KINGAZI BLOG: 10/19/16

HABARI KARIBU YAKO ZAIDI.

Breaking News
Loading...

Wednesday 19 October 2016

MPYA: HII HAPA LIST YA MAJINA YA FIRST YEAR WALIOPATA MKOPO CHUO KIKUU SUA 2016/17

                             Image result for SUA


Loan Allocations for SUA First Year Students in Academic year 2016/2017

Click to Download >> BOFYA HAPA KUONA MAJINA YOTE


"SCORPION" MTOA MACHO AFUTIWA KESI ILIYOKUWA INAMKABILI.


Mahakama ya Wilaya ya Ilala, imemfutia shtaka linalomkabili mshtakiwa Salumu Njwete baada ya upande wa mashtaka kuomba shtaka hilo liondolewe mahakamani kwa sababu hawana nia ya kuendelea na kesi hiyo.

Kutokana na maombi hayo, Hakimu Adelf Sachore amekubaliana na ombi hilo kwa kuzingatia kifungu namba 91 kifungu kidogo cha kwanza cha sheria ambacho kinampa Mamlaka Mkurugenzi Wa Mashtaka nchini (DPP) kuondoa shtaka mahakamani muda wowote ili mradi kama kesi hiyo haijatolewa hukumu.

Lakini kifungu hicho kinampa Mamlaka DPP kumshtaki mshtakiwa huyo endapo kama ana nia ya kuendesha shtaka hilo.

Njwete anakabiliwa na shtaka la unyang'anyi wa kutumia silaha na kumjeruhi Saidi Mrisho.

Lakini shtaka hili limefutwa hata hivyo anaweza kufunguliwa shtaka lingine

 afunguliwa mashtaka upya



Mahakama ya Wilaya ya Ilala, imemfungulia mashtaka mapya Salum Njwete (Scorpion).Amefunguliwa mashtaka mengine yanayofanana na ya awali ya unyang’anyanyi wa kutumia silaha.

Hata hivyo Njwete amekana shtaka na kurudishwa rumande,huku Hakimu Flora Haule anayesimamia kesi hiyo akizuia dhamana.

Awali Mahakama hiyo ilimfutia mashtaka yanayomkabili Scorpion baada ya upande wa mashtaka kuomba shtaka hilo liondolewe mahakamani kwa sababu hawana nia ya kuendelea na kesi hiyo nakutokana na maombi hayo, Hakimu Adelf Sachore alikubaliana na ombi hilo kwa kuzingatia kifungu namba 91 kifungu kidogo cha kwanza cha sheria ambacho kinampa Mamlaka Mkurugenzi Wa Mashtaka nchini (DPP) kuondoa shtaka mahakamani muda wowote ili mradi kama kesi hiyo haijatolewa hukumu.

Njwete anakabiliwa na shtaka la unyang'anyi wa kutumia silaha na kumjeruhi Saidi mrisho

HAYA HAPA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KOZI YA MEDICINE CHUO KIKUU CHA HUBERT KAIRUKI

Image result for Chuo Kikuu cha Hubert Kairuki

BOFYA HAPA KUONA MAJINA YOTE

MPYA:SECOND BATCH YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA CHUO KIKUU CHA SUA 2016/2017

                              Image result for SUA

UPDATED:Second batch of Students Selected to Join Undergraduate and Non Degree Programmes for Academic Year 2016/2017

The following applicants have been selected to join various undergraduate and Non degree programmes for the 2016/2017 academic year which starts on the 17th October, 2016. Candidates are advised to observe all instructions. BOFYA HAPA KUONA JINA LAKO

MPYA:AWAMU ZOTE TATU ZA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA CHUO CHA SEKOMU-TANGA

MPYA:HAYA HAPA MAJINA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA CHUO KIKUU IRINGA THIRD BATCH 2016/2017

Image result for UNIVERSIT OF IRINGA.AC.TZ

THIRD SELECTION FOR DEGREE PROGRAMMES 2016 - 2017
Congratulations! The following students have been admitted to join various first degree programmes for 2016-2017 Academic year for the third selection batch
Bachelor of Arts in Journalism
S/NLASTNAMEFIRSTNAMEMIDDLESEX
1MOHAMMEDAHMEDABDIM
2WAZIRIMWANAIDITF
Bachelor of Laws
1OMARYHABIBASAIDF
2MAKWAIACLARAAF
3YUSUPHJANEMF
Bachelor of Education (Mathematics)
1KALINGAMICHAELJANUALYM
2DEUSELIZABETHDAUDF
Bachelor of Arts in Community Development
1URIOCHRISTABELLAEF
2NGANYILAMATANGAMM
3STANSLAUSSUNDAYSYLVANUSM
4MAKWABEROBINJM
5DANIELPIUSM
6NOVATHAIDANM
7MTEICATHERINEALBERTF
Bachelor of Accounting  and Finance 
1BENJAMINWAKILIMUGAMBIM
2ATHUMANIJUMAMIRAJIM
Bachelor of Education (Arts)
1KAMONONGOELIPHASWILLIAMM
2SAMWELISTELAMF
3JILALAJUMAM
4SAIDJAFARIM
5REDSONLUCYF
6JOHNLIMBUM
Bachelor of Human Resource Management
1AUGUSTINOAUGUSTINOFESTUSM
Bachelor of Business in Procurement and Supply Chain Management
1BUNYANYAEMILIANAJOHNF
2ISACKDANIELM

Panya Road Apewa Kipigo Kizito na Wananchi .....Azinduka Akiwa Mochwari


Mtoto Isack Ernest (16) anayetuhumiwa kuwa ni mhalifu, maarufu Panya Road, amezinduka akiwa chumba cha kuhifadhia maiti (mochwari) katika Hospitali ya Temeke, Dar es Salaam.

Isack ni miongoni mwa vijana watano waliopigwa na wananchi wenye hasira kwa madai ya kuiba mali zao hali iliyosabisha apoteze fahamu na kudhaniwa amefariki dunia.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa kipolisi Temeke, Kamishna Msaidizi Mwandamizi, Gilles Muroto, alisema baada ya polisi kupigiwa simu na raia wema kuwa kuna vijana watatu wamefariki dunia, walikwenda eneo la tukio na kuwakuta wakiwa na hali mbaya.

“Mmoja wao anayeitwa Kelvin Nyambocha (14) alifariki dunia baada ya kupigwa na kuchomwa moto na wananchi.

 

“Kabla ya kufariki, Kelvin alifuatana na wenzake kwa lengo la kwenda kuangalia tamasha la kuibua vipaji vya muziki wa singeli lililoandaliwa na Radio Clouds Fm lililofanyika Mbagala Zakhem,” alisema Kamishna Muroto.

Alisema wakati wanarudi nyumbani, kundi la vijana hao wanaojiita Panya Road waliokuwa na silaha za jadi (mapanga), waliwavamia watembea kwa miguu na kuwaibia mali zao na ndipo wananchi walipofanikiwa kuwakamata watano. 

Alisema Isack alipigwa hadi akazimia kiasi ambacho walijua amefariki dunia na ndipo alipopelekwa chumba cha kuhifadhia maiti na kufanyiwa taratibu zote, ikiwa ni pamoja na kuvuliwa nguo na kuwekewa namba tayari kwa kuingizwa kwenye jokofu.

“Wakati amewekwa chini kwa ajili ya kuingizwa kwenye jokofu, alizinduka kwa kupumua na kuonekana bado yupo hai, hali iliyosababisha kupelekwa chumba cha uangalizi maalumu (ICU),” alisema Kamishna Muroto.

Alisema baada ya kupata fahamu na afya yake kutengemaa, alihojiwa na Jeshi la Polisi, akawataja wenzake 10 waliokuwa kikundi kimoja. Vijana hao ni Menso Somba (16), Adam Jumanne (16), Bakari Amir (14), Ally Said (17), Abdillah Yusuf (16), Brown Mathias (15), Jafari Salum (13), Hamisi Mwanda (16), Siraji Hamisi (16) na Jeremia Gaudence (13).

Wakati vijana hao wakipewa mapanga yao mbele ya ofisi ya Kamanda wa Polisi wa Temeke huku wazazi wao wakishuhudia, walianza kuyagombea wengine wakidai kuwa yao yamebadilishwa na kupewa wenzao.

Kamishna Muroto alisema kikundi hicho kina bendera inayoonyesha michoro mbalimbali ikiwamo askari mwenye silaha anakimbia huku anatiririka damu, mtu ameanguka chini akiwa amekatwa mkono, nyumba na vijana wawili wakiwa wameshika panga.

Alisema kundi hilo la vijana ambalo linazunguka maeneo mbalimbali, limekuwa likijiita ‘Taifa Jipya’.


Kamishna Muroto alisema kijana mwingine, Faraji Suleiman (19) ambaye pia hali yake ni mbaya, amelazwa Hopitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kwa matibabu zaidi.

Kamanda Muroto alisema vijana wawili aliowataja kuwa Hamisi Mponda (18) na Abdallah Omari (15) walitibiwa hospitali ya Temeke na kuruhusiwa.

Alisema jeshi hilo kupitia Sheria ya Watoto ya mwaka 2009 kifungu 7-9, linakusudia kuwafikisha mahakamani wazazi wa watoto 16 ambao walitajwa na kuthibitisha kufanya uhalifu huo, kwa kushindwa kuwaangalia watoto wao.

Kamishna Muroto alisema wazazi wana wajibu wa kuhakikisha mtoto anakuwa chini ya uangalizi ambao hauwezi kumsababishia madhara ya kimwili na kisaikolojia.

“Hii ina maana kila mzazi ahakikishe mtoto wake ana ulinzi, yuko salama muda wote dhidi ya udhalilishaji na hatari zote ili watoto hawa wakue vizuri,” alisema Kamishna Muroto.

Alisema jukumu la mzazi ni kuhakikisha mtoto anakuwa kwenye malezi bora na si kumwacha akilelewa na walimwengu.

“Mzazi atakayeshindwa kumsimamia vyema mtoto wake na kukiuka sheria ya mtoto ya mwaka 2009 katika kifungu cha 14, atafikishwa mahakamani na akitiwa hatiani atafungwa miezi 6 au kulipa faini ya Sh milioni 5,” alisema Kamanda Muroto.

Alisema kutokana na mazingira waliyokutwa watoto hao, wazazi wao wanatuhumiwa kwa kukiuka sheria hiyo ya watoto.

Akisimulia mkasa huo, Isack Ernest alisema yeye ni mwanafunzi wa kidato cha tatu katika Shule ya Sekondari Lumo na hajawahi kufanya vitendo vya kihalifu.

Alisema wakati yupo kwao, wenzake walimfuata na kumwambia waende kwenye tamasha la singeli Mbagala.

 

“Tulienda na baada ya kumaliza tamasha, wenzangu wakasema twende tukale (walimaanisha wakapore), mimi nikajibu sina pesa, ndipo waliposema wakienda kula hawatanigawia kwa kuwa aliyekula kala, ndipo walipokwenda kuvamia watembea kwa miguu na kuiba.

“Wakati nikiwa ng’ambo ya pili, nikasikia sauti ya watu wanasema mwizi mwizi, mwizi,” alisema Isack.

 

Alisema baada ya kupigiwa kelele za wezi, walikimbia na kumfuata alipo ndipo kipigo kilipomwangukia yeye hadi kupoteza fahamu.

“Nilikuja kushtuka nipo ICU, huku nikiwa sijui niko wapi, nimekoma kujihusisha na makundi kwa sababu sijawahi kuiba katika maisha yangu,” alisema Isack.

Baba mzazi wa kijana huyo, Ernest Chalo, alisema mtoto wake alimuaga anakwenda kuangalia mpira Mbagala Oktoba 15, mwaka huu.

Alisema wakati yeye anafuatilia mchezo wa timu ya Simba na Kagera Sugar, alipigiwa simu na mtu asiyemfahamu akimpa taarifa ya kuwa mtoto wake amefariki dunia.

“Kiukweli nilichanganyikiwa kwa sababu nimetoka kumzika mke wangu wiki moja iliyopita, tena napokea taarifa ya mtoto kufariki, nilitoka mpaka kwa mwenyekiti wangu wa mtaa na kumpa taarifa, nikachukua usafiri wa pikipiki kwenda Hospitali ya Temeke,” alisema Chalo.

Alisema alipofika hospitalini hapo, aliambiwa mtoto wake yupo chumba cha kuhifadhia maiti, lakini alipoletewa mwili kuutambua haukuwa wa mtoto wake, ndipo akatokea msamaria mwema akamwambia mtoto wake alizinduka.

“Kutokana na baridi kali ya chumba cha kuhifadhia maiti, mtoto wangu alipoingizwa mle ndani alipumua na hivyo kuhamishiwa ICU,” alisema Chalo.

MPYA:HAYA HAPA MAJINA YA WANAFUNZI MWAKA WA KWANZA WALIOPANGIWA VYUMBA CHUO KIKUU MUHIMBILI 2016/2017

MUHIMBILI UNIVERSITY OF HEALTH AND ALLIED SCIENCES

Rooms Allocations at MUHAS Hostels

Kindly informed that rooms have been allocated to both Undergraduate and Postgraduate Students  for Academic Year 2016/2017. For more details, download the Rooms Allocation and Important Notice Regarding Room Allocation.
 

Gallery

Popular Posts

About Us