KINGAZI BLOG: 03/10/17

HABARI KARIBU YAKO ZAIDI.

Breaking News
Loading...

Friday 10 March 2017

Shilole afunguka kuhusu Barnaba Boy

Jana malkia wa muziki Bongo, Shilole ameachia wimbo wake mpya uitwao Hatutoi Kiki. Kama zilivyo ngoma zake zilizopita, ngoma hii pia imeandikwa na Barnaba Classic.

Kwenye interview na kipindi cha Supermega Cha Kings Fm kinachoongozwa na Prince Ramalove, mrembo huyo ameweka wazi sababu za kupenda kumtumia Barnaba kwenye utunzi wa ngoma zake.

“Barnaba ananijulia sana katika uimbaji wangu, yaani akiandika ngoma,anauvaa uhusika wangu,” amesema Shilole.

Shilole amedai kuwa hiyo ndiyo sababu kubwa ya yeye kupenda kuandikiwa ngoma na mkali huyo wa High Table Sound.

Lema atarajia kufunguka ya moyoni leo

MBUNGE wa Arusha Mjini, Godbless Lema leo anatarajiwa kuhutubia wananchi wa jimbo lake katika uwanja wa Shule ya Msingi Ngarenaro baada ya kuachiwa kwa dhamana na Mahakama Kuu Kanda ya Arusha.

Hatua hiyo imeelezwa kuwa ni mtego kwake, kwani inaweza kumjenga kisiasa ama kumharibia kutokana na kile atakachotamka katika mkutano huo wa hadhara.

Lema aliyekaa gerezani kwa zaidi ya miezi minne, aliachiwa kwa dhamana Machi 3 mwaka huu na Jaji Fatuma Maghimbi na wadhamini wawili, waliosaini hati ya dhamana ya thamani ya Sh milioni moja kila mmoja.

Gari la matangazo lilikuwa likipita kila kona ya Jiji la Arusha na kutangaza kuwepo kwa mkutano huo na kuhamasisha wananchi wa Jiji la Arusha, kujitokeza kwa wingi kuhudhuria mkutano huo bila ya kukosa, kwani mbunge huyo ana ujumbe mzito kwa ajili yao.

Hata hivyo, si Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Kaskazini, Amani Gulugwa wala Lema mwenyewe aliyekuwa tayari kueleza ajenda ya mkutano huo, kwani simu zao za kiganjani zilikuwa zikiita bila ya kupokewa.

Hata hivyo, mmoja wa madiwani wa Chadema waliotakiwa kutokosa katika mkutano huo, ambaye aliomba kuhifadhiwa jina lake, alisema kuwa mkutano huo unatarajiwa kuanza saa 9 mchana katika shule hiyo ya Ngarenaro.

Diwani huyo alisema lengo la mkutano huo wa hadhara wa Lema ni kutaka kuwashukuru wale wote walioshiriki kwa namna moja ama nyingine kufika gerezani, kumfariji na kumwombea kwa siku zote akiwa mahabusu katika Gereza la Kisongo, nje kidogo ya Jiji la Arusha.

Alisema pili ni kutaka kujua kero walizonazo wananchi wa jimbo la Arusha Mjini maana kwa muda aliokaa gerezani ni muda ambao huenda kero zimekuwa nyingi ili aweze kuzifanyia kazi mbali ya yeye alizonazo ambazo anataka kuwaeleza wananchi namna ambavyo ataanza kuvifanyia kazi.

“Hakuna kipya zaidi ya hicho na huenda mkutano huo utakuwa wa amani kubwa sana na wananchi wanahamu ya kumwona mbunge wao waliomkosa kumwona zaidi ya miezi minne,’’ alisema diwani huyo.

Akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu jana, Kamanda wa Polisi Mkoani Arusha, Charles Mkumbo alisema kuwa taarifa ya kufanyika kwa mkutano hupelekwa na viongozi wa vyama vya siasa kwa wakuu wa polisi wa wilaya (OCD) na ofisi hiyo ndio wenye jukumu la kuweka ulinzi katika mkutano huo.

Mkumbo alisema huenda taarifa za kuwepo kwa mkutano huo zimeshawasilishwa kwa kiongozi huyo wa wilaya na yeye ndiye mwenye mamlaka ya kuweka ulinzi katika mkutano ili kila kitu kiwe salama mwanzo wa mkutano na mwisho wa mkutano.

Alisema mara nyingi viongozi wa vyama vya siasa katika Jiji la Arusha wanapotaka kufanya mikutano ya hadhara huwasiliana na OCD wa Arusha Mjini na viongozi hao wanajuwa taratibu.

Habari kuu Katika Magazeti ya Leo Ijumaa ya March 10




Vipimo vya Faru John Kugharimu ,Mil. 700/- Chuo Kikuu Pretoria..!!!


VINASABA vya faru John vinatarajiwa kupelekwa nchini Afrika Kusini kwa vipimo vya vinasaba (DNA ) muda wowote kuanzia wiki hii baada kupatikana kwa mfadhili wa kulipia gharama za vipimo hivyo, 

Faru John alizua gumzo nchini mwishoni mwa mwaka jana baada ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, kufanya ziara katika Hifadhi ya Bonde la Ngorongoro (NCAA) na kuwatuhumu maofisa wa shirika hilo na wale wa Idara ya Wanyamapori kwa ‘kumuuza’ faru John kwa kampuni ya Grumeti kwa takriban shilingi milioni 200.

Kutokana na tuhuma hizo maofisa zaidi ya watano kutoka Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, Idara ya Wanyapori na Tawiri walitiwa mbaroni kwa mahojiano na vyombo vya usalama. Hata hivyo, baada ya muda maofisa hao waliachiwa huru.

Kampuni hiyo ya Grumeti ambayo imewekeza katika shughuli za biashara ya hoteli, utalii na uhifadhi inamiliki hifadhi ndogo (sanctuary) ya Faru Weusi pembezoni mwa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.

Aidha katika mfululizo wa matukio kuhusu sakata la faru huyo baadaye ilibainika alifariki dunia Agosti mwaka jana na waziri mkuu aliunda kamati maalumu kuchunguza kifo chake na pia kupimwa DNA.

Taarifa zilizofika  kutoka ndani ya Wizara ya Maliasili na Utalii zimeeleza kuwa tayari nyaraka zote muhimu kuhusu kupelekwa kwa vipimo hivyo nchini humo zimekamilika.

Habari zaidi zinaeleza kuwa pamoja na kukabidhi  nyaraka, maofisa wa Wizara ya Maliasili na Utalii watakabidhi pia sampuli za vinasaba hivyo kwa ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali  ili visafirishwe kwenda Afrika Kusini.

Awali ilidaiwa kuwa kulikuwa na hali ya utata kuhusu nani hasa atalipa gharama za vipimo hivyo vya DNA baada ya Wizara ya Maliasili na Utalii kushindwa kupata fedha za kugharimia vipimo hivyo.

“Taarifa ni kwamba kuna mfadhili amepatikana (hakutaja jina) na kulipia gharama za vipimo vya DNA nchini Afrika Kusini katika maabara ya kupima vinasaba ambayo iko kitivo cha wanyama katika Chuo Kikuu cha Pretoria,” kilieleza chanzo chetu ndani ya Wizara hiyo.

Chanzo hicho kiliongeza kuwa gharama za vipimo hivyo ni katika ya dola za Marekani 300,000 hadi 500,000 ambazo ni zinaweza kufikia kati ya shilingi za Tanzania milioni 700 hadi bilioni moja.

“Kwa kweli gharama za kufanya vipimo vya DNA ziko juu sana na serikali haikuwa na fedha zilizotengwa kwa kazi hiyo, amepatikana mfadhili ambaye atalipia gharama hizo hivyo muda wowote kuanzia sasa vipimo vitapelekwa Afrika Kusini baada ya kukamilika kwa nyaraka zote muhimu,” alieleza mmoja wa maofisa wa wizara hiyo aliyeomba asitajwe jina gazetini kwa kuwa si msemaji wa suala hilo.

Majibu ya vipimo hivyo ndiyo yanayotarajiwa kutengua kitendawili cha iwapo sampuli za vinasaba zilizochukuliwa kutoka katika mabaki ya mnyama huyo zinaoana na zile zilizoko kwenye pembe yake na kujua iwapo faru huyo alikufa kama watendaji wa Idara ya Wanyapori wanavyodai au la.

Juhudi za kumpata msemaji wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dorina Makaya hazikuweza kufanikiwa kutokana na simu yake kutokuwa hewani kwa muda mrefu lakini Afisa Mawasiliano wa Wizara hiyo, Hamza Temba, alisema kwa kifupi kuwa suala hilo liko chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu na pia Mkemia Mkuu wa Serikali.

 “Sidhani kama jambo hilo liko chini ya wizara kwa kifupi ninavyofahamu suala hilo liko chini ya ofisi ya waziri mkuu na pia mkemia mkuu wa serikali,” alisema ofisa huyo.

Maabara ya Chuo Kikuu cha Pretoria nchini Afrika Kusini ( Veterinary Genetics Laboratory – VGL))  kwa mujibu wa mtandao wa researhmatters.up.ac.za ilianzishwa mwaka 2009 baada ya kuwapo kwa wimbi kubwa la ujangili dhidi ya wanyama hao nchini humo.

Kwa mujibu wa mtandao huo wataalamu wa chuo hicho kitivo cha utafiti na tiba ya wanyama wakiongozwa  na Dk. Cindy Harper walifikia uamuzi wa kuanzisha maabara hiyo kwa lengo la kukusanya sampuli za vinasaba kutoka kwa wanyama hao na kuhifadhi katika kanzidata (database) ya maabara ili zitumike kama sehemu ya ushahidi mahakamani katika kesi za ujangili wa faru.

Ugunduzi na uamuzi wa wataalamu hao ulitokana na kesi nyingi dhidi ya majangili kukwama na wengi kuachiwa huru baada ya kukosekana kwa ushahidi dhidi yao.

Kwa mujibu wa mtandao huo wataalamu hao wa chuo hicho hutumia sampuli za vinasaba na kuoanisha na alama za vidole vya majangili kisha kuwapa waendesha mashitaka ili kujenga ushahidi thabiti wa kuwatia hatiani washitakiwa.

Takwimu zinaonyesha kuwa dunia ina faru wasiozidi 29,000 kati ya faru 500,000 waliokuwepo mwanzoni mwa karne ya 20 na Afrika Kusini ndiyo nchi inayoongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya wanyama hao kwa sasa.

Kutokana na ujangili wa muda mrefu dhidi ya faru na mahitaji ya pembe zake katika nchi za kiarabu na zile za Asia ya Kusini ambazo wakati mwingine hutumika kama dawa za kiasili kumesababisha dunia kubakiza karibu asilimia moja tu ya faru. 

Nchini Afrika Kusini pekee kati ya mwaka 2010-2015 zaidi ya faru 500 waliuawa na majangili na mwaka 2013 ulivunja rekodi kwa faru 1,008 kuuawa na majangili.

Kwa upande wake Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe, alishindwa kulitolea ufafanuzi suala hilo kwa maelezo kuwa alikuwa katika kikao cha wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Ardhi, Mazingira na Maliasili.

 

Gallery

Popular Posts

About Us