KINGAZI BLOG: 02/09/17

HABARI KARIBU YAKO ZAIDI.

Breaking News
Loading...

Thursday 9 February 2017

BREAKING NEWS: Askofu Gwajima naye atinga na wafuasi wake kituo cha kati cha Polisi Dar


Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima,Mchungaji Gwajima akiwasili kituo cha polisi kati majira ya saa 7:30 mchana akiwa ameongoza na wafuasi wake,kutii agizo la Mkuu wa Mkoa Paul Makonda,ambaye watuhumiwa wote 65 aliowataja jana katika sakata la dawa za kulevya,aliwataka kufika kesho Ijumaa saa 5 asabuhi kituo cha Polisi kati kwa mahojiano zaidi.

Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima,Mchungaji Gwajima akiwasili kituo cha polisi kati majira ya saa 7:30 mchana akiwa ameongozana na wafuasi wake, kutii agizo la Mkuu wa Mkoa Paul Makonda,ambaye watuhumiwa wote 65 aliowataja jana katika sakata la dawa za kulevya,aliwataka kufika kesho Ijumaa saa 5 asabuhi kituo cha Polisi kati kwa mahojiano zaidi.

Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima,Mchungaji Gwajima akionekana kufurahia jambo wakati akiwasili kituo cha polisi kati majira ya saa 7:30 mchana akiwa ameongoza na wafuasi wake,kutii agizo la Mkuu wa Mkoa Paul Makonda,ambaye watuhumiwa wote 65 aliowataja jana katika sakata la dawa za kulevya,aliwataka kufika kesho Ijumaa saa 5 asabuhi kituo cha Polisi kati kwa mahojiano zaidi.

Zari Afungukia Harusi Yake na Diamond na mengine mazito.


Zari The Bosslady amedai kuwa anataka harusi yake na Diamond Platnumz iwe kubwa na yenye gharama kuwahi kufanyika Afrika Mashariki.Hata hivyo, itafanyika baada ya kuwa wamefanya mambo ya muhimu zaidi ikiwemo kujijenga zaidi walivyo sasa. 

Akizungumza kwenye kipindi cha Leo Tena cha Clouds FM Alhamis hii, Zari amedai kuwa suala la kufunga ndoa sio kitu kinachowapa pressure.

Amedai kuwa hawajawahi kukaa chini na kuwa na majadiliano ya kina kuhusu ndoa, licha ya hadi sasa kuwa na watoto wawili, Tiffah na Nillan. Staa huyo wa Uganda amedai kuwa moja ya mambo ambayo wanataka kufanya ni kuhakikisha kwanza wanawajengea watoto wao apartments zao zitakazowasaidia katika maisha yao hata kama wazazi wao wasipokuwepo.

Hata hivyo Zari amedai kuwa mwezi March mwaka huu Diamond ataenda rasmi kujitambulisha kwa baba yake na kuhalalisha uhusiano wao pamoja na kuomba mkono wa ndoa.

Kauli ya Freeman Mbowe Baada ya Makonda Kumtaja kwenye Orodha ya Wahusika wa Madawa ya Kulevya

K

Muda mfupi baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kuwaita polisi kuhojiwa kwa tuhuma mbalimbali, baadhi ya walioitwa wamelaani hatua hiyo wakisema inalenga kuwachafulia majina na heshima mbele ya jamii.

Miongoni mwa waliotwa ni Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, ambaye amezungumza na kueleza kutofurahishwa na hatua hiyo.

Mbowe aliyekuwa safarini kwenda bungeni Dodoma, alisema ameshangazwa kutuhumiwa kwa jambo asilolijua.

“Kama amemtaja mbunge wa Hai anajulikana ni mmoja, hata kama asingesema Freeman, Mbunge wa Hai anajulikana ni Freeman Mbowe.

“The only thing (kitu pekee) ninaweza kusema nchi haiendeshwi hivyo. Yametajwa majina mengi ambayo sijui Makonda ana evidence (ushahidi) gani!

“Anasema tukiwaita tukiridhika na maelezo yao tutawaachia. Huwezi kusema tu, yaani kwa kusema ni Mbowe... mimi ni Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, mimi ni mbunge, mimi ni mzazi, nina wanachama, maaskofu, mapadri, mashehe na viongozi mbalimbali.

“Unapokuwa unamhusisha kiongozi na ‘drug trafficking au drug business’ (usafirishaji wa dawa au biashara ya dawa za kulevya), sijui ana ushahidi gani hadi akanihusisha na jambo hilo, mimi sielewi, kwa hivyo siwezi kusema kwa kitu ambacho sielewi,” alisisitiza Mbowe.

Mbowe aliendelea kusema kuwa kesi za dawa za kulevya hazina dhamana, hivyo alimtaka Makonda awe na ushahidi wa kutosha anapowataja watuhumiwa.

“Tuache habari ya kuitwa, wewe umepata tuhuma, hujafanya uchunguzi, hakuna mtu aliye juu ya sheria, lakini unatakiwa kufanya uchunguzi ili ukimkamata mtu unamshtaki, siyo unataja mtu unachafua hadhi yake. Halafu ukija kusema hatuna ushahidi juu yako umeshaharibu jina lake,” alisema na kuongeza:

“Mimi sijui kama jeshi la polisi linafanya kazi hii au ni Makonda amejipa kazi ya kuwa mpelelezi. Au labda yeye kwa kuwa ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ndiyo amejipa kazi ya kutaja majina kwenye mambo yenye kashfa kama haya? Sielewi. This is very wrong precedence (Hii ni rejea mbaya) kwa utawala wa sheria.”

Mbowe alisema inawezekana ni mikakati ya Serikali kuendelea kukandamiza upinzani kwa kuwakamata viongozi wake.

“Sijui kama kuna watu wanaolengwa, lakini tumeona viongozi wetu wanakamatwa hawapewi dhamana, (Tundu) Lissu amekamatwa, (Godbless) Lema amekamatwa ... mtu anakaa miezi minne, kwa hiyo wanaweza kufanya lolote. Inawezekana ni mkakati wa kutesa wapinzani. Wamenitafuta kwenye biashara wameona haitoshi... sina uhakika lakini sioni kama wana nia njema na sisi,” alisema Mbowe.

Alipoulizwa kama ataitikia wito wa Makonda, Mbowe alisema bado anawasiliana na wanasheria wake kabla ya kuchukua hatua.

Picha 4: Yusuf Manji awasili Polisi Leo badala ya Kesho baada ya kutajwa na Makonda kwenye list ya jana.

Mfanyabiashara maarufu nchini, Yusuph Manji amefika kituo cha Polisi cha Kati leo saa 4:54 asubuhi kwa ajili ya mahojiano baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kumtaka afike polisi.

Manji amefika leo badala ya kesho ambapo yeye na wengine 64 walitakiwa kufika kituoni hapo.

Manji ambaye pia ni Mwenyekitu wa Klabu ya Yanga jana alizungumza na waandishi wa habari na kusema hatoweza kufika kituoni hapo siku ya Ijumaa.

Amewasili leo na gari aina ya Range Rover rangi nyeusi huku.

Manji amefika kituoni hapo  akiwa na wanasheria wake 8 ambapo wanasheria 6 ni raia wa Tanzania na wanasheria wawili ni raia wa Uingereza. Aidha, mashabiki wa Yanga wamejitokeza kwa wingi kituoni hapo kumuunga mkono kiongozi wao.

Mbali na Manji, wengine waliotajwa katika orodha hiyo ni Pamoja na Fremaan Mbowe, Askofu Josephat Gwajima, Iddi Azan. 


JPM amtumbua Kigogo Huyu wa Wizara ya fedha


Rais John Magufuli amemsimamisha kazi Kaimu Katibu wa Tume ya Mipango (Wizara ya Fedha), Florence Mwanri aliyeidhinisha kuanza kwa awamu ya pili ya ujenzi wa jengo jipya la Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) (Terminal 3) kabla ya kumalizika kwa awamu ya kwanza.

Rais Magufuli alifikia uamuzi huo baada ya kufanya ziara ya kushtukiza katika mradi wa ujenzi wa jengo jipya na kuagiza shughuli za ujenzi wa uwanja huo ziendelee kuanzia leo.

Katika ziara aliyoifanya jana ilielezwa kuwa mkandarasi anayejenga uwanja huo,  kampuni ya BAM International alitangaza kusitisha ujenzi kuanzia jana kutokana na kutolipwa madai yake. Hata hivyo, Rais Magufuli ameahidi kulipa fedha hizo haraka.

Taarifa iliyotolewa jana na Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Gerson Msigwa ilieleza kuwa Rais Magufuli alisikitishwa na namna mradi huo unavyotekelezwa, ikiwamo Serikali kukubali gharama kubwa za mradi ambazo ni Sh560 bilioni kiwango ambacho ni kikubwa ikilinganishwa na jengo linalojengwa.

“Hivi kulikuwa na sababu gani za ninyi wataalamu wa Serikali kukubali gharama kubwa namna hii, hivi hili jengo linafanana na Sh560 bilioni? 

“Halafu mlikuwa na haraka gani kuidhinisha kuanza awamu ya pili ya ujenzi kabla ya kumaliza awamu ya kwanza?” alihoji Rais Magufuli.

Alimuagiza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa kuunda timu ya wataalamu watakaofanya tathmini ya utekelezaji wa mradi huo ikiwa ni pamoja na kuzungumza na mkandarasi anayejenga uwanja huo na mhandisi mshauri ambao wamekubali kupunguza gharama za ujenzi wa mradi huo.

Habari kuu Katika Magazeti ya Leo Alhamisi ya February 9



 

Gallery

Popular Posts

About Us