KINGAZI BLOG: 02/07/17

HABARI KARIBU YAKO ZAIDI.

Breaking News
Loading...

Tuesday 7 February 2017

Maamuzi ya Mahakama kuhusu Watuhumiwa wa dawa za kulevya Leo Feb, 7

Mahakama ya hakimu mkazi Kisutu imeridhia ombi lililowasilishwa Mahakamani hapo na upande wa Jamuhuri  la kuwakata watuhumiwa 8 wa Dawa za kulevya kuwa chini ya uangalizi kwa kipindi cha miaka 3,huku wakitakiwa kufika katika Kanda maalum ya Dar es Salaam Mara mbili kwa mwezi.

Ambapo kwa mujibu wa Hakimu mkazi Mkuu wa Mahakama hiyo akisoma maamuzi ya Mahakama Huruma Shaibu amesema Mahakama imeridhia ombi hilo ambapo watuhumiwa hao  watakuwa chini ya uangalizi kwa kipindi cha mwaka mmoja tofauti na ombi la Jamuhuri  la miaka mitatu, lakini pia ameagiza Jeshi la Polisi kuwafanyia uchunguzi wa Mara kwa Mara katika maeneo yao, na si  kufika kituo cha Polisi Kanda maalum ya Dar es salaam kama Jamuhuri  ilivyoomba.

Picha 16 : Wema sepetu hakupanda kizimbani leo .TID, Tunda Na Wasanii Wengine Wanaotuhumiwa Kwa Madawa ya Kulevya wafikishwa MahakamaniWema

Takriban watuhumiwa 10 wa dawa za kulevya ambao ni miongoni mwa watu waliotajwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu asubuhi hii.
Miongoni mwa waliofikishwa mahakamani sasa ni wasanii Rommy Jones, TID, Babuu wa Kitaa, Petit Man, Tunda (model wa kike), Lulu Diva, Recho, Joan, na wengine.
Watuhumiwa wote wamesomewa kiapo cha Mahakama ambapo upande wa Jamuhuri umeomba watuhumiwa hao waamrishwe kuwekwa chini ya uangalizi kwa kuripoti polisi mara 2 kwa mwezi kwa kipindi cha miaka 2 ili kuangaliwa kama wameacha tabia ya kutumia dawa hizo hususani bangi
               
Wakili wa upande wa utetezi amedai taarifa hizo hazijakamilika kwani hazioneshi wanaojiusisha na dawa za kulevya na walikamatwa lini na wapi na hakuna ushahidi wa kujitosheleza wa madai hayo kiasi cha wao kupata dhamana ya kuangaliwa tabia zao bila polisi kutoa ufafanuzi wa kina wa kwanini wanahitaji kupata dhamana ya uangaliz
i

Mwimbaji T.I.D na wengine wakiwa kwenye gari kuelekea Mahakamani

T.I.D baada ya kufika Mahakamani

Waandishi wa habari

Rommy Jones na Nyandu

Tunda, Rachel na wengine wakiwa tayari Mahakamani

Mama wa Mwigizaji Wema Sepetu akiwa anatoka kituo cha kati cha Polisi





















































































































































Mama m Diamond Platnumz ni miongoni mwa ndugu waliojitokeza kufatilia 
PICHA: MILLARD AYO

Mbunge Adai yuko tayari kutaja Wabunge Wanaouza Madawa ya Kulevya


Kuanzia wiki iliyopita, vita dhidi ya Madawa ya kulevya iliyoibuliwa na mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, inazidi kuchukua sura mpya kila kukicha huku wengine wakitega masikio kwenye vyombo vya habari kutaka kujua kitu gani kinaendelea huko Mahakamani.

Vita hiyo juu ya madawa ya kulevya imefika mpaka bungeni na baadhi ya wabunge walikuwa wakitoa hoja mbalimbali huko mjini Dodoma. 

Mbunge wa Ulanga, Goodluck Mlinga jana alisema yeye yupo tayari kuwataja baadhi ya wabunge wanaohusika na biashara hiyo.

Mbunge huyo awali alizungumzia mambo mbalimbali yakiwemo masuala ya elimu lakini la mwisho aliweza kuzungumzia suala hilo ambalo kwa sasa kila mtu anataka kutambua nini kinaendelea.

” Suala ninalotaka ni hili suala linashika headline ni suala la madawa ya kulevya, naomba niwaambie sisi viongozi naomba niquote, ‘nitasema ukweli uongo kwangu mwiko.’ Kwahiyo nitakachotaka kukisema mtu yeyote akitaka anihukumu akihukumu chama changu kwanza, na kama wewe ni mwana CCM utanichukia rudisha kadi ndo unichukie.
"Wafanya biashara wa madawa ya kulevya hakuna asiowajua, tunawajua humu ndani wapo, nje ya bunge wapo, kwanini hatuwataji?"alihoji.
Aliongeza, “Kwanini hatuwataji tunakaa kimya? Mheshimiwa mwenyekiti kama kwa ridhaa yako unaniruhusu mimi nitawataja hata humu ndani. Madawa ya kulevya ni pamoja na bangi, kuna mbunge alisimama humu alisema bangi hazina madhara alijuaje kama hazina madhara kama hatumii? tungeanza na huyu. 
"Viongozi wenzangu naomba niwahakikishie kama tutakuwa wanafiki mbinguni sisi ndiyo tutakaokuwa kuni, tutakuwa kuni mbinguni tunawafumbia macho watumiaji wa madawa ya kulevya tunakula nao. 
"Nimpongeze ndugu yangu Paul Makonda kwa kuthubutu kutaja neno madawa ya kulevya lakini nimhakikishie kila marafiki watano wanaomzunguka watatu ni wafanyabiashara wa madawa ya kulevya, aanze na hao.”
 HEBU TAZAMA ALICHOKISEMA KUPITIA VIDEO HII HAPA CHINI 

 
A

Ray Vanny kuja na ngoma aliyomshirikisha Diamond

Good News kwenye muziki wa Bongo Fleva wiki iliyopita ni Ishu ya watanzania Diamond Platnumz,Alikiba na Navy Kenzo kushinda tuzo za Hipipo Music Awards huko Uganda. Moja ya tuzo alizoshinda Diamond ni tuzo ya Video bora East Africa kupitia video ya Salome aliyomshirikisha msanii wa label yake, Ray Vanny.

Good News kwenye muziki wa Bongo Fleva wiki iliyopita ni Ishu ya watanzania Diamond Platnumz,Alikiba na Navy Kenzo kushinda tuzo za Hipipo Music Awards huko Uganda. Moja ya tuzo alizoshinda Diamond ni tuzo ya Video bora East Africa kupitia video ya Salome aliyomshirikisha msanii wa label yake, Ray Vanny.

Baada ya ushindi huo, Raymond amefunguka kuhusu kufanya tena ngoma a Diamond ambapo amedai kuwa itakuwa ni ngoma yake yeye. “Lazima,watu wasubiri,” amesema Ray kupitia Supermega ya Kings Fm.

Tayari Rich Mavoko na Harmonize wamemshirikisha bosi wao huyo kwenye nyimbo zao, Kokoro na Bado.

Video! Hii hapa kauli ya Rais Magufuli kuhusu madawa ya kulevya

Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dokta John Pombe Magufuli jana wakati akitoa hotuba yake baada ya kumaliza zoezi zima la kumuapisha Mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama,  Aligusia masuala kadhaa likiwemo suala la madawa ya kulevya na wahusika wake. 

Rais alisema Serikali na vyombo vyote vya dola vinatakiwa kupambana na suala hili na kukamata yeyote anayehusika na uuzaji ana usambazaji ana utumiaji wa madawa ya kulevya hapa nchini bila kuangalia umaaraufu alionao mhusika, cheo chake, mtoto wa fuklani N.K 


ZAIDI HEBU TAZAMA VIDEO HII HAPA CHINI

                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                     
 

Gallery

Popular Posts

About Us