KINGAZI BLOG: 09/09/16

HABARI KARIBU YAKO ZAIDI.

Breaking News
Loading...

Friday 9 September 2016

Picha 17: JAMAA ANAYEDAIWA KUFANYA MAPENZI NA WAKE ZA WATU KICHAWI SHINYANGA AKAMATWA,ASHUSHIWA KIPIGO


Wananchi wenye hasira kali katika kijiji cha Bugayambele kata ya Kizumbi katika manispaa ya Shinyanga wamemshushia kichapo jamaa anayedaiwa kuwaingilia wanawake nyakati za usiku kisha kufanya nao mapenzi kwa njia za kishirikina. 

Tukio hilo limetokea leo majira ya saa kumi jioni ambapo wakazi wa kitongoji cha Bugayambelele jirani na kijiji cha Nhelegani kilichokumbwa na taharuki ya kuwepo mtu anayefanya mapenzi na wake za watu kimazingara,walimshtukia jamaa huyo baada ya kuonekana akifanya vitendo walivyodai kuwa vya kishirikina katika familia mbili za kitongoji hicho. 

Malunde1 blog baada ya kupata taarifa za kuwepo kwa tukio hilo ilifika eneo la tukio haraka zaidi na kushuhudia umati mkubwa wa watu ukiwa umemzingira jamaa huyo huku askari polisi wakiwa eneo la tukio kuzuia wananchi wasiendelee kumshushia kipigo jamaa huyo. 

Wakazi wa eneo hilo walisema mtu huyo aliingia kwenye nyumba mbili(kaya mbili) bila kupiga hodi huku akidai kuwa alikuwa anatafuta mke wake, akidai kuwa ametoka kwa mganga wa kienyeji kaelekezwa kuwa mke wake yupo eneo hilo. 

Hata hivyo baada ya kumtilia mashaka jamaa huyo alianza kukimbia na kutupa simu zaidi ya tatu za mkononi alizokuwa nazo,wananchi wakafanikiwa kumkamata kisha kumpeleka kwenye mkutano wa sungusungu na walipompekua wakamkuta na dawa za kienyeji zinazodaiwa kuwa za mapenzi,zikisomoka kama ifuatavyo; 

“Imala yose -kuchoma kuomba mke wako roho yake irudi kwako akupende” na nyingine maandishi yakisomeka kuoga na kuchoma kuomba mkeo akupende na arudi kwako”.
Wakazi wa eneo hilo walisema kutokana na maelezo yake,pia kuingia katika familia moja bila hodi huku akidaiwa kupotea kimiujiza eneo hilo na kuibukia katika familia nyingine pamoja na dawa za kienyeji alizokuwa nazo walimhusisha moja kwa moja na tukio la ubakaji kwa njia za kishirikina.

Mwenyekiti wa kitongoji cha Bugayambelele Donald Francis alisema alipigiwa simu na kuelezwa kuwepo kwa mwanamme anayehusishwa na tukio la kubaka wanawake kishirikina katika kijiji jirani cha Nhelegani kata ya Kizumbi.
Alisema mwanamme huyo alikutwa na dawa za kienyeji huku akitoa maelezo yasiyoeleweka ikiwemo kudai amefika hapo kwa ajili ya kutafuta kazi ya kufyatua matofali,kutafuta mke wake na anatoka kwa mganga wake wa kienyeji aliyemnyweshwa dawa za ajabu.
Tutawaletea taarifa kamili hivi punde.... 

Mwanamme aliyejitambulisha kwa jina la Shaban Charles kutoka Kitangiri katika manispaa ya Shinyanga anayedaiwa kujihusisha na vitendo vya kubaka wanawake kishirikina nyakati za usiku-Picha na Kadama Malunde-Malunde1 blog

Polisi wakiwa eneo la tukio


Wananchi wakiwa eneo la tukio

Dawa za kienyeji alizokutwa nazo jamaa huyo

Dawa za kienyeji za jamaa pamoja simu yake

Dawa za kienyeji

Polisi na wananchi wakiwa wamemzunguka jamaa huyo

Mwandishi wa habari wa Radio Faraja Steve Kanyeph akifanya mahojiano na jamaa huyo

Wananchi wakiwa eneo la tukio

Wananchi wakiwa eneo la tukio

Gari la polisi likiwasili eneo la tukio


Jamaa akipanda kwenye gari la polisi

Baiskeli ya mtuhumiwa ikipandishwa kwenye gari la polisi


Polisi wakiondoka na mtuhumiwa

Wananchi wakiondoka eneo la tukio
Mwenyekiti wa kitongoji cha Bugayambelele Donald Francis akizungumza na waandishi wa habari ambapo alisema alipigiwa simu na kuelezwa kuwepo kwa mwanamme anayehusishwa na tukio la kubaka wanawake kishirikina katika kijiji jirani cha Nhelegani kata ya Kizumbi.

YALIYOJIRI KUTOKA BUNGENI MJINI DODOMA LEO

Waziri wa Habari, Utaamduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye (MB) akiwaeleza jambo Mbunge wa Jimbo la Iringa Mjini Mhe. Peter Msigwa (Katikati)na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (TAMISEMI) Mhe. George Simbachawene wakati wa kikao cha bunge leo Mjini Dodoma.

Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson akiongoza kikao cha bunge leo Mjini Dodoma.

Naibu Waziri Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, wazee na Watoto Dkt. Hamis Kigwangalla akijibu swali wakati wa kikao cha bunge na kuahidi kuwa serikali kuendelea kuboresha huduma za afya katika hospitali nchini ikiwemo upatikanaji wa madawa na vifaa tiba.

Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo akiwaeleza wabunge mipango ya serikali kuendelea kushughulikia changamoto za nishati ya umeme nchini hasa katika maeneo ya Lindi na Mtwara

Baadhi ya Wabunge wakiingia katika ukumbi wa bunge mapema leo.

Naibu Waziri Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji akijibu swali kwa wabunge ambapo alisema kuwa Serikali inafanya kila jitihada ya kuwaongezea uwezo katika watendaji wake ili kuendana na mabadiliko ya teknolojia nchini. 

Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Mhe. Charles Tizeba akieleza bungeni leo kuhusu hali ya chakula nchini na kuwahakikishia watanzania kuwa nchi ina utoshelevu wa chakula kwa zaidi ya asilimia 123 kwa mazao ya nafaka na 140.

 PICHA NA HASSAN SILAYO-MAELEZO 

Mambo 10 Ambayo Mwanaume Hupenda Kusikia Toka Kwa Mpenzi Wake

10. Kukosolewa – “I think you are wrong”

Wanaume wanaweza kujikweza sana lakini daima hawachukii kurekebishwa. Wanachojali zaidi ni jinsi gani au njia gani imetumika kuwarekebisha. Mwanaume akikosea, anataka mpenzi wake amkosea lakini kwa mapenzi, sio kwa mikwaruzano au dharau au mbele ya kadamnasi. Mrekebishe au mkemee faragha, toa maoni yako na wala usimlazimishe, itamfanya aone unajali na unataka kumjenga.

9. Kujali – “How was your day?”

Wanawake wengi hutaka wao tu ndio waulizwe kuhusu jinsi siku zao zilivyoenda kila siku, wanasahau kabisa hata wanaume nao walikua kwenye mihangaiko. Mzoeshe kumuuliza mpenzi wako siku yake ilikuwaje? utaona hata nuru ya mapenzi yenu itang’aa na mtakua marafiki, japo mwanzoni atakua hakuambii kila kitu lakini baada ya muda atazoea. Kila mtu anataka wa kumsikiliza, mtu atakayezungumza nae chochote kilichotokea ndani ya siku yake, na pengine kukuuliza ushauri.

8. Ucha Mungu – “Can we pray?”

Mwanaume, anayesali au kutosali, lazima huwa ana imani kwamba Mungu yupo. Mwanamke mcha Mungu siku zote huwa ni wazo la kila mwanaume endapo ana mpango wa kuoa. Mwanaume huwa na amani kwa kiasi fulani akiongozwa na mwanamke wake kwa upande huo wa sala.

7.  Msamaha – “I forgive you”

Vikombe kwenye sahani havikosi kugongana, vivyo hivyo na kwa wapenzi, kuumizana hisia hakuepukiki, iwe kwa makusudi au bahati mbaya, mwenzio akikosea sasa isiwe ndo adhabu, akiomba msamaha ukamwambia nimekusamehe na kweli umemsamehe, funika kurasa endeleeni na maisha. Usililete tena mezani jambo ulilosema umesamehe.

6. Sifa – “That was great sex”

Kama amefanya kazi nzuri, mwambie. Wote tunajua sio kila siku watu hufanya kiwango che Maradona au Pele, siku akiwa kwenye kiwango hicho hata yeye anajua, usisite kumpa sifa zake. Wazungu wanasema, ‘Yes, you can kiss and tell some of the times’. Na kama unaona kuna sehemu anahitaji kujisogeza, mwambie pia, tena kimahaba. Hii itawasaida nyote.

5. Upekee  – “I admire you. No other man is like you”

Ni kweli kwamba kuna wanaume ambao ni wazuri na wenye uwezo mkubwa zaidi ya huyo ulienaye, lakini kwake hujisikia vyema zaidi ukimwona yeye ni zaidi ya wote hao. Sio mbele ya macho yake tu, matendo yako na hata nyuma yake msifie kwamba yeye ndio mwanaume pekee duniani unayempenda na hakuna mwingine zaidi yake.

4. Uaminifu – “I trust you”

Mwanaume akijua anaaminika sana kwa mwanamke, na yeye hujiachia. Na kwa hili huwa anaweza kugombana na watu kabisa kwa ajili ya mwanamke wake. Japo wengine hulitumia hili kwa uchafu wao lakini wengi wao ni kitu chema kwao.

3. Mapenzi –  “Make love to me”

Ni mtazamo wa wengi kwamba mwanaume ndio siku zote awe mwanzilishi wa tendo. Lakini mwanaume kwa wakati mwingine hupenda mwanamke wake ampe vishawishi na yeye vya kumleta kwenye mood. Sio kila siku aanze yeye tu, wakati tendo ni la kuwafurahisha wote. Hata kama ni ngumu kusema kwa mwanamke, ishara kibao zipo za kumuonyesha mwenzi wako akaona ‘Leo baby anataka na yeye’.

2. Malengo -“What’s your dream?”

Mwanaume anaweza asionyeshe kama anahitaji msaada, lakini kwa kutumia njia za mapenzi, unakuta ni mwanaume tu anayehitaji uwepo  wa mwanamke anayempenda yeye. Mungu alimtengeneza mwanaume na kumpatia msaidizi kwa kumpatia mwanamke. Kuwa mwanamke mwenye msimamo na mpangilio mahiri usiotikisika, ambaye unauwezo wa kumuuliza anaenda wapi katika maisha yake, na akakukumbusha huko siko ni huku. Ndoto za mwanaume mara nyingi huendana na zile na mwenzi wake, na mwanamke huwa pale kuhakikisha ndoto za pamoja zinatimia.

1. Upendo wa dhati – “I love you”

Wanaume wengi hujiona wagumu kwenye kutamka neno ‘I love you’ kwa wanawake zao na hata akisema itakua ni mara chache chache hata kama kweli kutoka moyoni wanapenda, lakini haina maana hawataki kuambiwa na watu wanaowapenda, hii huwaaminishia nafasi yao kwenye moyo wa mwanamke.

Aje ya Alikiba yapata shavu MTN

Wimbo wa Aje wa Alikiba umepata shavu kwenye mtandao wa simu wa MTN wa nchini Nigeria.

Aje umekuwa miongoni kati ya nyimbo zinazopatikana kwenye mtandao huo ambao wananchi wanaweza kuuchagua wimbo huo kuwa kama muito kwenye simu zao.

Hatua hiyo itamwezesha staa huyo kuendelea kuingiza mkwanja kulingana na mikataba yake aliyosaini ikiwemo ule wa Sony Music aliosaini mwezi Mei mwaka huu.

Msafara wa Makamu wa Rais Wapata Ajali Mtwara


WATU wanne wajeruhiwa leo baada ya gari moja lililokuwa kwenye msafara wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Bi. Samia Hassan Suluhu kutoka Mtwara kwenda wilayani Tandahimba kuanguka maeneo ya Nanguruwe mkoani humo.

Operesheni Dadapoa, Kakapoa Dar es Salaam Yashika Kasi

JESHI la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limesema linafanya operesheni ya kuwakamata wamiliki wa nyumba za kulala wageni wanaofanya biashara kinyume cha sheria.

Taarifa iliyotolewa na Kamishna wa Kanda hiyo, Simon Sirro, ilisema wamebaini baadhi ya nyumba za kulala wageni zinatumika kuhifadhi magenge ya majambazi na wahalifu wengine.

Alisema nyumba hizo zimekuwa zikitumiwa na wanawake na wanaume wanaofanya biashara ya kuuza miili yao maarufu ‘dadapoa’ na ‘kakapoa’.

“Ni wajibu wa Polisi kufanya ukaguzi wa mara kwa mara kwenye nyumba za kulala wageni, hoteli, migahawa, vilabu vya vileo, kumbi za starehe zinazokesha na zisizokesha na watakaobainika kuvunja sheria hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao,” alisema.

Katika hatua hiyo, Kamishna Sirro aliwatahadharisha wafanyabiashara wa nyumba hizo kufuata utaratibu wa kupokea wageni kwa kuandika majina yao kwenye vitabu, namba za vitambulisho vyao na sehemu wanapotoka na pale watakapomtilia shaka mteja yeyote watoe taarifa kituo chochote cha polisi.

Aidha wenyeviti wa Serikali za mitaa na wajumbe wa nyumba kumi wametakiwa kuwajibika na kuwatambua wageni wote wanaoingia kwenye himaya zao na kuwachukulia hatua stahiki  kwa lengo la kuimarisha ulinzi ndani ya jiji la Dar es Salaam.

Hata hivyo Kamanda huyo aliwataka wageni wanaotoka mikoani kupuuza taarifa zilizoenea katika mitandao ya kijamii kuwa polisi wanawakamata  watu wanaolala kwenye nyumba za kulala wageni mchana kwa kosa la uzembe na uzururaji.

“Taarifa hizo si za kweli na watu wanaotoka mikoani nawaomba waendelee na shughuli zao kama kawaida na wapuuzie taarifa hizo, “alisema Kamishna Sirro.

CHECK PICHA JACKLINE WOLPER NA HARMONIZE WAKILA BATA PAMOJA LIVE  


  

  

  


MAGAZETI YA LEO IJUMAA SEPT 92016



 

Gallery

Popular Posts

About Us