KINGAZI BLOG: 04/07/17

HABARI KARIBU YAKO ZAIDI.

Breaking News
Loading...

Friday 7 April 2017

UMEIPATA HII....!!!!????Mwili wa Mkuu wa Freemason kuchomwa moto



MAZISHI  ya Mkuu Sir Andy chande aliyefariki akiwa na umri wa miaka 88  huko Nairobi Kenya yanatarajiwa kufanyika Jumanne ijayo kwa mwili wake kuchomwa moto mpaka kuteketea wote.

Wageni zaidi ya 300 kutoka nje ya nchi wakiongozwa na Freemason mkuu watahudhuria mazishi yatayofanyika hapa Dar es Salaam.
Booking za guest watazofikia wageni mashughuli wa freemason zinaendelea kufanyika kwa kasi ya ajabu hapa jiji zina la dsm.

Kumbuka sir Andy chance alikuwa kiongozi wa Freemason, mmiliki wa shule ya shaaban Robert, Ashawahi kuwa mkuu wa makumbusho ya Taifa (mkabala na IFM).


Kamanda Siiro Afunguka kuhusu kupotea kwa Msanii Roma Mkatoliki

Kamishna wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam, Simon Sirro amesema kuwa tayari wameshapata taarifa za kupotea kwa Msanii wa Bongo Fleva hapa nchini, ‘Ibrahim Mussa’ maarufu kwa jina la Roma Mkatoliki na kuongeza kuwa tayari timu yake ya upelelezi imeshaanza kazi.

Ameyasema hayo mapema hii leo wakati akizungumza na Katibu wa Chama cha Wanamziki wa Kizazi Kipya Tanzania, Samweli Mbwana alipotaka kujua kama Jeshi la Polisi lina taarifa ya kupotea kwa mwanamziki huyo.

Sirro amesema kuwa taarifa za kupotea kwa msanii huyo tayari wameshazipata na Jalada la upelelezi tayari limeshafunguliwa kwa ajili ya upelelezi.

Ameongeza kuwa timu yake ya upelelezi iko mtaani kwa ajili ya kujua kinachoendelea, na amewaomba wasanii na baadhi ya watu kutokuwa wepesi wa kusambaza uvumi usiokuwa na ukweli ndani yake.

“Jamani mambo ya uvumi yaacheni, sio kitu kizuri unamvumishia mtu kitu ambacho hakijui na wengine wanasema kuwa Serikali inahusika kitu ambacho si cha kweli”,amesema Kamanda Sirro.

Aidha, Sirro amesema kuwa amepanga kukutana Waandishi wa Habari kesho saa tano Ofisini kwake ili kuweza kutoa ripoti kamili kuhusu kupotea kwa msanii huyo wa Bongo fleva kwani timu ya upelelezi tayari iko kazini.

Hata hivyo, amewatoa hofu wasanii na wananchi kwa ujumla kwamba suala hilo linafanyiwa kazi, hivyo hakuna haja ya kuogopa na kuendelea kuvumisha vitu visivyokuwa vya msingi.

MAITI Yaokotwa Ufukwe wa Ziwa Victoria Ikiwa Imefungwa Kwenye Baiskeli

Tukio la kusikitisha Wakati familia kadhaa za watanzania zikiendelea kupoteza ndugu zao bila kujulikana walipo, leo huko mkoani Mara katika ufukwe wa ziwa Victoria imeokotwa maiti ya mtu mmoja asiyefahamika ikiwa imetupwa ziwani. Mazingira ya kifo chake yanaonesha mtu huyo mwanaume aliuawa, akafungwa kama kifurushi kwenye baiskeli, kisha yeye na baiskeli yake wakatoswa ziwani. Hapa ndipo tulipofika kama taifa.! TAHADHARI: Picha inatisha

Utapeli Magroup ya WhatsApp

Katika kutafuta namna ya kujipatia kipato kwa wakati huu ambapo njia zote za ujanjaujanja zimezibwa na serikali ya awamu ya tano, baadhi ya watu wamebuni mbinu ya kuwatapeli wananchi kupitia makundi ya mitandao ya kijamii hasa WhatsApp.

Kwa mujibu wa mmoja wa watu ambao alijikuta akiingia katika mtego huo kutokana na tamaa yake ya ngono, (jina lake linahifadhiwa) alipata rafiki katika Mtandao wa Kijamii wa Facebook ambaye baadaye alimweleza kuwa ana mtandao wa wasichana mastaa na wasio mastaa wanaojiuza na angeweza kuwapata kirahisi kwa kupewa mawasiliano yao na pia kuona picha na baadhi ya video wakiwa watupu.

Madai yaliyofikia katika dawati la gazeti hili, vijana wengi ambao ndiyo watumiaji wakubwa wa mitandao ya kijamii, wamekuwa wakitapeliwa mara kwa mara kwa kujiunga katika makundi hayo.

Inaelezwa kuwa, mchezo mzima huanzia Mitandao ya Instagram na Facebook ambapo wengi wa matapeli hao huweka picha za wanawake wakali wa Kibongo na kudanganya kuwa wanapatikana kwa njia ya picha na video wakiwa utupu katika makundi yao ya WhatsApp huku wakianika namba za simu watumiwe kiasi cha pesa waunganishwe. Wakishaweka posti hizo katika mitandao hiyo, vijana wengi hukimbilia kujiunga kwa kutumia namba zilizowekwa katika mitandao hiyo kwa kiingilio cha kiasi cha kuanzia shilingi 5,000 hadi 10,000 kwa mmoja lakini wakishajiunga katika makundi hayo hakuna kinachoendelea na hata ukiwatafuta hawapokei simu.

OFM KAZINI Katika siku za hivi karibuni ilibainika kuwa, kuna makundi mengi ya WhatsApp yanayoendesha biashara ya ukahaba. Kikosi kazi cha Operesheni Fichua Maovu (OFM) kikaingia kazini kubaini kama kweli biashara hiyo inaendelea kwa njia ya mtandao ambapo mmoja wa mapaparazi aliomba kuunganishwa na kundi linalojinadi kuwa, ukitaka kahaba wa kila aina unampata.

Kufuatia paparazi kutaka aungwe ili apate huduma, alitakiwa kutuma kiingilio cha shilingi 15, akatuma na kuomba aunganishwe na mmoja wa warembo wakali waliokuwa wamewekwa kwenye group hilo. Heh, imeliwa! Baada ya pesa kutumwa, hakukuwa na mawasilino tena na simu ikawa haipatikani.

Ijumaa linawashauri watumiaji wa mitandao hiyo, kuwa makini na watu wa aina hii kwani kila siku wamekuwa wakiongezeka katika mitandao na kujipatia pesa kwa njia rahisi. Ukishaona unaungwa au unashawishiwa kujiunga na kundi ambalo limekaa ‘kihelahela’, akili kumkichwa.

GPL

Taarifa mpya ya Wizara ya Habari na sanaa kuhusu Roma kutoweka


Taarifa za kupotea kwa Msanii Roma Mkatoliki na wenzake wawili baada ya kutekwa na kuchukuliwa na Watu wasiojulikana kwenye studio za TONGWE Dar es salaam, zilianza kusambaa kuanzia juzi usiku (April 5 2017)

Leo April 7 2017 Wizara ya Sanaa, Utamaduni na michezo ambayo iko chini ya Dr. Mwakyembe imetoa taarifa ifuatayo >>>> “kwa dhamana yake katika tasnia ya Sanaa Wizara imepokea kwa mshtuko taarifa za kutoweka kwa Mwanamuziki Ibrahim Mussa kwa jina la kisanii “Roma Mkatoliki””

Wizara imefuatilia kwa karibu suala hili kwa kuwa lina muelekeo wa jinai. Hata hivyo taarifa kutoka vyombo vya dola zinathibitisha kuwa Roma Mkatoliki hashikiliwi katika kituo chochote cha polisi.

Kutokana na hali hiyo, Wizara inawaomba wadau mbalimbali na wananchi kwa ujumla kushirikiana na Jeshi la Polisi kwa kutoa taarifa zozote zitakazo saidia kujua alipo msanii huyo.

Maneno matatu ya Nape Nnauye kuhusu Roma

 Baada ya mastaa mbalimbali kuguswa juu ya stori ya Roma mkatoliki na wenzake watatu kuchukuliwa na watu wasiofahamika kwenye Studio za Tongwe Records na kupelekwa sehemu isiyojulikana, sasa leo April 7 2017 Mbunge wa Mtama (CCM) Nape Moses Nnauye ameonesha hisia zake juu ya tukio hilo.

Kupitia account yake ya twitter Nape Nnauye ameyaandika maneno haya matatu kuhusu Roma…>>>”Roma! Oooooh No!” – Nape Nnauye.



Wasanii: Paul Makonda Anajua Alipo Roma, Atafutwa Vituo Vyote vya Polisi Dar Bila Mafanikio.


Wasanii kupitia kwa kikao chao kilichofanyika leo Tongwe records wamepaza sauti na kushusha lawama kwa mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam ndugu Paul Makonda kuwa anajua vizuri alipo msanii Roma Mkatoliki. 

Wasanii hao wamesema kuwa watekaji hao walitamka wazi kuwa wanamtaka msanii Roma na producer wake na walipoona watajulikana ndipo walipoamua kuondoka na watu wote waliokuwepo ndani ya studio za Tongwe records siku hiyo ya alhamisi juzi. 

Aidha Babu Tale ambaye ni meneja wa wasanii kadhaa akiwemo Diamond amesema kuwa kwa hili kamwe hamuogopi Paul Makonda na amemtaka kumrejesha mara moja msanii mwenzao. 

Aidha Babu Tale amesema kuwa anashangaa kuona Paul Makonda yupo kimya juu ya hili huku yeye akiwa kama kiongozi mkuu wa ulinzi na usalama ndani ya Dar es Salaam.

Hii hapa video ya Nay Wa Mitego - WAPO (Official Music Video)

nay-640x426Msanii Nay wa Mitego ameachia video yake mpya ya wimbo unaitwa “Wapo”, video imeongozwa na Khalfani Khalmandro, tazama hapa chini alafu toa komenti yako.

BOFYA PLAY KUIONA
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

Spika wa Bunge akutana na Rais wa TLS, Tundu Lissu


Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai akisalimiana na Rais wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS) Mhe.Tundu Lissu walipofika na Ujumbe kutoka TLS kumtembelea ofisini kwake Bungeni Mjini Dodoma.Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai akizungumza na Rais wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS) Mhe.Tundu Lissu na ujumbe wake walipomtembelea ofisini kwake Bungeni Mjini Dodoma.Rais wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS) Mhe.Tundu Lissu akimueleza jambo Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai alipofika kumtembelea Ofisini kwake Mjini Dodoma pamoja na viongozi wengine wa TLS.Rais wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS) Mhe.Tundu Lissu akimuonesha kitabu chenye nyaraka kadhaa za Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS) Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai alipofika kumtembelea Ofisini kwake Mjini Dodoma pamoja na viongozi wengine wa TLS.Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai akipokea kitabu chenye nyaraka kadhaa za Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS)kutoka kwa Rais wa chama hicho Mhe.Tundu Lissu wakati viongozi wa Chama hicho walipofika kumtembelea Ofisini kwake Mjini Dodoma pamoja na viongozi wengine wa TLS.

Faru Fausta Atikisa Bunge..Habari Vichwa vya Magazeti ya Leo 7/4/2017.




 

Gallery

Popular Posts

About Us