KINGAZI BLOG: 12/20/16

HABARI KARIBU YAKO ZAIDI.

Breaking News
Loading...

Tuesday 20 December 2016

Alichokisema mmiliki wa Jamii Forums baada ya kupata dhamana leo

Leo December 19, 2016 kutoka Mahakama ya hakimu mkazi Kisutu, Dar es salaam, mwanzilishi wa mtandao wa kijamii wa JAMII FORUMS Maxence Melo ameachiwa kwa dhamana baada ya kushikiliwa kwa zaidi ya siku 5 ambapo baada ya kupata dhamana hiyo Max ameyaongea yafuatayo.

“Nawashukuru mawakili wangu najua wamekuja kwasababu ya kutetea uhuru wa vyombo vya habari, jukumu hili sio la Max peke yake ni jukumu la wote, Max amekuwa mfano tu wakati mwingine atakuwa mtanzania yeyote anayetaka kutetea uhuru wake, mimi sina shida na vyombo vya dola vinafanya kazi yake” – Maxence Melo

Wanaume wafanyiwa Tohara hadharani maeneo ya shule

Walimu wa shule ya Msingi Nyakabungo jijini Mwanza wameiomba serikali kuingilia kati swala la ufanyaji wa tohara katika maeneo ya viwanja vya shule jambo ambalo limeonyesha kuwa kero .

Akizungumzia tukio hilo Mwl. Patrick Kamugisha amesema ameshangazwa sana kuona tohara ikifanyika hadharani na si kama mikoa mingine ambayo hufanya matukio hayo katika maeneo yaliyojificha na kwa usiri mkubwa.

Pia wanafunzi wa shule hiyo wamelalamikia matukio hayo hasa nyakati za asubuhi wanafunzi hao wanapokuja kujisomea masomo ya ziada kwa kipindi hiki cha likizo wanakutana na uchafu hasa mabaki yanayotokana na tendo hilo pamoja na kutapakaa kwa damu jambo ambalo wamesema ni hatari kwa afya zao.

Kutokana na tukio hilo la maandamano ya vijana hao wa kabila  la wakurya hivyo barabara ya Isamilo hulazimika kufungwa kwa muda ili kupisha maandamano hayo yapite,tofauti na Wilayani Tarime na Rorya ambako tohara hufanyika katika maeneo rasmi.

Kutokana na tukio hilo Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Mary Tesha amemtaka Mkurugenzi, uongozi wa kata, na uongozi wa mtaa wachukue hatua mara moja kuhakikisha zoezi hilo haliendelei kufanyika na pia uongozi wa shule kuweka walinzi.

Baba Mzazi Wa Ben Saanane Kukagua Maiti Iliyowekwa Kwenye Kiroba

Wakati polisi wakisema kuwa wanaufanyia mchakato wa vipimo vya vinasaba (DNA), mwili wa mtu anayedaiwa kuuawa nje kidogo ya mji wa Moshi na kuwekwa kwenye kiroba na kuchomwa moto, familia ya Ben Saanane, msaidizi wa Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe ambaye hajulikani aliko imesema inaenda kuuangalia mwili huo. 

Hatua hiyo ya polisi kupima DNA ilielezwa na Kamanda wa Polisi Mkoa Kilimanjaro, Wilbroad Mutafungwa baada ya hadi jana, mwili huo kutotambuliwa. 

Mauaji hayo yaligunduliwa Ijumaa iliyopita, baada ya watu waliokuwa na gari ndogo ambao hawajafahamika, kumchoma moto mtu huyo katika Kijiji cha Ongoma na kisha kutoweka kusikojulikana. 

Kamanda Mutafungwa aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa mtu huyo hajafahamika na wala hakuna mtu aliyejitokeza kuutambua mwili huo hivyo kulilazimu jeshi kufanya uchunguzi huo wa kisayansi. 

Kamanda Mutafungwa alitoa wito kwa ndugu, jamaa na marafiki waliopotelewa na ndugu, wafike katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC kuutambua mwili huo. 

Kuhusu madai ya marehemu kwamba alikuwa amevaa suruali inayofanana na sare za wafungwa, Kamanda Mutafungwa alisema si kweli kwani nguo iliyoonekana ni blanketi jepesi la rangi ya chungwa. 

Mzazi wa Saanane 

Wakati polisi ikijiandaa kwa mchakato huo, baba wa Saanane, Focus Saanane, jana alikuwa anajiandaa kwenda KCMC kuangalia mwili huo. 

Akizungumza jana mjini Moshi, Saanane alisema japokuwa mtoto wake alipotelea Dar es Salaam, watakwenda kuuangalia mwili huo ili kujiridhisha. 

Juzi Saanane alikaririwa akiiomba Serikali kufanya uchunguzi wa kupotea kwa mwanaye akisema ndiyo pekee yenye vyombo vya kiuchunguzi. 

Kuokotwa kwa mwili huo kunashabihiana na tukio la kupatikana kwa miili mingine saba katika Mto Ruvu mkoani Pwani ikiwa imefungwa katika viroba na kuwekewa mawe ili izame. 

Miili hiyo ilizikwa na wananchi wanaoishi jirani na mto huo bila kufanyika kwa vipimo vya DNA wala kutoa tangazo la watu waliopotolewa na ndugu zao kujitokeza kutambua maiti hizo hali iliyoibua utata. 

Tayari Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, alishaagiza kufanyika kwa uchunguzi wa miili hiyo na kutaka wale wote waliohusika na mauaji hayo watafutwe na kukamatwa.

 

Gallery

Popular Posts

About Us