KINGAZI BLOG: 03/26/17

HABARI KARIBU YAKO ZAIDI.

Breaking News
Loading...

Sunday 26 March 2017

Haya ndio aliyoyasema Gwajima leo kanisani kwake!!

Dar es Salaam.  Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima amesema ataendelea kusema ukweli na hataogopa chochote.

“Nitaendelea kusema ukweli fitina kwangu mwiko” alisema hayo katika mahubiri yake ya leo kanisani kwake Ubungo.

Pamoja na mambo mengine, Askofu huyo, alisema Clouds Media ni rafiki zake kwa sababu wamewaeleza ukweli watanzania.

Alisema hata waislamu ni rafiki zake kwani ndiyo waliomlea baada ya kutelekezwa akiwa mdogo.

Wasanii maarufu wa redio ya EFM, Mkude Simba na Stanley walikuwa kanisani hapo leo huku Mchungaji Gwajima akiongoza misa kwa mada ya vipaji na vipawa.

Breaking News..Rais Magufuli Afanya tena Utenguzi Wizara ya Nishati na Madini


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Joseph Pombe Magufuli ametengua uteuzi wa Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, Prof. Justin Ntalikwa kuanzia leo tarehe 26 Machi 2017.

Katibu Mkuu Ntalikwa aliteuliwa Desemba 2015 na kuapishwa Ikulu Januari 2, 2016.

Kwa mujibu wa taarifa ya Ikulu, nafasi yake itajazwa hapo baadaye.

Mashehe, Wasanii Watinga Kanisa la Askofu Gwajima

WASANII wa Vichekesho nchini Mussa Kitale na Stan Bakora, wameungana na mashehe leo kwenye ibada katika kanisa la Ufufuo na Uzima la Askofu Josephat Gwajima jijini Dar es Salaam.

Wasanii wa vichekesho wakiingia Kanisa la Ufufuo na Uzima Dar.

Jeshi la Polisi Morogoro latoa sababu kukamatwa kwa Nay wa Mitego

Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Polisi Mkoani Morogoro, Kamanda Ulrich Matei amethibitisha kukamatwa kwa msanii Nay wa Mitego usiku wa kuamkia leo mkoani Morogoro.

Kamanda Ulrich Matei ametoa sababu kubwa ya kukamatwa kwa msanii huyo ni kutokana na kutoa wimbo unaofahamika kwa jina la 'Wapo' ambao anadai unaikashfu Serikali iliyopo maradakani.

Kamanda Matei amesema shauri la Nay wa Mitego lipo jijini Dar es Salaam hivyo msanii huyo atasafirishwa na kupelekwa Dar es Salaam kuhojiwa kwa Mkuu wa Upelelezi wa mkoa.

 

Gallery

Popular Posts

About Us