KINGAZI BLOG: 09/15/16

HABARI KARIBU YAKO ZAIDI.

Breaking News
Loading...

Thursday 15 September 2016

TCU YALEGEZA VIGEZO VYA KUJIUNGA NA ELIMU YA CHUO KIKUU KWA WALIOSOMA DIPLOMA KUTOKA ALAMA ZA GPA YA 3. 5 HADI GPA YA 3.0 SOMA ZAIDI HAPO CHINI👇👇👇👇

Taarifa kwa waombaji wote wa nafasi za chuo, bodi ya vyuo vikuu TCU  imetoa vigezo vipya vya alama zitakazomuwezesha mwombaji kujiunga na elimu ya chuo kikuu, awali  ilikuwa ni GPA  ya 3. 5 lakini imepungua hadi kufikia GPA ya 3. 0 ili kuwawezesha watu wengi zaidi kuapply na kupata nafasi ya kujiendeleza.

BREAKING NEWS:HAYA HAPA MAJINA YA WANAFUNZI(FORM SIX) WALIOCHAGULIWA KAMPALA UNIVERSITY-KIU 2016/2017

Kampala International University-dar
First selection List of : Bachelors Programmes 71.32 KB

HIVI HAPA VYUO NA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA KWA MWAKA WA MASOMO 2016/17



Image result for tcu tanzania
HIVI HAPA VYUO NA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA


  • Chuo Kikuu cha Ardhi, (ARU)
  • Chuo Kikuu cha Hubert Kairuki (HKMU),
  • International Medical and Technological University (IMTU)
  • Moshi University College of Cooperative and Business Studies(MUCOOBS-MOCCU)
  • Chuo Kikuu cha Mlima Meru
  • Chuo Kikuu cha Muhimbili (MUHAS)
  • Chuo Kikuu cha Morogoro (MUM)
  • Chuo Kikuu cha Mzumbe (MU)
  • Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT)
  • Chuo Kikuu cha Ruaha (RUCO)
  • Chuo Kikuu St. Augustine cha Tanzania (SAUT)
  • Chuo Kikuu St. John cha Tanzania (SJUT)
  • Chuo Kikuu cha Sokoine (SUA)
  • Chuo Kikuu cha Zanzibar
  • Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji-TEKU
  • Chuo Kikuu cha Tumaini (TU)
  • Chuo Kikuu cha Bukoba
  • Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), established in 1970 from the split of the Chuo Kikuu cha Afrika Mashariki
  • Chuo Kikuu cha Dodoma,UDOM
  • Chuo Kikuu cha Zanzibar (ZU)


NOTE:LINK IMEKAA POA ,ANDAA USERNAME NA PASWORD YAKO ILI UONE KAMA UMECHAGULIWA KWA KU LOGIN KWENYE PROFILE YAKO! 

 kuangalia  umechaguliwa wapi bofya HAPA 

AU

==>Ingia hapa kuona ulipochaguliwa ==>TCU CAS | Search Selection



AU
KUONA VYUO VYENYE NAFASI BONYEZA HAPA

Hatuhusiki Kumtafutia Mtu Ajira - Bodi ya Mikopo

Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu imesema kuwa haihusiki kumtafutia mnufaika wa mkopo ajira badala yake inahusika kumpatia mwanafunzi mkopo na akishamaliza muda wa masomo atatakiwa kurejesha mkopo wake.

Hayo yamesemwa jana Jijini Dar es salaam na Mkurugenzi Msaidizi wa Habari, Elimu na Mawasiliano kutoka Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu Cosmas Mwaisobwa wakati akijibu maswali ya wananchi kupitia kipengele cha Kikaango cha EATV.

“Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu inatoa mikopo suala la kutafuta ajira halituhusu hivyo mnufaika yoyote asiwe na kigezo kwamba hajapata kazi , hiyo siyo kazi yetu, kazi yetu ni kuwawezesha kupata elimu basi” Alisema Mwaisobwa.

Aidha Mwaisobwa alisema wanufaika wote ambao walipata mikopo wanatakiwa kukatwa asilimia 8% ya pato la mwezi, na kama mtu anafanya kazi binafsi na hakatwi popote atatakiwa kutoa kiwango cha 120,000/= na kwa ambao wamenufaika na hawataki kuanza kulipa mkopo watapigwa penati ya 10% ya mkopo kwa mwaka.

Pamoja na hayo Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu imewataka walioomba mikopo kuvuta subira kwani Bodi inasubiri majina kutoka Tume ya Vyuo Vikuu ili Bodi ya Mikopo iweze kufahamu vyuo walivyopangiwa na kiwango cha ada ili haki iweze kutendeka kwa waombaji.

Maneno ya Diamond kuhusu kumsaliti ZARI


Zari Hassan na Dimaond Platnumz

Msanii Diamond Platnumz alipokuwa kwenye kipindi cha Planet bongo ya East Africa Radio wiki kadhaa zilizopita alifunguka na kusema kuwa katika maisha yake toka ameanza kuwa na mahusiano na Zari hajawahi kumsaliti.
Diamond Platnumz anasema kuwa moja ya sababu kubwa kwa yeye kutomsaliti mpenzi wake huyo kwanza ni kwa sababu wanaonana mara kwa mara lakini kingine alidai kuwa kazi ya muziki siku zote inamfanya kuwa 'busy' kuhangaika na muziki hivyo hapati nafasi hiyo ya kuhisi anaweza kumsaliti mpenzi wake huyo."Mimi sijawahi kusaliti, kweli kabisa bado sijapangiwa nadhani lakini unajua mimi na Zari tunaonana mara kwa mara kwa kuwa nasafiri sana na huwa nina waambia watu kama Zari angekuwa anakaa Tanzania asingepata muda mzuri wa kukaa na mimi, kwa kuwa nasafiri sana kwa sababu za kikazi hivyo hata angekuwa Tanzania ningekuwa napishana naye, unajua masuala ya muziki yana stress sana kila siku unawaza nyimbo, unawaza video mara unatakiwa usimamie kazi za Harmonize atengeneze video kali, uhakikishe Rayvanny atengeneze ngoma kali mara Rich Mavoko aweze kuwa mkubwa zaidi kwa hiyo unakuwa kuna vitu vingi unavitazama hivyo unakosa muda wa mapenzi. Kwa mfano siku mbili nzima nimelala WCB sijalala nyumbani kwa ajili ya kazi za muziki." alisema Diamond Platnum




Kilichoandikwa Leo Septemba 15, 2016 Katika Magazeti ya Tanzania


Karibu tukuletee kilichoandikwa kwenye vichwa vya habari vya  magazeti ya Tanzania. 






















Visit website






Serikali Yabariki Wenye Jinsia Mbili Kuchunguzwa  

Mamlaka  ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali itakuwa na uwezo na mamlaka ya kuchunguza watu waliozaliwa na jinsi mbili na kubaini jinsi tawala yenye nguvu zaidi. 

Muswada wa Sheria ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali wa Mwaka 2016, uliopitishwa juzi usiku saa nne bungeni unampa Mkemia Mkuu mamlaka ya kuchunguza na kubaini jinsi ya mtu na kutatua utata kwa mtu atakayekuwa amezaliwa na jinsi mbili.

“Waheshimiwa wabunge naona wengi wenu mnadhani mkemia mkuu kazi yake ni kuchunguza vinasaba kubaini uhalali wa mzazi na mtoto, maana naona wabunge wengi wamelishabikia hilo, lakini katika teknolojia ya vinasaba yanahusu pia utambuzi wa jinsi, watu unakuta wanawake au wanaume wanazaliwa jinsi ya kike na kiume, kwa hiyo tunaangalia jinsi tawala ni ipi ina nguvu,” alisema Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu.

Ummy alikuwa akijibu michango ya wabunge waliochangia wakati wa kujadili Muswada wa Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu 2016 kabla ya kuupitisha juzi usiku, waliotaka mamlaka ya maabara ya mkemia mkuu kutoa elimu kwa wananchi juu ya shughuli zake.

Alisema kwa sheria hiyo, sasa mkemia mkuu kupitia maabara yake anaweza kusema jinsi ya kike au ya kiume ndio yenye nguvu, lakini pia kuna suala la kuhakikisha utambuzi wa mwanadamu hasa wakati yanapotokea majanga pamoja na watu wanaosafiri kwa makundi.

Alikubaliana na wabunge kuwa iko haja ya kuwaelimisha wananchi juu ya kazi za maabara ya mkemia mkuu ambao wengi wao wanadhani inafanya kazi hiyo tu ya kubaini vinasaba vya mzazi na mtoto, lakini sasa wafahamu hata waliozaliwa na jinsi mbili wanaweza kutegua utata huo kwa kubaini jinsi tawala au jinsi yenye nguvu zaidi kama ni ya kiume au ya kike.

Alisema Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali imekuwepo kihistoria tangu mwaka 1890 na imekuwa chombo cha kiserikali cha uchunguzi cha kikemia wa kimaabara kwa bidhaa mbalimbali na kuongeza kuwa imekuwa ikifanya uchunguzi wa kikemia wa vyakula, dawa na vipodozi hasa pale inapotokea utata au kuhusisha masuala ya kesi za jinai.

Akifafanua zaidi, alisema kwa upande wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) wao wanafanya udhibiti wa ubora wa chakula, dawa na vipodozi na maabara hii inafanya uchunguzi wa kikemia.

“Maabara ya Mkemia Mkuu kazi yake ni kufanya uchunguzi wa kikemia, vinasaba, kesi za jinai na sayansi jinai. Chombo hiki hakipimi kudhibiti ila kufanya uchunguzi kwa ajili ya vitu vyenye maslahi ya taifa au masuala yenye utatanishi na ushindanishi,” alisema waziri huyo.

Akitoa mfano wa mahindi, alisema kulikuwa na tatizo la sumu kuvu, kwa hiyo mkemia mkuu anafanya uchunguzi wa kimaabara na kusema wamekuta mahindi yana sumu au la, au anaweza mfanyabiashara kuleta maziwa ya mtoto TFDA ikapata mashaka, mkemia mkuu atayafanya uchunguzi wa maabara atasema kama kuna sumu ama kuna kemikali isiyo salama kwa matumizi wa binadamu.

“Baada ya uchunguzi wa kimaabara mwenye jukumu la kusema mahindi haya yasiuzwe au maziwa haya yasiuzwe ni TFDA na sio maabara ya mkemia mkuu. Vile mfanyabiashara anaweza kuleta bidhaa, TFDA ikaitilia mashaka, kwa hiyo huyu mwenye bidhaa anaweza kukata rufaa kwa mkemia mkuu ili apimiwe bidhaa yake kuithibitishia TFDA kuwa bidhaa yake ni salama,” alisema.

Waziri Ummy alikuwa akijibu hoja za wabunge, ambao walikuwa wana hofu kuwa Maabara ya Mkemia Mkuu inaweza kuingilia kazi za taasisi kama TFDA na Shirika la Viwango Tanzania (TBS).

Alizungumzia pia kuhusu kuipa mamlaka ya mwisho maabara hiyo, akisema katika nchi zote duniani zenye maabara hizo, lazima serikali iwe na msemaji wa mwisho wa uchunguzi wa masuala ya kimaabara na kikemia, vinasaba, sayansi jinai na kesi za jinai, lakini pia haifuti sheria wala maabara zingine za uchunguzi zilizoanzishwa kwa mujibu wa sheria mbalimbali.

Kuhusu kutenga bajeti ya kutosha, Ummy alisema serikali imepokea maoni ya wabunge na kuwa baada ya kupitisha muswada huo maabara hiyo imepewa hadhi ya mamlaka na sasa imepewa hadhi na hivyo fungu lake lazima liwe zuri kwa ajili kuendesha shughuli za maabara lakini pia kuajiri watumishi 400 kwani waliopo sasa 192 hawatoshi.

Waziri Ummy alisema wamepokea ushauri wa Kamati ya Kudumu ya Bunge, kufanya uchunguzi wa matumizi ya shisha na kuongeza kuwa tayari mkemia mkuu alifanya uchunguzi na kubaini watumiaji wa shisha wanachanganya bangi, heroine na kokeni na ndio maana serikali ilipiga marufuku kuitumia.

Hata hivyo, alisema sasa itajikita zaidi kuchunguza ili kubaini viambata kiasi gani vilivyopo katika shisha na kwa nini serikali iendelee kupiga marufuku matumizi ya shisha nchini.

Mtuhumiwa: Niliiba mtoto wa siku 10 nimlee

POLISI mkoani Morogoro inamshikilia Anna Luambano (33) ambaye ni mkazi wa Kipawa jijini Dar es Salaam kuwa tuhuma za wizi wa mtoto, Angel Meck mwenye umri wa siku 10 baada ya kumlaghai mama wa mtoto huyo, Maimuna Mahamudu (20) mkazi wa Chamwino katika Manispaa ya Morogoro.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa, Ulrich Matei amesema wizi huo ulitokea Septemba 13, mwaka huu saa 5 asubuhi katika Mtaa wa Kilimahewa Manispaa ya Morogoro.

Akielezea mazingira ya wizi huo, Kamanda Matei amesema mtuhumiwa alimdanganya mama wa mtoto huyo wakiwa njiani kutoka Kituo cha Afya Mafiga, akimwomba ampe mtoto wake akamwoneshe mume wake kuwa huyo ni mtoto wa mdogo wake, ambaye amejifungua ili awape fedha za hongera na kisha wagawane.

Amesema mtuhumiwa huyo baada ya kupewa mtoto huyo, alipotea katika mazingira ya kutatanisha.

Baada ya mama wa mtoto kutambua mwanawe ameibwa, alienda kutoa taarifa Kituo cha Polisi kutoa taarifa ya wizi huo.

Amesema Polisi baada ya kupata taarifa hiyo, walifanya msako kwenye mabasi ya abiria yanayosafiri maeneo mbalimbali, na kufanikiwa kumkamata mtuhumiwa akiwa katika basi la Upendo eneo la Mdaula mkoani Pwani akienda jijini Dar es Salaam.

“Polisi bado inaendelea kumhoji kuhusiana na tukio hilo na hatua za kumfikisha mahakamani zinafuata,” amesema Kamanda Matei.

Akizungumza na waandishi wa habari katika Ofisi za Kamanda wa Polisi Mkoa, mtuhumiwa Anna alidai hakuwa na nia mbaya ya kumwiba mtoto huyo, bali ni kumtunza kwa kuwa hana mtoto.

“Sijabahatika kuzaa mtoto wala sijaolewa na nimehangaika kupata mtoto wa kumleta hadi kufikia hatua ya kuomba mtoto Ustawi wa Jamii lakini sijafanikiwa. Nami ninapenda niwe na mtoto wa kumlea na kuishi naye, nikaamua nimchukue huyu mtoto,” amesema mwanamke huyo.

Kwa upande wake, mama wa mtoto huyo alithibitisha mbele ya mwandishi wa habari hizi nje ya Ofisi ya Kamanda wa Polisi wa Mkoa kuhusu kuibwa mwanawe huyo akiwa njiani akitoka Kituo cha Afya cha Mafiga alipokuwa amejifungulia.

Alisema alikuwa hamfahamu mwanamke huyo wala makazi yake, isipokuwa walikutana njiani, yeye akitoka eneo hilo la Mafiga kurejea nyumbani kwao na hakuweza kuendelea kuelezea kwa kina kisa hicho, isipokuwa kulishukuru Jeshi la Polisi kuwezesha kupatikana kwa mwanawe.

Tukio hilo la wizi wa mtoto mchanga ni la pili kufanywa na wanawake wa kutoka Dar es Salaam kwani Agosti mwaka huu, Polisi Morogoro iliwashikilia wanawake wawili wakazi wa Mbezi jijini Dar es Salaam, Sarafina Henry (28) na Johari Hussein (22) kwa tuhuma za wizi wa mtoto wa kike.

Mtoto huyo aliibwa kutoka kwa wenye mtoto, Ashura Shabani (33) mtaa wa Karume, Manispaa ya Morogoro akiwa na umri wa mwaka mmoja na nusu mwaka 2013. Alipatikana Agosti 7, mwaka huu akiwa ametimiza umri wa miaka minne na nusu huku watuhumiwa wakimwandaa kumwanzisha kusoma elimu ya awali.

Watano kortini kwa kumdhalilisha Rais Magufuli

VIJANA watano wamefikishwa mahakamani kwa tuhuma za kumdhalilisha Rais Dk. John Magufuli na Jeshi la Polisi kutokana na mauaji ya askari polisi wanne waliouawa na majambazi katika eneo la Mbande na Vikindu, Dar es Salaam hivi karibuni.

Washtakiwa hao walifikishwa jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam mbele ya mahakimu watano tofauti na kusomewa mashtaka na Wakili wa Serikali, Salum Mohammed.

Walisomewa mashtaka mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Emmilius Mchauru, Huruma Shahidi, Margareth Bankika, Dk. Yohana Yongolo na Respicius Mwijage.

Akisomewa mashtaka, mshtakiwa Dennis Mtegwa anadaiwa Agosti 24, mwaka huu eneo la Ubungo External kupitia mtandao wa WhatsApp, aliweka maoni katika group linaloitwa Dsm 11 4u Movement, akisema ‘JPM sijui anawaza nini kichwani… hata samahani hajui au nilikosea hajui’, ‘nchi imefika hapa kwa sababu ya mtu mmoja aliyeamua kujilipua ufahamu wake’, ‘sijaona tatizo kwa hilo, ila kwa huyu bwana misimamo ambaye amesema msinijaribu na ilhali kajaribiwa na ubwabwa wa jubilee kusema yote’.

‘Siasa si chuki wala upinzani si uadui, ajifunze kushindana kwa hoja sio mitutu ya bunduki na mazoezi yasiyo na kichwa wala miguu ya polisi’.

Mshtakiwa Suleiman Saidi anadaiwa Agosti 25, mwaka huu maeneo ya Kigogo, kwa kutumia mtandao wa Facebook, aliandika ‘Safi sana aisee, mi naona wangekufa kama 20 hivi halafu Simon Sirro tumuulize mazoezi wanafanyia wake zao au’.

Katika kesi nyingine, mshtakiwa Juma Mtatuu akiwa eneo la Ocean Road, Agosti 24, mwaka huu anadaiwa kuwa alituma ujumbe katika Facebook akisema ‘Huyu hata akifa ataenda peponi, na kufanya mazoezi kote kule wamekufa Mbagala, mimi nitakuwa wa kwanza kuandamana  kule Kahama, tarehe moja naelekea Kahama kwa Ukuta, mimi nitakuwa namba moja kushika bendera ya Ukuta, kifo kipo tuu, usiogope kwani mawe na mapanga yameisha’


 

Gallery

Popular Posts

About Us