KINGAZI BLOG: 04/22/17

HABARI KARIBU YAKO ZAIDI.

Breaking News
Loading...

Saturday 22 April 2017

VIDEO: Diamond alivyoizindua Chibu Perfume, na bei yake hii hapa


Msanii kutoka Bongoflevani Naseeb Abdul (Diamond Platnumz) Leo April 21 2017 D ar es Salaam ameizindua rasmi ‘Chibu Perfume’, Perfume ambayo imetengenezewa Dubai na pia Meneja wake Salam ametangaza  jinsi ya kuipata CHIBU PERFUME  na Gharama yake itakayouzwa.

Fundi Simu Kizimbani Kwa Kufufua Simu Zilizofungiwa Na Tcra

Fundi simu, Juma Maulid (30) mkazi wa Tabata jijini Dar es Salaam, leo amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu tuhuma za kuingilia na kuchezea simu zilizofungiwa.

Mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Godfrey Mwambapa imedaiwa na mwendesha mashtaka, Wakili wa Serikali,  Elizabeth Mkunde kuwa, mshtakiwa ametenda kosa hilo Novemba 8, 2016 katika maeneo ya Kariakoo mtaa wa Aggrey wilaya ya Ilala.

Mkunde amedai kuwa mshtakiwa huyo alighushi IMEI za simu aina ya Tecno L8 zenye namba 357085075221523 na 357085075221531 ambazo zilifungiwa na TCRA  na kuzibadilisha namba hizo zikasomeka  kama 352167055726443 na 352167055726450.

Mshtakiwa amekana kutenda kosa hilo na amerudishwa rumande kwa kushindwa kutimiza masharti ya dhamana. Hakimu Mwambapa alimtaka mshitakiwa kuwa na wadhamini wawili wenye barua za utambulisho watakaosaini hati ya dhamana ya maneno ya milioni tano kila mmoja.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Mei 4 mwaka huu, kesi hiyo itakapokuja kwa ajili ya mshtakiwa kusomewa maelezo ya awali(PH) baada ya upande wa mashta kuileza mahakama kuwa upelelezi wa shauri hilo umekamilika.

Akizungumza nje ya mahakama,  Mwanasheria Mkuu Mwandamizi wa TCRA, Johannes Kalungula akiwa nje ya mahakama aliwaonya wale wote wanaojihusisha na kuingilia na kuchezea  Imei za Simu zilizofungiwa ama kuibiwa watachukuliwa hatua za kisheria.

Ameongeza kuwa kitendo hicho kinarudisha nyuma zoezi  lililofanyika la kufungia simu na kudhibiti wizi wa simu.

Serikali imetangaza Ajira Mpya 52,436

Serikali  inakusudia kuajiri watumishi wapya wa umma 52,436 katika mwaka ujao wa fedha. 

Aidha, madaktari wapya 258 waliokuwa waende kufanya kazi nchini Kenya, lakini wakakwama kutokana na kuwekewa pingamizi la kimahakama na wenzao wao huko na hivyo Rais, Dk John Magufuli kuamuru waajiriwe mara moja nchini, wanatarajiwa kuanza kazi keshokutwa Jumatatu.

Hayo yalisemwa bungeni juzi usiku na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais anayeshughulikia Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angellah Kairuki alipokuwa anatoa ufafanuzi wa lini Serikali itaendelea kuajiri watumishi wa kada nyingine, kama ilivyoulizwa na Mbunge wa Viti Maalumu, Anna Lupembe (CCM).

“Azma ya serikali, kwanza kabisa hatuwezi kuajiri wananchi wote, tumekuwa tukisikia hapa wahitimu hawana ajira, wengine wanaendesha bodaboda… tunapopanga idadi ya watumishi wa kuajiriwa, tunaangalia mambo mengi, kuanzia mahitaji, vipaumbele hadi uwezo wa kibajeti.

“Tayari tumeshaanza kutoa vibali vya ajira zaidi ya watu 9,700 na tutaendelea kufanya hivyo, na hivi karibuni Rais amebariki kuajiriwa kwa madaktari wapya 258 na Jumatatu (keshokutwa) wanaripoti kazini.

"Tutaendelea kuajiri na wataalamu wa kada nyingine, kabla ya kumalizika kwa mwaka huu wa fedha mwezi Juni tutakuwa tumejiajiri kwa idadi tutakayoipanga kwa awamu, na katika mwaka ujao wa fedha tutaendelea kuajiri watumishi wengine wa umma zaidi ya 52,436,” alisema.

Hata hivyo, alisisitiza Serikali itahakikisha hairudii makosa ya kuajiri watumishi hewa, wasio na sifa na weledi unaohitajika. 

Alisema kwa kiasi kikubwa uhakiki wa watumishi wa umma kwa ujumla umekwisha, lakini kazi hiyo ni endelevu, kwani serikali itaendelea kufanya hivyo mara kwa mara.

Alisema matunda ya uhakiki wa watumishi wa umma umebaini watumishi hewa 19,708 na ambao wameshaondolewa katika orodha ya mishahara ya watumishi wa umma. 

“Hawa wangeachwa, Serikali ingekuwa inapoteza kiasi cha Sh bilioni 19.8 kila mwezi, lakini fedha hizi zimeokolewa kupitia uhakiki wa watumishi wa umma.

"Tunafanya haya kwa nia njema. Mathalani tusingewatoa hawa, si wangeziba nafasi za ajira za wengine na fedha ngapi zingepotea?” alihoji. 

Alisisitiza kuwa, wizara hiyo itaendelea kutimiza majukumu yake kwa vitendo ili kurejesha nidhamu ya serikali na utumishi wa umma kwa kuongeza uwazi na kusimamia sheria, kanuni na taratibu za uwajibikaji wa viongozi wa watumishi wa umma ili wawajibike kwa wananchi ambao ndio wateja na waajiri wakuu wa watumishi wa umma.

Naye Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), George Simbachawene, akijibu hoja za wabunge, hasa la uhamisho wa watumishi wakiwemo wanandoa wanaotenganishwa, alikemea tabia ya maofisa watumishi kuzuia wenye ndoa kuhama kutoka kituo kimoja cha kazi kwa lengo la kuwafuata wenzao.

Alisema kuwazuia ni kuwanyima haki ya msingi, na kuwaagiza wabunge katika maeneo yao wasaidia kusimamia haki za watumishi. 

"Lazima sheria za utumishi zizingatiwe, walimu hawa au watumishi wanayo haki ya kutoka sehemu moja kwenda nyingine, lakini pia kuishi na wenza wao, lakini utadhani mtumishi anapoomba ni kama anasaidiwa, hapana ni haki yake ya msingi, waheshimiwa tusimamie haki za watumishi,” alisema Simbachawene

Atembezwa Nusu UCHI Na Kisha Kulazimishwa Kula Kinyesi kwa Kosa la Kumtukana Mama Yake

Wanawake wa kijiji cha Kisungamile kilichopo katika Kata ya Matai wilayani Kalambo katika mkoa wa Rukwa wamemwadhibu Vitus Nyami (26) kwa kumtembeza nusu uchi na kulazimisha kula kinyesi cha ng’ombe kwa kosa la kumtukana mama yake mzazi matusi ya nguoni.

Aidha wanawake hao walitumia mfuko wa ‘salphate’ kufunika sehemu za siri za kijana huyo kisha wakaanza kumtembeza mitaani kijijini  humo huku wakiimba nyimbo za kabila la Kifipa wakilaani tabia ya kijana huyo ya kumtukana mama yake mzazi matusi ya nguoni kila kukicha .

Walidai kukasirishwa na tabia ya kijana huyo wa kiume kumtukana mzazi wake wa kike matusi ya nguoni, hivyo walilazimika kumfunga kamba na kumtembeza mitaani kijijini humo akiwa nusu uchi.

Mwenyekiti wa kijiji cha Kisungamile, Didas Musa alikiri kutokea kwa mkasa huo juzi ambapo mtuhumiwa huyo alitembezwa mitaani kwa saa sita kuanzia saa 1:00 asubuhi hadi saa 6:00 mchana.

Akifafanua alisema kuwa licha ya adhabu hiyo ya kutembezwa nusu uchi mitaani na kucharazwa viboko 15, pia ameamriwa kulipa mbuzi mmoja, unga wa sembe debe moja na mafuta ya kupikia lita moja.

“Adhabu hii kwa kijana hutolewa na akina mama ambapo mimi kama kiongozi kazi yangu ni kuibariki tu,” alisisitiza . Mkazi wa kijiji hicho, Obedi Mwanakatwe alisema kijana huyo amekuwa akimtukana mama yake mara kwa mara , tabia ambayo imekuwa ikiwachukiza akinamama kijijini humo ambapo waliandamana na kumkamata kijana huyo .

“Baada ya akinamama hao wenye hasiri kumkamata kijana huyo walimpeleka kwenye shimo lililojaa kinyesi cha ng’ombe kisha wakampaka kinyesi hicho mwili mzima wakiwa wamechanganya na unga wakisaidiwa na wanaume, walimtembeza uchi kijana huyo mitaani kijijini humo,” alieleza.

Stela Tenganamba alisema baada ya kumtembeza kwa muda mrefu waliamua kumlisha kinyesi cha ng’ombe na kumpaka mwili mzima sambamba na kumroweka kwenye matope.

Adhabu hiyo iliwekwa enzi za mababu zao , ambapo mtu yeyote anayetukana matusi hadharani huchukuliwa hatua hiyo sambamba na kulipishwa ng’ombe mmoja, mbuzi, unga debe moja na mafuta ya kupikia lita moja.

Akifafanua alisema kuwa baada ya kutembezwa mitaani akiwa uchi hupelekwa kwa Mwenyekiti wa Kijiji ambaye hutoa adhabu kulingana na akinamama watavyoona inafaa

Lowassa Amchapa Mwakyembe..Habari kwenye Magazeti ya Leo 22/4/2017..!!!



 

Gallery

Popular Posts

About Us