KINGAZI BLOG: 04/09/17

HABARI KARIBU YAKO ZAIDI.

Breaking News
Loading...

Sunday 9 April 2017

GWAJIMA AZUNGUMZIA ISHU YA KUTEKWA KWA ROMA, FREEMASON NA KUHUSU MDEE KUMTUKANA SPIKA WA BUNGE. SOMA ZAIDI HAPA.

Askofu  wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat

Dar es Salaam. Askofu wa kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima amezungumzia suala la utekwaji na kusema kuwa endapo watajaribu kumteka atapiga picha kwa kutumia simu yake kwanza na kutuma kwenye mitandao ya kijamii kisha ndipo ataondoka na watekaji hao.




Mwanamuziki Roma Mkatoliki.

Akizungumza kanisani kwake leo, Gwajima alisema  Mkuu wa Mkoa wa Dar es  Salaam ndiye anayejua alipokuwa mwanamuziki Roma Mkatoliki

“Nampenda sana Rais wangu, lakini huyu Bashite analeta picha mbaya. Alisema atapatikana kabla ya Jumapili maana yake unayeee,” alisema

Kuhusu ishu ya freemasom Tanzania

Dar es Salaam. Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima  anaendelea na mahubiri yake ya kila Jumapili huku leo akiibua mada ya watanzania waliojiunga na Freemason.

Katika mahubiri hayo, Gwajima alisema wapo watanzania ambao umaarufu wao unatokana na dini ya Freemason huku akihusisha Freemason na imani za kichawi.

Nataka kabla hujamuimba mchungaji gwajima, urudie mara mbili, natetea wafungwa, askari, walioumizwa, walioachwa, matajiri na maskini,” alisema

LIVE VIDEO KUTOKA KANISANI KWENYE MAHUBIRI YA GWAJIMA MUDA HUU.

UNGANA NASI HAPA KUONA KINACHOENDELEA KANISANI KWA GWAJIMA
MUDA HUU


BONYEZA HAPA KUONA LIVE 

Khaa!! Hivivukiyaona Mapokezi ya Nape jimboni kwake....Wanawake walala chini ili apite migongoni mwao.!!



Mbunge wa Jimbo la Mtama mkoani Mtwara kupitia tiketi ya CCM, Mhe. Nape Nnauye amtaka Rais Magufuli aunde tume huru ambayo itaweza kuchunguza matukio ya uhalifu ya uvamizi wa studio unaoendelea nchini.


Mbunge Nape Nnauye akilia kwa furaha baada ya wananchi wa jimbo lake wakimtaka kupita juu ya migongo ya wamama ambao walijipanga ili kiongozi wao huyo apite juu yao, kwa heshima.

Hatua hiyo inatokana na matukio ya kiuhalifu yanayoendelea Tanzania na kuacha maswali mengi vichwani mwa wananchi kushindwa kufahamu kuwa watu hao na vikundi hivyo vya kihuni vinavyofanya vitendo hivyo vinapata wapi mamlaka hayo kuwa na nguvu kushinda Dola.

“Ombi langu kwa Rais namuomba aunde tume huru ichunguze matendo haya yasijirudie tena kwa sababu yasipochukuliwa hatua yataharibu sura ya Tanzania pia yataweza kuibuka makundi ya wahuni kuanza kuteka watu nao kwa kuwa hakuna hatua zinazochukuliwa. Tumsaidie Rais Magufuli kwa kumwambia ukweli naimani atasikia na atafanyia kazi kwa kuwa Rais wetu anapenda kusikiliza watu”. Alisema Nape 

Aidha Mbunge huyo amesema watu wanaofanya mambo hayo wanalengo la kuwagombanisha wananchi na Rais wao jambo ambalo sio zuri kwa taifa.

 "Juzi amepotea msanii Roma Mkatoliki na wengine lakini mpaka sasa haifahamiki wapo wapi, yaani kama vile amepotea Nzi, tulisikia kijana mmoja wa CHADEMA anaitwa Ben Sanane amepotea saizi miezi mitano imepita, matendo haya ya kina Ben Sanane, Roma Mkatoliki, na wengine yanajenga chuki ya wananchi kwa Rais, lakini pia yanajenga chuki kwa wananchi na Chama Cha Mapinduzi (CCM) ". Alisema Nape Nnauye

Vile vile Nape amesema yeye mpaka sasa haamini yule mtu aliyemtolea silaha siku ya mkutano wake na wanahabari kama alitumwa ila shida aliyokuwa nayo ni kutaka kujua vyombo vya ulinzi na usalama vinafanya nini mpaka matukio yote yanatokea.

Nape atema nyongo....Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumapili ya April 9






Roma Afunguka Haya baada ya kupatikana jana usiku.


Hatimaye msanii Roma Mkatoliki akiwa na wenzake watatu amezungumza na vyombo vya habari kwa mara ya kwanza kufuatia tukio la kutekwa na watu wasiojulikana kwa takribani siku tatu.

Roma na wenzake wamejitokeza mbele ya vyombo vya habari baada ya kutoka katika hospitali ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam, walikoenda kupimwa afya zao baada ya kuhojiwa kwa takribani saa sita katika kituo cha polisi cha Oysterbay.

Msanii huyo amewashukuru watanzania kwa ushirikiano wao waliouonesha na kuwahakikishia kuwa wako salama kiafya. Alisema ingawa hajaingia kwenye mitandao lakini ameelezwa juhudi zilizofanywa na watanzania.

“Niwahakikishie mimi ni mzima kabisa mpaka sasa hivi, niko salama kiafya na hata kiakili. Na hata wenzangu watatu, Moni, Laden na Imma… niwahakikishie kabisa kuwa sisi wote ni wazima na tunaendelea vizuri,” alisema Roma na kuomba wapewe nafasi kwanza wakapumzike.

Aliongeza kuwa kwa sasa wako katika taratibu za kuelezea vyombo vya usalama kuhusu tukio zima la kutekwa kwao hivyo hawawezi kuweka wazi kwa umma kwa sasa.

Aidha, Roma ameahidi kuwa siku ya Jumatatu watazungumza na vyombo vya habari na kuueleza umma kuhusu undani wa kilichojili.

Roma na wenzake walitekwa na watu wasiojulikana katika studio za Tongwe Records ambapo watu hao walichukua pia vifaa vya studio hiyo ikiwa ni pamoja na ‘computer’ na runinga bapa, kwa mujibu wa mmiliki wa studio hizo.

 

Gallery

Popular Posts

About Us