KINGAZI BLOG: 10/05/16

HABARI KARIBU YAKO ZAIDI.

Breaking News
Loading...

Wednesday 5 October 2016

HIVI HAPA VYUO VILIVYOTOA MAJINA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA SECOND ROUND VYUO VIKUU MBALIMBALI 2016/2017

Image result for TCU TZ


Habari yako,

HII HAPA list ya vyuo vikuu ambavyo vimetoa majina ya wanafunzi waliochaguliwa na joining instructions za  kujiunga na vyuo vikuu 2016/2017-SECOND ROUND




CHUO CHA JORDAN (SECOND ROUND)            >>BONYEZA HAPA<<

CHUO CHA AMUCTA(SECOND ROUND)            >>BONYEZA HAPA<<

CHUO CHA KIU(SECOND ROUND)                      >>BONYEZA HAPA<<

CHUO CHA MUM(SECOND ROUND)                   >>BONYEZA HAPA<<


CHUO CHA MWEKA SECOND ROUND)              >>BONYEZA HAPA<<

 
CHUO CHA AJUCO SONGEA( 2ND ROUND)       >>BONYEZA HAPA<<

Viwango vya nauli za ndege vyatangazwa


Baada ya kumalizika kwa ofa iliyokuwa imetangazwa na shirika la ndege Tanzania (ATCL), Nauli halisi zitakuwa kama ifuatavyo;-


Dar es Salaam – Mwanza kwenda ni shilingi 160,000 hivyo kwenda na kurudi ni shilingi 320,000.
Dar es Salaam – Kigoma kwenda ni shilingi 395,000 hivyo kwenda na kurudi ni shilingi 610,000.
Dar es Salaam – Arusha kwenda ni shilingi 180,000 hivyo kwenda na kurudi 360,000.
Arusha – Zanzibar kwenda ni shilingi 249,000.
Zanzibar – Dar es Salaam ni shilingi 123, 000.

Baada ya Dogo Janja kutangaza kuoa, Madee afunguka haya

Dogo Janja ambaye sasa anafanya vizuri na wimbo wake mpya ‘Kidebe’ amefunguka na kutangaza rasmi kuwa ana mpango wa kutaka kuoa na kusema kwamba muda si mrefu anaweza kuvuta jiko na kuweka ndani.

Dogo Janja alisema haya kupitia kipindi cha Planet Bongo ambacho kilikuwa kinarushwa moja kwa moja kutokea Manzese na kusema kuwa suala hilo lipo kwenye mchakato ila ni kweli ana mpango wa kuoa muda si mrefu.

‘Yah ni kweli nataka kuoa muda si mrefu nitavuta jiko hivyo siwezi kusema ni lini ila suala hilo lipo kwenye mchakato” alisema Dogo Janja.


Kwa upande wa Madee ambaye ni mlezi wa Dogo Janja kimuziki na katika maisha ya kila siku alisema kuwa kitendo cha Dogo Janja kutaka kuoa kabla yake itakuwa kama dharau hivyo anapaswa kusikilizia kwanza mpaka yeye afanye mambo kwanza ndipo na yeye atangaze.

RAIS MAGUFULI AFANYA ZIARA YA KUSHITUKIZIA UWANJA WA NDEGE TIZAMA ALIYOGUNDUA LEO LIVE!!


Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Mhe. Joseph Kabila Kabange leo tarehe 05 Oktoba, 2016 amemaliza ziara yake ya kiserikali ya siku tatu hapa nchini na kurejea nchini kwake.

Katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam Rais Kabila ameagwa na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.

Viongozi wengine walioungana na Rais Magufuli wakati wa kumuaga Rais Kabila ni Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Mawaziri, Mabalozi wa nchi mbalimbali, Wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Bw. Paul Makonda na Viongozi wa Dini.

Katika hatua nyingine, mara baada ya kuondoka kwa Rais Kabila, Rais Magufuli amefanya ukaguzi wa kushitukiza katika sehemu ya kukagulia mizigo na abiria ya uwanja huo upande wa Terminal Oneambako Mwezi Mei mwaka huu alitembelea kwa kushitukiza na kubaini kuwa mashine za ukaguzi (Scanners) zilikuwa hazifanyi kazi. Mara hii Rais Magufuli amebaini kuwa mashine hizo zinafanya kazi, baada ya kujionea yeye mwenyewe uhalisia wa namna mizigo inavyokaguliwa.

Hata hivyo amemuagiza Mkurugenzi wa uwanja wa ndege wa Julius Nyerere Bw. Paul Rwegasha kuwachukulia hatua za kinidhamu maafisa wawili  walitoa taarifa za uongo pindi alipofanya ukaguzi wa kushitukiza mara ya kwanza.

“Leo kweli mashine zinafanya kazi na mimi nimeona lakini wale walionidanganya mara ya kwanza nilipokuja, Mkurugenzi hakikisha unawachukulia hatua” amesisitiza Dkt. Magufuli.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
05 Oktoba, 2016

 

Gallery

Popular Posts

About Us