KINGAZI BLOG: 10/07/16

HABARI KARIBU YAKO ZAIDI.

Breaking News
Loading...

Friday 7 October 2016

Serikali Yachachamaa....Walimu Waliomfanyia Ukatili Mwanafunzi Watimuliwa Chuoni, Mkuu wa Shule Apotezama

S

Walimu  wanne wa Chuo Kikuu cha Elimu Dar es Salaam (Duce) na cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere waliohusika kumpiga vibaya mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Mbeya wamefukuzwa chuo huku Jeshi la Polisi mkoani Mbeya likiwashikilia kwa mahojiano walimu wengine watano wa shule hiyo kutokana na tukio hilo.

Aidha, serikali imemvua madaraka Mkuu wa shule hiyo, Magreth Haule kwa kutochukua hatua baada ya kitendo hicho kufanyika shuleni hapo Septemba 28, mwaka huu.

Hatua hizo zimechukuliwa baada ya jana katika mitandao ya kijamii kusambaa kipande cha video kikionesha walimu zaidi ya watatu wakiwa eneo la ofisi wakimshambulia kwa kumpiga makofi, mateke na fimbo sehemu mbalimbali za mwili hasa kichwani mwanafunzi Sebastian Chinguku.

Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako ametangaza kuwafukuza chuo walimu wanafunzi hao walioshiriki kitendo cha kumpiga mwanafunzi huyo wa kidato cha tatu wa Shule ya kutwa ya Sekondari ya Mbeya.

Walimu hao ni Frank Msigwa (anayedaiwa kumpiga zaidi mwanafunzi huyo kwa makofi kichwani), John Deo na Sante Gwamaka wote wa Duce na Evans Sanga wa Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere.

Akizungumza na vyombo vya habari jijini Dar es Salaam jana, Profesa Ndalichako alisema kitendo hicho ni cha kikatili, jinai na kuwa walimu hao wanafunzi hawafai kuendelea na taaluma hiyo ya ualimu na kuwa hatua zaidi za kisheria zinaendelea kuchukuliwa dhidi yao.

Profesa Ndalichako alisema kwa mujibu wa taratibu za vyuo vikuu kitendo kilichofanywa na walimu wanafunzi hao ni kosa la jinai na kuwa hakiwezi kufumbiwa macho.

Alitoa onyo kali kwa wanafunzi wanaokwenda kwenye mafunzo kwa vitendo na kwenda kinyume cha taaluma yao kuwa wanapoteza sifa hivyo amewataka kuzingatia maadili ya fani na taaluma wanazosomea.

Mkoani Mbeya, Kamanda wa Polisi wa Mkoa, Dhahiri Kidavashari alisema wanawashikilia walimu wa shule hiyo watano kwa mahojiano kuhusu tukio hilo. Hata hivyo, alisema si kwamba walimu hao wanaohojiwa ndio waliohusika na tukio hilo bali wameanza na wale waliopo ili kupata taarifa zaidi.

“Hatuwezi kusema sasa hivi kama wale walimu ndio walioonekana katika kipande cha video kinachosambaa mitandaoni kwa kuwa hili ni suala la mahojiano, tunaamini hawa tulionao wanaweza wakatupa mwanga,” alisema.

Akieleza sababu ya adhabu hiyo, Kamanda alisema katika mahojiano ya awali imebainika kuwa mwalimu wa Kiingereza alitoa kazi, lakini baadhi ya wanafunzi hawakufanya baadaye mwalimu huyo aliwapa adhabu ya kupiga magoti, lakini mwanafunzi huyo alionekana kupinga kwa kueleza ana tatizo la goti hatoweza kufanya adhabu hiyo na mwalimu aliamua kumpeleka ofisini na kumpiga kwa kumchangia.

“Mwalimu aliwaadhibu wanafunzi darasani na alipotaka kumuadhibu mwanafunzi huyo mbele ya darasa, alionesha kupinga kupigwa mbele ya wanafunzi wenzake ndipo alipoamua kumpeleka ofisini na kutokea tukio linalosambaa,” aliongeza Kidavashari.

Katika taarifa yake, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba, alisema Septemba 28 mwaka huu, mwanafunzi Chinguku wa kidato cha tatu wa Shule ya Sekondari Mbeya, mkazi wa Uyole, alipigwa na walimu watatu.

“Nimeelekeza vyombo vya dola Dar es Salaam wawatafute chuoni kwao hao walimu kuhusiana na shambulio hilo kwa mwanafunzi huyo,” ilisema Mwigulu.

Naye Waziri katika Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), George Simbachawene ameagiza mamlaka za nidhamu kumvua madaraka Mkuu wa Shule hiyo, Haule kwa kushindwa kuchukua hatua na kutoa taarifa mara baada ya tukio hilo kufanywa na walimu hao shuleni hapo.

"Kwa kuwa waliotenda kosa hili wametoweka tangu Septemba 29, 2016 na hawajulikani walipo, nimesikitishwa kwa kitendo cha mwalimu mkuu wa shule hiyo, Magreth Haule kutochukua hatua. Hii inaonesha kulikuwa na dalili za kutaka kulificha tukio hili baya.

“Na kwa sababu hiyo, pamoja na kwamba wanaendelea kuhojiwa na Polisi, naagiza mamlaka yake ya nidhamu kumvua madaraka mkuu huyo wa shule," alisema Simbachawene katika taarifa yake kwa umma jana.

 Katika hatua nyingine, Rais wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Gratian Mukoba amelaani kitendo kilichofanywa na walimu hao na kukieleza kuwa ni cha mwituni na cha kinyama kwa kuwa hakuna adhabu kama hiyo katika utumishi wa ualimu.

"Nami nimeona hiyo video katika mitandao ya kijamii, kuna sheria za adhabu za viboko lakini si hii walioifanya hao walimu vijana maana walikuwa wakipiga makofi, ngumi, mateke, ngwara. Hizi hazipo kwenye ualimu, lazima wafuate sheria zinazosimamia utumishi wa walimu," alisema Mukoba.

Alishauri vyuo vya ualimu viweke mkazo katika kufundisha walimu vijana namna ya kuwa zaidi ya walimu, kuwa na uvumilivu, subira na kuzingatia sheria. Wafunzwe kisaikolojia kukubali kuwa hawaishii kuwa walimu bali wanaingia kwenye kundi la malezi.

Alisema kwa tukio hilo, ni lazima sheria ichukue mkondo wake ili iwe fundisho kwa wengine wenye tabia hizo hasa walimu vijana kwa kuwa kitaaluma ni tukio la kinyama lisilokubalika.

“Hata kama mwanafunzi ana makosa, amevuta bangi, huwezi kumuadhibu vile, maana pale hujui nani kavuta bangi nani mzima,” alisema Mukoba.

Awali, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla alisema serikali inalifuatilia kwa karibu tukio la kupigwa kama mwizi mwanafunzi huyo wa shule hiyo ya jijini Mbeya na kusema tayari baadhi ya walimu akiwemo mkuu wa shule, wanashikiliwa na Polisi.

Makalla alibainisha hayo jana kwenye Maadhimisho ya Siku ya Fimbo Nyeupe Duniani yaliyofanyika kitaifa mkoani Mbeya na kusisitiza kuwa walimu waliohusika na tukio la kumpiga mwanafunzi wao kama mwizi wanasakwa na lazima watapatikana.

Alisema Septemba 26, mwaka huu, mwalimu aliyekuwa katika mafunzo kwa vitendo katika shule ya Sekondari ya Mbeya Day aliyemtaja kwa jina la Frank Msigwa alitoa kazi kwa wanafunzi darasani na Septemba 28 alipokuwa akisahihisha kazi zilizofanyika alibaini baadhi ya wanafunzi hawakufanya.

Makalla alifafanua kuwa miongoni mwa wanafunzi aliobaini hawakufanya kazi yake ni pamoja na Chinguku na ndipo aliwatoa nje ya darasa na kuwapa adhabu ya kupiga 'push up' lakini mwanafunzi huyo akagoma akidai kuwa na matatizo ya kiafya katika mbavu zake.

Alisema baada ya kugomea adhabu hiyo mwalimu aliwaamuru wapige magoti lakini pia mwanafunzi huyo aligoma akisema ana matatizo ya goti katika moja ya miguu yake ndipo mwalimu alilazimika kutoa adhabu ya kuwachapa viboko viwili kila mmoja na aliwapiga wote isipokuwa Chunguku ambaye kama alivyofanya kwenye adhabu za kwanza hii pia alikataa.

Alisema baada ya hapo mwalimu huyo alilazimika kwenda kuwaita wenzake wawili ambao nao walikuwa kwenye mafunzo ya ualimu kwa vitendo shuleni hapo na wakambeba mwanafunzi huyo hadi ofisini kwao ambako huko ndiko walianza kumchapa kwa kumchangia kama inavyooneshwa kwenye kipande cha video kilichosambazwa kwenye mitandao ya kijamii.

Kwa mujibu wa Makalla, walimu waliotenda kitendo hicho walitoroka na hawajulikani walipo. Alisema serikali inaendelea kuwasaka huku walimu wengine wakihojiwa Polisi.

Rais Magufuli atimiza ahadi yake kwa Balozi Omben Sefue...Amteua kushika nafasi hii

Hatimaye Rais John Magufuli ametimiza ahadi yake kwa aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue baada ya kumteua kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo Cha Diplomasia.

Balozi Sefue amepata uteuzi huo jana ikiwa ni miezi kumi tangu Rais Magufuli atengue uteuzi wake [kama Katibu Mkuu Kiongozi]kwa sababu ambazo hazikutajwa huku akiahidi kumpangia kazi nyingine na nafasi yake ikajazwa na Balozi John Kijazi, .

Aidha, kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Waziri wa wizara hiyo, Balozi Augustine Mahiga amewateua wajumbe sita wa Bodi ya chuo hicho cha Diplomasia.

Wajumbe hao ni Balozi Begum Taj, Balozi John Haule, Juma Salum, Profesa Mohamed Bakari, Profesa Innocent Zilihona na Mathias Abias.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa uteuzi huo umeanza rasmi Oktoba 6 mwaka huu.

Diamond Afunguka Asema Zari Ndiye Model Aliyewahi Kumlipa Hela Nyingi.

Mkali wa wimbo ‘Salome’ na Mkurugenzi wa WCB, Diamond Platnumz amesema katika ma Model ambao amewahi kuwalipa hela nyingi ni Zari ambaye ni mpenzi wake na Mama watoto wake pia.

Diamond Platnumz akiongea katika kipindi cha The play list cha Radio Times Fm na mtangazaji Lil Ommy baada ya kuulizwa ni model gani amewahi kumlipa hela nyingi.

“Zari ndo mtu ni mlipa hela nyingi katika video ya “Utanipenda” unajua hata kama ni Family ni mpenzi wangu lakini inapokuja kazi lazima iwe kazi japo kuwa nilicho mlipa haikuwa thamani yake japo alifanyia kidogo fever lakini nilimlipa zaidi ya Milion kumi ndo model ambaye nimewahi kutoa hela nyingi tokea nimeanza kufanya muziku” alisema Diamond.

Rais Magufuli Atishia kumfukuza kazi mtoto wa dada yake

Rais Dkt John Pombe Magufuli ametishia kufukuza kazi mtoto wa dada yake kutokana na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kutopeleka umeme katika kiwanda kipya cha kusindika matunda cha Bakhresa.

Rais Magufuli alisema jana alipokuwa akifungua rasmi kiwanda cha kusindika matunda cha Bakhresa kilichopo Mwandege, Mkuranga mkoani Pwani.

Wakati wa hafla hiyo ya ufunguzi, kiongozi mmoja wa kiwanda hicho akieleza changamoto wanazokumbana nazo alisema kuwa tatizo linalowakabili ni la umeme ambapo wameongea na TANESCO lakini hadi leo umeme haijafikishwa kiwandani hapo hivyo kuwalazimu kutumia jenereta kuendesha mitambo kitu kinachopelekea kuongezeka kwa gharama za uzalishaji.

Aliposimama kuhutubia Rais Magufuli aliuliza kama kuna kiongozi yeyote wa TANESCO mkoa wa Pwani ndipo akasimama mtoto wa dada yake. Rais Magufuli akamwambia anafahamu kuwa amefanya kazi nzuri alipokuwa Kagera na Tanga na kuwa anataka ahakikishe umeme unafika katika kiwanda hicho la si hivyo ataanza kumtumbua yeye ambaye ni mtoto wa dada yake.

Rais Magufuli alielekeza maswali mawili kwa TANESCO wakati wa hotuba yake, kwanza, kama TANESCO wanania ya kufanya biashara, kwanini hawapeleki umeme kiwandani hapo kwa sababu ni fursa ya kibiashara, pili aliuliza kama TANESCO wanania ya kuona Tanzania inakuwa ya viwanda, kama wanania, kwanini hawapeleki umeme kiwandani hapo.

Rais Magufuli ametoa miezi miwili kwa TANESCO kuhakikisha kuwa wanafikisha umeme kiwandani hapo kama wanataka kuendelea na kazi zao.

Kuhusu ombi la uongozi wa kiwanda hicho kutumia  gesi asilia inayopita jirani na kiwanda hicho, Rais Magufuli alisema kuwa watakaa na Wizara ni Nishati na Madini na Wizara ya Viwanda na Biashara kuona namna wanaweza kulishughulikia hilo.

VIDEO: Maamuzi ya serikali baada ya kuona ile video walimu wakimpiga mwanafunzi


Moja ya headline iliyochukua nafasi katika baadhi ya mitandao ya kijamii ni pamoja na tukio linaloonyesha mwanafunzi wa shule ya sekondari Mbeya Day akipigwa na baadhi ya walimu huku wakimchangia kwa pamoja, tumeona baadhi ya viongozi wa kiserikali wakitumia nafasi hiyo pia kulaani tukio hilo.
October 6 2016 Mkuu wa mkoa wa Mbeya Amos Makala amezungumza na waandishi wa habari mkoani hapo na kuelezea mazingira halisi ya tukio hilo..
Tukio lilitokea Sept 26 mwalimu Frank Msigwa alitoa jaribio kwa wanafunzi lakini baadhi ya wanafunzi hawakufanya, wanafunzi walipewa adhabu ya viboko lakini Sebastian akakataa kuchapwa ndipo walimu wakamchangia kumpiga na kutoroka‘ –Amos Makala
Licha kwamba watuhumiwa w
ametoroka tangu siku ya tukio lakini nimeagiza vyombo vya sheria kuwasaka popote pale walipo, hadi sasa walimu wote wa shule hiyo akiwemo mwalimu mkuu wanashikiliwa ktk kituo cha polisi kwa ajili ya kutoa maelezo‘ –Amos Makala
Taarifa kamili pamoja na video ya tukio hilo nimekuwekea hapa chini…

Uchini…

U

HAYA HAPA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE YA MWALIMU ALIEPIGA MWANAFUNZI MBEYA,PAMOJA NA MATOKEO YA FORM TWO MWANAFUNZI ALIEPIGWA


14572901_1076048742513514_1596917034318518338_n.jpg
mwalimu Frank Msigwa

MATOKEO YAKE


MATOKEO YA MWANAFUNZI ALIEPIGWA


 

Gallery

Popular Posts

About Us