KINGAZI BLOG: 02/16/17

HABARI KARIBU YAKO ZAIDI.

Breaking News
Loading...

Thursday 16 February 2017

KAMA WEWE MWANAUME UNA TATIZO LA KUFIKA KILELENI HARAKA KABLA MPENZI WAKO HAJARIDHIKA SOMA HAPA

                                       
.
                                                         

 WAKUBWA TU (18+)  BOFYA HAPA CHINI 
Image result for ABOVE 18

Pre mature ejaculation ni nini?
Hii ni hali ambayo mwanaume anatoa mbegu mapema sana kipindi cha tendo la ndoa na mara nyingi huambatana na kushindwa kumridhisha mpenzi wake.

Tatizo hili limekua likiwapata wanaume wengi na kujisikia aibu mbele za wenzi wao pale wanaposhindwa kuendelea kabisa baada  ya hali hii kutokea.
Kimsingi  mwanaume anatakiwa achukue dakika nne mpaka nane kabla ya kutoa mbegu za kwanza lakini watafiti wanasema tatizo hili hugundukiwa mtu anapotoa mbegu ndani ya dakika moja au kabla ya dakika moja.
Tatizo hili huweza kutokea mara tu baada ya kubalehe,{primary pre mature ejaculation} mda mrefu baada ya kubalehe{secondary PE} au kutokana na aina ya mwanamke uliompata.{situational PE}

Chanzo ni nini?
Tatizo hili halina sababu za kitaalamu zilizofanyiwa utafiti zikakakubalika ila wanasayansi wanaamini sababu zifuatazo zinaweza kua chanzo kikuu cha tatizo hilo.

kupiga punyeto au kujichua; mara nyingi watu wanaopiga punyeto hua wanafanya haraka kwa kujificha ili wasikutwe na mtu. tabiaile ya kulazimisha mbegu zitoke haraka huweza kuleta tatizo hili.

kukaa muda mrefu bila kushiriki tendo la ndoa; kukaa mda mrefu sana bila kushiriki tendo la ndoa husababisha mkusanyiko mkubwa wa mbegu za kiume ambazo zinaleta msisimko mkubwa na ukichelewa sana kushiriki tendo la ndoa zitatoka kwenye ndoto nyevu. kawaida mwanaume anatakiwa ashiriki tendo angalau mara nne kwa wiki.

kuwa na wasiwasi wakati wa tendo la ndoa; mtu akiwa na historia ya kupata  hali hii kabla, hua hajiamini na kua na wasiwasi kwamba litatokea tena na matokeo yake hulipata kweli.

madhara ya dawa zinazofanya kazi kwenye mishipa ya fahamu; baadhi ya dawa za usingizi, mawazo na zingine zinazofanya kazi kwenye mishipa ya fahamu huleta tatizo hili mfano amitriptyline.

kurithi; baadhi ya koo au familia fulani hurithi vimelea vya kua na ugonjwa huu kwa vizazi mbalimbali vya familia husika.

magonjwa ya mfumo wa uzazi wa mwanaume mfano prostatitis.


Diagnosis{ kuutambua ugonjwa]
Mwanaume yeyote ambaye anatoa mbegu chini ya dakika moja au mbili ni muhanga wa hili tatizo na anatakiwa apewe matibabu.
   

Matibabu
Matibabu ya ugonjwa huu yamegawanyika sehemu kuu mbili kulingana na ukali wa tatizo husika.

·         Non pharmacological treatment{matibabu yasiyo hitaji dawa}:  matibabu haya hupewa watu ambao wanahimili mpaka dakika tatu bila kutoa mbegu.

·         Pharmacological treatment{matibabu yanayohusu dawa}: matibabu haya hupewa watu ambao hutoa mbegu ndani ya dakika moja baada ya kuanza kushiriki tendo la ndoa, watu hawa hushauriwa kutumia na mbinu zote mbili za matibabu.
Yafuatayo ni matibabu yasiyohitaji dawa.


·         Tumia condom:
Condom ni moja ya tiba nzuri ya tatizo hili kwani hufanya kazi kwa kupunguza hisia kali za mapenzi mtu anazozipata pale ambapo hatumii condom.

·         Kandamiza perineum kwa kidole:Perineum ni eneo kati ya mkundu na korodani, ile sehemu ikikandamizwa na kidole huweza kuzuia kukojoa haraka wakati wa tendo la ndoa.
.
·         Punguza wasiwasi: hebu lifikirie tendo hili kama njia ya kujifurahisha sio njia pekee ya kutafuta kutoa mbegu,  hii itakusaidia kuondoa mawazo ya kutafuta mbegu na kuchelewa kumaliza.

·         Fanya taratibu: picha za ngono zinadanganya sana watu kwamba kulala na mwanamke lazima ufanye kwa haraka haraka kama mbwa. HAPANA; ukifanya taratibu ndio njia nzuri ya kumfikisha mwenzako na wewe kuchelewa kufika kileleni.


·         Badilisha style: ile style ya zamani ya kumlalia mwanamke kwa juu{missionary position} inaleta msuguano mkubwa kwenye kichwa cha uuume hivyo itakufanya ufike haraka sana.

·         Tumia style ya wewe mwanaume kutangulia chini afu mwanamke juu au kulala kwa upande wote mnaangalia upande mmoja hii itakusaidia sana kuchelewa


·         Toa mawazo kwamba unafanya ngono: hebu jaribu kufikiria mambo mengine ya kikazi au masomo wakati unafanya tendo hilo, hii itakupunguzia hisia kali za mapenzi na kuchelewa kufika.


·         Fanya na kuacha: hii ni ile hali ya kuzuia msuguano pale unapoona unakaribia kutoa mbegu kwa kama sekundi 30 kisha unaanza upya. Hakikisha haufiki “point of no return”. pointi ambayo huwezi kujizuia tena kumaliza.

·         Kandamiza sehemu ya shingo la uume: hii sehemu ya shingo ya uume kwa chini ambayo ukiibana itakusaidia kuanza upya tena kihisia. Nimetumia shingo la uume kwasababu najua uume hauna mabega.

tumia kilevi: unywaji wa pombe mfano bia mbili kwa siku kwa wanaume pombe hupunguza kidogo nguvu ya mishipa ya fahamu na kufanya mtu aliyekunywa kuchelewa sana kufika kileleni, [watu wanaokunywa pombe lazima mtakubaliana na hili] hivyo unaweza kunywa bia, wine au whisky nusu saa kabla ya tendo na kuondoa shida hii.
·      
Matibabu ya kutumia dawa.
hizi hupewa iwapo tatizo lako ni kubwa sana na hizo njia hapo juu zimeshindikana...
1.       Serotonin reuptake inhibitors mfano paroxetine na  clomipramine zimefanya kazi nzuri ya kuzuia kufika kileleni haraka..... humezwa saa moja kabla ya tendo la ndoa.[dawa hizi hazipatikani ndani ya nchi hivyo tunaagiza nje, ukihitaji wasiliana nasi kwa namba hapo chini]

2.       anesthetic creams:  hii hupakwa kwenye kichwa cha uume saa moja kabla ya tendo la ndoa kuzuia msisimuko na kufanya mwanaume achelewe kufika kileleni wakati wa tendo.[dawa hizi hazipatikani ndani ya nchi hivyo tunaagiza nje kama ukihitaji wasiliana nasi kwa namba hapo chini

MWANAUME USIPOZINGATIA HAYA WANAWAKE WAZURI UTAISHIA KUWAITA SHEMEJI AU DADA. SOMA ZAIDI HAPA

Image result for Uume
TUNZA UUME UHESHIMIKE
Uume imara ni heshima kwa mwanume na furaha
ya mwanamke, bila uume huwi mwanaume. Uume
ndio kiungo muhimu katika mwili wa mwanaume.
Ndio mana mtoto akizaliwa mama na manesi kwa
haraka huchungulia kuona ni wa kike au wa
kiume? Uume hutambulisha nasaba za ndani
zilizopo ndani ya mwili wa mwanaume.
Lakini tangu zama za Adamu hasa baada ya
gharika kuu wakati wa Sodama na Gomora
mwanaume amekuwa anatumia uume wake
vibaya hadi kupelekea uume kuwa goigoi na
legelege na hatimaye kushindwa kutimiza
majukumu yake ya awali. Tangu awali uume
uliundwa na Mungu ili uyatimize kikamilifu
mambo yafuatayo.
(1) kutumika katika kuzalisha (reproduction)
(2) kustarehesha
(3) kusafisha mwili na uchafu (chumvi na sumu
mbalimbali) na pia
(4) kutumika kama utambulisho (identity)
Uume bora ni ule wenye uwezo wa kufanya
shughuli zote yani kuzalisha, kuondoa sumu
mwilini na kustarehesha bila usumbufu wala
maumivu. Uume bora huwa imara ukiwa katika
majukumu yake na kuweza kutimiza malengo
yaliyokusudiwa. Chakula bora, afya bora,
saikolojia sahihi na mzunguko mzuri wa damu
katika uume ni muhimu sana kwa afya ya uume
bora.
Katika mada iliyopita nilikuelezea kwa uchache
maadui wa uke katika ile mada ya “tunza uke
ukutunze” leo ningependa pia tujikumbushe
maadui 18 wa uume katika mada mpya ya “tunza
uume uheshimike”
Sasa kila unapoona jambo la tofauti linajitokeza
kuhusu uume wako kwa mwonekano, utendaji
kazi na utuliaji (pozi) basi tambua ya kwamba
kuna jambo linalofanyika ndani ya mwili wako au
ndani ya uume wako ambalo wewe huwezi kulijua
mpaka umwone daktari. Ni muhimu kujenga tabia
ya kuonana na madaktari mara kwa mara ili
kujua afya ya uume wako
Kwa ujumla ubora wa uume unaathiriwa na vitu
vingi sana lakini viko katika makundi yafuatayo
(1) UOGA na WASIWASI, UVIVU wa kujifunza na
uvivu wa kufanya MAZOEZI.
(2) Ulaji mbaya wa CHAKULA, unywaji wa vileo
badala ya maji na utumiaji wa madawa makali.
(3) TABIA MBAYA kama vile kutokuoga angalau
mara 2 kwa siku, kutojisafisha mara ukojoapo na
kwenda haja kubwa, kuwa mchepukaji, punyeto,
uangaliaji wa picha chafu za ngomo, ufanyaji wa
ngono kinyume na maumbile, uvutaji wa sigara,
ulaji wa mirungi, uvutaji wa bangi, utumiaji wa
madawa ya kulevya na uchafu wa roho na moya
kama kuwaza ngono tu siku nzima unajichosha.
(4) KUTOKUMJALI MKE/MPENZI wako na pia
kutokuujali uke wake
(5) MAGONJWA HASA SUGU ambayo mara nyingi
yanatokana na vipengere 1-4 hapo juu
(6) Kukaa na uume usiyo na TOHARA. Hii
sitaielezea kwa leo.
Dalili za uume wako kushambuliwa na MAADUI ni
kama zifuatazo.
1. Kupata maupele, michubuko, miwasho na
vidonda sehemu za siri
2. Uume kushindwa kusimama au kuwa imara
3. kushindwa kufanya tendo la ndoa kwa ufasaha
4. kuwa na magonjwa mbalimbali kama tezi dume
na bawasiri, kukojoa mkojo kwa shida na
maumivu, kuwa na STDs nakadhalika.
5. kupata mshindo mwepesi au kufika kileleni kwa
haraka au kwa shida
6. Kupungua kwa mbegu za kiume na kuwa
mgumba
7. Mwanaume kukose kuutumia uume kama
kitambulisho, I mean mwanaume anaishi na
mwanaume mwenzie (sasa haijulikani mwanaume
na mwanamke ni yupi)
Sasa ni vizuri ukajua pia kuwa unapokuwa na
dalili hizi lazima uangalie nini hasa chanzo chake
ndio upate tiba kamilifu itakayokuweka huru.
Maadui hawa mimi huwafananisha na KAA (crab)
kwa sababu ni maadui wanaosambaa mwilini
haraka sana bila hata ya wewe kupenda.
Kumbuka hawa wanaitwa maadui kwa sababu tu
wanasababisha uume usifanye kazi zile
zilizokusudiwa tangu awali. Kumbuka pia ya
kwamba maadui hawa wengine ni dalili tu ya
jambo flani linaloendelea mwilini ambalo sio
rahisi kulijua mpaka uingie kiundani au uende
kupima hospitalini.
ADUI WA #01. MAGONJWA
Magonjwa ni adui namba 1 wa uume wako.
Magonjwa ya sehemu za siri, magonjwa ya mwili
kwa ujumla, na magonjwa ya wanaume kama -
tezi dume ni adui wa uume wako. Ugonjwa kama
kisukari na presha, figo na ini kutokufanya kazi
vizuri LAZIMA uume uwe dhaifu. Kuna magonjwa
mengine pia kama viupele vya ajabu ajabu huko
magogoni pamoja na ugonjwa wa bawasiri.
MAGONJWA HAYA LAZIMA YATIBIWE HARAKA.
Kumbuka chakula ndio dawa pekee ambayo
Mwenyezi Mungu alitupatia wanadamu.
Magonjwa ya zinaa hata kukojoa mkojainakuwa
ngumu, mtu mwenye tezi dume kwa mfano
anakojoa mkojo unaunguza kama anakojoa maji
ya moto, bawasiri inaumiza mgongo ile mbaya.
Je uume utakuwa imara hapo?
ACTION: KULA CHAKULA BORA NA EPUKA UZITO
NA KITAMBI
ADUI WA #02. ULEVI NA SIGARA - Ulevi ndio, Na
ulevi haufai kabisa kwa afya ya uume wako. Ulevi
unakufanya uwe mlaji wa nyama hasa nyekundu,
unakuwa sio mwepesi wa kunywa maziwa na
kula matunda, unakuwa mzembe wa majukumu
yako ya ndani, unapata vitambi, unaharibu
balansi ya homoni >> unaelekea upotevuni”
Kunywa maji ya kutosha, maji fresh ili
kuuburudisha mwili na kuondoa msongo wa
mawazo.
DRINK WATER NOT ALCOHOL & SODA
ADUI WA #03. PUNYETU NA MICHEPUKO
Watu walionishuhudia ambao walifungwa katika
minyororo ya kufanya punyetu hadi mara 6 kwa
siku, waliokuwa wanafanya hadi vyoo za ofisi na
wengine kujificha hata majumbani wake zao
wakiwa wamelala au hawapo. Vijana wa boarding
school na vyuo, mabachela na wengineo wanatoa
shuhuda zinazotisha. Punyeto imekuwa utumwa.
Wanashuhudia kupata majipu, michubuko,
msongo wa mawazo, kushuka kwa kujiamini,
wengine wameshuhudia kufika kiwango cha juu
cha kutokuvutiwa na wanawake kabisa. Kwa
kifupi punyeto huharibu vipokezi (receivers) vya
hisia mwilini na saikolojia yako ya mapenzi kwa
ujumla, kuharibu mishipa na nerve za ufahamu
katika uume na kukukosesha mawasiliano sahihi
kati ya uume na akili yako. Unaporudi kufanya
tendo la ndoa kawaida (na mwanamke) unakuwa
tayari umeathirika na inakuwa kama upo
ulimwengu wa nje ya mapenzi. Wengine
wanasema haina madhara na pia kutoa namna
nzuri ya kufanya ili usipate madhara, lakini kila
waathirika wanasema haifai….KINGA NI BORA
KULIKO TIBA
ACTION: ANZA PROGRAM YA KUACHA PUNYETU
HARAKA ONA KAMA HUO NI UGONJWA KAMA
MAGONJWA MENGINE.
ADUI WA #04. MADAWA
Hapa kuna madawa ya kulevya na madawa ya
kawaida, pia madawa makali ya presha na
kisukari ni hatari kwa afya ya uume wako.
Madawa yanayowekwa katika baadhi ya makopo
ya vyakula vilivyosindikwa na mengine
yanayonyunyiziwa mashambanin wakati mimea
inakuwa katika ukuaji wake ni hatari tupu.
Madawa ya kulevya nadhani wote tunayajua
yalivyonoma. Unalegea mwili mzima, uume
unajifia tu kama bamia.
ACTION: JENGA TABIA YA KUTUMIA CHAKULA
CHA ASILI KAMA DAWA ILI MAGONJWA YA TABIA
YASIKUPATE
ADUI WA #05. UCHAFU WA MWILI, NGUO NA
NGUO ZA MBANO
Nguo chafu, za mbano na zisizo za pamba
zinasababisha magonjwa ya ngozi. Pia uume
unatakiwa upate free range yaani ubembee na sio
kutulia kama jiwe. Hii inaufanya uume kuwa
active na kuwa tayari kwa kushughulika. Pia
wanaume wengi ni mabingwa wa kuvaa suruali si
chini ya siku 3 hadi 7. Wengine wanavaa jinsi
kauka nikuvae - huo ni uchafu na ni hatari uchafu
kuingia ikulu. Oga mara kwa mara fua nguo zako
hata kama wife hafanyi fanya mwenyewe, vaa
boxer chupi sio zile za chupi za V kama za
wanawake. Ukikojoa na kwenda haja kubwa
jitawaze vizuri. Kuwa msafi mwili na roho, Sasa
wengine wanafuga rasta maeneo ya Ikulu. … OK
decide yourself kama ni usafi huo au uchafu,
unavaa jinsi week nzima!!!!
ACTION: ACHANA NA SKINI JEANS, CHUPI
ZINAZOBANA NA TAITI UNAZOVAA SIKU NZIMA,
KUWA MSAFI MUDA WOTE SIO SIKU YA KWENDA
UKWENI NDIO UNAOGA NA KUVAA SUTI
ADUI WA #06. BAADHI YA CHAKULA
Hapa lazima tuambiane ukweli ivi mwanaume
unakula chips na soda 24/7 unataka uwe nini
kama sio kituko, vyakula vyepesi vyepesi
visivyokuwa na nguvu vinavyokuongezea sukari
na presha mwilini achana navyo. Mwambie waifu
kabisa aachane na mapishi ya ugali uliokobolewa.
Vyakula vya kukujaza gesi tumboni havifai,
vyakula vinavonenepesha tumbo achana navyo
kabisa. Wengine wanapiga pombe kali eti
zinaongeza nguvu, at least kwa leo au kesho
“energy drinks is not a long lasting solution”.
Mara moja moja penda kutumia asali na
mdalasini, tende, matunda kwa wingi hasa yale
yenye zink kama tikiti maji, avocado, uyoga na pia
machungwa. Hakikisha unakula matunda dakika
kadhaa kabla au baada ya chakula. Usichanganye
matunda yenye acid na alkali mara moja na ukala
yaani mtindo wa cocktail, mfano chungwa lina
acid, parachichi ni alkaline (haya usiyale yote
mara moja).
ACTION: BADO NASISITIZA KULA CHAKULA BORA
NA PIA KULA MATUNDA SAHIHI KIUSAHIHI.
ADUI WA #07. HOMONI KUVURUGWA
Hapa ndugu zangu pana uhusiano sana na
namba 4 hapo juu. Vyakula na madawa
tunayotumia pamoja na madawa yaliyotumika na
wakulima ndio yanaleteleza hormoni katika mwili
wako kuwa na balansi ya tofauti. Matokeo yake
hormoni zinazohitajika kuamsha vichocheo vya
kuufanya uume ufanye kazi vema zinashindwa
kuwa katika balansi nzuri na hatimaye kuufanya
uume kushindwa kufanya kazi zake kwa ufasaha.
ACTION: KULA CHAKULA BORA NA EPUKA UZITO
NA KITAMBI
ADUI WA #08. UMRI
Kadri umri wako unavozidi kwenda mbele ndivyo
uwezo wa kiafya wa uume wako unavyozidi
kupungua ingawa wanasema "old wine gets
better" Magonjwa pia ni rahisi kukuingia,
magonjwa kama tezi dume, kansa ya uume,
ubovu wa kibofu cha mkojo na pia kukosekana
kwa damu katika sehemu zako za siri.
ACTION: BADO NASISITIZA KULA CHAKULA BORA,
KAMA UNAWASIWSI PATA VIRUTUBISHO VYA
KUONDOA SUMU KUIMARISHA MIFUPA NA AKILI
ADUI WA #09. KUONGEZA UREFU NA UJAZO WA
UUME NA PIA KUUCHORA UUME KWA KUTOBOA
AU KUPAKA RANGI
Wanaume wengine hujichora katika uume wao na
kuweka alama mbalimbali au majina mbalimbali.
Kwa kuwa kazi hizi katika mazingira ya kiafrica
hufanywa kwa siri basi vitogeo huwa dhaifu na
huenda vikaambukiza magonjwa, lakini pia ukisha
chora uume wako kwa kutoboa ngozi ni rahisi
kwa magonjwa kukuingia wakati ukiwa katika
harakati zako za kinyumba. Kuongeza saizi na
ujazo wa uume pia ni adui wako wa baadae
(future enemy) ingawa huwezi jua mara moja.
Baada ya muda kupita utabaini mapungufu
makubwa ya uume wako kutokana na kuongeza
urefu au ujazo wake. Watu wengi wapo na
wanalalamika, uume umelala pamoja na kuwa
mnene na mrefu. Njia za asili ni zile zinaongeza
mzunguko wa damu uumeni na kuzuia magonjwa
sugu kama kisukari, presha, matatizo ya ini na
figo pia kufanya mazoezi ya viungo vya mwili na
misuli.
ACTION: ACHA KABISA HIZO TABIA, UACHE UWE
KAMA MUNGU ALIVYOUUMBA. JIZOEZE NA
JIFUNZE MBINU MABALIMBALI ZA KUWA NA
UUME UNAOFANYA KAZI ZAKE VIZURI BILA
KUUJAZA AU KUUREFUSHA
ADUI WA #10. ACROBATIC AND ATHLETIC SEX
Hawa pia ni maadui wakubwa, kuna baadhi ya
wanandoa hufanya mapenzi kwa kutumia staili za
tofauti tofauti na zingine huufanya uume kupenya
kwa shida au kukunjana na hivyo kusababisha
michubuko na uvimbe katika kichwa na shingo ya
uume. Na pia wengine hufanya mapenzi muda
mrefu sana kama vile wako mashindanoni -
Jiulize unabakia salama? Starehe isiwe kero.
Pima faida ya starehe na hasara yake.
ACTION: ENJOY SEX OTHERWISE YOU GET
SEXUAL INJURY
ADUI WA #11. MSONGO WA MAWAZO
Au stress huyu ni adui endapo utashindwa
kumdhibiti kwa kuwa stress husababisha milango
ya fahamu kuziba na pia kuunyima uume damu
na oxygen ya kutosha na hivyo uume kushindwa
kufanya kazi yake vizuri. Ikiwa utashindwa
kuusimamisha uume huenda ukashindwa mara
nyingine tena kwa kuwa swala hilo linaweza
kuathiri saikolojia yako ya mapenzi na hivyo
kujikuta kila wakati unashindwa wakati ki-ukweli
upo fiti. Jifunze kuwa nje ya stress kama vile
kupangilia mambo yako vizuri ya kijamii, kiofis na
kipesa (kwa sababu stress au msongo hutokea
wakati matokeo halisi yamekuwa madogo kuliko
matokeo tarajiwa na inaonekana hamna namna
ya kufanya na muda umekwisha) – Siku zote
panga siku yako vizuri na yaangalie mambo yote
kwa kutumia akili chanya. Katika kila ubaya kuna
uzuri, fuata uzuri.
ACTION: KULA CHAKULA BORA NA SAHIHI,
JIPANGE, JIACHIE NA PIGA MAZOEZI YA
KUTOSHA.
ADUI WA #12. NGONO KINYUME CHA MAUMBILE,
VIDOLE NA MIDOLI
Ufanyaji ngono kinyume na maumbile ni hatari
kwa afya ya uume wako, iwe unafanya au
unafanywa yote yanapelekea kuwa na hali ya
sintofahamu mara uume unapokutana na uke. Sio
mazoea yake na sio utaratibu wa dini zetu hata
wapagani wanakataa wala sio uhalisia. Wengine
wana vimidoli vyao na vitu vinavyofanana na
hivyo. Unasinyaisha uume wako…. STOOOOP & BE
A MAN.
ACTION: KWA WENYE WATOTO: ANGALIA MTOTO
ANAPOKUWA NA TABIA ZA AJABU AJABU
MKAGUE, NA ONGEA NAYE MARA KWA MARA.
SIO KILA SIKU UNARUDI UNAKUTA WAMELALA –
yasijewatokea ya Moshi (Mbaya sana).
ADUI WA #13. WASIWASI WOGA NA UVIVU
WAKATI NA KABLA YA TENDO LA NDOA.
Hapa ndugu zangu hakuna maelezo mengi sana
ila kumbuka tu ya kwamba kuwa na wasiwasi na
woga kunaondoa uwezo wa damu kufika maeneo
ya uumeni hivyo kuukosesha uume malighafi
muhimu ya damu na oxygeni ili uume ufanye kazi
vizuri. Pia wewe mwenyewe mwanaume unakosa
focus (target) ya jambo unalolifanya. Kuwa
mwanume jiamini unaweza; YOU CAN DO IT EVEN
BETTER
ADUI WA #14. UPUNGUFU WA TESTESTORENE
Testosterone ndio homoni ya kiume inayohusika
na uundaji wa viungo vya kiume wakati mtoto
akiwa tumboni hajazaliwa na kisha kuanza
kujenga mwili wa kiume wakati kabla ya
kubalehesha na kumtayarisha kijana wa kiume
kuwa baba akisha balehe. Na baada ya hapo
homoni hii huhusika na matendo mabalimbali ya
kimapenzi na mvutano kati ya mwanamke na
mwanaume. Pia huhusika na uzalishaji na
ukomazaji wa mbegu za kiume. Homoni hii
ikipungua uwezo wa uume kufanya kazi vizuri
hupungua. Uzuri ni kwamba unaweza kuongezwa
homini hii katika mahospitali lakini pia kuna
vyakula unavyoweza kula na kuiongeza taratibu.
Action:IJUE TESTOSTERONE.
ADUI WA #15. PICHA CHAFU, ROHO CHAFU NA
AKILI CHAFU
Uangaliaji wa picha chafu za ngono ni hatari kwa
ujumla wa saikolojia yako. Mwili wako unauwezo
wa kubadili tabia na vionjo kama utafanya hivyo
ndani ya siku 15 hadi 21. Ikiwa utazoea kuangalia
picha za ngono ambazo wataalamu wengi wa
holywood wanasema si za kweli basi unajikuta
upo katika ulimwengu ambao sio halisia. Ukija
kuonana na mkeo halisi unajikuta mwili wako wa
hisia bado upo Holywood. Akili yako imetekwa.
Huwezi fanya vizuri tena, wengine wanasema
wanatafuta apetite, lakini kumbuka apetite hii sio
ya asili baada ya muda unazoea unakuwa sugu
na huwezi tena kuwa boosted na hizo picha. Best
apetizer ni mkeo.
ACHA KABISA PICHA CHAFU, UKIJIZOESHA
NDANI YA SIKU 15 HADI 21 UNAACHA KABISA.
MPENDE MKEO TU
ADUI WA #16. MWANAMKE MWENYE DHARAU NA
MATUSI
Tabia za baadhi ya wanawake zimekuwa kero
kabisa kwa uimara wa uume. Mwanamke
anakuwa mchafu kupindukia. Wengine ni kutoa
matusi mfululizo kama vile hawajaenda jandoni,
wengine ni dharau zisizokuwa na mpango hadi
wakati wa tendo la ndoa. Wanawake wengine
hawachangamki hata mwanaume ajitahidi vipi
yaani wapo wapo tu as if ni magogo. Hii ni hatari
sana. Mwanamke ni ufunguo mzuri sana kwa afya
ya mwanaume hasa kama mwanamke ameutunza
vizuri uke wake na pia kama mwanaume
hajaathirika na uoga, wasiwasi na mashaka,
magonjwa na tabia zile mbaya kama punyeto,
michepuko, ulevi na madawa ya kulevya. Wewe
mwanume unatakiwa utengeneze mazingira ya
mkeo kuwa msafi na mwema kwako, anayejituma
na ambaye ni mkweli daima. Love your wife she
will pay you back 100%.
ACTION: Mwanamke ndio kiongozi wa Ndoa,
mwanamke mpumbavu huvunja nyumba yake
mwenyewe. Kuwa kiongozi wa mumeo mara tu
anapoingia chumbani, Ubos wake auache nje ya
mlango wa chumbani.
ADUI WA #17: UZITO, KITAMBI NA KIRIBA
TUMBO CHA MWANAMKE
Wanwake wengi siku hizi wana vitambi, owk
unaweza sema hii inakujaje hapa? Ukweli ni
kwamba baadhi ya shughuli za msingi za uume
zinashindikana kufanyika kwa sababu ya kitambi
cha mwanamke, ofcourse hata kitambi cha
mwanaume ni adui lakini adui namba moja ni
kitambi cha mwanamke na pili ni kitambi cha
mwanaume. Wanawake wengi wanaoshindwa
kufika kileleni wanavitambi au uzito mkubwa. Hii
inauletea uume shida sana ya kutimiza majukumu
ya kinyumba.
ACTION: Anzeni program za kutoa uzito, vitambi
na viriba tumbo kwa kutumia chakula asili tu,
mazoezi ukipenda pia dieting ukipenda.
ADUI WA #18: UKE USIOTUNZWA, uume unakuwa
bora ikiwa uke pia ni bora.
ACTION: Mwanaume lazima ujiunge na mkeo
kumweka vizuri
ADUI WA #19: KUKOSA USINGIZI
Kuangalia mpira kuanzia saa11 mpaka saa7
usiku, wengine wanaangalia movie huku wanakula
mirungi nab ado asubuhi unawahi kazini. My
friend unaharibu mwili wako na uume wako
unapata stress. Ukilala mwili unapata muda wa
kurekebisha misuli, kuweka balansi nzuri ya
homoni na kurudisha hamu za mwili za kawaida
pia kuboresha kinga ya mwili. LALA USINGIZI WA
KUTOSHA UPUMZIKE UBONGO UJIPANGE, MISULI
ITULIE SELI ZA MWILI ZIZALIANE.
ADUI WA #20: TOO MUCH SEX IS HARMFUL.
Ukifanya sana ngono unahatari ya kupata
madhara yafuatayo uume kuvunjika (hauvunjiki
kama kijiti ila misuli inaumia), kuishiwa maji
mwilini, UTI, kuumiza nerve za uume, kupunguza
nguvu ya misuli na kushindwa au kuuma misuli
ya mwili. AMUA NI KIASI GANI KINAFAA
Kwa ujumla utakuwa umegundua ya kwamba
chakula ndio suluhisho la kudumu la kupambana
na maadui hawa, ingawa pia utalazimika kuwa
mwenye tabia nzuri. Endapo wakati mwingine
inakuwa ngumu kwa chakula kufanya kazi na
kuleta matokea ya haraka itakulazimu kupata
ushauri wa kitabibu kama kupata dawa za
hospitalini (kemikali) au virutubisho. Ikiwa
utapata dawa au vitutubisho hivi na ukapona
huna budi kuendelea kutumia chakula bora na pia
kuwa na tabia njema kwa ajili ya kupata matokeo
ya kudumu, yenye furaha na amani.
Basi ndugu yangu wa kiume (hata wa kike), hii
ndio mada yetu moto ya leo na nadhani itakuwa
msaada kwako sana.

IMEANDALIWA KWA MSAADA WA MTANDAO NA KUPITIA  GROUP LA WHATSAPP LIITWALO DARASA LA MAFUNZO.

Mfumo Mpya wa Kutumia Namba za Simu Kuanzishwa Mwezi Ujao,Utaweza Kuhama Mtandao Mmoja Kwenda Mwingine Bila Kununua Laini Mpya

Mfumo mpya wa matumizi ya namba za simu (Number Portability) unatarajiwa kuanzishwa ifikapo Machi Mosi kwa ushirikiano wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na kampuni za simu nchini.

Kampuni za simu zilizoingia katika mkataba huo ni pamoja na Tigo, Vodacom, Airtel, TTCL, Zantel, Smile, Smart na Halotel.

Jana, TCRA ilitangaza huduma hiyo mpya kwa watumiaji wa simu nchini, itakayomwezesha mteja kuhama mtandao mmoja kwenda mwingine na kuendelea kutumia namba yake ya awali.

Mpango huo tayari umeshatekelezwa kwenye nchi nyingi za Ulaya na hata Afrika Kusini.

Mmoja wa watumiaji wa mitandao ya simu za mkononi, Musa Aziz amesema pamoja na faida zilizopo bado kuna hofu kwa watumiaji kutokana na usumbufu wa mawasiliano.

“Nafikiri kutakuwa na gharama za ziada mimi nikimpigia mwenzangu sitajua kwa wakati huo anatumia mtandao gani, hapo ninaweza kuingia gharama kubwa zaidi, sina hakika kama italeta unafuu japokuwa ni mpango mzuri,” amesema Aziz.

Masogange apelekwa kwa Mkemia Mkuu wa Serikali

Dar es Salaam. Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalumu Dar es Salaam, Simon Sirro amesema mtuhumiwa Agness Gerald, maarufu Masogange amepelekwa kwa Mkemia Mkuu wa Serikali kwa ajili ya kuchukua vipimo vya damu ili kubaini kama anatumia dawa za kulevya.

Masogange ambaye ni mrembo maarufu anayetamba katika video za wasanii mbalimbali wa bongo fleva alikamatwa na polisi juzi.

Kamishna Sirro amewaambia wanahabari leo kuwa Masogange amepelekwa kwa Mkemia Mkuu wa Serikali na kwamba majibu yakipatikana kesho atafikishwa mahakamani

"Tunamchunguza Masogange katika mambo matatu ili kujua kama anauza , anatumia au anasafirisha dawa za kulevya, " amesema Kamishna Sirro.

Katika hatua nyingine, Kamishna Sirro amesema watuhumiwa 349 wamekamatwa kwenye operesheni ya kupambana na dawa za kulevya iliyoanza Februari Mosi mwaka huu.

NEY WA MITEGO: MUDA WETU.(New Official video)

DOWNLOAD

                                

Nikki Mbishi Atoa Onyo Kwa Vyombo vya Habari Kwa Watakao Sambaza na Kupiga Wimbo wake wa "I am Sorry JK"

Ikiwa ni saa zisizodi ishirini na nne (24) toka itoke taarifa ya MwanaHiphop Tanzania Nikki Mbishi kutoa taarifa ya kuitwa na Baraza la Sanaa Taifa (BASATA) kuhojiwa kuhusu wimbo wake unaomzungumzia Rais Mstaafu Jakaya Kikwete ‘I am sorry JK‘ Rapper huyo ameandika sentensi kadhaa.

“Salaam, baada ya salamu naomba niombe radhi kwa vyombo vyote vya habari kuwa sitoweza kuwapa ushirikiano wowote kuhusu wimbo wangu wa “I’M SORRY JK” uliositishwa na hii ni kwa usalama wao na wangu pia‘

Ameendelea kuandika kuwa

’Napokea simu nyingi sana zikihitaji maelezo juu ya suala hilo ila kiukweli kwa watakaohitaji taarifa kamili wanaweza kufika ofisi za BASATA, naomba nisiwe msemaji tena juu ya jambo hili‘

Nikki alitoa tahadhari pia

 ‘Kwa yeyote atakae endelea kuusambaza au kuucheza popote pale mimi sitohusika naye maana technology iko huru popote Duniani na siwezi kuzuia watu wasiupate kwa kuwa ulishasambaa, hivyo chukua tahadhari ili usijikute mikononi mwa sheria [​IMG] .

#Asanteni sana, naomba msubiri ujio wangu mpya wa #SINGELI na aina nyingine za muziki kama #NAIJA #MCHIRIKU n.k. MUZIKI NI AJIRA,MUZIKI NI KAZI YANGU #Mungu_Simama_Kweli_Idhihirike

Ni wako mtanzania mvumilivu:
Nikki Mbishi @2017
With no offence!

SHILAWADU__U-Heard- Irene Uwoya afafanua kwanini anawapenda kimapenzi wanaume wenye sura mbaya


 

Gallery

Popular Posts

About Us