KINGAZI BLOG: 03/31/17

HABARI KARIBU YAKO ZAIDI.

Breaking News
Loading...

Friday 31 March 2017

Picha 4: Gari aina ya Lamborghini Huracan iliyozinduliwa kwa ajili ya trafiki wa Italia


 Kila nchi inatumia fedha nyingi kuhakikisha ulinzi na usalama wa nchi na raia wake lakini kuna nchi ambazo zimeenda mbali zaidi kwa kununua magari ya polisi ambayo mara nyingi tulizoea kuyaona yakitumika na matajiri kwenye matanuzi.

Jeshi la Polisi nchini Italia limefanya uzinduzi wa gari aina ya Lamborghini Huracan kwa ajili ya kufanyia doria kwa askari wa barabarani ‘Trafiki’. Uzinduzi huo ulifanywa na Waziri wa Mambo ya Ndani Marco Minniti katika sherehe iliyofanyika Alhamisi March 30, 2017 ambapo miongoni mwa sifa za gari hilo ni pamoja na V10 engine, 610 horsepower, na kasi ya 0-62 hadi 3.2 kwa sekunde na kasi ya juu kabisa ni 201 mph (325 km/h).







Mbunge Peter Lijualikali atoa ya moyoni baada ya kukaa jela siku 70.

Dar es Salaam. Siku moja baada ya Mbunge wa Kilombero (Chadema) Peter Lijualikali kuachiwa huru na mahakama kuu kanda ya Dar es Salaam, ametoa ya moyoni na kusema kuwa alichofanyiwa ni uonevu.

Ameyasema hayo leo baada ya Waziri Mkuu Mstaafu, na Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Pwani, Frederick Sumaye, kukamilisha taratibu za kumtoa gerezani.

Lijualikali amefutiwa mashtaka yake jana na mahakama kuu kanda ya Dar es Salaam baada ya kukaa jela kwa zaidi ya siku 70 akituhumiwa kufanya vurugu katika uchaguzi wa mwaka 2015. Katika hukumu hiyo, Lijualikali alihukumiwa bila kupewa masharti ya faini.

Utata mkubwa waibuka malori ya mafuta yaliyoibwa jijini Arusha hivi karibuni.

Arusha. Utata waghubika kuibwa na kupatikana kwa magari mawili ya mafuta mali ya Kampuni ya Mount Meru.

Taarifa za kuibwa kwa magari hayo mkoani Arusha yakiwa na mafuta aina ya dizeli lita 77, 000 na kupatikana siku ya pili yakiwa wilayani Hai, mkoani Kilimanjaro zinaelekeza kuwa kamera maalumu za (CCTV) ziliondolewa sehemu yalipokuwa yameegeshwa magari hayo.

Meneja Mkuu wa Kampuni ya Ulinzi ya Ultimate, Eliuta Mwanjawike alisema kampuni yao baada ya kupata taarifa ya kuibwa magari hayo na walinzi wake wawili, waliunda kamati ya uchunguzi iliyobaini upungufu ukiwapo wa tofauti ya taarifa kati ya meneja mkuu wa kampuni hiyo na mkurugenzi.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Yusuph Irembo alikiri kupata taarifa za magari hayo kuibwa na kudai kuwa wameamua kuyaondoa eneo la polisi.

“Magari hayo tumemkabidhi mmiliki kwa sababu yalikuwa na mafuta mengi na tusingeweza kukaa nayo hapa ila kesi ikishafika mahakamani basi yataletwa hapa,” alisema Yusuph.

Mkurugenzi wa Kampuni ya Mount Meru, Atuli Mittaal mwishoni mwa wiki iliyopita  alisema magari yake yaliibwa saa sita usiku yakiwa na mafuta na yalikutwa  yametelekezwa mkoani Kilimanjaro, huku walinzi wawili wa Kampuni ya Ulinzi ya Ultimate wakiwa hawajulikani walipo.

Dk Slaa afunguka baada ya kukaa kimya mda mrefu akiwa ughaibuni kaongea haya mazito.

BAADA ya kuishi nchini Canada kwa zaidi miaka miwili sasa, aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willbrod Slaa amesema anakuna kichwa ili kupima mazingira yaliyomfanya aondoke nchini na familia yake kama yapo au laa.

Septemba,2015 wakati wa Uchaguzi Mkuu Dk. Slaa alijiweka kando na siasa, kwa kile alichokieleza kutofautiana na chama chake juu ya masharti ya kumpokea aliyekuwa mgombea urais wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa),Edward Lowassa.

Hata hivyo Dk. Slaa ambaye amekuwa mbunge wa Karatu kwa vipindi vitatu mfululizo, hakuweza kuainisha mazingira yaliyomfanya aondokea nchini na kwenda kuishi ughaibuni.

“Sina tabia ya kuyumbishwa…sina chuki na mtu yeyote, sipendi siasa za udanganyifu na propaganda. Nimeachana na siasa tangu Julai 28,2015, baada ya kuona misingi ya chama nilichoshiriki kukijenga imepotoshwa,”alisema Dk. Slaa siku alipotangaza kuachana na siasa.

Pamoja na mambo mengine, alisema sharti la kwanza ambalo alitaka Chadema izingatie ni kiongozi huyo wa zamani ndani ya serikali ya CCM, kujisafisha dhidi ya tuhuma ya kashfa ya sakata la Kampuni ya Kufua Umeme ya Richmond aliyohusishwa nayo akiwa Waziri Mkuu.

Kurudi nchini

Akizungumza na MTANZANIA akiwa nchini Canada jana, Dk. Slaa alisema amemaliza masomo yake na baada ya kufanya tafakari atarejea nchini wakati wowote.

“Ni kweli nimemaliza masomo yangu. Bado napima mazingira yaliyonifanya niondoke na familia yangu. Baada ya hapo tutaangalia uwezekano wa kurejea,”alisema.

Alisema kuhusu matarajio yake ya kisiasa, watu wameshindwa kumwelewa siku ambayo alitangaza kustaafu siasa za vyama.

Alisema alichomaanisha ni kwamba, pamoja na kuachana na siasa za vyama,atakuwa tayari kupiga kelele pale anapoona masilahi ya Taifa yanaumia.

“Hadi sasa sijapiga kelele kwa kuwa sijaona masilahi ya Taifa yakiangamizwa, hatua mbalimbali zinazochukuliwa ni kweli zinawaumiza wasiohusika.

“Ndio maana nilitumia katika makala mojawapo mtego wa panya huwakamata wanaohusika na wasiohusika. Hivyo, makosa madogo mimi hayanisumbui kwa kuwa hakuna binadamu kamilifu ,”alisema.

Rais Magufuli

Akizungumzia utendaji wa Rais Dk. John Magufuli, alisema watu waelewe hakuna nchi hata moja ambapo kiongozi atakubalika na watu wote kwa asilimia 100.

Alisema wako watu ambao masilahi yao yataguswa kwa namna moja au nyingine hivyo lazima watapiga kelele.

Kutokana hilo, alisema Rais Dk. Magufuli katika kundi ambalo halihitaji fedha ameyatekeleza yote kwa asilimia 99.9, ikiwa ni pamoja na uwajibikaji serikalini, kuchukua hatua kali dhidi ya rushwa, uwizi wa mali za umma, uwindaji haramu na kudhibiti dawa za kulevya.

“Hatua zote zimechukuliwa,zinapaswa kuwa endelevu. Kwa bahati mbaya mchwa wengine waliopenya mpaka ndani ya Ikulu na Serikali na huwezi kufagia Serikali nzima kwa siku mmoja.

“Kwa jinsi Rais ambavyo hayumbi na wala hayumbishwi, nina hakika atafikia malengo na kurudisha Taifa kwenye misingi ya tunu za Taifa ya uwazi, ukweli, uadilifu, kuheshimiana na kuthaminiana na hasa kujali utu.

“Hii ndiyo hali ambayo JPM kila siku anaiita ‘Transition’ (kipindi cha mpito). Tutafika tu, tunatakiwa kuwa wavumilivu na wenye uzalendo wa kweli ana nia njema ya kufikisha Taifa mahali pazuri. Hii inahitaji kuweka pembeni maslahi yetu binafsi kama mtu mmoja mmoja, viongozi wa Serikali au hata wa kisiasa,”alisema Dk. Slaa.

Upinzani

Kuhusu mwenendo huo endapo utasaidia upinzani kuingia Ikulu 2020, Dk. Slaa alisema wakija na ajenda mbadala na makini yenye kuwalenga wananchi moja kwa moja itawasaidia.

Dk. Slaa ambaye pia alipata kugombea urais kupitia Chadema mwaka 2010, alisema endapo wataendelea kurukia kauli za Rais, basi upinzani utafutika kabla ya 2020. 

“Kama nilivyorejea mara kadhaa, upinzani makini utaingia Ikulu kwa ajenda mbadala. Ajenda makini yenye kuwalenga wananchi moja kwa moja katika kuwatoa kwenye kero zao mbalimbali.

“Hadi sasa ninachoona ni ‘kurukia’ kauli za JPM, lakini kauli si ajenda na hatupeani maksi kwa kuzungumzia usahihi wa lugha. Wako wanaotazama usahihi wa lugha na mahali pa kutazama usahihi huo. Kimsingi hayo ni masuala ya darasani au kwenye uandishi wa vitabu.

“Aidha kumtuhumu JPM kukiuka Katiba na sheria nayo haina tija. Wote wanaomtuhumu wanajua kuwa wakiambiwa waonyeshe kifungu mahususi alichokiuka yeye mwenyewe katika utendaji wake hawana majibu ya kuridhisha.

“Hivyo mimi sijaona mwenendo wa JPM unaosaidia kuingiza upinzani Ikulu. Isitoshe kama hawatakuja na ajenda makini na mkakati ulioandaliwa unaowatoa wananchi hapa walipo kwenda kwenye raha, upinzani unaweza kufutika kabla ya 2020,”alisema Dk. Slaa.

Breaking news!!!! Mbunge wa CHADEMA afariki dunia

 Dkt Elly Macha (Enzi za uhai wake)

Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Viti Maalum (CHADEMA) akiwakilisha walemavu Dkt. Elly Macha amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Msemaji wa CHADEMA Tumaini Makene amethibitisha kutokea kwa kifo hicho, ambapo amesema mbunge huyo alikuwa akipatiwa matibabu mkoani Arusha.

"Taarifa ni za kweli, mbunge Viti Maalum Dkt. Elly Macha amefariki, lakini sijapata bado taarifa za kina, lakini ninachojua ni kwamba amekuwa akipatiwa matibabu kwa muda mrefu Arusha" Amesema Makene

Miongoni mwa wabunge wa kwanza kutoa taarifa za msiba huyo ni Lazaro Nyalandu ambaye kupitia mtandao wa twitter ameandika "Mbunge mwenzetu, Mhe. Dr. Elly Macha amefariki dunia leo.

Wabunge wote tumeguswa sana na tukio hilo. Upumzike kwa amani dada yetu mpendwa"

Taarifa zaidi kuhusu msiba huu zitaendelea kukujia hivi punde



Waziri Mkuu Ataka Mkataba Uvunjwe....Ni wa Mkandarasi aliyenyang’anywa pasipoti na Rais Magufuli

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali haitavumilia wakandarasi wasio na uwezo na ambao wanapewa kazi lakini wanashindwa kuzimaliza katika muda uliopangwa.

Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo, jana (Alhamisi, Machi 30, 2017) wakati akizungumza na watumishi wa Halmamshauri ya Chalinze na wale wa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira (CHALIWASA) katika ofisi zao, karibu na daraja la mto Wami, wilayani Bagamoyo, mkoani Pwani.

Alikuwa ameenda kukagua mradi wa upanuzi wa mtambo wa maji Chalinze na ujenzi wa mfumo wa kusafirisha na kusambaza majisafi pamoja na matenki ya kuhifadhia maji ambao umechukua muda mrefu lakini haujakamilika. Awamu ya kwanza ilianza mwaka Septemba mosi 2001 na kukamilika Desemba mosi 2003.

Alimuagiza Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Gerson Lwenge ahakikishe kuwa kazi ya ujenzi wa mradi huo inaimarika na kufikia asilimia 80 la sivyo, wakamilishe taratibu za kukatisha mkataba na kutafuta mkandarasi mwingine.

Agizo la Waziri Mkuu linafuatia taarifa aliyopewa kwamba mkandarasi wa mradi huo, Overseas Infrastructure Alliance (OIA) Pvt Ltd ya India alipaswa kumaliza kazi hiyo Februari 22, mwaka huu lakini hadi sasa mradi huo umekamilika kwa asilimia 23 tu.

“Nimeelezwa kwamba mmempatia nyongeza ya siku 100 ambayo inaisha tarehe 31 Mei 2017, kama kazi yake haitakuwa ya kuridhisha na kufikia walau asilimia 80, itabidi Mheshimiwa Waziri uendelee na taratibu zako za kukatisha mkataba, tuanze kutafuta mkandarasi mwingine,” alisema.

“Hii kampuni niliikuta Lindi kwenye mradi mwingine wa maji kama huu. Nilitoa maagizo ya kuharakisha ujenzi ukamilike lakini hawakufanya hivyo hadi Mheshimiwa Rais alipoenda na kuagiza mkandarasi anyang’anywe pasi yake ya kusafiria mpaka atakapomalizia kazi.”

“Kwa kifupi ni kwamba hii kampuni haina uwezo wa kufanya hizi kazi, na ndiyo maana hadi sasa wamekamilisha asilimia 23 tu ya mradi wakati walipaswa kuwa wamemaliza hivi sasa,” amesema Waziri Mkuu na kuongeza: “Mheshimiwa Waziri endelea na utaratibu wa kuwaondoa kisheria sababu hata tukiwaongezea muda bado hawatakamilisha kazi.”

“Nimesikitika sana kukuta mkandarasi hajafikia malengo. Mtu akipewa kazi anapaswa awe na uwezo wa kifedha wa kuifanya ile kazi ili hata Serikali ikichelewesha malipo yake, yeye aendelee na kazi,” aliongeza Waziri Mkuu.

Akizungumzia kuhusu ufanisi wa mradi huo, Waziri Mkuu alimtaka Mkurugenzi Mtendaji wa CHALIWASA, Eng. Christer Mchomba, ahakikishe kuwa wanapeleka maji hadi majumbani mwa wateja na kuweka mita ili wananchi waweze kulipa bili zao badala kuishia kutoa huduma hiyo kwenye vioski (viula).

“Kazi ya kupeleka maji majumbani ni yenu CHALIWASA na siyo ya Wizara. Pelekeni maji na mfunge mita ili watumiaji waweze kulipa bili zao. Pia toeni elimu kwa wananchi kupitia mikutano ya hadhara, waelezeni mipango yenu na wapi mlipofikia. Kazi yenu siyo kutandika mabomba tu, bali kutekeleza majukumu mliyopewa kwa niaba ya Serikali,”alisema.

Kuhusu mitambo inayotumika, Waziri Mkuu alisema mashine zilizopo ni za siku nyingi tangu 2003; hivyo amemuagiza Waziri Lwenge afuatilie upatikanaji wa mashine za kisasa kwani hilo suala ni kubwa na haliwezi kubebwa na CHALIWASA. “Bora mngeanza kuagiza mashine mpya hivi sasa, badala ya kusubiri zichakae kabisa, ndipo muanze kufikiria kuagiza.”

Mapema, akitoa taarifa ya mradi huo, Eng. Mchomba alisema awamu ya tatu ya ujenzi wa mradi huo ilisainiwa Mei 18, 2015 kati ya DAWASA na OIA yenye ubia na kampuni ya Pratibha Industries kutoka India kwa gharama ya dola za Marekani milioni 41.36 ambazo zilikuwa ni fedha za mkopo nafuu kutoka benki ya Exim ya India.

“Kazi zilizopangwa kufanyika ni upanuzi wa mtambo wa maji ili kuongeza uzalishaji wa maji kutoka mita za ujazo 500 hadi 900 kwa siku; ujenzi wa mfumo wa mabomba ya kusambaza maji wenye kilometa 1,022; ujenzi wa matenki makubwa 19 ya kuhifadhia maji; vituo tisa (9) vya kusukumia maji (booster stations) na vioski (viula) vya kuchotea maji 351.”

Alisema hadi sasa mkandarasi huyo amekwishalipwa dola za Marekani milioni 15.81 sawa na asilimia 38 na anaendelea na ulazaji mabomba ambapo hadi sasa amekwishalaza mabomba yenye urefu wa km.141 sawa na asilimia 12.4.

Alisema mradi huo umelenga kuvinufaisha vijiji 68 ambavyo 19 kati ya hivyo viko Kaskazini mwa mto Wami na 49 viko Kusini mwa mto huo.

Akizungumzia utendaji kazi wa mkandarasi huyo, Eng. Mchomba alisema Serikali imechukua hatua za kimkataba dhidi yake kwa kumtoza gharama ya kuchelewa kumaliza mradi (liquidated damages) kuanzia Februari 23, 2017.

“Pia mkandarasi amepewa notisi ya siku 100 ya kumtaka aongeze kasi ya kazi, vinginevyo tutasitisha mkataba ifikapo terehe 31 Mei, 2017 kulingana na kipengele namba 8.7 cha mkataba,”alisema.

IMETOLEWA NA:

OFISI YA WAZIRI MKUU,

ALHAMISI, MACHI 30, 2017.

Tundu Lissu Azidi Kumshambulia Magufuli,Safari Hii Amemuibukia Katika Issu Hii!!


Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu akiwa anahojiwa na Mwananchi amezungumzia maswala ya Lipumba na CUF na future ya upinzani

Amedai Lipumba kutumiwa na CCM ni kutawafanya wapinzani waungane kuliko hata mwazoni

Akaziungumzia bajeti amedai kati ya bajeti ya trilioni 29 ambazo 11 ni za fedha za maendeleo imepelekwa trilioni 3 tu, 

Katika fedha za matumizi ya kawaida, Halmasahauri zimepata fedha kidogo kuliko miaka yote,

Amesema takwimu za makusanyo ya matrilioni niza uongo, kwani zingekuwa za kweli fedha zingeonekana katika miradi ya maendeleo , matumizi ya serikali na ajira

Tundu lIssu amesema pia yeye ni wakili na mawakili kwa sasa hivi kazi kubwakwa sasa hivi ni kufunga makampuni kitu kinachoonyesha biashara nyingi zinafungwa

Aliyemtishia Bastola Nape Hakamatiki..Habari kwenye Magazeti ya Leo Ijumaa 31/3/2017..!!!



 

Gallery

Popular Posts

About Us