KINGAZI BLOG: 02/06/17

HABARI KARIBU YAKO ZAIDI.

Breaking News
Loading...

Monday 6 February 2017

Rais Magufuli atoa kauli hii kuhusu sakata la madawa ya kulevya na list ya Makonda.

Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli amempongeza Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, IGP Ernest Mangu kwa kuwasimamisha kazi Polisi 12 waliotuhumiwa kujihusisha na biashara ya madawa ya kulevya.

Pongezi hizo zimetolewa na Rais huyo mapema Jumatatu hii, Ikulu jijini Dar es Salaam, wakati wa kumuapisha Mkuu mpya wa majeshi, Luteni Jenerali Venance S. Mabeyo.

“Naomba nitoe pongezi kwa mkuu wa Polisi kwa kuwasimamisha kazi wale Polisi. Nikupongeze mkuu umefanya vizuri na umetoa heshima kwa nchi yetu, tembea kifua mbele, katika vita hii ya madawa ya kulevya hakuna cha mtu aliye maarufu atakayeachwa, hakuna mwanasiasa, hakuna askari, hakuna waziri, au watoto wa fulani ambaye akijihusisha aachwe,” amesema Rais Magufuli.

“Hata angekuwa mke wangu Janeth akijihusisha we shika tu, kwa sababu madhara ya madawa ya kulevya katika taifa letu imefikia mahali pabaya, haiwezekani watu wawe wanauza kama Njugu, sisi sote hapa tuliopo tunafahamu hii vita ni ya kila mtu,” ameongeza.


Diamond, Alikiba na Navy Kenzo Washinda Tuzo za Hipipo za Uganda..!!!


Diamond Platnumz, Alikiba na Navy Kenzo wameshinda tuzo za Hipipo 2017 zilizotolewa Jumamosi hii nchini Uganda.

Kwenye tuzo hizo, Navy Kenzo walitumbuiza.

Hizi ndizo tuzo walizoshinda wasanii hao:

East Africa Best Video – Salome by Diamond Platnumz ft Ray Vanny

East Africa Best New Act – Navy Kenzo

East Africa Super Hit – Unconditional Bae by Sauti Sol & Alikiba

Song of the Year Kenya – Unconditionally Bae by Sauti Sol & Alikiba

Song of the Year Tanzania – Aje by Alikiba

Quinquennial Africa Music Vanguard Award – Diamond Platnumz

Hawa ndio mabingwa wa Afcon 2017

Timu ya Taifa ya Soka ya Cameroon imetawazwa kuwa mabingwa wa Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) mwaka 2017 baada ya kuilaza timu ya Taifa ya Misri kwa mabao 2-1,  yaliyofungwa na Nicolas N'Koulou na Vincent Aboubakar.

Cameroon imepata ubingwa huo katika fainali za mashindano hayo yaliyofanyika nchini Gabon, ukiwa ni ubingwa kwa mara ya tano na ni mara ya kwanza tangu mwaka 2002.

Katika mtanange huo uliovuta hisia za mashabiki na wapenzi wengi wa soka,  Misri ndiyo ilianza kutikisa nyavu za Cameroon baada ya Mohamed Elneny kufunga goli kwa shuti kali katika dakika ya 21.

Hata hivyo, katika dakika ya 58, N'Koulou aliamsha matumaini ya Cameroon kutwaa ubingwa huo, baada ya kuisawazishia timu yake kwa kichwa, kabla ya Aboubakar kuihakikishia ubingwa kwa kupachika wavuni bao la pili katika dakika ya 88 na hivyo kuzamisha kabisa jahazi la Misri.

Ubingwa wa mwaka huu kwa Cameroon unaandika rekodi mpya na ya kwanza baada ya timu hizo kukutana katika hatua ya fainali mwaka 1986 na 2008, ambazo zote Misri iliibuka mbabe.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatatu ya February 6



 

Gallery

Popular Posts

About Us