KINGAZI BLOG: 11/24/16

HABARI KARIBU YAKO ZAIDI.

Breaking News
Loading...

Thursday 24 November 2016

BASATA KUTOA TAMKO KUHUSU VIDEO YA RICH MAVOKO

Rich Mavoko na Diamond Platnumz wamezichezea sharubu za simba mkali aliyekuwa usingizini.

Baraza la Sanaa la Taifa, BASATA limehisi kuna udhalilishwaji wa wanawake kwenye video hiyo na limesema litatoa tamko lake iwapo litaifungia video hiyo au lah!

“Ktk kusimamia maadili ktk Sanaa & udhalilishaji wanawake tuko thabiti.Video ya #kokoro ya #Mavoko inapitia uhakiki.Taarifa itatoka,” limeandika baraza hilo kwenye akaunti yake ya Twitter.

Video ya wimbo huo iliyofanyika nchini Afrika Kusini inaonesha wanawake waliopo kwenye Jacuzzi huku maziwa yao yakiwa wazi licha ya kupakwa rangi ya dhahabu.


Hii hapa njia sahihi ya Punguza kilo tano kwa siku saba

NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha maradhi mbalimbali bali pia mwonekano wako unakuwa si mzuri. Makala haya yanaeleza namna ya kupunguza unene ndani ya siku saba.

Siku ya 1: Asubuhi kula matunda (lakini usile ndizi). Mchana chemsha kabichi, weka chumvi kidogo na nyanya, chemsha na upate supu. Kula mchanganyiko huo na utajiona umeshiba. Jioni kula tikiti maji na mbogamboga au kabichi uliyotengeneza mchana.

Siku ya  2: Kula mboga za majani asubuhi (usile mboga za majani zenye wanga kama karoti).  Mchana kula kabichi iliyochemshwa, tengeneza na kachumbari. Katika kabichi weka chumvi, pilipili na mafuta ya olive.  Jioni unaweza kula mlo kama wa mchana lakini unaweza kukaanga mboga nyingine za majani.

Siku ya 3: Kula mboga za majani na matunda, unaweza kuongeza kiazi kitamu kimoja.

Siku ya nne 4: Kula ndizi moja na unywe na maziwa ya mtindi wakati wa asubuhi. Mchana kula kabichi kama ulivyoitengeneza kwenye siku ya kwanza, usiku rudia mlo wa mchana.

Siku ya  5: Kula nyanya nne pamoja na samaki au kipande cha kuku asubuhi. Mchana unaweza  kula samaki wa kuchemsha kiasi ambaye amechanganywa na nyanya.  Wakati wa jioni unaweza kula chakula kama cha mchana.

Siku ya 6:  Unaweza kula chakula cha protini na mboga za majani. Anza kwa kula kachumbari asubuhi. Mchana kula tambi kiasi na kipande kidogo cha samaki. Usiku tengeneza supu ya kabichi.

Siku ya 7: Anza kwa matunda na juisi. Mchana kula mboga za majani na usiku kula supu ya kabichi na kiazi kimoja.

Kumbuka: Unatakiwa kunywa maji angalau glasi nne kila siku. Usiendelee kwa muda mrefu, kumbuka dayati hii ni ni kwa siku saba. pekee.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Alhamisi ya Novemba 24



Bodi ya Mikopo yawaponza wanafunzi 1,132 wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine (Saut) cha Mwanza

Wanafunzi 1,132 wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine (Saut), cha Mwanza hawatapewa matokeo yao ya kuhitimu shahada wala kushiriki katika mahafali baada ya Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) kutolipa ada zao za mwaka huu wa masomo.

Kwa mujibu wa orodha ya wanafunzi iliyobandikwa katika ubao wa matangazo chuoni hapo, ni wanafunzi 933 tu watakaoshiriki katika mahafali yaliyopangwa kufanyika Desemba 16 na 17. 

Tangazo hilo lililosainiwa na Makamu wa Mkuu wa Chuo (Taaluma), Dk Negussie Andre limewataka wanafunzi kuhakiki majina yao kwenye orodha na kuwasilisha malalamiko au hoja zao kabla au ifikapo Jumapili ijayo.

Kuhusu madai hayo, Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB, Abdul Razaq Badru alisema hawezi kuyazungumzia kwa sababu kila chuo kina mamlaka yake.

Alisema Bodi hiyo ipo kwa miaka 10 na kwamba bila shaka kuna taasisi zinazoidai na zinalipwa kulingana na makubaliano na mipango iliyopo akisema kila wakati kuna malipo yanayoendelea katika vyuo mbalimbali.

Hata hivyo, alisema hana takwimu sahihi kama na chuo hicho kimeanza kulipwa. 

“Tunafanya malipo kulingana na mipango iliyopo, kama kuna changamoto katika vyuo tunavyolipa au vinavyotudai huwa tunajadili kwa pamoja na kupata majibu, kwa hilo lililotokea Saut sisi kama Serikali hatuwezi kukemea wala kupongeza kwa sababu ni mamlaka ya chuo,” alisema Badru.

Akizungumza kwa simu jana jioni, Ofisa Mikopo wa Saut, Wilfred Medard alisema uamuzi huo umechukuliwa kutokana na malimbikizo ya ada ya wanafunzi wanaolipiwa na bodi hiyo.

“Siwezi kutaja ghafla ni kiasi gani tunachodai, lakini kwa hakika ni zaidi ya Sh500 milioni,” alisema Medard.

Alisema si rahisi kujua iwapo wanafunzi hao wote watashiriki mahafali kwa sababu bado kuna fursa ya bodi kulipa madeni hayo na kuwapa nafasi ya kushiriki mahafali na wenzao wanaojilipia au wanaolipiwa na kampuni, taasisi na mashirika mbalimbali.

Ingawa tangazo hilo limetoa hadi Jumapili ijayo kwa wahitimu ambao majina yao hayapo kwenye orodha kuhakiki na kuwasilisha taarifa zao, Medard alisema bado kuna fursa ya wahusika kukamilisha taratibu hadi Desemba 2 ambayo ni siku ya mwisho ya maandalizi ya mahafali.

Rais wa Serikali ya Wanafunzi Saut (Sautso), Emmanuel Ayo alisema wanafunzi wanaunga mkono uamuzi wa chuo kuishinikiza Serikali kulipa madeni hayo ili kukiwezesha kujiendesha.

“Hiki ni chuo binafsi kinachojiendesha kupitia ada za wanafunzi. Kutolipa ada ni kukwamisha shughuli na masomo na sisi hatuko tayari kuona tunakosa masomo kwa sababu tu Serikali haitimizi wajibu wake wa kuwalipia wanafunzi inaowadhamini,” alisema Ayo.

Alisema iwapo muda uliotolewa na chuo kuhakiki utapita bila ya kulipwa kwa ada hizo, Sautso imepanga kuonana na Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako kuwasilisha kilio chao.

“Waziri asipotusaidia, tutakwenda hadi Ikulu kumwona Rais John Magufuli ambaye pengine wasaidizi wake hawampi taarifa sahihi kuhusu kinachoendelea Bodi ya Mikopo,” alisema Ayo.

Kiongozi huyo ambaye ni mwanafunzi wa mwaka wa tatu wa shahada ya ualimu, alijitolea mfano kuwa ada yake ya muhula wa pili mwaka jana haijalipwa hadi sasa na bodi hiyo.

 

Gallery

Popular Posts

About Us