KINGAZI BLOG: 11/26/16

HABARI KARIBU YAKO ZAIDI.

Breaking News
Loading...

Saturday 26 November 2016

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumamosi ya Leo Novemba 26




Muuguzi anayedaiwa kumwambia mama wa mgonjwa ‘ataisoma namba kumchagua Magufuli’ atambuliwa

Mbeya. Muuguzi wa Hospitali ya Mkoa wa Mbeya anayedaiwa kumkamshifu Junes Elias, mkazi wa Mbozi mkoani Songwe na Rais John Magufuli ametambuliwa.

Mganga mkuu wa hospitali hiyo, Dk Gloria Mbwille alisema muuguzi huyo ametambuliwa na kwamba tume imeundwa kuchunguza tuhuma zinazomkabili.

Hata hivyo, alikataa kuzungumzia zaidi kuhusu muuguzi huyo wala kumtaja jina akisema taarifa zaidi zitatolewa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla baada ya tume kukamilisha uchunguzi huo. Juzi mchana, Junes alimueleza Makalla kwamba alifika hospitalini hapo Novemba 22 asubuhi akitokea wilayani Mbozi.

Alisema baada alifuata taratibu za kufungua kadi kwa gharama ya Sh5,000 kwa ajili ya kutaka matibabu ya mtoto wake, Joyce Asifiwe (9), lakini alikashfiwa kwenye dirisha la dawa akiambiwa ataisoma namba kwa kumchagua Rais Magufuli.

Alisema baada ya kumuona daktari aliandikiwa dawa za kwenda kuchukua kwenye dirisha ambako ndiko alikotolewa maneno ya kashfa.

“Kwenye dirisha hilo nilimkuta muuguzi mmoja ambaye aliniambia kwamba dawa zote zinauzwa. Hapa hakuna dawa za bure, si mlimchagua Magufuli, sasa mtaisoma namba,’’ alisema akidai kumnukuu aliyemtaja kuwa ni muuguzi.

Baada ya kumsikiliza malalamiko hayo, Makalla aliagiza mganga mkuu aitwe, lakini ilielezwa alikuwa safarini, hivyo kaimu wake, Dk Ismail Macha alifika.

Makalla alimueleza Dk Macha kwa kifupi yaliyojiri kutoka kwa mlalamikaji huyo na kumtaka waongozane hadi hospitalini na kuwaita wauguzi waliokuwa zamu Novemba 22 dirisha la dawa ili amtambue mhusika na achukuliwe hatua jambo ambalo limefanyika.

Rais za Zamani wa Cuba, Fidel Castro Afariki Dunia

Rais wa zamani wa Cuba na kiongozi wa mapinduzi ya kikomunisti, Fidel Castro amefariki akiwa na umri wa miaka 90, mdogo wake Raul ametangaza.

Amefariki usiku wa saa nne na dakika 22, kwa mujibu wa Rais Raul Castro.

Fidel Castro aliiongoza Cuba kama nchi ya chama kimoja kwa takriban miaka 50 kabla ya Raul kushika madaraka mwaka 2008.

Mazishi yake yanafanyika Jumamosi hii kwa mwili wake kuchomwa moto. Kutakuwepo na siku kadhaa za maombolezo ya nchi nzima.

 

Gallery

Popular Posts

About Us