KINGAZI BLOG: 10/04/16

HABARI KARIBU YAKO ZAIDI.

Breaking News
Loading...

Tuesday 4 October 2016

TCRA yakipa onyo kali kituo cha runinga cha Clouds.........Yakifungia kwa miezi 3 kipindi cha 'Take One' kwa kukiuka kanuni za utangazaji.

Kamati ya Maudhui ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imetoa onyo kali kwa kituo cha Televisheni cha Clouds sambamba na kukifungia kwa kipindi kwa miezi mitatu kipindi cha Take One kinachorushwa na Kituo hicho.

Makamu mwenyekiti wa kamati hiyo Method Mapunda amesema sababu ya kukifungia kipindi hicho ni kutokana na ukiukwaji wa kanuni za utangazaji za mwaka 2005, kwa kumhoji na kurusha kipindi cha mtu kinachohamasisha biashara ya ngono, kuingilia faragha ya mtu na kutolinda maadili ya watoto.

“Clouds tv inapaswa kukitathimini upya kipindi hicho kwa lengo la kupata njia bora ya kukiendesha na kupeleka mapendekezo TCRA kwa ajili ya kujiridhisha kabla ya kipindi hicho kufunguliwa,”alisema mapunda.

Mahojiano yaliyopekea kipindi hicho kufungiwa ni kati ya mtangazaji wa kipindi hicho Zamaradi Mketema na Gift Stanford Maarufu kama ‘Gigy Money’ na yalirushwa Agost 09 saa 3.00 usiku na kurudiwa kesho yake saa 7.00

MTOA MACHO DAR AKAMATWA...MAARUFU "SCOPION" ANATUMIA KISU KUTOBOA WATU MACHO

KAMANDA wa Polisi Kanda Maalum ya Mkoa wa Dar es Salaam, Simon Sirro amesema jeshi hilo limemkamata mtuhumiwa ‘Scopion’ aliyehusika katika matukio ya unyang’anyi wa kutumia silaha eneo la Buguruni jijini humo. Sirro alitoa kauli hiyo jana Buguruni kwa Mnyamani jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano wa kujadili usalama katika eneo hilo ulioandaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.Alisema mtuhumiwa huyo anayejulikana kwa jina maarufu kama Scopion alikamatwa baada ya polisi kupewa taarifa za matukio ambayo ameyafanya ikiwemo la kumchoma kisu, kumtoa macho na kumsababishia upofu, Said Ally. "Nimesikia wananchi wanalalamika hapa kuwa tumeshindwa kumkamata Scopion, ni nani kwa Jeshi la Polisi asikamatwe, tayari tumemkamata na sheria itachukua mkondo wake, hakuna mtu anayeweza kushindana na jeshi," alisema. Aidha Sirro alisema baada ya kumkamata mtuhumiwa huyo na kuhojiwa aliutaja mtandao wake wote na tayari wameukamata, hivyo amewataka wakazi wa eneo hilo kutokuwa na hofu kwani mtuhumiwa huyo hayupo tena katika eneo hilo. "Najua suala hili bado lipo mahakamani hatuwezi kulizungumzia sana, bahati nzuri alipokamatwa alieleza aliyoeleza na tukafanikiwa kuukamata mtandao wote, hivyo hakuna haja ya kuwa na uwoga eneo hili lipo salama," alisema. Kabla ya kauli hiyo ya Sirro, wananchi wamelalamikia askari wa eneo hilo ambao walishindwa kuchukua hatua kwa mtuhumiwa huyo ambaye alikuwa akifahamika muda mrefu. Sadiki Mgaya ambaye alishuhudia tukio la kuchomwa kisu na kutolewa macho kwa Said Ally, alisema mtuhumiwa huyo alisema kuwa amekuja kwa ajili ya kulipa kisasi kwa wakabaji baada ya yeye kukabwa. Alisema baada ya kufanya tukio hilo, askari walifika katika eneo hilo na mtuhumiwa huyo akiwa hapo na wananchi waliwaonesha askari lakini hawakuchukua hatua zozote badala yake waliwataka wananchi wamkamate. Aidha wananchi hao pia wamemlalamikia Mkuu wa Kituo cha Polisi Mnyamani na kudai kuwa amekuwa akipelekewa taarifa za uhalifu ikiwemo za vibaka lakini mtu anapokamatwa akifika kituoni hapo anatoa rushwa na kuruhusiwa kuondoka. Lakini akiondoka askari wengine wanatumwa tena kumkamata. Kauli hizo za wananchi zikamfanya Sirro kutoa kauli ambapo alisema askari na maofisa wote ambao wanashindwa kutimiza wajibu wao watachukuliwa hatua ikiwemo kufikishwa mahakamani pamoja na kufukuzwa kazi. 
"Najua wapo askari na maofisa wa ovyo ambao hawajui kutimiza wajibu wao, lakini nikuahidi Mkuu wa Mkoa tutawachukulia hatua, nimesikia hapa wananchi wanalalamika askari wanachukua rushwa, tutachunguza tukijiridhisha basi ni lazima tuchukue hatua," aliongeza. 
Aidha Sirro alisema watafanya doria kubwa katika eneo hilo ili kuwakamata wote wanaohusika na matukio ya kihalifu kwani wamebaini katika eneo hilo bado kuna uporaji mdogo mdogo. 
"Tutarudi hapa tunaomba ushirikiano wenu bila ninyi kutuambia hatuwezi kujua, nawaomba wazazi muwakanye watoto wenu ambao wanahusika na matukio hayo kwani tutakapoanza msako huo wasije wakalalamika, uhalifu haulipi na mwisho wa siku utamkosa mtoto wako," alisisitiza. 
Kwa upande wake Makonda aliwataka wananchi hao kujitolea kufanya ulinzi shirikishi na kuwataka wananchi kuchangia ulinzi huo ili vijana hao wahusike kufanya ulinzi na kulifanya eneo hilo libaki na amani. 
"Tuna wajibu wa kufanya ulinzi shirikishi wananchi mtoe michango, hapa Sirro amesema mapungufu yaliyopo kwenye vituo yanafanyiwa kazi, niwaase tu mjiepushe na matukio ya kuhalifu kwani wale watakaokamatwa sheria itachukua mkondo wake," alisema Makonda.
Imeandikwa na Sophia Mwambe-Habarileo

Waziri atolea maelezo taarifa ya serikali kuhakiki watumishi wanavyotumia mishahara yao

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora,  Angellah J. Kairuki amekanusha taarifa inayosambazwa kwenye mitandao ya kijamii kuwa serikali ina mpango ya kuhakiki namna watumishi wake wanavyotumia mishahara yao.

Waziri Kairuki kupitia akaunti yake ya matandao wa Twitter amesema kuwa taarifa hiyo ni ya uongo na kuwataka wananchi kuipuuza kwani ina lengo la kupotosha umma.

“Kuna taarifa ya uongo inayosambazwa mtandaoni kwamba “kutakuwa na zoezi la kuhakiki watumishi wa umma wanavyotumia mishahara yao”.Ipuuzieni.”

“Si dhamira wala desturi ya Serikali yetu kuingilia maisha binafsi ya watumishi wa umma hususan matumizi ya mishahara yao.Puuzieni uzushi huo.”

Taarifa hiyo imemnukuu Waziri Kairuki kuwa serikali baada ya kukamilisha uhakiki wa vyeti kwa watumishi wake, wataanza uhakiki wa jinsi watumishi wa umma wanavyotumia mishahara yao ili kurejesha maadili kwa watumishi wa umma.

Kuhusu uhakiki wa vyeti kwa watumishi wa serikali, Rais Magufulii alisema kuwa lengo la zoezi hilo si kuwafukuza watumishi lakini ni kujiridhidha kama malipo yanayofanyika kwa watumishi hao yanalandana na viwango vya elimu wanavyoeleza kuwa wanavyo.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumanne ya October 4

MTOA MACHO DAR AKAMATWA...MAARUFU "SCOPION" ANATUMIA KISU KUTOBOA WATU MACHO

KAMANDA wa Polisi Kanda Maalum ya Mkoa wa Dar es Salaam, Simon Sirro amesema jeshi hilo limemkamata mtuhumiwa ‘Scopion’ aliyehusika katika matukio ya unyang’anyi wa kutumia silaha eneo la Buguruni jijini humo. Sirro alitoa kauli hiyo jana Buguruni kwa Mnyamani jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano wa kujadili usalama katika eneo hilo ulioandaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.Alisema mtuhumiwa huyo anayejulikana kwa jina maarufu kama Scopion alikamatwa baada ya polisi kupewa taarifa za matukio ambayo ameyafanya ikiwemo la kumchoma kisu, kumtoa macho na kumsababishia upofu, Said Ally. "Nimesikia wananchi wanalalamika hapa kuwa tumeshindwa kumkamata Scopion, ni nani kwa Jeshi la Polisi asikamatwe, tayari tumemkamata na sheria itachukua mkondo wake, hakuna mtu anayeweza kushindana na jeshi," alisema. Aidha Sirro alisema baada ya kumkamata mtuhumiwa huyo na kuhojiwa aliutaja mtandao wake wote na tayari wameukamata, hivyo amewataka wakazi wa eneo hilo kutokuwa na hofu kwani mtuhumiwa huyo hayupo tena katika eneo hilo. "Najua suala hili bado lipo mahakamani hatuwezi kulizungumzia sana, bahati nzuri alipokamatwa alieleza aliyoeleza na tukafanikiwa kuukamata mtandao wote, hivyo hakuna haja ya kuwa na uwoga eneo hili lipo salama," alisema. Kabla ya kauli hiyo ya Sirro, wananchi wamelalamikia askari wa eneo hilo ambao walishindwa kuchukua hatua kwa mtuhumiwa huyo ambaye alikuwa akifahamika muda mrefu. Sadiki Mgaya ambaye alishuhudia tukio la kuchomwa kisu na kutolewa macho kwa Said Ally, alisema mtuhumiwa huyo alisema kuwa amekuja kwa ajili ya kulipa kisasi kwa wakabaji baada ya yeye kukabwa. Alisema baada ya kufanya tukio hilo, askari walifika katika eneo hilo na mtuhumiwa huyo akiwa hapo na wananchi waliwaonesha askari lakini hawakuchukua hatua zozote badala yake waliwataka wananchi wamkamate. Aidha wananchi hao pia wamemlalamikia Mkuu wa Kituo cha Polisi Mnyamani na kudai kuwa amekuwa akipelekewa taarifa za uhalifu ikiwemo za vibaka lakini mtu anapokamatwa akifika kituoni hapo anatoa rushwa na kuruhusiwa kuondoka. Lakini akiondoka askari wengine wanatumwa tena kumkamata. Kauli hizo za wananchi zikamfanya Sirro kutoa kauli ambapo alisema askari na maofisa wote ambao wanashindwa kutimiza wajibu wao watachukuliwa hatua ikiwemo kufikishwa mahakamani pamoja na kufukuzwa kazi. 
"Najua wapo askari na maofisa wa ovyo ambao hawajui kutimiza wajibu wao, lakini nikuahidi Mkuu wa Mkoa tutawachukulia hatua, nimesikia hapa wananchi wanalalamika askari wanachukua rushwa, tutachunguza tukijiridhisha basi ni lazima tuchukue hatua," aliongeza. 
Aidha Sirro alisema watafanya doria kubwa katika eneo hilo ili kuwakamata wote wanaohusika na matukio ya kihalifu kwani wamebaini katika eneo hilo bado kuna uporaji mdogo mdogo. 
"Tutarudi hapa tunaomba ushirikiano wenu bila ninyi kutuambia hatuwezi kujua, nawaomba wazazi muwakanye watoto wenu ambao wanahusika na matukio hayo kwani tutakapoanza msako huo wasije wakalalamika, uhalifu haulipi na mwisho wa siku utamkosa mtoto wako," alisisitiza. 
Kwa upande wake Makonda aliwataka wananchi hao kujitolea kufanya ulinzi shirikishi na kuwataka wananchi kuchangia ulinzi huo ili vijana hao wahusike kufanya ulinzi na kulifanya eneo hilo libaki na amani. 
"Tuna wajibu wa kufanya ulinzi shirikishi wananchi mtoe michango, hapa Sirro amesema mapungufu yaliyopo kwenye vituo yanafanyiwa kazi, niwaase tu mjiepushe na matukio ya kuhalifu kwani wale watakaokamatwa sheria itachukua mkondo wake," alisema Makonda.
Imeandikwa na Sophia Mwambe-Habarileo

Gallery

Popular Posts

About Us