KINGAZI BLOG: 04/13/17

HABARI KARIBU YAKO ZAIDI.

Breaking News
Loading...

Thursday 13 April 2017

MPYA: Hii hapa Orodha ya majina ya Walimu wa Sayansi na vituo vya kazi walivyopangiwa

Serikali kupitia Ofisi ya Rais TAMISEMI imetangaza ajira mpya kwa Walimu wa masomo ya Hisabati na Sayansi leo tarehe 12 Aprili, 2017.

Majina ya Walimu yaliyotangazwa yanatokana na tangazo la nafasi ya kazi ya Ualimu lililotolewa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia mnamo tarehe 01 Desemba, 2016.

 

Jumla ya Walimu wapya wapatao 3,081 wakiwemo 1,544 ni wa ngazi ya Shahada na Walimu 1,537 ni wa Stashahada.

 

Walimu hao watatakiwa kuripoti kwenye Ofisi za Wakurugenzi wa Halmashauri na baadaye kwenye Shule walizopangiwa kuanzia tarehe 18 Aprili, 2017 hadi tarehe 25 Aprili, 2017. Walimu wote waripoti wakiwa na vyeti halisi vya taaluma vya kidato cha nne (IV) na kidato cha sita (VI), vyeti halisi vya kitaalaam vya kuhitimu mafunzo ya Ualimu ngazi ya Stashahada na Shahada na Cheti cha kuzaliwa.

 

Angalizo :

i. Walimu waliopangiwa vituo ni wa masomo ya Hisabati na Sayansi waliohitimu hadi mwaka 2014/2015.

ii. Kituo cha kazi cha mwalimu ni shule aliyopangiwa na sio makao makuu ya Halmashauri.

 

iii. Mwalimu atakayeripoti na kuchukua posho ya kujikimu na baadae kuondoka atachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria.

 

iv. Walimu wote watakiwa kuripoti katika vituo vyao kuanzia tarehe 18 Aprili, 2017 hadi 25 Aprili, 2017, watakaochelewa nafasi zao zitajazwa na mwalimu mwingine.

 

v. Hakutakuwa na uhamisho ndani ya Mkoa au Halmashauri.

Majina ya Walimu hao yanapatikana katika tovuti ya Ofisi ya Rais-TAMISEMI ya www.tamisemi.go.tz

 

Imetolewa na:

Katibu Mkuu

Ofisi ya Rais TAMISEMI

==>Orodha ya Walimu wa Shahada wa Ajira Mpya kwa Masomo ya Sayansi na Hisabati.

<<Bonyea hapa kudownload>>

==>Orodha ya Walimu wa Ajira Mpya kwa Masomo ya Sayansi na Hisabati.

<<Bonyeza  Hapa  Kuya Download>>

Uliipata hii ya Mwana FA kupigiwa simu na Rais Magufuli

Rais Dkt John Magufuli ni shabiki wa muziki wa Mwana FA. Na ndio maana ameamua kunyanyua waya na kumpigia simu rapper huyo kumwambia kuwa ni msikilizaji mzuri wa ngoma zake.

Cha kuvutia zaidi, Rais amemweleza FA kuwa wimbo anaoupenda ni Dume Suruali aliomshirikisha Vanessa Mdee.

“Nimefurahi kupokea simu ya Mheshimiwa Rais @MagufuliJP kunisalimia na kuniambia yeye ni mpenzi wa kazi zangu,haswa #DumeSuruali,” ametweet Mwana FA.

“Utoe heRa kwani ina tv ndani?” (in his voice) 😀😂…,” ameongeza

Bashe Awavuruga Vigogo CCM..Wahaha Kumzima HarakaHaraka..Habari Vichwa vya Magazeti ya Leo 13/4/2017..!!!





























 

Gallery

Popular Posts

About Us