KINGAZI BLOG: 05/19/17

HABARI KARIBU YAKO ZAIDI.

Breaking News
Loading...

Friday 19 May 2017

Linah apiga dili la Diamond Platnumz

Wakati watoto wa mwanamuziki Diamond Platnumz wakiwa mabalozi wa maduka ya nguo za watoto, mwanamuziki  Linah Sanga anayetarajia kujifungua hivi karibuni amepata ubalozi wa duka la nguo za watoto.

Linah ambaye ni mwanamziki wa nyimbo za kizazi kipya amepata dili hilo la kuwa balozi wa duka la nguo za watoto la Kids City Shopping (KCS), zikiwa zimebaki wiki chache kabla ya kujifungua mtoto wake wa kwanza.

Linah ambaye mapema wiki hii alitambulisha herufi ya mwanzo ya jina la mtoto anayemtarajia baada ya kuweka picha ya ujauzito kwenye ukurasa wake wa Instagram na kuandika ‘Baby T on the way’,anakuwa miongoni mwa mastaa ambao watoto wao wamepata bahati ya kuwa mabalozi.

“Kwa mara ya kwanza nitazungumza na mashabiki wangu mwishoni mwa wiki hii kwa niaba ya KCS ambao ni  wauzaji wa bidhaa mbalimbali za watoto na akinamama wajawazito,” amesema Linah.

Hivi karibuni Linah alizindua wimbo wake mpya ‘Upweke’ na kupita katika vituo mbalimbali vya redio, televisheni na magazeti kwa ajili ya kuutangaza wimbo wake huo mpya.

Mwanadada huyo ambaye hivi karibuni alimtangaza mpenzi wake anayetarajia kuwa baba wa mtoto wake aitwaye Shabani ambaye pia ni bosi wake, Linah amedai kuwa anafuraha kuwa mjamzito kwa kuwa ni kitu ambacho alikuwa akitamani kwa muda mrefu.

“Ninafuraha kubwa kwa sababu ni kitu ambacho kama mwanamke nilikuwa nakitamani siku zote kwamba na mimi nije niitwe mama, nafuraha nimepata mtu sahihi wa kuwa mzazi mwenzangu ambaye nitalea naye watoto,”amesema.

Mzazi mwenzake ambaye pia ni mkurugenzi wa Kampuni Drops Up Entertainment ambayo inamsimamia Linah, amesema wamejipanga kuhakikisha Linah anafika mbali zaidi kimziki.

Aumwa na Nyoka usoni baada ya kujaribu kumbusu

Nyoka huyo anaaminika kutokeka baada ya kisa hicho.

Mwanamume mmoja katika jimbo la Florida nchini Marekani ambaye alijaribu kumbusu nyoka na badala yake nyoka huyo akamuuma, anaendelea kupata matibabu hospitalini.

Nyoka huyo alipatwa na Charles Goff, mkaazi wa kaunti ya Putnam kaskazini mwa jimbo la Florida siku ya Jumatatu.

Siku moja baadaye jirani wake ambaye alitajwa na kituo cha CBS kama Ron Reinold alianza kucheza nyuko huyo kwa kujaribu kumbusu.

Bwana Reinold alisafirishwa kwa njia ya ndege na kwa sasa anaendelea kupata nafuu hospitalini,.

Kijana mmoja alisema, "nitambusu mdomoni," ndipo nyoka huyo akamuuma usoni, bwana Goff alililiambia shirika la habari la Action News Jax.

Kituo cha First Coast News kilisema kuwa muathiriwa alikuwa na fahamu lakini katika hali mbaya.

Nyoka huyo anaaminika kutokeka baada ya kisa hicho.

Haijulikani sababu iliyochangia bwana Reinold ajaribu kumbusu nyoka huyo.

Red Bull Ni Kinywaji Hatari Sana Kwa Afya Yako

RED BULL Huuzwa katika maduka makubwa (Supermarkets) na madogo (Retail Shops) katika nchi ya Tanzania, watu wazima na watoto wengi wana mazoea ya kunywa kinywaji hiki ambacho kinaweza kusababisha kifo. Kemikali zinazopatikana katika kinywaji cha RED BULL zilitengenezwa maalum katika maabara za kijeshi za Marekani kwa ajili ya kutuliza mzuka wa maaskari wao wakati wakitekeleza mauaji ya kikatili sana dhidi ya wananchi wa Vietnam miaka ya sitini na sabini. Kemikali hizo zilitumika pia kama dawa ya kuwazindua watu waliozirai (“stress coma”).

Hazikukusudiwa kutumiwa kama kinywaji au kilevi cha kawaida! Duniani kinywaji hiki
(RED BULL) huuzwa kama kitu cha kuleta msismko (Energizer Drink) na matangazo
yake yanataja sifa zake kama ifwatavyo. “Ni kinywaji kinachompa mtu nguvu ya kustahimili na umakini. Humpa mtu kasi ya vitendo” na kadhalika.

RED BULL imesambaa katika nchi 100 kwa mpigo (nchi masikini!). Na matangazo yake huwalenga vijana na watoto, hasa wanamichezo. Hawa ni rahisi kushabikia kinywaji hiki kibaya na kudhurika kiafya baadaye. Katika hali yake ya matumizi ya sasa kinywaji hiki kiligunduliwa na Mjerumani Dietrich Mateschitz ambaye alikikuta huko Hong Kong kikiwa ni mojawapo ya madawa yaliyotumika katika kutengeneza dawa ya mswaki wa meno.
Dawa hiyo ilitengenezwa kwa kemikali ambazo zina kafeni na taurini (“caffeine and “taurine).

Mjerumani huyo aliona vijana wajinga wa huko wakishabikia unywaji wake akaona mwanya wa kufanya biashara na akafanikiwa kukileta ulaya. ATHARI ZA KUNYWA RED BULL Kinywaji kinachotengenezwa na kusambazwa leo hii kina kemikali mbaya iitwayo “Glucuronolactone”, kemikali hatari ambayo ilitengenezwa na idara ya jeshi la Marekani wakati wa vita na Vietnam kwa ajili ya kutuliza mvurugiko wa mawazo wa maaskari wake uliotokana na mauaji ya kinyama waliokuwa wanafanya huko Vietnam.

Kwa sababu ya madhara makubwa ya kinywaji hiki nchi za FRANCE na DENMARK zimepiga marufuku kinywaji hiki na kibatiza jina la “MKOROGO WA UMAUTI”. Katika nchi hizi, utafiti uligundua kuwa maaskari wa Marekani waliotumia kinywaji chenye
kemikali ya “GLUCURONOLACTONE” waliishia kupata madhara ya maumivu makali ya kichwa, uvimbe wa ubongo na hata ugonjwa wa ini (Migraines, Cerebral tumours and liver diseases).

Na kwa sababu hiyo wamarekani waliacha kuwapa maaskari wao hicho kinywaji katika miaka ya sitini na sabini. Jambo la kushangaza ni kuwa lebo ya RED BULL inaonyesha wazi kuwa kinwaji hiki kimetengenezwa kwa kemikali hatari ya “GLUCURONOLACTONE”! Ni kwa sababu hiyo serikali za Denmark na Ufaransa nazo zikapiga marufuku unywaji wa RED BULL. Pamoja na wauzaji wa RED BULL kuweka bayana kuwa ndani mwake mna hiyo kemikali hatari ya “GLUCURONOLACTONE” lebo ya RED BULL hailezi madhara makubwa yanayoletwa na kemikali hiyo.

Madhara ambayo hayakuwekwa bayana kwa mnywaji ni kama yafuatayo:

1. Ni hatari kwa mtu ambaye hafanyi kazi au mazoezi mazito sana kukitumia kwani kina tabia ya kuongeza msukumo wa damu na kasi ya mapigo ya moyo kiasi kwamba mtumiaji anaweza kupatwa na ugonjwa wa moyo.

2. Mtumiaji anaweza kupatwa na ugonjwa wa damu kuvuja ubongoni kwani RED BULL ina kemikali zinazoifanya damu iwe nyembamba ili moyo upate kusukuma damu nyingi bila kutumia nguvu nyingi.

3. Ni hatari kuchanganya RED BULL na pombe ya aina yoyote kwani mchanganyiko wake huwa ni sumu (“Deadly Bomb”) inayoathiri musuli za ini la mtumiaji na kuiacha katika hali ambayo haitapona kamwe.

4. RED BULL Ina vitamini B12 kwa wingi, vitamini ambayo hutumiwa kama dawa ya kuwazindua wagonjwa mahututi. Matumizi ya vitamini hii katika watu wazima ina athari za kuleta shinikizo la damu na humfanya mtu ajisikie kama mlevi.

5. Unywaji wa RED BULL mara kwa mara huvuruga mfumo ya neva za fahamu na husababisha maradhi mithili ya mfadhaiko wa akili usioponyeka.

HITIMISHO:
RED BULL ni kinywaji HATARI SANA ambacho hapana budi kipigwe marufuku katika nchi zote zinazoendelea kwani ni dhahiri kimetengenezwa na kusambazwa ili kiathiri afya za wananchi wasiojiweza wa nchi hizi masikini. Kwa kuwa wengi katika nchi hizi hutumia pombe za kila aina ni wazi kuwa kinywaji hiki kinalenga kuwamaliza watu watu wetu– kana kwamba ukimwi uliobuniwa na hao wabaya wetu hautoshi!

Hii hapa siri kubwa kuhusu Yamoto Band kupotea Aslay afunguka.

Msanii Aslay ambaye hivi sasa ameanza kufanya kazi peke yake nje ya kundi la Yamoto band amefunguka na kusema kundi hilo hapo katikati walikwama na ndiyo maana walirudi nyuma badala ya kusonga mbele zaidi. 

Aslay anasema kipindi cha nyuma walikuwa wanapata show nyingi sana jambo ambali lilipelekea kuwa na uwezo wa kufanya video kubwa hata nje ya nchi lakini baadaye mambo yalibadilika na kupelekea kufanya video zao hapa hapa bongo. 

"Mimi nafikiri kwamba mipango yetu tu wenyewe, kipindi kile tunatoa ile video ' Madoido' kulikuwa na show nyingi zinaongozana ambazo zilituzuia kwenda kutengeneza video nyingine lakini si unajua tulikuwa tunajenga pia kwa hiyo kifupi ni kama tulijisahau na kuteleza kusema ukweli. Tukarudi tena tukafanya 'Suu' ambayo tuliifanya Zanzibar na tukawa na pesa kabisa ambayo ingetuwezesha kutengeneza video nyingine Afrika Kusini lakini hapo katikati tulifanya vitu fulani mchanganyiko ambavyo siwezi kuvisema vikaturudisha tena nyuma"alisema Aslay 

Mbali na Aslay msanii mwingine kutoka kundi hilo Beka Flavour naye ametoka na wimbo wa peke yake akiwa chini ya menejimenti nyingine. 

Makalio yangu ni Orijino sio mchina - Snura


Msanii wa bongo fleva Snura Mushi maarufu kama Malkia wa uswazi mwenye 'hit song' ya 'nionee wivu' amefunguka na kudai hajawahi kutumia dawa za kichina za kuongeza makalio kama watu wanavyomwambia bali umbo lake ni 'original'.

Snura amesema hayo kupitia eNewz kutoka EATV baada ya watu wengi kuamini mwanadada huyo anatumia dawa za kuongeza maungo yake ya mwili kama baadhi ya wanawake wengine wa mjini wanavyofanya ili waweze kuwapata kuwanasa wanaume kiuwepesi zaidi.


“Nina utofauti kidogo jinsi nilivyoumbwa mimi kiukweli ukiacha hiyo shepu yangu watu wanayoiongelea …Mimi ukiniangalia tu unajua tu ni ‘Original’ kwa sababu kwanza naweza kuongeza kalio kwa kuliongeza lakini je na nilivyokatika ? naweza kuchukua kisu nikajichimba, mimi nilivyo hapa katikati nimetumbukia kabisa yaani nimegawa mgongo pekee yake na chini peke yake". Alisema Snura

Kutana na Mama aliyejifanya mwanaume ili afanye kazi mgodini Tanzania

Pili Hussein alitamani kujiimarisha kimaisha na mawe ya thamani yanayosemekana kuwa nadra mara elfu mia moja kuliko almasi, lakini kwa kuwa wanawake hawakuwa wanaruhusiwa kwenye migodi hiyo alivalia mavazi kama mwanamume na kuwadanganya wafanyikazi wenzake kwa zaidi ya mwongo mmoja.

Pili alilelewa katika familia kubwa mjini Tanzania. Mtoto wa mchugaji ambaye aliyekuwa na mashamba makubwa, babake Pili alikuwa na wake sita na alikuwa miongoni mwa watoto 38.

Licha ya hayo yote alilelewa vyema kwa njia tofauti.

''Babangu alinichukulia kama mwanamume na nilikuwa nikichunga mifugo yake, lakini sikuyapenda maisha hayo kabisa'', alisema.

Hata ndoa yake haikuwa ya furaha, akiwa na umri wa miaka 31 Pili aliikimbia ndoa yake iliyokumbwa na migogoro ya kinyumbani.

Alipokuwa akitafuta ajira alijipata katika mji mdogo wa Mererani, Tanzania, uliopo chini ya mlima mkuu wa Kilimanjaro.

Eneo hilo ni maarufu sana duniani kwa kuwa na madini nadra ya rangi ya samawati ya tanzanite.

''Sikwenda shule , kwa hivyo sikuwa na mambo mechi kuchagua,'' Pili alisema.

''Wanawake wahakuruhusiwa kwenye maeneo ya migodi hiyo, nikajitosa kama mwanamume shupavu na mwenye nguvu. Nilichukua suruali ndefu na kuzikata zikawa kama kaputula ili kufanana na mwanamume. Hivyo ndivyo nilivyofanya.''

Ili kukamilisha mabadiliko yake , alibadilisha pia jina lake.

''Niliitwa Uncle Hussein {akimaanisha mjomba Hussein}, sikumwambia yoyote kuhusiana na jina langu halisi la Pili.

Hata leo ukija katika kambi hiyo utanitafuta kwa jina hilo la Uncle Hussein.''

Kwenye migodi hiyo yenye joto ,uchafu mwingi na wenye kina cha mita mia moja chini ya ardhi Pili angefanya kazi kwa saa 10-12 kwa siku , akilima na kuchunga akiwa na matumaini ya kupata mawe hayo ya thamani kwenye mishipa ya mawe hayo ya grafiti.

''Ningeenda hadi mita 600 chini ya mgodi, mara kwa mara nikiwa shupavu kuliko wanaume wengine.

Nilikuwa na nguvu nyingi na niliweza kufanya kazi kama matarajio ya wanaume wengine wangefanya.''

Pili amesema hakuna aliyemshuku alikuwa mwanamke.

''Nilijifanya kama nyani aina ya Gorilla'' alisema, Nilipigana, lugha yangu ilikuwa mbaya , nilibeba kisu kikubwa kama Maasai.

Hakuna mtu alifahamu kwamba mimi ni mwanamke kwa sababu kile nilichokuwa nikifanya nilikifanya kama mwanamume.''

Baada ya mwaka mmoja, alipata utajiri , alipopata mawe mawili makubwa ya Tanzanite. Kutokana na pesa alizozipata alimjengea babake, mama na pacha wake nyumba mpya na akajinunulia vifaa zaidi na akaanza kuajiri wachimba migodi kumfanyia kazi.

Na kujificha kwake kuliwashawishi kwamba alichukua hatua zisizo za kawaida kwa utambulisho wake kujulikana.

Mwanamke mmoja aliripoti kwamba alikuwa amebakwa na wachimba migodi Pili akiwa miongoni mwa washukiwa.

''Polisi walipokuja, wanaume waliotekeleza ubakaji huo wakasema: 'Huyu ndio mwanamume aliyetekeleza hilo'' na nilipopelekwa katika kituo cha polisi , Pili akasema alikuwa hana namna bali kutoboa siri yake.''

''Aliwauliza polisi kumleta polisi mwanamke ili amchunguze kwamba yeye hakutekeleza kitendo hicho na baadaye aliachiliwa huru. Hata baada ya hilo wachimba migodi wenzake waliona vigumu kuamini walikuwa wamedanganyika kwa siku nyingi''.

''Hawakuamini hata polisi waliposema kwamba alikuwa mwanamke," alisema, ''haikuwa rahisi kwao kukubali hadi mwaka 2001 nilipoolewa na nikaanza familia.''

Kutafuta bwana wakati kila mtu amenizoea kama mwanamume haikuwa rahisi, Pili alipata bwana na akafanikiwa.

Swali lililokuwa akilini mwake lilikuwa,'je ni mwanamke kweli?'' anakumbuka. ''ilimchukua miaka mitano ndipo aliponikaribia.''

Pili aliikuza taaluma yake na hivi leo anamiliki kampuni yake ya migodi ambayo ameajiri wachimba migodi 70 , watatu kati yao ni wanawake, lakini wanafanya kazi ya upishi.

Pili amesema licha ya kwamba kuna wanawake wengi katika makampuni ya migodi kuliko wakati wake, hata leo ni wanawake wachache wanaofanya kazi kwenye migodi hiyo.

''Wanawake wengine huyaosha mawe hayo , wengine ni wakala na wengine ni wapishi'' , alisema, ''lakini hawaingii ndani ya migodi , si rahisi kumpata mwanamke akifanya nilichofanya wakati wangu.''

Mafanikio ya pili yamemuezesha kuwalipia karo watoto wa ndungu zake 30 na wajukuu. Licha ya hayo amesema hawezi kumrai mwanawe kufuata nyayo zake.

''Najivunia kwa kile nilichokifanya, imenifanya tajiri lakini ilikuwa vigumu kwangu'', amesema.

''Nataka kuhakikisha mtoto wangu ataenda shule apate elimu na ataweza kujiendeleza kimaisha kwa njia tofauti mbali na nilivyopitia.''

MRISHO Gambo: Serikali Itaendelea Kuwadhibiti Wote Watakaotaka Kuingiza Siasa Kwenye Majanga


Serikali mkoani Arusha imewataka wananchi na taasisi zinazoendelea kutoa rambirambi kwa familia za wanafunzi waliofariki katika ajali ya basi la wanafunzi kufuata taratibu zilizowekwa ili kuepusha migongano isiyo ya lazima. Aidha amesema serikali itaendelea kuwadhibiti wote watakaotaka kuingiza siasa kwenye majanga likiwemo la vifo vya wanafunzi na amesisitiza umuhimu wa kila mmoja kufuata sheria taratibu na maelekezo yanayotolewa na serikali.

Nape Nnauye afunguka kuhusu ukimya wa Kinana, Mwenendo wa shughuli za Bunge pamoja Polisi Kutumia Nguvu Kubwa

Na Regina Mkonde 

 Mbunge wa Jimbo la Mtama, Nape Nnauye amefunguka kuhusu masuala mbalimbali ikiwemo, ukimya wa Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, muenendo wa shughuli za Bunge pamoja na tukio lililotokea hivi karibuni la Askari Polisi mmoja wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) kufyatua risasi hewani mbele ya aliyekuwa Naibu Waziri wa Fedha, Adam Malima baada ya kutokea majibizano yaliyosababishwa na dereva wa Malima kuegesha gari vibaya.

Nape amefunguka hayo jana  jijini Dar es Salaam, wakati akizungumza na wanahabari ambapo alisema, Kinana ambaye baadhi ya watu wanadai kuwa ukimya wake umetokana na kujiuzulu, yuko katika wadhifa wake wa ukatibu mkuu na anaendelea kufanya kazi za chama.

“Mimi sio msemaji wa chama, lakini Katibu Mkuu yupo na anafanya kazi yake kama kawaida…., mimi bado ni mwanachama na muumini mzuri wa CCM inayopenda haki, na nina amini hiki ndicho chama pekee bora kitakachoweza kuwakomboa watanzania pamoja na kuamiwa ikiwa kitatekeleza mkataba wake na wananchi ambao ni wa kutimiza ahadi zake ilizo ziahidi,” alisema.

Kuhusu tukio la Askari Polisi kufyatua risasi hewani, ambalo Kamishna wa Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamanda Simon Sirro alisema ulikuwa uamuzi wa busara wa kuondoa taharuki katika tukio hilo, na mbinu ya kuwatia nguvuni watuhumiwa.

Nape alishauri vyombo vya dola kutotumia nguvu kwani kitendo hicho kitajenga hofu na chuki baina ya serikali na wananchi na hata kwa chama tawala CCM, huku akiisihi serikali kuondoa vitendo vinavyotia hofu wananchi.

“Ni vizuri vyombo vya dola vikatimiza majukumu yake kwa kuwa ni vyombo vya wananchi, si vizuri vikitumia nguvu kubwa pale isipostahili. Ifikie hatua raia asiye na silaha Polisi wasitumie nguvu kushughulika naye kwa kutumia silaha. Nimeona ile video ikionyesha Malima alikuwa anauliza chanzo cha tatizo,”alisema na kuongeza.

“Kuna nchi tamaduni zake ni kutumia mabavu na nyingine zinatumia demokrasia, nchi yetu utamaduni wake si wa kutumia nguvu, tumezoea kuelewana kwa mazungumzo. Vyombo vya dola visitumie nguvu kwa kuwa tunajenga usugu usio na maana. Na kama kuna mazingira hatarishi basi nguvu itumike.”

Kuhusu mienendo ya shughuli za Wabunge Bungeni, aliwataka wabunge kutekeleza majukumu yao ikiwemo kuwawakilisha na kusimamia vema masilahi ya wananchi wanaowawakilisha, pamoja na kuisimamia serikali kutekeleza vizuri majukumu yake.

“Bunge ni mkutano wa wananchi, na wabunge wapo kwa niaba ya wananchi katika kupitisha na kushauri mipango ya serikali. Ni vizuri wasimame katika maeneo yao, wasiwe wapiga makofi, pale serikali inapofanya vizuri ipongezwe na inapofanya vibaya ikosolewe,” alisema.

Kuhusu Uhuru wa Vyombo vya Habari, alisema ifikie hatua wananasiasa wawe na ngozi ngumu ya kuvumilia kukosolewa  na watu kupitia vyombo vya habari. Pia ameshauri wananchi wanaotaka maonesho ya vikao vya bunge moja kwa moja, kuuomba mhimili huo kubadilisha sheria zake ambazo zimeipa mamlaka ya kuamua namna ya kuendesha shughuli zake.

“Naamini uamuzi wa siku ile wa kuzuia shughuli za bunge live ulikuwa sahihi sababu sheria zinasema Bunge litaendeshwa kwa sheria zake. Wananchi wanaozungumzia Bunge live, waliombe libadilishe sheria zake ili lianze kuonyeshwa live,” alisema


Mgahawa Wakumbwa na Kashfa ya Kuuza Nyama ya Binadamu

Mgahawa wakumbwa na habari bandia za kuuza ''nyama ya binadamu''

Mgahawa mmoja mjini London umekumbwa na habari bandia za kuuza nyama ya mtu.

Wafanyikazi katika mkahawa wa Karri Twist katika eneo la New Cross nchini Uingereza wamehangaishwa kwa kupigiwa simu kutoka kwa wateja wanaosema ''Kwa nini hamujafunga''?.

Mkahawa huo wa chakula cha jioni ni mwathiriwa wa habari za mzaha zilizodai kwamba mmiliki wake alikamatwa kwa kuweka nyama ya binadamu katika chakula na kwamba miili 9 ilipatikana katika jokovu la mkahawa huo.

Na watu wengine waliamini mzaha huo.

Habari hiyo ilichapishwa katika chombo cha habari cha channel23news.com, mtandao ambao wateja wake wanaweza kuchapisha habari za uwongo ili kuwafanyia mzaha rafiki zao kwa kuchapisha moja kwa moja katika mtandao wa fecbook.

Shinra Begum ambaye ndio mmiliki wake aliambia Newsbeat kwamba biashara hiyo ya familia imekumbwa na wakati mgumu tangu habari hiyo ilipochapishwa siku ya Alhamisi.

''Wakati watu walipoanza kunipigia simu na kuuliza iwapo tulikuwa tukiuza nyama ya binadamu sikuamini''.

''Nilishtuka nilipoaana habari hiyo katika mtandao na kuendelea kusambazwa katika mtandao wa facebook''.

Sasa watu wametishia kulivunja jengo letu na nimelazimika kuketi chini na mteja ili kumuelezea kwamba yote hayo ni madai ya uwongo.

Shinra anasema kuwa alilazimika kuripoti kwa maafisa wa polisi kwa sababu lilikuwa swala lililomtia wasiwasi mkubwa.

Njia ya pekee ambapo Karri Twist iliweza kukabiliana na chuki hiyo ni kupitia kuchapisha katika mtandao wao ili kuhakikisha kwamba watu wanajua kwamba hilo halikuwa la kweli.

PICHA ya Nusu Utupu ya ‘Ben Pol’ Yachafua Hali ya Hewa Mtandaoni..!!!


Msanii wa Bongo Fleva, Ben Pol amejikuta akizua minong’ono kwa mashabiki wake na watanzania kiujumla baada ya kuposti picha akiwa nusu utupu kwenye ukurasa wake wa Instagram .

Kwenye picha hiyo Ben Pol hakuweka maneno yoyote yale lakini alionekana amefungwa na kamba kama mtu aliyetekwa.

Picha hiyo iliyowekwa jana usiku mpaka sasa ina maelfu ya likes na Maoni kibao ya mashabiki wake wengi wakionekana kukerwa na kitendo hicho.

Pitia maoni ya wadau hapa chini



NAFASI ZA MASOMO KWA NGAZI YA CERTIFICATE/CHETI NA DIPLOMA CHUO KIKUU -SUA - MOROGORO



Application for Admission into Non-Degree Programs 2017/2018

Sokoine University of Agriculture (SUA) invites applications from qualified Tanzanians and non-Tanzanians to certificate and diploma programs offered by Sokoine University of Agriculture for academic year 2017/2018. Applicants should apply directly to SUA by filling in online application forms or physically submit the forms to the admission office,...


MPYA : TANGAZO MAALUMU KWA WANAFUNZI WOTE WA UDOM

MPYA: KUFUNGULIWA KWA UDAHILI KWA NGAZI YA JUU KABISA YAANI POSTGRADUATE PROGRAMMES KWA MWAKA 2017/18 CHUO KIKUU CHA UDOM

 

Gallery

Popular Posts

About Us