KINGAZI BLOG: 02/18/17

HABARI KARIBU YAKO ZAIDI.

Breaking News
Loading...

Saturday 18 February 2017

Hivi ndivyo Mbowe alivyowatoroka polisi huku wakiendelea kumsaka.



Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es salaam, limemtaka Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kujisalimisha Polisi mara moja kwa ajili ya Mahojiano yanayohusu vita vya dawa za kulevya baada ya juhudi za kumsaka katika makazi yake kushindikana huku simu yake ya mkononi ikiwa imezimwa 

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Simon Sirro amesema Bw. Mbowe aliahidi kwenda mwenyewe juzi tarehe 15, lakini hakwenda lakini jeshi la hilo lilimtafuta usiku na mchana katika makazi yake na kumpigia simu lakini simu yake ilizimwa 

Aidha jeshi hilo limesema watuhumiwa watatu Agnes Masogange, Rashid Idd au Chid Mapenzi na Wallis Latif Nasher ambaye ni muuza magari katika eneo la mikocheni watapandishwa kizimbani Jumatatu kwa kosa la kukutwa na dawa za kulevya lakini pia walibainika wanaotumia dawa hizo baada ya kupelekwa kwa Mkemia Mkuu 

Katika kupambana na Askari feki, jeshi limemtia mbaroni aliyekuwa askari Magereza wa cheo cha Koplo Peter Elias Msigwa aliyekuwa mtumishi katika gereza la keko, ambaye alifukuzwa kazi Desemba mwaka jana, lakini alikamatwa jana akiwa na mavazi ya kiaskari tena akiwa amejipandisha cheo kutoka koplo hadi Sajenti wa Polisi 

Jeshi hilo pia limesema limewatia mbaroni watu 65 kwa kosa la kukutwa na dawa za kulevya pamoja na watuhumiwa 73 wa wizi na ujambazi wa kutumia silaha, mitambo mitano ya Gongo, lita 270 pamoja na Puli 250 za bangi. 

Hali ya Afya ya Manji Yazidi Kudorora,Akimbizwa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete..!!


BAADA ya kupata dhamana ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu juzi, mfanyabiashara maarufu nchini, Yusuf Manji, amelazwa tena kwenye Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) iliyoko katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Kwa mujibu wa taarifa zilizothibitishwa na Ofisa Uhusiano wa Taasisi hiyo jana, Anna Nkinda, Manji alifikishwa hospitalini hapo juzi jioni ikiwa ni muda mfupi baada ya kupata dhamana dhidi ya kesi ya kutumia dawa za kulevya aina ya heroin inayomkabili.

“Ni kweli Manji yupo hapa, aliletwa jana jioni (juzi) kwa matibabu ambapo hadi leo (jana) ninavyoongea na wewe bado yupo hapa amelazwa anaendelea na matibabu kama kawaida,” alisema Anna.

Hii ni mara ya pili kwa Manji ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Mbagala Kuu, kulazwa kwenye taasisi hiyo.

Mara ya kwanza ilikuwa ni Februari 12, mwaka huu alipolazwa hapo akitokea katika Kituo Kikuu cha Polisi Dar es Salaam, alipokuwa ameshikiliwa tangu Februari tisa akifanyiwa mahojiano.

Mfanyabiashara huyo alifika mwenyewe kwenye kituo hicho cha polisi kutokana na wito uliotolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, aliyetaja majina 65 ya watu aliodai wanajihusisha na biashara ya dawa za kulevya.

Mbali na Manji, baadhi ya watu wengine waliotajwa na Makonda na kutakiwa kufika kituoni hapo ni Mchungaji wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima, Mbunge wa zamani wa Kinondoni, Idd Azzan ambao tayari wamehojiwa polisi huku Mbunge wa Hai, Freeman Mbowe, akiwa bado hajahojiwa licha ya kutajwa kwenye orodha hiyo.

Juzi Alhamisi, Manji alifikishwa kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, ambapo shauri lake lilisikilizwa na Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Cyprian Mkeha.

Karani wa mahakama hiyo, Sarah Mulokozi, alimsomea mshtakiwa shtaka lake ambapo alidai kuwa kati ya Februari 6 na 9, mwaka huu eneo la Upanga Sea View jijini Dar es Salaam, Manji alitumia dawa za kulevya aina ya heroin.

Mtuhumiwa huyo alikana shtaka hilo na Mkurugenzi wa Mashtaka Msaidizi (ADPP), Osward Tibabyekomya, alidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika na kuiomba Mahakama kupanga tarehe nyingine ya kutajwa.

Upande wa mawakili wa utetezi ambao ni Alex Mgongolwa na Hudson Ndusyepo, waliiomba Mahakama kumpa mshtakiwa dhamana  kwa sababu ya mashtaka yanayomkabili yanadhaminika.

Hakimu Mkeha alisema mshtakiwa atakuwa nje kwa dhamana kwa kutakiwa kusaini hati ya dhamana ya Sh milioni 10 pamoja na mdhamini mmoja wa kuaminika ambapo Katibu Mkuu wa Klabu ya Yanga, Charles Mkwasa, alimdhamini Manji, ambaye aliachiwa kwa dhamana hadi Machi 16.

Mara baada ya kupata dhamana, Manji aliondoka mahakamani hapo saa 9:40 akiwa kwenye gari yenye namba T670 BBX aina ya Hummer.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumamosi ya February 18



 

Gallery

Popular Posts

About Us