KINGAZI BLOG: 09/06/16

HABARI KARIBU YAKO ZAIDI.

Breaking News
Loading...

Tuesday 6 September 2016

Serikali Yakanusha Taarifa Inayosambazwa Katika Mitandao ya Kijamii Kwamba Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan Ameomba Kujiuzulu



Ofisi ya Makamu wa Rais inakanusha taarifa inayosambazwa kwenye mitandao ya kijamii kwamba Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan, ameomba kujiuzulu nafasi yake na kwamba taarifa hiyo ni ya uzushi na uongo haina ukweli wowote.

Taarifa hiyo ni ya uchochezi inayolenga kuliweka Taifa kwenye taharuki.  Mhe. Makamu wa Rais yuko bega kwa bega na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kufanya kazi zao kwa mujibu wa Katiba ya nchi ili kuwaletea wananchi maendeleo.

Ofisi ya Makamu wa Rais inawataka wananchi na Watanzania kwa ujumla kupuuza taarifa hiyo ambayo inalenga kupotosha umma kuhusu ushirikiano mzuri uliopo baina ya Viongozi wetu.

Mwisho, Ofisi ya Makamu wa Rais inawasihi Watanzania kufanya kazi kwa bidii na wajiepushe na vitendo vinavyolenga kuvuruga amani na utulivu nchini.

TENGENEZA PESA UKIWA UMEKAA NYUMBANI KWAKO SHULE NA MAHALI POPOTE

Image result for referral program
WADAU HABARI YENU VIPI?LINK NLOSHARE HAPO CHINI NI KAMPUNI YA MATANGAZO,,,AMBAPO UNAVOZIDI KUIPROMOTE KIPATO CHAKO KINAKUA,,,INGIA KWENE LINK UJIUNGE UANZE KUTENGEZA CASH UKIWA HOME
[ Ukiwa unaitangaza kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii na kushare na watu kuhusu hiyo software unakua unalipwa,,


 

Gallery

Popular Posts

About Us