KINGAZI BLOG: 01/31/17

HABARI KARIBU YAKO ZAIDI.

Breaking News
Loading...

Tuesday 31 January 2017

BREAKING NEWS: UPDATED HAYA HAPA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE MWAKA 2016. TUMEKUWEKEA HAPA LINK AMBAZO ZINAFUNGUKA HARAKA .

Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) limetangaza matokeo ya kidato cha nne mwaka 2016 ambapo umefaulu wa jumla umeongezeka kwa 2.56% kutoka 67.53% mwaka 2015 hadi 70.09% mwaka 2016.

Katibu Mtendaji wa barza hilo, Dkt Charles Msonde amesema kati ya wanafunzi 408,372 waliofanya mtihani, jumla ya wanafunzi 277,283 wamefaulu, wakiwemo wasichana 135,859 sawa na asilimia 67.06 na wavulana 141,424 sawa na asilimia 73.26.

Kwa upande wa watahiniwa wa shule, Dkt Msonde amesema kuwa 244,762 sawa na asilimia 70.35 ya waliofanya matihani wamefaulu ikilinganishwa na wanafunzi 240,996 sawa na asilimia 67.91 waliofaulu mwaka 2015.

Kwa upande wa ubora wa ufaulu, amesema watahiniwa wa shule wenye ufaulu mzuri wa Daraja la kwanza hadi la tatu ni 96,018 sawa na asilimia 27.60 


>>>BONYEZA HAPA KUONA MATOKEO

 YAKO YOTE <<<..

>>>FOR QT RESULT BONYEZA HAPA..



<<<<


 Ukihitaji msaada wa kuangaliziwa matokeo yako

 kwa haraka zaidi ndani ya dakika 2 tu tuma 

meseji kwenda namba hizi 

0716528779 au 0755542721

pia whatsapp kwa namba hii 0716528779

gharama ni sh 1000/= tu

tunafanya kazi yetu kwa Uaminifu zaidi na

 umakini.


KUMBUKA!!!!! UKISHAONA JINA LAKO MWAMBIE NA 

MWENZAKO PIA AINGIE KWENYE LINK HIZO AU 

ATEMBELEE BLOG HII

Mke wa mtu sumu!! Jamaa auawa kikatili baada ya kufumaniwa akimla uroda mke wa mtu


WATU watatu wilayani Igunga mkoani Tabora wamekufa akiwemo mwanaume aliyeuawa na kundi la wananchi baada ya kufumaniwa akifanya mapenzi na mke wa mtu. Watoto wawili wa familia moja wamepoteza maisha kwa kuzama kwenye shimo la maji.

Akizungumza jana mjini Tabora, Kamanda wa Polisi wa Mkoa, Kamishna Msaidizi Hamisi Selemani amesema katika tukio la Januari 28, mwaka huu katika Mtaa wa Stoo, Kata ya Igunga Mjini, mkazi wa Mtaa wa Masanga, Khalid Kassim (50) aliuawa na kundi la wananchi zaidi ya 100 ikidaiwa alifumaniwa akifanya mapenzi na mke wa mtu.

Kamanda Selemani amefafanua kuwa Kassim alifumaniwa na mwenye mke, Muungano Isaack (44) mkazi wa Mtaa wa Stoo.

Amesema baada ya kumfumania, Isaack alipiga kelele kuomba msaada, ndipo wananchi walitoka kwa wingi na kumshambulia kwa kipigo Kassim.

Amebainisha kuwa polisi walipata taarifa na kufika katika mtaa huo na kukuta wananchi wakiwa wamekimbia, hivyo askari walimchukua mtuhumiwa na kumpeleka Hospitali ya Wilaya ya Igunga ambako aliaga dunia wakati akipatiwa matibabu.

Kamanda Selemani amesema katika tukio la pili lilitokea siku hiyo, katika Kijiji cha Mwazizi Kata ya Bukoko, watoto wawili wa familia moja, Gumba Ngasa (2) na Kija Ngasa (1) wote wa kike, walizama maji na kufariki dunia wakati wakivuka maji.

Kamanda amesema watu wawili, Muungano Isaack na Maria Joseph wanashikiliwa na Polisi huku wengine walioshiriki mauaji ya Kassim wanaendelea kutafutwa na jeshi hilo.

Ametoa mwito kwa wazazi kuwa makini na kipindi cha masika kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha.

Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya ya Igunga, Dk Godfrey Mgongo amesema uchunguzi wa awali unaonesha kifo cha Kassim kilisababishwa na kuvuja damu nyingi kichwani kutokana na majeraha aliyokuwa nayo.

Aidha, Dk Mgongo alibainisha kuwa vifo vya watoto wawili Gumba na Kija vilisababishwa na maji mengi waliyomeza baada ya kuzama.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumanne ya January 31.



 

Gallery

Popular Posts

About Us