KINGAZI BLOG: 03/01/17

HABARI KARIBU YAKO ZAIDI.

Breaking News
Loading...

Wednesday 1 March 2017

10 Vyakula vya Kuongeza Nguvu za Kiume


Mara nyingi ndoa huvunjika kutokana na tatizo la upunguvu wa nguvu za kiume. Dalili kuu za tatizo hili ni mwanamume kutokuwa na uwezo wa kutoa mbegu bora zilizo na uwezo wa kutungisha mimba. Pia, kutosimama kwa uume wakati wa kujamiiiana ni dalili nyngine ya tatizo hili.

Tatizo hili limewaathiri watu wengi kati mabara totafauti ulimwengu mzima. Takwimu zilizopo zinadhihirisha kwamba asilimia sitini ya wanandoa katika nchi tofauti tofauti wanakambiliwa na upunguvu wa nguvu za kiume.

Pia karibu ndoa 2 kati ya 5 zilizo na umri wa miaka miwili na kuendelea zinakambiliana na tatizo la kutoweza kumudu vizuri tendo la ndoa.

Jambo la kushangaza ni kwamba, ndoa nyingi amabazo zimevunjika kutokana na tatizo hili kwa sababu wahusika hawakuwajibika ipaswavyo ili kusuluisha tatizo hili. Badala ya wanandoa kufichuliana ukweli kuhusu tatizo hili, mara nyingi wanaume huficha kabisa na kuanza kumlaumu mwanamke kwa kukosa mtoto.

Wanaume wengi wameshauriwa kuwa kutumia madawa ya kuchochea nguvu wakati wa tendo la ndoa kunaweza kuwa suluhu. Nataka uelewe ya kwamba madawa haya yana madhara si haba.

Natumahi umesikia habari kuhusu wananume waliohaga kutokana na shida za moyo wakiwa vyumbani na vimanda wao.  Kwa hivyo ongopa hayo madawa na pia uelewe kuwa ukitaka tiba stahiki la tatizo la upunguvu wa nguvu za kiume lipatikane, lazima kiini chake kichunguzwe kwa makini.

Nini kinachisababisha upunguvu wa nguvu za kiume?

Tatizo la nguvu za kiume huhusishwa na kuvaa ngua za kubana sana, kuugua kwa muda murefu, miozi ya compyuta au simu, ugonjwa wa kisukari, na mengineyo. 

Pia, upunguvu wa nguvu za kiume husabibabishwa na kupiga punyeto kwa muda mrefu, matatizo ya kisaikolojia,  dawa za wadudu ambo zina viambata sumu viitwavyo ‘estrogen’, na kutumia vyakula vilivyo na kemikali kwa muda mrefu.

Vyakula vya kuongeza nguvu za kiume

watafiti wa masuala ya usihano wa kimapenzi wamebaini aina mbalimbali ya vyakula ambavyo vina uwezo wa kuongeza nguvu za kiume. Baadhi ya vyakula hivi ni:

1. Pweza na chaza

Hizi ni aina za samaki ambazo huvuliwa baharini. Kulingana na watafiti, samaki hawa huwa na madini ya zinc na chumvi kwa wingi.

Madini hayo yanajulikana kwa kusaidia uzalishaji wa vichocheo vinanvyoleta msisimko wa mwili wakati mume na mke wanajamihiana.

2. parachichi

Hili ni tunda ambalo watafiti wamebaini kwamba lina uwezo wa kuongeza nguvu za kiume. Tunda hili lina uwezo mkubwa wa kuzalisha vitamini E. Vitamini E husaidia katika uzalishaji wa homoni zinazosaidia kuongeza nguvu za  kiume.

Kulingana na watafiti tofauti, watu wanaotumia tunda hili kwa wingi huwa na msisimko mkali haswa wakati wa kufanya mapenzi. Pia, faida za tunda hili haziengemei upande wa wanaume pekee.

Katika upande wa wanawake, tunda hili husaidia kuongeza majimaji yaliyo na utelezi katika sehemu za siri za mwanamke ili kuzuia uwezekano wa kuchubuka wakati wa tendo la ndoa.

3. Karanga

Utafiti umebaini kuwa karanga ni chanzo kikuu cha kujenga protini mwilini. Karanga huwa na kiwango kikubwa cha amino asidi ambayo  husaidia mwili kuwa na mfumo wa damu unaotakikana.

Ni vizuri kuelewa kuwa mwanamume huhitaji kiwango fulani cha mfumo wa damu ili kushiriki tendo la ndoa kikamilifu. Kwa hivyo, kiungo kikuu cha karanga ambacho ni amino asidi husaidia mwili kuwa na mfumo mzuri wa damu, hivyo, husababisha kiwango cha juu cha ufanyaji mapenzi.

4. kitunguu saumu

Sifa kuu za kitunguu saumu zinazokifanya kuwa na uwezo na faida nyingi mwilini ni kuwa na viasili kadhaa ambavyo vina uwezo tofauti tofauti.

Baadhi ya viasili hivi husaidia kutanuka kwa mishipa ya damu (vasodilation kwa lugha ya kiingereza) kwa kubadilishapolysulphides zilizo ndani yake kuwa hydrogen sulphides kwenye seli nyekundu za damu.

Pia, kitunguu saumu husaidia kuthibiti kiwango cha kemikali iitwayo homocystine mwilini na hivyo kupunguza madhara ya kisukari. Kitunguu saumu kinaallicin, kiambato ambacho husaidia mwili kuwa na mzinguko mzuri wa damu hadi kwenye viungo vya uzazi.

Kuwa na damu ya kutosha katika uume husababisha hiki kiungo kusimama na hivyo kustaimili tendo la ndoa kwa muda mrefu.

5. Ndizi

Unapofikiria kufyanya vyema katika tendo la ndoa, unatakiwa kuwaza kuhusu uimara wa misuli ya mwili ambayo hutajwa kuwa ni sehemu kuu na yenye umuhimu mkubwa katika kujamihiana.

Kwa msingi huo, hulaji wa ndizi mbivu husaidia kujenga misuli mwilini na pia kumfanya manamume kuwa hodari katika tendo la ndoa.

6. Chokoleti

Chokoleti huwa na viamabato kama vile alkaloid naphenylethylamine. Hivi viambato huongeza stamina ya kufanya mapenzi. Phenylethylaminehusaidia mtu kuhisi vizuri wakati wa kufanya mapenzi.

Kwa hivyo, kama una tatizo la kutoshiriki tendo la ndoa vizuri, jaribu kula chokoleti kila siku.

7. tikiti maji

Tikiti maji ni tunda ambalo lina faida nyingi sana katima mwili. Kwanza, tunda hili ni huwa na virutubisho kama vile potasium, calcium, magnesium, carotene. Pia, tunda hili huwa na vitamini muhimu sana kwa miili yetu.

Vitamini hizi ni kama vile vitamini A, B6, na C. Kwa hivyo, tikiti maji, haswa mbegu zake huupa mwili chembechembe muhimu za kuongeza kuvu za kiume mwilini.

8. mbegu za matunda

Mchanganyiko wa mbegu mbalimbali za matunda kama ile maboga, tikiti, na matunda mengineo husaidia kupunguza asidi mwilini na kumfanya mtu awe na afya njema.

Ni vizuri kujua kuwa kuwa na afya njema husaidia mwanamume kushiriki tendo la ndoa ipaswavyo.

9. Mfinyo mwekundu

Utafiti umedhihirisha kuwa mvinyo mwekundu una wezo wa kuongeza msukumo wa damu.  Elewa kwamba kiwango cha msukumo wa damu ni muhimu ili kuhakikisha kuwa uume umesimama wakwati wa kujamiiana.

Pia, mfinyo mwekundu huuchangamsha mwili kiasi cha kumuondolea mtu uchovu kabla na baada ya kufanya mapenzi.

10. Tangawizi

Tangawizi husisimua sana mfumo wa mzunguko wa damu mwilini. Kwa hivyo, ni bayana kuwa kiungo cha mwanamume kinachoshiriki tendo la ndoa kitakuwa na damu ya kutosha na pia kusimama kwa muda mrefu. Pia, ulaji wa tangawizi husaidia kuongeza hamu ya tendo la ndoa.

Kilele cha juu zaidi cha furaha katika ndoa yoyte ile, kama inavyojulikana, ni furaha inayopatikana wakati wa kufanya mapenzi. Ni vizuri kuelewa kuwa kuishiwa na nguvu za kiume kunaweza kuhusishwa na  kuongezeka kwa umri. 

Tafiti mbalimbali zinadhihirisha kuwa wanume wa umri kuanzia miaka 61 na kuendelea hupatwa na tatizo hili zaidi kulikuko wanaume wa miaka 41 kushuka chini.

Ni muhimu kuelewa kuwa kuna visababishi vya upunguvu wa nguvu za kiume ni vyingi.

Kwa hvyo, badala ya kutapata hapa na pale ukitafuta msaada au kugobana na bibi yako kila siku, jaribu vyakula amabvyo vimejadiliwa katika makala haya na utasaidika.

Mambo 5 mazito yatakayotikisa nchi nzima mwezi huu


Mwezi wa tatu maarufu kama Machi ulioanza leo, umegubikwa na matukio matano ambayo Watanzania kutoka pande zote za nchi wanatarajiwa kuyashuhudia.

Tayari Chama cha Walimu Tanzania (CWT) kilishazungumza takriban mwezi mzima uliopita juu ya kusudio la kutangaza mgogoro na Serikali unaolenga kudai haki ya madai ya wanachama wake.

CWT imekuwa ikilalamika kwa muda sasa juu ya madai mbalimbali ya walimu, yakiwamo yanayohusiana na mishahara na malipo mengine.

Rais wa chama hicho, Gratian Mkoba anasema madai ya walimu yanafikia takriban Sh800 bilioni na awali waliitaka Serikali iwe imeyalipa ifikapo Februari 28, vinginevyo wataanza mgogoro huo leo.

Katika kukoleza chumvi kwenye kidonda, Rais wa Shirikisho la Wafanyakazi Tanzania (Tucta), Tumaini Nyamhokya alisema jana kwamba, wanaunga mkono hatua zozote zitakazochukuliwa na CWT kwa lengo la kuishinikiza Serikali kuwalipa madai yao.

“Tunawanga mkono CWT waendelee na mchakato wao kwa sababu Serikali haitaki kutoa kauli zenye kuwaletea matumaini walimu,” alisema.

Mbali ya sakata hilo, suala lingine linalokusudiwa kuutikisa mwezi huu nchini ni mfumo wa kubadili mtandao wa simu bila ya kubadili kadi (MNP).

Mfumo huo unawapa uhuru wateja wa mitandao yote ya simu nchini kuhama kutoka mtandao mmoja kwenda mwingine wakati wowote wanaoona unafaa.

Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa atazindua rasmi mfumo huo leo katika ofisi za Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Mawasiliano Tanzania (TCRA).

Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Mhandisi James Kilaba alisema lengo ni kuwapa uhuru wateja kutumia mtandao bora zaidi na kuongeza ushindani kwa kampuni ili kuboresha huduma zao.

“Uanzishwaji wa MNP ni kwa mujibu wa kanuni za mwaka 2011. Kanuni hizi zinawataka watoa huduma za simu za kiganjani kuwezesha huduma hii katika mitandao yao,” alisema Kilaba.

Mbali na mambo hayo mawili, lingine la tatu ni lile la waumini wa madhehebu ya Kikristo nchini na duniani kote kuanza mwezi wa kujinyima kukumbuka mateso ya Yesu Kristo kwa kufunga kula, maarufu kama kipindi cha Kwaresma.

Wakristo duniani kote kuanzi leo watasali katika Jumatano ya Majivu, misa ambayo ni ufunguzi rasmi wa kipindi cha Kwaresma.

Ibada ya Majivu huhusisha waumini kupaka majivu ikiwa ni ishara ya mwanzo wa kuanza mfungo wa siku 40 wa kukumbuka mateso ya Yesu Kristo.

Jambo lingine ni lile la marufuku ya viroba ambalo zuio lake linaaza leo.

Iwapo utekelezaji wake utakuwa na ufanisi utasaidia kuzuiliwa kwa pombe hizo kali zinazowekwa kwenye pakiti za plastiki, maarufu kama viroba.

Utekelezwa wa marufuku hiyo ya Serikali unaanza huku kukiwa na uwezekano wa wadau wa biashara hiyo kufungua kesi kupinga utekelezwa wa agizo hilo lililotolewa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.

Sakata hilo lilianza Februari 20 wakati Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Mazingira, January Makamba alipotangaza marufuku hiyo huku akiwataka watengenzaji wa pombe hizo watafute utaratibu ulioandaliwa na Serikali wa kutumia chupa badala ya mifuko midogo ya plastiki.

January aliwaambia waandishi wa habari jana kwamba, operesheni ya kukagua utengenezaji, uuzaji na matumizi  ya pombe ya viroba itaendeshwa na kamati za ulinzi na usalama na kamati za mazingira za ngazi zote kuanzia mkoa hadi mtaa ambazo zitawajibika kuwasilisha taarifa za operesheni hiyo Tamisemi.

“Ukikutwa unakunywa, unauza na utengeneza au kuingiza viroba utachukuliwa hatua kali zikiwamo faini na kifungo au vyote kwenda sambamba,” alisema waziri huyo.

Mwezi huu pia unaanza huku awamu ya kwanza ya taasisi za Serikali kuhamia na kuanza rasmi shughuli zake mjini Dodoma baada ya kazi ya uhamaji kumalizika jana.

Agizo la kuhamia Dodoma lilitolewa na Rais John Magufuli mwaka jana kuwa, kabla ya kumaliza miaka mitano ya awamu ya kwanza ya utawala wake, Serikali itakuwa imehamia Dodoma.

Baada ya tangazo hilo la Rais Magufuli, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa aliitikia wito huo wakati wa sherehe za maadhimisho ya kumbukumbu ya siku ya Mashujaa mjini Dodoma, akitaka nyumba yake ikamilike haraka.

Pia alitangaza kuwa awamu ya kwanza ya uhamaji itahusisha mawaziri na manaibu wao, makatibu wakuu na manaibu wao na wasaidizi wao, huku ile ya pili itaanza Julai baada ya Bunge la Bajeti. Uhamaji huo utakuwa kwa awamu sita na unatarajiwa kukamilika mwaka 2020 pale

Rais atapohamia rasmi mjini humo

UKIFUATA NJIA HIZI UTAPONA TATIZO LA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME.

Image result for nguvu za kiume
UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME
Wanaume Wengi Hapa Duniani Huamini Kuwa, Mwanaume Hasa Ni Yule Anayeweza Kufanya Tendo Hilo Kwa Muda Mrefu Na Mara Nyingi Ndio Maana Vijana Wengi Utawasikia Wakijisifu Kuwa, Mpenzi Wake Hakulala Usiku Mzima Kutokana Na Dozi Ya Maana Aliyompa Na Ukimuuliza Mtu Wa Namna Hii Atakwambia Kuwa Alikwenda Mizunguko Sita Usiku Mzima.
Hata Hivyo, Ukweli Ni Kuwa, Watu Wengi Hufikia Hatua Ya Kusema Uongo Ili Waonekana Kuwa Ni Wanaume Hasa Mbele Ya Wenzao Huku Wengine Wakigubikwa Na Nadharia Kuwa Ukubwa Wa Uume Unaashiria Jinsi Gani Walivyo Wanaume Kitu Ambacho Si Kweli.
Ni Mtazamo Huu Ndio Unaowafanya Wanaume Wakitaniwa Au Kuambiwa Kuwa Wako Kama Wanawake Wanaweza Waue Mtu. Tunaamini Kuwa Uanamke Ni Udhaifu Na Uanaume Ni Ushujaa Fulani Hivi.
Wakati Hali Ikiwa Hivyo, Hivi Sasa Wanaume Wengi Wamekuwa Wakihangaika Na Jambo Moja Kubwa, Kutafuta Dawa Za Kuongeza Nguvu Za Kiume Ili Kujiongezea Heshima Faragha!
Ukitaka Kuthibitisha Hili Jaribu Kuangalia Karibu Katika Kila Gazeti Utakalo Soma, Ni Nadra Sana Kukosa Tangazo Dogo La Biashara Lililotolewa Na Mganga Wa Kienyeji Anayejigamba Kuwa Anazo Dawa Za Kuongeza Nguvu Za Kiume, Na Matangazo Hayo Hayaishii Magazetini Tu, Bali Hata Redioni Pia Yapo.
Mbaya Zaidi Dawa Zinazoongelewa Hupewa Majina Mengi Ya `Kusisimua` Kama Kombora, Simba Na Nyati Siushasikia Mziki Wa Nyati Akikasirika Sasa Jenga Picha Nuvu Ya Hiyo Dawa, Hata Hivyo, Dawa Nyingi Ni Uzushi Tu Na Hupewa Majina Hayo Ili Kuwavuta Wateja Na Kuwashawishi Kuzijaribu, Enewei Ndivyo Biashara Zilivyo.
Wingi Huu Wa Matangazo Umeanza Kuonekana Katika Miaka Ya Hivi Karibuni, Na Kadiri Siku Zinavyozidi Ndivyo Idadi Ya Waganga Wanaojigamba Kuwa Na Dawa Hizo Inavyozidi Kushamiri, Kuna Waganga Wenye Dawa Za Kiswahili, Kiarabu Na Za Kichina Ndio Usiseme!
Binafsi Utitili Wa Matangazo Haya Umenifanya Niamini Kuwa, Kuna Tatizo Kubwa La Wanaume Kupungukiwa Nguvu Hizo, Na Ingawa Hakuna Utafiti Wa Kitaalamu Uliofanywa Rasmi, Lakini Inaonyesha Kuwa Tatizo Hilo Kwa Sasa Ni Kubwa Sana Na Si Tanzania Tu, Bali Ni Dunia Nzima.
Kutokana Na Hali Hiyo Ndipo Waganga Wa Kienyeji Pamoja Na Makampuni Mengi Makubwa Duniani Hujaribu Kuelekeza Nguvu Zao Katika Kufanya Utafiti Wa Kutengeneza Dawa Za Kusaidia Watu Wenye Tatizo Hilo, Na Bahati Nzuri Kwa Makampuni Na Waganga Hao Ni Kwamba Inaonekana Kama Biashara Inawaendea Vizuri.
Kwa Mujibu Wa Utafiti Wa Taasisi Moja Ya Biashara Ya Dawa Za Aina Hiyo Nchini Uingereza, Imebainika Kuwa Asilimia 46 Ya Wanaume Nchini Humo Hutumia Dawa Hizo, Hata Hivyo Wengi Wao Huzitumia Bila Ya Kupata Ushauri Wa Daktari Na Maduka Mengi Ya Dawa Yametozwa Faini Kwa Kuwauzia Dawa Hizo Bila Ya Kuwa Na Vyeti Vya Daktari.
Kupungua Kwa Nguvu Miongoni Mwa Wanaume Wengi Kumesababisha Wengi Wao Waishi Katika Maisha Na Hali Ya Usononekaji Na Wengine Wamekumbwa Na Umauti Kutokana Na Hali Hiyo Ya Kuishi Na Sononi Kwa Muda Mrefu.
Kuna Mambo Mengi Yanayosababisha Wanaume Wengi Wajikute Wakipungukiwa Nguvu Za Kiume, Wataalamu Wa Masuala Ya Saikolojia Wanaamini Kuwa Mara Nyingi Suala Hilo, Hasa Kwa Watu Wenye Umri Wa Chini Ya Miaka 45, Husababishwa Na Msongo Wa Akili Kuliko Ufanyaji Kazi Wa Misuli Ya Mwili.
Watu Wengi Wanaofikiri Kuwa Wamepungukiwa Na Nguvu Hizo Huwa Hawako Hivyo, Inasema Sehemu Moja Ya Utafiti Uliofanywa Na Wataalamu Wa Chuo Kikuu Cha Havard, Nchini Marekani Na Kufafanua Kuwa:
Tatizo La Watu Hao Huwa Ni Kushiriki Tendo Hilo Kwa Wakati Usio Muafaka Kwao, Wanashiriki Wakati Bado Hawajajitayarisha Kiakili Au Wanapokuwa Wamejitayarisha, Basi `Njiani` Hukutana Na Wenzi Ambao Hawaafiki Mwelekeo Wa `Safari` Yao.
Wataalamu Wa Masuala Ya Vyakula Nao Wanaeleza Kuwa Tatizo Hilo Huwapata Wanaume Wengi Kwa Sababu Ya Utumiaji Wa Vyakula Vyenye Kuongeza Kiwango Kikubwa Cha Mafuta Mwilini Ambao Hawashiriki Katika Mazoezi Ya Viungo Ambayo Huifanya Misuli Ya Damu Mwilini Kutokufanya Kazi Vizuri Na Hivyo Kusababisha Matatizo Mengi Ya Mwili Kushindwa Kufanya Kazi Zake Vizuri.
Kumbukumbu Yangu Inaonesha Kuwa, Mheshimiwa Mbunge Wa Viti Maalumu Kuputua Tiketi Ya Chama Cha Mapinduzi, Janet Bina Kahama, 10 Aprili 2007 Katika Kikao Cha Saba Cha Bunge Aliulizwa Swali Ambalo Lilikuwa Namba 8 Lenye Kipengele A, B, Na C Ambapo Kwenye Kipengele B Aliuliza: Je, Serikali Inafahamu Ni Sababu Gani Zinasababisha Kupungua Kwa Nguvu Za Kiume Kunakotangazwa Sana Na Waganga Wa Jadi?
Waziri Wa Afya Na Ustawi Wa Jamii, Prof. David Homeli Mwakyusa Alijibu Kuwa, Upungufu Wa Nguvu Za Kiume Unasababishwa Na Mambo Mengi, Baadhi Yao Ni Lishe Duni Hasa Mboga Za Majani, Kutokula Aina Mbalimbali Za Jamii Ya Karanga (Nuts), Matumizi Yasiyofaa Ya Ulevi Kama Pombe, Sigara Na Dawa Za Kulevya, Dawa Zinazotibu Baadhi Ya Magonjwa Kama Kisukari, Shinikizo La Damu, Magonjwa Ya Akili Na Vilevile Kutopumzika Kunakosababishwa Na Shughuli Nyingi Za Kijamii Hivyo Kusababisha Uchovu.
Lakini Ni Kweli Dawa Hizi Za Asili Zinauwezo Wa Kutatua Tatizo La Upungufu Wa Nguvu Za Kiume? Pro. Mwakyusa Anathibitisha Kwa Kusema Kuwa, Dawa Nyingi Za Tiba Asili Ni Virutubisho Ambavyo Muhitaji Angeweza Kuvipata Endapo Angekula Vyakula Vyenye Virutubisho Hivyo.
Pamoja Na Kuwa Dawa Hizo Hazijafanyiwa Utafiti Wa Sayansi Ya Leo Na Kutokana Na Unyeti Wa Usiri Wa Watumiaji Wa Dawa Hizo Zingekuwa Na Madhara Zisingetumiwa Na Wananchi Hata Huko Zinakotoka Yaani Maeneo Yake Ya Asili.
Na Kusisitiza Kuwa, Wizara Ya Afya Na Ustawi Wa Jamii Haijapokea Taarifa Ya Tukio Kutoka Kwa Walalamikaji Wanaotumia Dawa Hizo Za Kuongeza Nguvu Za Kiume.
Hata Hivyo, Hali Ni Tofauti Kidogo Katika Nchi Zilizoendelea Kama Marekani Na Baadhi Ya Nchi Za Ulaya, Matumizi Ya Dawa Hizi Hutolewa Kwa Watu Baada Ya Kuandikiwa Cheti Na Daktari, Na Watu Wenye Matatizo Ya Msukumo Wa Ndamu (Bp), Mara Nyingi Wamekuwa Wakishauriwa Kutotumia Dawa Hizo Kwa Sababu Ni Hatari Kwa Maisha Yao.
Hii Ni Kwa Sababu Dawa Nyingi, Kama Viagra, Ciallis, Levitra, Yohimbine Na Nyingine Mbali Ya Kuwa Na Nafasi Ya Kusababisha Magonjwa Ya Moyo, Kwa Watu Wasiokuwa Nayo, Pia Yana Madhara Mengine Kama Vile Kusababisha Upofu Na Kuleta Hali Ya Mwili Kuwa Na Kitetemeshi.
Madhara Mengine Ya Dawa Hizo Ni Pamoja Na Kumsababishia Mtumiaji Hali Ya Kuumwa Na Kichwa Mara Kwa Mara, Macho Kuwa Mekundu, Kuziba Kwa Hewa Puani Na Maumivu Ya Tumbo Pamoja Na Kuharisha.
Haya Ni Aina Ya Madhara Yanayotokana Na Dawa Za Kizungu, Ambazo Kabla Ya Kuingia Madukani Kufanyiwa Utafiti Wa Kina Kuangalia Madhara Yake Kwa Watumiaji, Na Ingawa Hayo Yote Yanafanyika Lakini Bado Athari Zake Kwa Watumiaji Zinaonekana.
Mwandishi Na Muandaaji Mkongwe Wa Filamu Nchini Ambaye Kwa Sasa Anaishi Marekani, Chemi Che-Mponda Alishawahi Kuandika Makala Isemayo ‘Kukosa Nguvu Za Kiume Si Mwisho Wa Dunia!’ Na Katika Makala Hiyo Kulikuwa Na Hadithi Hii Isome Ili Ujue Kinachoweza Kukutokea Kwa Kujifanya Mjuaji Na Kuagiza Dawa Za Kuoneza Nguvu Kwenye Mtandao.
Chemi Alianza Hivi: “Jamani, Jamani, Jamani, Kuna Jirani Yangu Kafa Hivi Majuzi. Alikuwa Ni Baba Wa Makamu, Mmarekani Mweusi. Alikuwa Mcheshi Na Ilikuwa Kila Tukionana Lazima Tusalimiane.
“Mara Ananinunulia Kahawa Halafu Tunakaa Namsimulia Kuhusu Afrika. Yule Baba, Alionekana Mzima Na Mwenye Afya Fiti Kabisa. Nilibakia Kushangaa Kusikia Kafa Na Si Kwa Ajali. Mke Wake Alifariki Mwaka Juzi, Lakini Miezi Ya Karibuni Alikuwa Anaonekana Mwenye Furaha Kwa Vile Alipata Mpenzi, Dada Mwenye Miaka 25 Hivi.
”Story Niliyosikia Ni Hivi: Kumbe Jamaa Alikuwa Na Matatizo Ya Moyo. Alifia Kitandani Akiwa Kwenye Shughuli Ya Kufanya Tendo La Ndoa Na Mpenzi Wake. Tena Wanasema Alifariki Mara Alipofikia Kilele Cha Tendo.“Navyosikia Ilikuwa Ni ‘Massive Heart Attack’. Kama Ni Massive Bila Shaka Na Utamu Wa Shughuli Hakujua Kuwa Yuko Hatarini. Mpenzi Wake Alipiga Sana Kelele, Majirani Walipigiga Simu 911 (Polisi) Kwa Vile Walidhania Wameingiliwa Na Majambazi.
“Kumbe Jamaa Alikuwa Mtumizi Wa Viagra, Yaani Vile Vidonge Vya Kuongeza Uume, Na Kumpa Mwanaume Uweza Wa Kufanya Tendo La Ndoa. Ndugu Zake Wanalamika Kweli, Maana Hakuzipata Kwa Prescription (Maelezo) Ya Daktari, Alizaiagiza Kwenye Mtandao (Internet).
Hiyo Ni Baadhi Ya Mifano Hai Inayoonesha Wazi Madhara Unayoweza Kupata Kwa Kuamua Kutumia Tu Dawa Bila Maelekezo Kutoka Kwa Daktari!
Binafsi Nina Hofu Juu Ya Dawa ‘Za Kienyeji’ Zinazotengenezwa Na Waganga Na Kuuzwa Kama Karanga Kila Kona Ya Miji Mbalimbali Ya Tanzania Bila Ya Kufanyiwa Utafiti Wa Kina, Ni Wazi Kama Kanuni Za Kiafya Zinavyosema, Kuwa Kila Dawa Ina Madhara Yake, Lakini Je, Ni Nani Anapima Madhara Mabaya Yatokanayo Na Dawa Hizi Za Kienyeji Zinazouzwa Kama Njugu?
Ukiacha Madhara Yatokanayo Na Dawa Hizo, Pia Wanaume Wengi Hukumbwa Na Tatizo Hili La Kupungukiwa Nguvu Kwa Sababu Ya Uvutaji Wa Sigara Kwa Wingi, Utafiti Mbalimbali Wa Kitabibu Duniani Unaonyesha Kuwa Matumizi Ya Bidhaa Zitokanazo Na Tumbaku Huwasababishia Wanaume Upungufu Wa Nguvu Hizo.
Ni Kweli Ulio Wazi Kwamba Tatizo La Wanaume Wengi Kupungukiwa Nguvu Za Kiume Nchini Kwetu Na Duniani Kote Linazidi Kushika Kasi Na Tiba Mbadara Zinahitajika Ili Kurudisha Heshima Na Furaha Miongoni Mwa Wanaume Wengi Duniani, Lakini Utumiaji Wa Dawa Za Kuongeza Nguvu Haupaswi Kufanyika Kiholela Kwa Kuzingatia Kuwa Matatizo Yake Kiafya Ni Makubwa Kuliko Faraja Ya Muda Mfupi Anayopata Mtumiaji!
Siku Moja Nilikuwa Nimekaa Kwenye Kijiwe Cha Kahawa Kariakoo Jijini Dar Es Salaam Nikachokonoa Wazee Kwa Kuchomekea Mada Hii, Mambo Mengi Walinieleza Lakini Kubwa Zaidi Ni Kuwa, Vijana Wa Siku Hizi Wanakubwa Zaidi Na Tatizo Hili Kutokana Na Kufakamia Vyakula Visivyo Vya Asili Na Kusahau Kuwa, Miogo, Asali, Karanga Na Pweza Huweza Kukusaidia Ukawa Na Nguvu Kama Nyati. Vyakula Vingi Vinavyoingizwa Nchini Vikiwa Vimesindikwa Ambavyo Vijana Wengi Hukimbilia Na Kujiona Kuwa, Babu Kubwa Wakivila Hivyo Na Kumcheka Mzalendo Anayepata Muogo Wa Kuchoma Na Chachandu Huku Akishushia Na Juisi Ya Mua Pale Kariakoo Bila Kujua Kuwa Sehemu Kubwa Ya Aina Nyingi Ya Vyakula Wanavyokula Ni Sumu Yenye Ladha Nzuri Inayonenepesha! Madhara Yake Ni Mengi Na Miongoni Mwake Ni Kuwasababishia Watumiaji Kukosa Nguvu Za Kurudia Tendo.

SABABU ZA KUPUNGUA NGUVU ZA KIUME:

1. Hata Hivyo, Kuna Wakati Pia Upendo Unapopungua Na Mvuto Unapungua Baina Ya Wanandoa, Mwanaume Anaweza Kujikuta Kila Akiwa Faragha Anashindwa Kuendesha Gari Kwa Muda Mrefu Na Anaweza Kudhani Kuwa Ana Matatizo Kumbe Hali Hiyo Inamkumbwa Kutokana Na Kutokuvutiwa Na Mwenzi Wake.
Tatizo Kama Hili Linaweza Kutatuliwa Kwa Kumueleza Wazi Mkeo Ama Mpenzi Wako Jinsi Gani Anaweza Kujipanga Na Kuonekana Na Mvuto Wa Hatari Utakaokufanya Uchanganyikiwe Kila Umuonapo Na Hata Mkiingia Kwenye Mambo Fulani Basi Kwa Hakika Utahamasika Na Kutoa Dozi Ya Maana.
2.Uchovu Wa Kazi Za Ajira Mkufunzi Wangu Wa Saikolojia Katika Chuo Kikuu Cha Tumaini Iringa Ambaye Ameshatangulia Mbele Za Haki, Pro. Samuel Mshana (Mungu Amlaze Mahali Pema Peponi) Aliwahi Niambia Kuwa Wanawake Wanataka Security Kutoka Kwa Mwanaume Nami Nikamtania Pro. Sasa Mbona Mimi Na Mwili Mdogo Nitampa Ulinzi Gani Mwanamke Akacheka Kisha Akaniambia Ulinzi Naouzungumzia Ni Wa Jumla Ikiwa Ni Pamoja Na Kuhakikisha Mambo Yanakwenda Sana Ndani Ya Nyumba Yani Watoto Wanakwenda Shule Na Mambo Ya Mlo Wa Uhakika.
Hivyo Ni Wazi Kuwa Wanaume Huhangaika Kwa Kiasi Kikubwa Kuhakikisha Wanamudu Majukumu Yao Ya Kila Siku Na Huko Makazini Kuna Mauzauza Mengi Na Usiombe Ufanye Kazi Kwenye Kampuni Binafsi Kila Kukicha Wewe Upo Roho Juu Sasa Katika Hali Kama Hiyo Ukikutana Na Mwenzi Wako Kunako Majambozi Utahisi Una Upungufu Wa Nguvu Za Kiume Kwani Mara Tu Baada Ya Kumaliza Mshindo Wa Kwanza Hutoweza Kurudia Tena! Hali Ni Hivyo Hivyo Kwa Watu Wanaofanya Kazi Nzito Zinazosababisha Wajikute Wanarudi Majumbani Wakiwa Wamechoka.
Hivyo Basi, Endapo Nawe Ni Miongoni Mwa Watu Wanaokumbana Na Tatizo La Kushindwa Kurudia Majambozi Kwa Sababu Ya Uchovu Na Msongo Wa Mawazo Kutoka Kazini Hakikisha Unapanga Muda Muafaka Na Mwenzi Wako Kupeana Raha.
Mfano Kama Jumamosi Unafanya Kazi Nusu Siku Ukitoka Usiende Kulewa Kama Ni Mtu Wa Kinywaji Bali Nenda Kapumzike Kisha Kesho Yake Waweza Kumtoa Out Mama Na Kwenda Mazingira Tofauti Kupeana Kitu Roho Inapenda Hakika Utajishangaa Jinsi Utakavyomudu Majambozi.
3. Kuchacha Nakumbuka Vema Miaka Ya 1990 Enzi Hizo Redio Tanzania Pekee Ndio Ilikuwa Ikitupa Burudani Na Moja Kati Ya Nyimbo Ambazo Ilikuwa Ikinikuna Ni ‘Kuchacha Usiombee’ Iliyoimbwa Na Juwata Jazz Na Hichi Ni Kibwagizo Chake ‘Maradhi Yote Ugua Lakini Kuchacha Usiombe…’ Ebwana Usije Ukawa Katika Hali Mbaya Kifedha Na Kila Jambo Unalolipanga Linakwenda Ndivyo Sivyo Hali Inayokusababishia Uchache Kisha Mwenzi Wako Akakuomba Unyumba Hapa Kuna Mawili Ama Kuchelewa Sana Kufika Safari Yenu Ama Kumaliza Halaka Kisha Jamaa Analala Chapchap Na Hataki Tena Kuonesha Ushirikioano Hata Mamaa Akimbembeleza Vipi!
Hivyo Basi, Si Vema Kukutana Kimwili Na Mwenza Wako Kipindi Ukiwa Umechacha Kwani Wanaume Wengi Pindi Wanapokuwa Na Msongo Wa Mawazo Hukimbilia Kuomba Unyumba Kwa Wenzi Wao Wakiamini Kuwa, Wao Ndio Watawasaidia Kuwapunguzia Mawazo Badala Ya Kutafuta Njia Mbadara Ya Kumaliza Tatizo.
4. Kuishiwa Hamu Ya Nyama Na Mapishi Yale Yale Kila Siku Uzoefu Wangu Unanionesha Kuwa Wanaume Wengi Hujikuta Wakikosa Hamu Ya Kurudia Tendo La Ndoa Mara Bada Ya Kumnaliza Mzunguko Wa Kwanza Kutokana Na Wake Zao Kutowaonesha Ubunifu Yaani Kila Siku Ni Kifo Cha Mende Tu Hakuna Jipya Linaloongezwa Hata Nakshi Za Miguno Ni Ile Ile Hali Inayosababisha Wanaume Wakose Hamy Ya Kuendelea Mara Baada Ya Kumaliza Mzunguko Wa Kwanza.
Wanaume Wengi Hujikuta Wanalazimika Kutafuta Kimada Ili Kupata Radha Mpya Na Huko Mambo Huwa Mulua Kwani Hufanikiwa Kwenda Raundi Hadi Tatu Na Bado Akawa Na Hamu Kwa Vile Tu Amekutana Na Vitu Adimu Hivyo Basi, Mwanaume Anapaswa Kumueleza Wazi Mkewe Kuwa Anahitaji Wakutane Faragha Ambapo Anataka Vutu Hadimu Vya Kabatini Na Si Kumsaliti Mwenza Wako Kwani Uwezo Wa Kumfanya Awe Bora Kunako Majambozi Unao Wewe Mnwenyewe Mwanamme.
Mfano Siku Akikwambia Anakwenda Kwenye Kitchen Party Mruhusu Kisha Akiwa Huko Mtumie Meseji Kuwa, “Mpenzi Najiandaa Kumalizia Sehemu Ya Pili Ya Soma Ulilojifunza Yaani La Vitendo, Hakika Leo Nitafaidi” Asikdanganye Mtu Hapo Hata Kama Bi. Harusi Mtarajiwa Hakufundishwa Mambo Fulani Ya Kumpagawisha Mumewe Atahakikisha Hakuangushi Atakuja Na Mambo Mapya Na Hapo Ndipo Mwanaume Hujikuta Akiganda Kifuani.
Nimalize Kwa Kusema Kuwa, Hakuna Haja Ya Kukurupuka Na Kukimbilia Kununua Dawa Za Kuongeza Nguvu Ya Kiume Bila Kutafakari Kwa Kina Chanzo Cha Tatizo Lako Kwani Yawezekana Tatizo Ulilonalo Linaweza Kutatulika Kwa Njia Nyingine Ambazo Hazitakufanya Uwe Hatarini.

Tatizo La Mwanaume Kuwahi Kufika Kileleni Mapema!

1. Malalamiko Yanayotolewa Na Baadhi Yao Yanaonesha Kwamba, Muda Wa Kumaliza Tendo Huwa Kati Ya Nusu Dakika Na Dakika Tatu Kwa Tendo La Kwanza, Huku Wengine Wakimaliza Hamu Katika Hatua Za Awali Tu Za Hamasa Ya Kimahaba.
2. Hata Hivyo, Kumetolewa Maelezo Na Nafuu Ya Ongezeko La Muda Katika Tendo La Pili Na Kuendelea, Ingawa Bado Suala La Kutangulia Kufika Kileleni Kabla Ya Wanawake Limekuwa Likiwahuzunisha Wanaume Wengi.
3. Ni Ukweli Usiopingika Kuwa, Mwanaume Anapowahi Kufika Kileleni Kabla Ya Mwenzake Humsababishia Kero Mwanamke Anayeshiriki Naye Tendo, Kwani Humwacha Njia Panda Pasipokuwa Na Hitimisho La Raha Ya Kujamiiana.
4. Hali Hii Inatokana Na Maumbile Ya Uume Wa Mwanaume Ambao Husinyaa Mara Baada Ya Kuhitimisha Mbio Zake, Lakini Kwa Mwanamke Kuwahi Si Tatizo, Kwani Hakumfanyi Ashindwe Kumsindikiza Mwenzake Hadi Kileleni.
5. Utofauti Huu Ndiyo Unaowafanya Wanaume Wahuzunike Zaidi Wanapokabiliwa Na Janga Hilo Kiasi Cha Kufikia Hatua Ya Kwenda Kwa Waganga/Matabibu Ili Iwasaidie Kuepuka Balaa Ya Kutoka Uwanjani Na Aibu.
6. Ingawa Kumekuwa Na Mafanikio Katika Tiba Za Kisayansi, Lakini Bado Wanaume Wameshindwa Kupata Ukombozi Wa Kudumu Wa Tatizo Hili. Wengi Wamejikuta Wakijiongezea Mzigo Wa Fikra Kwa Kuzitumaini Zaidi Dawa Au Kuzitumia Na Kupata Matokeo Mabaya Zaidi Ya Kuishiwa Nguvu Kabisa.
7. Kwa Kufahamu Mikinzamo Iliyopo Kati Ya Akili Na Tiba Ya Nguvu Za Kiume Na Madhara Yachipukiayo Imebainika Kuwa, Mtu Anaweza Kujitibu Tatizo Hilo Kwa Kutumia Kanuni Za Kisaikolojia Na Mafanikio Yasiyo Na Madhara Yakapatikana.
Wataalamu Wa Kisaikolojia Wanatambua Kuwa Kanuni Ya Ufanyaji Mapenzi Iko Zaidi Kwenye Ubongo Kuliko Mwilini.
8. Kinachotokea Hadi Mtu Akapata Msisimko Wa Kufanya Mapenzi Si Mwitikio Wa Mwili, Bali Ni Utambuzi Wa Akili Juu Ya Kiwango Cha Mapenzi Kilichopokelewa Kwenye Ubongo Unaojihusisha Na Hisia.

FAHAMU VYAKULA VINAVYOONGEZA NGUVU

Image result for nguvu za kiume
Kuna Aina 2 Ya Vyakula Ambavyo Vimefanyiwa Utafiti Na Kubaini Kuwa Ni Moja Ya Vyakula Vinavyosaidia Kuongeza Nguvu Za Kiume Na Havina Madhara Katika Engezeko La Nguvu Za Kiume, Katika Vyakula Hivyo Vyenye Uwezo Wa Kuongeza Nguvu Za Kiume Kiasili Ni:
1. TANGAWIZITangawizi Ni Moja Ya Chakula Kinachoweza Kurejesha Nguvu Za Kiume, Unaweza Kuichemsha Tangawizi Na Ukatumia Kwa Kuinywa Kama Chai Asubuhi, Mchana Na Jioni Pia Tangawizi Unaweza Ukaitumia Katika Mchanganyiko Wa Kiasili Kwa Kutumia Asali,Kitunguu Saumu Na Tangawizi Yenyewe.
JINSI YA KUTUMIA MCHANGANYIKO HUU:
Chukua Tangawizi Na Kitunguu Saumu Vitwange Kisha Vichanganye Na Asali Pamoja Na Unga Wa Habat Soda Na Uwe Unakunywa Mchanganyiko Huu Kwa Kutumia Kijiko Cha Chai Kimoja Kutwa Mara 3 Kwa Muda Wa Wiki Moja Na Utaona Mabadiliko.
2. TIKITI MAJI:
-Chakula Kingine Kinachosaidia Katika Upande Wa Kuongeza Nguvu Za Kiume Ni Tunda La Tikiti Maji, Unaweza Ukachukua Tikiti Lako Ukalikata Na Kutengeneza Juice Ya Tikiti Kisha Unakunywa Ila Sio Lazima Utengeneze Juice Hata Lenyewe Tu Unaweza Ukalila. Ila Jitahidi Kutumia Tunda Hili Hata Kila Siku Kwani Linasaidia Sana Kwa Wenye Matatizo Ya Nguvu Za Kiume.
Si lazima utumie chemicals tumezungukwa na suluhisho ya matatizo mbalimbali kwa kutumia matunda na mbogamboga …………Jaribu ujionee…..

Haya hapa matunda matano yenye uwezo wa kuongeza nguvu za kiume


Habari za leo mdau wangu wa tovuti yetu ya www.dkmandai.com bila shaka utakuwa upo vizuri karibu tuendelee kufahamishana umuhimu wa lishe bora pamoja na matunda mbalimbali kiafya.

Leo ninayo orodha ya matunda ambayo huweza kusaidia kupunguza tatizo la upungufu wa nguvu za kiume kutokana na virutubisho yaliyonayo.

1. Embe 


Kwa embe hili linauwezo wa kupunguza tatizo hilo la upungufu wa nguvu za kiume kutokana na kuwa na vitamin E ambayo huwa na nafasi kubwa ya kuongeza hisia za kushiriki tendo la ndoa.


2. Tikitimaji



Hili ni miongoni mwa tunda nzuri pia kwa wenye tatizo hilo kwani husaidia kuboresha mzunguko wa damu ndani ya mwili jambo ambalo huweza kumsaidia mwanaume mwenye upungufu wa nguvu za kiume kupata ahueni.

3. Komamanga

Tunda hili lina kirutubisho kiitwacho antioxidants ambacho nacho huimarisha mzunguko wa damu kuwa vizuri ndani ya mwili na hivyo kupunguza ukubwa wa tatizo la upungufu wa nguvu za kiume.

4. Parachichi

Ndani ya tunda hili kuna utajiri wa madini ya potassium, vitamin B6, vitamin E kwa pamoja virutubisho hivyo husaidia kuboresha afya ya moyo na kurekebisha mzunguko wa damu kuwa vizuri zaidi.


5. Ndizi


Ndani ya ndizi kuna madini ya potassium ambayo pia huwa na mchango kwenye masuala ya tendo la ndoa.

Tafadhali endelea kuwa karibu na tovuti yetu ya www.dkmandai.com, lakini pia unaweza kuwasiliana nasi kwa simu namba:- 0784 300 300, 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com.

Kumbuka kuwa, ushauri huu umetolewa chini ya Shirika lisilokuwa la Kiserikali la The Work Up Tanzania (WUTA) ambalo linadhamira ya dhati ya kupambana na umasikini, ujinga na maradhi kwa kuhamasisha jamii kuhusu matumizi ya lishe bora zitokanazo na mimea na matunda. Pia unaweza kufika ofisini kwetu Ukonga Mongolandege jijini Dar es Salaam kwa ushauri zaidi.
Usisahau kushare posti hii!! Share Facebook, Twitter bila kusahau Whatsapp!!
Toa maoni yako kuhusu, UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME. hapa..

Kimenukaa...Wabunge Wamlipua Steve Nyerere,Wakataa Kuombwa Msamaha..!!!


Kusambaa kwa sauti iliyorekodiwa mazungumzo ya mwigizaji Steven Mengele ‘Steve Nyerere’ na mama wa Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu, Mariam Sepetu halijafutika, mengine yamefumka kwani baadhi ya wabunge waliotajwa kwenye sauti hiyo wamelimpua Steve. Mbali na wabunge kutajwa katika sauti hiyo iliyosambaa wiki iliyokatika, wasanii pia walitajwa ambao ni Khaleed Mohamed ‘TID’, Romeo George ‘Rommy Jones’ na Ahmed Hashim ‘Petit Man’.

Kwa upande wa wabunge ni Goodluck Millinga (CCM-Ulanga), Ahmed Shabiby (CCM-Gairo), Joseph Musukuma (CCMGeita Vijijini), Freeman Mbowe (Chadema-Hai) na Zitto Kabwe (ACT-Wazalendo, Kigoma Mjini).

Steve pia aliwataja mawaziri wawili. Steve alisikika akiwataja wabunge hao akimwambia mama Wema kuwa, aliwafuata bungeni mjini Dodoma, Februari 6, mwaka huu ili wamsaidie bintiye aliposhakiliwa kwenye Kituo Kikuu cha Polisi Dar ‘Sentro’ kwa madai ya kujihusisha na matumizi ya madawa ya kulevya, ikiwemo kukutwa na bangi.

STEVE AOMBA RADHI WOTE

Hata hivyo, baada ya sauti hiyo kusambaa mitandaoni Februari 23, mwaka huu na kuwa gumzo, Jumamosi iliyopita, Steve alifanya mkutano na waandishi wa habari katika Jengo la Millennium Tower, Kijitonyama na kuwaomba radhi wote aliowataja huku akikiri sauti ni yake na kwamba, hakuzungumza nao kama ‘alivyomwongopea’ mama Wema bali aliwataja katika hali ya kudumisha ukaribu wake na familia ya mama huyo.

UWAZI NA WABUNGE

Baada ya mkutano huo, Uwazi liliwatafuta wabunge hao, kasoro Mbowe hakupokea simu, na waliopatikana walikuwa na haya ya kusema: SHABIBY: “Steve Nyerere namfahamu. Lakini sina ukaribu naye. Niliwahi kukutana naye muda mrefu kwenye hoteli yangu ya Moleno, Dodoma.

“Nakumbuka alikuja na mwanamuziki Ray C (Rehema Chalamila), lakini baada ya hapo sijawahi kuonana naye popote maana hata baada ya kukutana naye sikuwahi kuwasiliana naye. “Kuhusu kunihusisha mimi katika sakata la Wema, yale mazungumzo nimeyasikia vizuri. Si kweli alichokisema eti alikuja kukutana na Musukuma kwenye hoteli yangu na mimi nikiwepo. Ni uongo mtupu.

“Sijaonana na Steve Nyerere katika siku za hivi karibuni na sijazungumza naye lolote lile hata kwa njia ya simu,” alisema Shabiby.

MILLI NGA: “Ninafahamu kila kitu kinachoendelea, maana Steve Nyerere ni mtu ambaye tunakutana mara kwa mara, ukizingatia ni kada mwenzangu kwenye Chama Cha Mapinduzi. Kuhusu yeye kunishawishi mimi kumtetea Wema bungeni, jambo kama hilo halipo maana sikuwahi kukutana naye kabla ya mimi kuzungumza bungeni. “Ila baada ya bunge, jioni nilikutana naye, akaniambia kuwa, nilichokiongea ni kama nilitazama kilichokuwa moyoni mwake.

Hata hivyo, nimemsamehe maana ameomba radhi kwenye mkutano na waandishi wa habari!”

ZITTO: “Mimi siwezi kusemea jambo hilo maana mimi kwangu halina maana yoyote.”

MUSUKUMA: “Nisikilize vizuri mwandishi, mimi Steve Nyerere hana mchango wowote kwenye maisha yangu. Mimi ni Mbunge wa Geita Vijijini na sifanyi kazi yangu ya ubunge kwa kushawishiwa na mtu. “Steve Nyerere anaweza kunishawishi mimi kwa kipi? Ngoja nikwambie kitu, kinachoendelea ni kiki ya Steve Nyerere na watu wake maana kama umesikia ile ‘place’ na waandishi aliyoitisha, anasema Makonda ni rafiki yake, sasa unaweza kupima kinachoendelea hapo.”

MUSUKUMA AKATAA RADHI YA STEVE

Alipoulizwa kuhusu radhi aliyoiomba Steve Nyerere kwa wote aliowataja yeye ameipokeaje, alisema: “Kama ameomba radhi basi amewaomba wananchi

wangu wa Geita waliyoniweka kwenye nafasi yangu kwa lengo la kuwatetea wananchi na si kufanya kazi kwa ushawishi wa mtu.”

TID KWENDA KORTINI? Taarifa zaidi zilisema kuwa, Mbongo Fleva, TID anajipanga kumfikisha Steve kortini baada ya sauti yake kumtaja akisema anamchukia sana yeye huku pia kukiwa na habari kwamba, baadhi ya wanasheria jijini hapa wamepanga kujitokeza kwa waliotajwa ili kuangalia uwezekano wa kumfungulia kesi mama Wema ambaye anatajwa na Steve mwenyewe kuwa, ndiye aliyemrekodi.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatano ya March 1




 

Gallery

Popular Posts

About Us