KINGAZI BLOG: 10/24/16

HABARI KARIBU YAKO ZAIDI.

Breaking News
Loading...

Monday 24 October 2016

Hivi hapa Vyakula muhimu Vinavyoongeza haraka Hamu na Nguvu ya Kufanya Tendo la Ndoa

Tatizo la uwezo wa kufanya tendo la ndoa linazidi kukua miongoni wa wanandoa na wapenzi wengi. Takwimu za kitafiti zinaonyesha kuwa karibu ndoa 4 kati ya 10 zenye umri wa miaka 3 na kuendelea zinakabiliana na tatizo hili. Aidha wanaume 6 kati ya 10 wanatajwa kulalamikia upungufu wa nguvu za kiume.

Pamoja na matatizo mengine kutajwa kuchangia upungufu wa nguvu za kiume na kushuka kwa msisimko wa tendo miongoni mwa wanandoa, uchunguzi umeonesha kuwa utumiaji holela wa vyakula hasa vyenye mafuta ni moja kati ya sababu zinazochangia kwa kasi tatizo hili.

Kwa kuzingatia hilo, watafiti wa masuala ya uhusiano wa kimapenzi wamebaini aina mbalimbali ya vyakula ambavyo vina uwezo wa kumuongezea mtu nguvu ya kufanya tendo la ndoa.  Vyakula hivyo ni hivi vifuatavyo:

1. PILIPILI
Kama tunavyojua wote mara nyingi chakula ambacho kimeungwa pilipili hufanya hata mapigo ya moyo kuwa tofauti na wakati mwingine hata jasho au kamasi hutoka. Ndani ya pilipili kuna kitu kinaitwa capsaicin ambacho hufanya pilipili iwe na hali ya ukali. Capsaicin huwezesha ubongo kutoa homoni ya endorphins ambayo huleta mgusu wa hisia za raha wakati wa kufanya tendo la ndoa.
Pia pilipili husisimua mfumo wa fahamu (nerves) wa ubongo na katika kufanya hivyo huwezesha kuamshwa haraka kimapenzi (kunyegeka) wakati wa tendo la ndoa na pia ukiguswa au kubusiwa au kunyonywa au kupapaswa unapata hisia kila sehemu ya mwili.

2. MATUNDA NA MBOGA ZA MAJANI
Ulaji wa matunda na mboga za majani una matokeo makubwa sana katika hamu ya tendo la ndoa kwa njia nyingi. Kwanza matunda na mboga za majani hupunguza kiwango cha mafuta na unene (cholesterol).  Kuongezeka kwa mafuta mwilini huzuia mzunguko wa damu kwa kubana mishipa ya damu.

Pia kula matunda na mboga za majani huhakikisha balance ya uzito kwani unene (obesity) kwa wanaume kuna matokeo mabaya katika kuzalisha homeni za testoeterone na hatimaye jogoo kushindwa kuwika na kuwa na pia mwanaume anakuwa na hisia za mapenzi (libido) kidogo.
Na pia wanandoa wanapozidi kunenepeana ndipo na hali ya kufurahia au kuwa na hamu ya tendo la ndoa huzidi kupungua. Kitalaam inashauriwa kula milo (potions) 3-5 za matunda kwa siku.

3. NAFAKA ZISIZOKOBOLEWA
Nafaka hasa zisizokobolewa kama mahindi, ngano, uwele, nk zina nyuzinyuzi (fibre) na sukari ngumu (complex sugar) ambazo kusaidia kutunza uzito wa mwili. Nafaka husaidia katika kuzalisha homoni za testosterone kwenye damu. Na pia nafaka huwezesha mtu kuwa na nguvu hatimaye kwenda masafa marefu wakati wa tendo.

Kula nafaka nzima kama vile brown bread badala ya white bread, pia kula nafaka halisi badala ya cornflakes ni jambo zuri linalokuhakikisha afya nejama na mahusiano mazuri ya ndoa yako.

4. TANGAWIZI
Tangawizi ni kiungo cha mboga ambacho husisimua sana na kusaidia mfumo wa mzunguko wa damu mwilini. Tangawizi zinajulikana sana kwa kusukuma damu kwenda sehemu za viungo vya uzazi yaani uke na uume hivyo kuwa na umuhimu sana katika kuboresha ufanyaji wa tendo la ndoa. Inaweza kuliwa mbichi, au kuliwa ikiwa imeungwa kwenye chakula au kusagwa na kuwa kama unga na kutumiwa kama chai.

5. ASALI
Asali ina madini yanayoitwa boron, ambayo husaidia mwili kutumia homoni ya estrogen ambayo ni homoni inayohusika na viungo ya uzazi na mapenzi kwa mwanamke.
Pia kuna utafiti unaoonesha kwamba asali huongeza nguvu, kitendo ambacho kitapelekea mwanamke kuwa uwezo na hamu ya tendo la ndoa au libido.

6. KARANGA
Karanga huhusika katika kuchochea mfumo wa mzunguko wa damu (vascular system). Mzunguko wa damu ulio sawasawa katika uke na uume huwezesha mwanaume na mwanamke kupata msisimko wa mapenzi haraka hatimaye tendo la ndoa kuwa murua. Pia karanga zina madini muhimu kama vile magnesium, asidi ya folic na zinc ambayo ni muhimu sana katika usalishaji wa mbegu za mwanaume.

7. CHAZA (OYSTERS) NA PWEZA
Hawa ni aina ya samaki ambao hupatikana katika maji chumvi. Huwa na kiasi kikubwa sana cha madini ya zinc na haya madini ndiyo huhusika zaidi na uzalishaji wa homoni ya testosterone kwa wanaume.
Pia imethibitika kwamba wanaume wenye ukosefu wa madini ya zinc huwa na matatizo ya nguvu za kiume.  Pia madini mengi ya zinc mwilini huongeza kiwango cha shahawa kwa wanaume.

8. SOYA
Pamoja na kuwa na kiwango kidogo sana cha mafuta (fat) na pia kuwa na kiwango kizuri cha protein, soya zina phytoestrogens ambayo husaidia sana wanawake ambao wamefikia menopause kutengeneza homoni estrogen ya ziada.
Husaidia uke kuwa laini (wet, lubricated) mwanamke akisisimuliwa wakati wa tendo la ndoa.

9. CHOKOLETI
Chocolate ina phenylethylamine, kemikali ambayo husababisha hisia (feelings) za furaha wakati wa mwanamke au mwanaume kufika kileleni (orgasm). Inasaidia sana kula chocolate masaa machache kabla ya kuanza kufanya tendo la ndoa.

10. PARACHICHI
Aina nyingine ya chakula ambacho husaidia kuongeza uwezo wa mtu kufanya tendo la ndoa ni Parachichi. Tunda hili linauwezo mkubwa wa kuzalisha vitamini E ambayo husaidia katika uzalishaji wa homoni. Inatajwa kuwa watu wanaotumia tunda hili kwa wingi huwana msisimko mkali wa kimapenzi na kwa upande wa wanawake husaidia kuongeza majimaji yenye utelezi sehemu za siri na hivyo kuzuia uwezekano wa kuchubuka wakati wa kujamiiana.



MANENO YA DIAMOND PLATNUMZ BAADA YA KUKOSA TUZO MTV MAMA’S

Mambo hayakuwa mazuri kwa watanzania baada ya kutofanikiwa kupata tuzo hata moja kwa wasanii wote ambao walikuwa wakiliwakilisha taifa katika tuzo za MTV Africa Music Awards (MAMA).

Diamond Platnumz ni mmoja wa wasanii kutoka Tanzania ambao walikuwa wakiwania tuzo hizo na alikuwa na haya ya kuwaambia mashabiki zake kupitia ukurasa wake wa Instagram baada ya utoaji wa tuzo hizo kumalizika.

“Shukran sana sana kwa kura na sapoti kubwa mlionipa na mnayoendelea kunipa… pia S/O tu my fellow Tanzanian Artist wote waliobahatika kuchaguliwa… Kamwe tusisononeke.. kuingia tu watanzania wengi kwenye MtvAwards ni hatua kwa Muziki wenu na ushinndi tosha kwa taifa letu…ila wanna congrats my brothers @sautisol for the Best Group award…my hommie @jahprayzah and @wizkidayo ya’all deserve the Trophies….”


KUTANA NA HUYU MWANAMKE MNENE ZAIDI DUNIANI. .ANA UZITO WA KILO 500

Kwa mujibu wa jarida la Daily Mail, inaelezwa kuwa mwanamke huyo aitwaye Iman Ahmad Abdulati mwenye miaka 36 hajawahi kutoka ndani kwa miaka 25 na amekua akiongezeka uzito wake kwa haraka mpaka kufikia kilo 500 zinazompa shida ya kujifanyia usafi na hata kula. Ripoti ya madaktari inaonesha kuwa mwanamke huyu anasumbuliwa na maambukizi ya bakteria wanaoshambulia ukuaji wa mwili.

Akiwa na miaka 11 alianza kusumbuliwa na tatizo hilo ingawa wazazi wake wanakiri kuwa hawakudhani kuwa ni tatizo lakini siku zilivyozidi kwenda ndipo wakabaini kuwa halikua jambo la kawaida hivyo wakaamua kutafuta wataalamu ambao walitoa ripoti kuwa ana matatizo ya mwili wake kukaa na maji mengi bila kuyatoa nje kitu ambacho sio cha kawaida kwa binadamu.


HABARI KUU KWENYE MAGAZETI YA LEO JUMATATU YA TAR 24 OKTOBA.


Shirika lingine la Ndege duniani lapiga marufuku Galaxy Note 7 Shirika la ndege la Uturuki la Turkish Airlines lapiga marufuku kwa wasafiri wake kutumia Galaxy Note 7 katika ndege zake.


Shirika la ndege la Ujerumani la Lufthansa kwa upande wake lilipiga marufuku Jumanne  matumizi ya smartphones Galaxy Note 7 za Samsung katika ndege zake.

Shirika la ndege la Uturuki la Turkish Airlines limefahamisha pia kwa upande wake Ijumaa kuwa linapiga marufuku Galaxy Note 7 katika ndege zake kwa kuhofia ya kwamba zinaweza kusababisha moto kuzuka.

Hatuo hiyo imechukuliwa kutokana na hitilafu katika betri la simu aina ya Samsung Galaxy Note 7.

DIAMOND PLATNUMZ KUACHIA NGOMA YAKE MPYA NA LADY JAY DEE

Baada ya kilio cha muda mrefu kutoka kwa mashabiki waliotamani kuona Diamond Platnumz na mwanadada Lady Jay Dee wakifanya kazi pamoja, wakali hao wa bongo fleva huenda wakaja na 'collabo' ya hatari, siku chache zijazo.Hatua hiyo inatokana na msanii Diamond kufunguka kuwa hakuna sababu yoyote inayowakwamisha kufanya kazi ya pamoja, isipokuwa muda na ratiba zao kubana.
Dangote ametoa kauli hiyo hivi karibuni alipotembelea ofisi za EATV, na kukutana na maswali mbalimbali ikiwemo sababu za wao kutofanya kazi ya pamoja licha ya mashabiki kuitamani 'collabo yao.
"Siku si nyingi tutafanya kazi pamoja na Jay Dee, kilichotukwamisha ni ratiba zetu, lakini pia nilikuwa sijafikiria hilo, ila sasa kwa kuwa mashabiki wamekuwa wakiomba kila mara, nitawasiliana naye, na tutafanya kazi ya pamoja muda mfupi ujao, hakuna sababu nyingine tofauti na kubanwa na kazi nyingi, pamoja na ratiba zetu kutoendana"
Kuhusu ni lini mashabiki wategemee kazi hiyo, Dangote alisema kuwa hawezi kuahidi tarehe, lakini ana uhakika 'collabo' hiyo inakuja.


 

Gallery

Popular Posts

About Us