri na umbo la kuvutia basi una asilimia 100 za kuolewa. Utafiti ambao nimeufanya unaonesha kwamba zaidi ya uzuri wa tabia na umbo, kuna kuna sifa nyingine za msingi ambazo mwanamke anatakiwa kuwa nazo ili aweze kuwa katika mazingira mazuri ya kupata mchumba wa kumuoa kiasi kwamba asipokuwa nazo ataishia kuchezewa tu lakini haitatokea mtu kumtakiwa kwamba anataka kumuoa.
1. MWEYE MAPENZI YA KWELI Lengo kubwa la mwanaume kuoa ni kutaka kupata mapenzi ya kweli kutoka kwa mwanamke na ikiwezekana waweze kupata watotoa ambapo watoto mara ndio wamekuwa furaha ya ndoa. Wapo wanawake wengine ambao wanonesha wazi kutokuwa na mapenzi ya kweli bali wanakuwa na mapenzi ya kuzuga. Wanachotaka wao aidha kupata umaarufu tu kwamba yuko na mtu fulani ama kuweza kupata pesa alizonazo mwanaume lakini sio kwamba ana mapenzi ya dhati kutoka moyoni mwake.
Mwanamke asiye na mapenzi ya dhati utamgundua tu, muda mwingiutamuona macho yake yako kwenye mfuko wa mwanaume. Akiona kwamba mfuko umetuna utaona anaonesha mapenzi ya hali ya juu lakini pindi hali inapokuwa kubwa mbaya kifedha mapenzi yanaanza kufifia.
Kwanini wanaume wanapenda wana wake wenye mapenzi ya dhati kutoka mioyoni mwao na si kutokana na fedha walizonazo? Hii inatokana na ukweli kwamba maisha siku zote yanabadilika, kama waswahili wanavyosema, kuna kupanda na kushuka.
Sio kwamba kila siku utakuwa na maisha mazuri na kama itatokea hivyo basi ushukuru mungu.Hivyo basi mwanamke wa kuoa lazima afahamu hivyo na awe tayari kuonesha mapenzi yake ya dhati wakati wote wa maisha yao na si kwa kipindi fulani tu cha neema.
Si hivyo tu pia asilimia kubwa ya maisha ya ndoa yanatawaliwa na mapenzi, kwa hiyo nyanja hiyo inakuwa ya msingi sana kwa wanaume wengi kuiangalia ili wasije wakajikuta wanaoa mwanamke ambaye baada ya muda mapenzi yanakwenda likizo hali ambayo inaweza kuwafanya wasiishi maisha ya raha mustarehe.
2. WENYE TABIA NZURI Tabia njema ndio silaha ya maisha, ukiwa na tabia nzuri kila mtu atakupenda, hiyo ni katika maisha ya kawaida. Lakini linapokuja sualana kuoa tabia inakuwa kitu cha awali sana kungaliwa na hiyo inaweza kuwa na ukweli kwa sababu wapo wasichana wazuri wenye mvuto wa aina yake na maumbile mazuri, lakini wanakosa wanaume wa kuwaoa, ukiuliza kwani utaambiwa anatabia mbaya. Naweza kusema hilo ndilo limekuwa tatizo kubwa kwa baadhi ya wanawake kukosa wanaume wa kuwaona. Hakuna mwanaume hata mmoja kati ya wale ambao nimejaribu kuongea naye ambaye ameonesha kulidharau suala hilo la tabia.
Si hivyo tu wapo wanaume ambao wameingia kichwa kichwa na kuoa kwa kuangalia sura tu bila kujali tabia, matokeo yake baada ya siku chache yanatokea machafuko ya aina yake hali ambayo imepelekea kuvunjika kwa ndoa kutokana na tabia mbaya alizonazo mwanamke.
3. WENYE UCHU NA MAENDELEO Hivi karibuni kumekuwepo na mabadiliko ya aina yake kwa wanaume, wengi sasa hivi hawapendi kabisa kuoa mwanamke ambaye hana kazi yaani 'golikipa'. Kama atakuwa hana kazi basi awe na uchu wa maendeleo kwa kujituma kufanya kazi mbalimbali za kimaendeleo kama vile kilimo kwa wale walio vijijini na biashara ndogondogo kwa wale ambao wako mijijini na hata vijijini.
Ile dhana ya kusema mwanamke ni mama wa nyumbani wa kukaa na kujipodoa akimsubiria mwnaume arudi amstarehesha, sasa hivi imepitwa na wakati. Wanaume wengi wanapenda wanawake ambao ni wahangaikaji, wenye ndoto za maendeleo katika maisha yao. Hata kama watakuwa si wafanyakazi lakini wawe wenye kutoa ushauri kwa waume zao juu ya jinsi gani wafanye ili wafanikiwe.
4. WASIOPENDA MAKUU Kuna wanawake wengine wanakuwa na tabia za ajabu sana kiasi kwamba yaweza kuwa kero kwa wanaume. Wapo wanawake ambao wanapenda makuu bila kujali hali halisi ilivyo. Kuna wanawake naweza kusema wana tamaa, kila wikiendi utamsikia "leo tunakwenda wapi dear?"
Akimuona rafiki yake kanunua simuya laki tatu na yeye utamsikia akisema, ‘na mimi naomba uninunulie simu kama ya Grace’. Ukienda naye Pub anakuambia,"mimi sinywi pombe za chupa natumia za kopo tena Heineken’. Yeye hajali kiasi cha pesa mwanaume alicho nacho na usipotekelezea anachukia na anaweza hata kupunguza mapenzi.
Wanawake kama hawa wako katika mazingira magumu sana ya kuweza kupata wanaume wa kuwaoa. Mara nyingi katika maisha fedha huzungumza, kama mwanaume atakuwa na pesa ya kutosha itakuwa rahisi sana kwa mwanamke kupata kila atakachopenda lakini si kwa kumwambia mimi nataka kitu fulani.Mwanaune mwenyewe utamsikia akisema, ‘unataka nikununulie simu ya aina gani, au leo unataka twende wapi?’ hapo ndipo utakuwa na nafasi ya kusema, ‘mimi nataka uninunulie simu kama ya fulani ama leo nataka twende sehemu fulani.’
Wanaume ni warahisi sana wa kuwapatia wale ambao wanatarajia kuwaoa chochote ambacho watahitaji kama tu pesa haitakuwa tatizo. Kitu ambacho kinawaudhi wanaume wengi ni ile tabia ya mwanamke kupenda mambo makubwa bila kuangalia uwezo uliopo kwa mwanume.
Kuna wanawake wengine wao si wasemaji kabisa, yeye anasubiri leoamemletea hiki, anapokea na kushukuru, kesho akiambiwa twende beach anakubali. Au wengine wanasubiri mpaka waulizwe wanataka nini, ndio wanasema.
Sisemi kwamba uwe mkimya tu hata kama una shida ya kitu fulani na unafahamu kwamba ukimweleza mwenza wako anaweza kukusaidia, hapana! kama unaona kwamba uwezekano wa kupata kile ambacho unakihitajiupo mweleze kwa utaratibu naamini atakuelewa na kukutimizia.Tabia ambayo hawaipendi wanaume wengi ni ile ya kulazimisha ufanyiwe kitu fulaniwakati inawezekana uwezekano haupo.
5. WAVUMILIVU Wapo wanawake ambao sio wavumilivu kabisa katika maisha.Tunajua kwamba maisha siku zote hayatabiriki, yanaweza kutokea matatizo ya kiafya ama kifedha.Huu ndio wakati wa kuona uvumilivu wa mtu.Kama mwanamke anatarajia kwamba siku zote ni za raha tu na pindi matatizo yanapotokea anachukua uamuzi wa kumtoroka mwanume, huyo siyo mwanamke wa kuoa.
Wangapi leo hii huwatoroka waume zao pindi inapotokea kuumwa, kufilisika ama kupatwa na tatizo lolote ambalo kwa namna moja ama nyingine yanaweza kuwafanya maisha yao kutingishika?
Uvumilivu kwa mwanamke utakuwepo kama tu atakuwa na mapenzi ya dhati kama nilivyozungumza hapo awali. Mwanamke mweye mapenzi ya dhati ni lazima atakuwa mvumilivu na atakuwa tayari kuishi katika maisha ya aina yoyote, yawe ya raha ama ya starehe.Hawa ndio wale ambao wanaume wengi wengependa kuwa nao maishani mwao.
Licha ya kupenda kuoa wanawake amabo wana tabia hizo nilizozitaja hapo juu, wanachukizwa sana na wanawake ambao wanavijitabia vidogo vidogo ambavyo kimsingi havikubaliki katka jamii.
Tabia hizo ni kama wambea, wasio wakweli na wawazi, wasioridhika, wagumu kusamehe na wapesi wa kuchukia, wagomvi na wenye roho ya kwanini. Utafiti huu umefanyikwa kwa baadhi ya wanaume ambao wanatarajia kuoa wanawake ambao wanaoishi katika maeneo mbalimbali
Kwa maana hiyo basi hiyo iwe changamoto kwa wanawake. Wajue kwamba wanaume wanafurahi kuwa na wanawake wa aina gani. Hata kama utakuwa umeshaolewa, kama kuna wakati kunakuwa na kutokuelewana baina yenu, chunguza yawezekana kwamba unakosa mojawapo ya tabia ambazo nimezitaja hapo juu. Waweza kubadilika kwani inawezekana.

Daraja la Kioo China Lasitishwa Kutumika Baada ya Wiki 2


Zhangjiajie, China:

Daraja la kioo ambalo limeelezwa kuwa liko juu zaidi liliziduliwa hivi karibuni nchini China ambapo lina urefu wa zaidi ya futi 1400, upana wa futi 20 na karibu futi 1000 kutoka kwenye ardhi na imeripotiwa kuwa kioo chake ni imara zaidi mara 25 zaidi ya kioo cha dirisha.

Daraja hilo la wapita kwa miguu lijulikanalo kwa jina la daraja la Zhangjiajie lilizinduliwa August 20 mwaka huu ambapo lina uwezo wa kuchukua watu hadi 800 kwa wakati mmoja. Imeelezwa kuwa daraja hilo limekuwa likitumika kwa shughuli mbalimbali za kiutalii.

Daraja hilo limelazimika kufungwa ili kufanyiwa maboresho ya ndani baada ya idadi kubwa ya watalii waliokusanyika kutembelea kweye daraja hilo. Daraja hilo ambalo liko Kusini mwa China liligharimu dola million 48 kujengwa, na lilifunguliwa August 20 na limesitishwa huduma zake leo.

Msemaji wa kivutio hicho aliiambia MailOnline kuwa daraja lilitengenezwa ili kuweza kuchukua kiwango cha juu cha watu ambao ni 800 kwa wakati mmoja, na limepokea takribani watu 10,000 ambao ni watalii tangu lifunguliwe, msemaji huyo alisisitiza kuwa ni sehemu ya kioo ya daraja ni salama.

source GPL

 

Gallery

Popular Posts

About Us