KINGAZI BLOG: 12/08/16

HABARI KARIBU YAKO ZAIDI.

Breaking News
Loading...

Thursday 8 December 2016

BASI LA NEW FORCE KUTOKA TUNDUMA KWENDA DAR LAGONGANA USO KWA USO NA LORI

BREAKING NEWS!

TAARIFA ZILIZONIFIKIA NI HIZI .

NEW FORCE YA KUTOKA TUNDUMA KQENDA DAR IMEGONGANA USO KWA USO NA LORI MAENEO YA IGULUSI.

KWAHIYO WENYE NDUGU WALIOKUWA WAKISAFIRI LEO KUTOKA TUNDUMA AU MBEYA KWA NEW FORCE, FANYENI MAWASILIANO NA NDUGU ZENU HAO KUWEZA KUJUA USALAMA WAO

SASA HAIJAJULIKANA KAMA KUNA KIFO KILICHO RIPOTIWA ILA MAJERUHI WAPO .

BASI LA NEW FORCE KUTOKA TUNDUMA KWENDA DAR LAGONGANA USO KWA USO NA LORI

BREAKING NEWS!

TAARIFA ZILIZONIFIKIA NI HIZI .

NEW FORCE YA KUTOKA TUNDUMA KQENDA DAR IMEGONGANA USO KWA USO NA LORI MAENEO YA IGULUSI.

KWAHIYO WENYE NDUGU WALIOKUWA WAKISAFIRI LEO KUTOKA TUNDUMA AU MBEYA KWA NEW FORCE, FANYENI MAWASILIANO NA NDUGU ZENU HAO KUWEZA KUJUA USALAMA WAO

SASA HAIJAJULIKANA KAMA KUNA KIFO KILICHO RIPOTIWA ILA MAJERUHI WAPO .

Taarifa kamili Kuhusu Habari Zilizoenea Kuwa Mgogoro wa Mpaka Kati ya Tanzania na Malawi Umerudi Tena

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushrikiano wa Afrika Mashariki inapenda kufafanua na kuweka sawa taarifa zilizoandikwa kwenye baadhi ya Magazeti ya tarehe 07 Desemba, 2016 kuwa mgogoro wa mpaka kati ya Tanzania na Malawi kwenye Ziwa Nyasa unakaribia kuiva na kwamba Mgogoro huo unatarajiwa kumalizwa na washauri wa kimataifa.

Taarifa hiyo haikuwa sahihi. Ukweli ni kuwa, mgogoro wa mpaka kati ya Tanzania na Malawi kwa sasa upo chini ya Jopo la Viongozi Wastaafu wa Afrika wanaotokea kwenye nchi za Ukanda wa Jumuiya ya Maendeleo  Kusini mwa Afrika (SADC). Jopo hilo linaongozwa na Mhe. Joachim Chissano, Rais Mstaafu wa Msumbiji akisaidiwa na Mhe. Festus Mogae, Rais Mstaafu wa Botswana na Mhe. Thabo Mbeki, Rais Mstaafu wa Afrika Kusini.

Aidha, Jopo hili ambalo liliundwa na Umoja wa Afrika kupitia Jukwaa la Viongozi Wastaafu wa Afrika (Forum for Former African Heads of State and Government) kwa ajili ya kusuluhisha mgogoro huu, linaendelea na kazi hiyo kwa kupitia taarifa mbalimbali na maandiko yaliyowasilishwa kwao na Tanzania na Malawi. Vile vile, Jopo lilikwisha zikutanisha pande zote mbili katika mashauriano ya awali yaliyofanyika nchini Msumbiji

Wizara inapenda kuujulisha umma kuwa licha ya kuwepo kwa mgogoro wa mpaka wa Tanzania na Malawi katika Ziwa Nyasa, mahusiano ya nchi hizi mbili yamezidi kuimarika siku hadi siku katika Nyanja zote za kiuchumi, kisiasa na kijamii. Hata wananchi wa pande zote mbili za Ziwa wameendelea kuishi kwa amani na ushirikiano wa karibu.

Aidha, katika kuimarisha uhusiano huu, Tanzania na Malawi zinatarajia kuwa na mkutano wa Tume ya Pamoja ya Ushirikiano mapema mwakani. Mkutano huu utawaleta watalaam wa nchi hizi mbili kutoka Sekta mbalimbali kwa lengo la kujadili changamoto za ushirikiano katika sekta hizo, kubaini maeneo mapya ya ushirikiano pamoja na kuweka mikakati ya kutekeleza miradi ya pamoja itakayokubaliwa baina ya pande hizi mbili.

Pamoja na mambo mengine, Mkutano huo unatarajiwa kujadili masuala ya ushirikiano katika sekta za biashara na uwekezaji, usafirishaji, fedha, nishati, utalii, ulinzi na usalama uhamiaji, uvuvi na ardhi.

Hivyo, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki inawaomba Waandishi wa Habari, Wadau mbalimbali na wananchi kwa ujumla inapohitajika kupata taarifa sahihi za suala hili kwenda kwenye Mamlaka husika na kuziandika kwa usahihi kwa ustawi wa nchi.

Imetolewa na:

Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki

Dar es Salaam, 07 Desemba, 2016.

Maiti Sita zaokotwa mtoni ndani ya viroba

Sehemu ya Mto Ruvu

MAITI sita ambazo hazijatambulika zimekutwa zikielea katika Mto Ruvu eneo la Bagamoyo, Mkoa wa Pwani zikiwa zimehifadhiwa kwenye mifuko ya sandarusi maarufu viroba vya uzito wa kilogramu 200, huku zikiwa zimeharibika vibaya.

Akizungumza na gazeti hili kwa simu jana, Diwani wa Kata ya Makurunge, Paul Kabile alisema maiti hizo ambazo ni za jinsia ya kiume ziligunduliwa na wavuvi.

Kabile alisema maiti tano ziligunduliwa Desemba 6, majira ya alfajiri kwenye Kitongoji cha Kitopeni wilayani Bagamoyo, ambako wavuvi hao waligundua miili hiyo wakati wakiendelea na shughuli zao za uvuvi kwenye mto huo.

“Maiti hizo kila moja ilikuwa imehifadhiwa kwenye kiroba huku zikiwa zimewekewa mawe na mifuko hiyo ikiwa imeshonwa juu kama vile yamehifadhiwa mahindi au mchele,” alieleza Kabile na kuongeza kuwa wavuvi hao baada ya kuziona maiti hizo walizizika kutokana na kuharibika sana na kushindwa kuzipeleka hospitali kuzihifadhi.

“Wavuvi hao walizizika maiti hizo huku kukiwa hakuna taarifa yoyote juu ya kuwa zimetokea wapi na ni watu gani waliofanya tukio hilo,” alisema Kabile na kubainisha kuwa maiti nyingine moja iligundulika jana.

Mwandishi wa Habari wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani, Hassan Mtengevu alithibitisha kutokea tukio hilo, na kueleza kuwa wanafanya uchunguzi kwa kushirikiana na daktari ili kufahamu watu hao walikufa kwenye mazingira gani

 

Gallery

Popular Posts

About Us