KINGAZI BLOG: 04/18/17

HABARI KARIBU YAKO ZAIDI.

Breaking News
Loading...

Tuesday 18 April 2017

Ripoti ya CAG Yazidi Kuiaibisha Serikali ya Magufuli..Yaanika Madudu Mengine Katika Sakata la Gesi Asilia ya Mtwara..!!!


RIPOTI ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ya mwaka 2015/16 iliyowasilishwa bungeni mjini hapa Alhamisi, imebaini udhaifu katika mradi wa bomba la usafirishaji gesi asilia kati ya Mtwara na Dar es salaam.

CAG, Prof. Mussa Assad, katika ripoti yake alisema matumizi ya bomba hilo yapo chini ya kiwango na wateja wa gesi asilia hulipa bei inayofanana ilihali wapo umbali tofauti.

Mengine ni kutokulipwa kwa ankara za mauzo ya gesi asilia kutoka Shirika la Umeme (Tanesco) kwenda Shirika la Maendeleo ya Petroli (TPDC), kuwapo kwa kipengele cha mkataba wa mkopo kisichoridhisha na tofauti ya bei ya gesi kwa wauzaji wa gesi kwa Tanesco.

Pia, CAG amegundua mapungufu ya mifumo ya usalama katika kituo cha kinyerezi, mikataba ya uuzaji wa gesi yenye kipengele cha serikali kulipia gesi hata kama haijatumia gesi hiyo na mgogoro usio na ufumbuzi wa bei ya mabaki yaliyotokana na uzalishaji wa gesi.

Katika ripoti hiyo, CAG alisema bomba hilo lilijengwa na kampuni ya maendeleo ya petroli na Teknolojia China (CPTDC) kwa gharama ya dola za kimarekani bilioni 1.283 ambapo kati ya hizo, dola za Kimarekani bilioni 1.225 zilipatikana kama mkopo wa masharti nafuu kutoka benki ya Exim ya China.

Alibainisha marejesho ya fedha za mkopo huo yalitegemea kupatikana kwenye mauzo ya gesi asilia baada ya kukamilika kwa mradi wa ujenzi wa bomba na kuanza kutumika kibiashara.

Prof. Assad alisema katika mapitio ya mkataba wa mikopo, hata hivyo, amebaini bomba hilo lilijengwa kabla ya kutafuta wateja.

Alisema mapungufu hayo yanaathiri malipo ya mkopo kwa vile mauzo halisi ya gesi asilia yatakuwa chini ya kiwango cha makadirio ya awali cha futi za ujazo milioni 138.8 kwa siku.

Pamoja na hayo, CAG alisema kwasasa Tanesco ndiyo mteja pekee wa gesi ambapo anatumia wastani wa futi za ujazo milioni 46.61 kwa siku ambapo makubaliano yalikuwa ni kutumia futi za ujazo milioni 80 kwa siku.

“Nashauri jitihada zaidi ziongezwe katika kuhakikisha wateja zaidi wa gesi asilia wanapatikana ili mkopo uweze kulipwa kabla ya marekebisho ya ulipaji ambayo yataongeza gharama kubwa kwa serikali,” alisema Prof. Assad.

CHINI ASILIMIA 94

Aidha, Prof. Assad alisema matumizi ya bomba hilo yapo chini ya kiwango kwa asilimia 94 kwa sababu lilijengwa ili kuwezesha usafirishaji wa gesi asilia kwa ajili ya matumizi ya kuzalisha umeme, viwandani, kupikia majumbani na kwenye magari.

Katika mapitio ya CAG, aligundua ingawa gesi ilikusudiwa kuwa na matumizi mengi, Tanesco ndiyo mteja pekee aliyeunganishwa kwenye bomba hilo na anatumia asilimia sita.

“Kiasi hicho ni pungufu futi za ujazo milioni 737.39 kwa siku ili kujaza bomba," anasema CAG katika ripoti. "Hii ni tofauti na mkataba wa mauziano na Tanesco inatumia gesi kwenye mitambo sita ya uzalishaji umeme.”

Alishauri TPDC iwasiliane na Tanesco na Wizara ya Nishati na Madini ili wajadiliane ni namna gani mitambo ya uzalishaji umeme ya Tanesco itaweza kumalizika kwa wakati ili bomba la gesi litumike kwa ufanisi na kuweza kulipa mkopo wa bomba hilo kutoka benki ya Exim ya China kwa wakati.

CAG pia alitaka nguvu zaidi zielekezwe kutafuta wateja zaidi wa gesi asilia ili kuongeza mapato ya gesi na kuiwezesha TPDC kutimiza wajibu wa kulipa madeni inapostahili.

Aidha, CAG alisema kutoza bei ya gesi inayolingana kwa wateja wa gesi asilia waliopo Dar es salaam na waliopo jirani na chanzo cha gesi sio njia sahihi ya kuhamasisha upatikanaji zaidi wa wateja.

Prof. Assad alishauri TPDC kuandaa rasimu ya bei ya gesi itakayotofautisha bei za gesi zitakazokuwa zikilipwa na wateja mbalimbali kulingana na umbali kutoka chanzo cha gesi.

CAG alibainisha Tanesco haijailipa TPDC kiasi cha dola za Kimarekani milioni 61.35 za ankra ya mauzo ya gesi asilia.

Alisema TPDC na Tanesco walikubaliana serikali iweke dhamana benki kiasi kinachoweza kulipa mauzo ya gesi kwa miezi mitatu au zaidi kwa ajili ya TPDC na dhamana hiyo iwepo hadi pale Tanesco itakapolipa madeni yanayohusu mauziano ya gesi hiyo.

“Serikali haijaweza kuweka dhamana hiyo, (na) hadi Desemba 2016 jumla ya deni la mauzo kiasi cha dola za kimarekani milioni 61.35 sawa na Sh. bilioni 133.4 kilikuwa kimelimbikizwa bila kulipwa na Tanesco,” alisema.

Alisema hali ya kuchelewa kuilipa TPDC inasababisha TPDC kuchelewa kuyalipa makampuni yanayouza gesi na hivyo kuongeza hali ya sintofahamu kwenye ulipaji wa mkopo wa benki ya Exim ya China.

Kadhalika, alisema kuchelewa huko kwa malipo kunaweza kusababisha gharama zaidi za riba ambayo itatakiwa kulipwa na TPDC kwa wadai wake na kushauri TPDC iandae mpango wa kufanya malipo kwa wauzaji wa gesi na mkopo kutoka benki hiyo ili kuepuka riba kubwa.

Askari wa JWTZ auawa kwa kuchomwa visu na vibaka

ASKARI wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi (JWTZ), MT 94293, aliyefahamika kwa jina la Tekeli Israel (29), ameuawa kwa kuchomwa kisu kifuani na watu wanaodaiwa kuwa ni vibaka. 

Akithibitisha kuuawa kwa askari huyo jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo, alisema tukio hilo lilitokea juzi, saa nne usiku, wakati marehemu, ambaye ni mkazi wa Mbaunda, alipokuwa akitoka kula chips. 

Alisema marehemu wakati akitoka baa ya Tarakea kwenda nyumbani kwake, alipofika eneo la Tarakea Super Car Wash, mtaa wa Simanjiro, kata ya Sombetini, asikia kelele za mtu akiomba msaada. 

Kamanda Mkumbo alisema mtu aliyekuwa anapiga kelele za kuomba msaada alifahamika kwa jina la Tumkislai Abdallah, ambaye alikuwa akiporwa simu ya kiganjani na vibaka. 

"Baada ya marehemu kufika eneo la tukio na kubaini kuwa ni vibaka, aliamua kupambana nao, lakini kwa bahati mbaya walimjeruhi kwa visu na mmoja wao alimchoma nacho kifuani,"alisema. 

Kwa mujibu wa Kamanda Mkumbo, wananchi kwa kushirikiana na polisi, walifanikiwa kumtia mbaroni kibaka mmoja, aliyefahamika kwa jina la Dickson Moses(19), maarufu kwa jina la 'Tukai', mkazi wa Olmatejoo, ambaye alimchoma kisu marehemu. 

Alisema baada ya mtuhumiwa kuhojiwa na polisi, aliwataja wenzake watatu, ambao walifanikiwa kutoroka na kwamba, polisi wanawasaka popote pale walipo. 

"Jeshi la Polisi mkoa wa Arusha linawataka watuhumiwa watatu, ambao majina yao tunayo, waliokuwa na Tukai kwenye tukio la mauaji ya mwanajeshi huyo, kujisalimisha mara moja kwani mkono wa serikali ni mrefu utawatia nguvuni popote pale walipo," alisisitiza. 

Mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo, aliyejitambulisha kwa jina la Ally Omaiy, alisema walimuona marehemu kwenye baa ya Tarakea, ambako alikula chispi kisha akaondoka. 

Alisema dakika chache baadaye, walisikia kelele za mtu anaomba msaada na baada ya kufika eneo la tukio, walimkuta marehemu akipambana na vibaka hao na ghafla walimuona ameanguka chini. 

Alisema baada ya kuanguka, vibaka hao walianza kukimbia, lakini wananchi kwa kushirikiana na madereva wa bodaboda, waliwakimbiza na kufanikiwa kumkamata mmoja wao. 

"Marehemu alipambana na vibaka hao kwa ajili ya kumsaidia Abdallah asiporwe simu, lakini kwa kuwa vibaka walikuwa wanne, walimzidi nguvu na mmoja alifanikiwa kumchoma marehemu kisu cha kifuani na kufariki dunia," alisema. 

Shuhuda mwingine, ambaye ni rafiki wa karibu wa marehemu (Jina linahifadhiwa), alisema marehemu alikuwa anajiandaa kwa ajili ya safari ya kwenda Darfur. 

"Marehemu alikuwa rafiki yangu wa karibu, tunaishi jirani hapa Mbauda, tulishirikiana kwa mambo mengi, licha ya mimi kuwa raia wa kawaida na aliniambia ameshakamilisha taratibu zote za kikosini na kwamba, alikuwa anajiandaa kwa ajili ya kwenda Darfur," alisema. 

Mwili wa marehemu Israel, umehifadhiwa kwenye chumba cha kuhifadhia maiti katika Hosptali ya Mkoa ya Mount Meru, ukisubiri taratibu za kusafirishwa kwenda nyumbani kwao Mbeya kwa maziko.

TUNAKULETEA MFULULIZO WA UIBUAJI WA UBADHILIFU MKUBWA WA FEDHA KATIKA MIRADI MBALI MBALI YA MAENDELEO KUTOKA KWA MKAGUZI NA MDHIBITI MKUU WA HESABU ZA SERIKALI (CAG)

1..Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Aibua Ubadhirifu wa Kutisha Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA)

UBADHIRIFU wa kutisha unaohusisha mabilioni ya fedha, umefichuliwa kwenye Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), ukihusisha uongozi, wafanyakazi, watoa huduma na wazabuni. 

Wanaodaiwa kuhusika na utafunaji wa mabilioni hayo, walitumia mabadiliko mapya ya usajili wa vitambulisho, yaliyoigharimu serikali kupitia manunuzi yasiyo na tija huku wadanganyifu wakitumia mianya iliyopo kujinufaisha wenyewe kinyume na taratibu. 

Kutokana na hali hiyo, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Profesa Mussa Assad, aliagiza wale vote waliohusika na ubadhirifu na udanganyifu wa mabilioni ya fedha, wachukulie hatua kali. 

"Ukaguzi umejiridhisha kwamba, uongozi, wafanyakazi, watoa huduma na wazabuni wameshiriki kwa namna moja au nyingine katika ubadhirifu na udanganyifu kwenye matumizi ya fedha katika mradi wa kuboresha vitambulisho vya taifa,"alisema.
 

Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG)    imeonesha ubadhirifu katika eneo la usajili na utambuzi ambako Sh bilioni 1.2 zililipwa kwa huduma za bima kupitia dalali wa Bima M/s Aste Insurance Brokers Company Limited. Kiasi hicho kililipwa zaidi ya gharama halisi isivyostahili.

Huduma hizi zilipaswa kugharimu Sh milioni 450.2, lakini mamlaka ililipa Sh bilioni 1.7. CAG alibaini kuwa dalali huyo wa bima, alitumia akaunti za biashara katika kupokelea fedha za malipo ya bima ya Sh bilioni 1.7 badala ya akaunti ya amana isivyostahili.

Kwa hali hiyo, CAG amependekeza kampuni ya uwakala wa bima irejeshe Sh bilioni 1.2 zilizolipwa zaidi isivyostahili; na hatua stahiki zichukuliwe dhidi ya Astery Ndege na kampuni hii kwa kufanya udanganyifu na kujipatia fedha kutoka mamlaka. 

Ubadhirifu mwingine alioutaja ulikuwa ni manunuzi ya bima ya vifaa vya usajili na magari yaliyotumika katika mradi wa vitambulisho vya Taifa ya jumla ya Sh milioni 494, yaliyofanyika bila kukihusisha Kitengo cha Manunuzi.

CAG pia ameshauri hatua stahiki zichukuliwe dhidi ya watumishi waliohusika katika udanganyifu, uliobainishwa na kutozingatia sheria za manunuzi ya umma na kuisababishia Mamlaka gharama zisizo na tija sanjari na kuhakikisha kuwa wahusika wanafidia hasara iliyopatikana, kisha kuhakikisha udhibiti wa vifaa. 

Uhakiki wa leja za mafuta, pia ulibaini kuwa lita 1,110 za mafuta ya dizeli yenye thamani Sh milioni 2.2 zilitumika kwa shughuli zisizo za Mamlaka.

Pia Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi ilikopa Sh milioni 455.3 kutoka NIDA kwa ununuzi wa magari manne mwaka 2014, ambazo hadi ukaguzi unafanyika Oktoba 2016 fedha hizo hazikuwa zimerejeshwa. 

Uhakiki wa fomu zenye ‘Barcode’ zilizotengenezwa kupitia mpiga chapa binafsi M/s MFI Solution, ulibaini kuwa fomu 7,762,907 zenye thamani ya Sh bilioni 2.5 zilizopokelewa na mamlaka hazikutumika.

Kadhalika, ilibainika kuwa fomu 8,220,000 zenye thamani ya Sh milioni 519.6 zilizochapishwa tangu mwaka 2011/2012 hadi 2013/2014 hazikutumika; hivyo kutelekezwa katika stoo za TANITA. 

“Hali hii ilitokana na mamlaka kutokuwa na Mpangokazi, hivyo kuingia hasara ya Sh milioni 932.8,” ilisema ripoti hiyo.

Matengenezo ya magari 
Aidha, kwa kipindi cha mwaka 2012/2013 mpaka 2015/2016, Mamlaka ilifanya matengenezo ya magari kupitia gereji binafsi yaliyogharimu Sh bilioni 1.3. 

Nida pia ilifanya matengenezo yaliyogharimu Sh bilioni 1.1 yaliyofanyika na kulipwa na Mamlaka bila kufanyika ukaguzi unaothibitisha kuwapo kwa ubovu wa gari na mahitaji ya matengenezo husika.

Pia kulikuwa na matengenezo yaliyogharimu Sh milioni 197.2, yaliyofanyika na kulipiwa na Mamlaka bila kufanyika ukaguzi wa awali wala ukaguzi baada ya matengenezo.

 Ripoti imeeleza kuwa ukaguzi ulibaini malipo ya Sh milioni 42.7 yalifanyika zaidi ya madai stahili kutokana na udanganyifu wa kuongeza tarakimu katika hati za madai na kutumiwa kwa hati moja ya madai zaidi ya mara moja katika malipo ya kuanzia mwaka 2012/2013 hadi 2015/2016.

Ajira za muda na za kudumu 
NIDA imegundulika kuwa ilikiuka sheria katika ajira za muda na za kudumu, zilizofanywa na mamlaka kuanzia mwaka 2012 hadi 2015, ambapo vibarua 1,071 walipatikana kwa kupigiwa simu bila kutangaza mahali popote kinyume na Sera ya mamlaka hiyo. Ukaguzi ulibaini kuwa NIDA iliomba kupatiwa vibarua kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu na Chuo cha Utumishi wa Umma wapatao 415.

Lakini baada ya kupatiwa vibarua hao, mamlaka haikuwatumia na kubainisha kwamba wangetumiwa siku za baadaye. Ripoti ilifafanua kuwa mamlaka iliamua kuajiri vibarua wengine wapatao 882 bila kutangaza mahali popote, tofauti na watumishi 415 ambao walikwishapatiwa. Pia Septemba 2015 Mamlaka iliajiri watumishi 213 licha ya kibali cha kuajiri kutoka Utumishi kuisha tarehe Aprili 2015.

NIDA pia inatuhumiwa kufanya malipo Sh milioni 16.6 ya kiinua mgongo kwa vibarua, kinyume na mkataba wa ajira ya muda na Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini ya mwaka 2004. 

Ubadhirifu mwingine uligundulika kwenye matumizi ya mafuta ya dizeli na petroli, yaliyonunuliwa na mamlaka yenye thamani ya Sh bilioni 2.3, yaliyotolewa kwenye magari na majenereta, ambapo hayakuthibitika matumizi yake kutokana na sababu mbalimbali.

CAG pia amebaini upotevu wa vifaa vyenye Thamani ya Sh milioni 93.7 katika stoo ya mamlaka. Ukaguzi umebaini kuwa hakukuwa na taarifa rasmi kutoka kwa mtunza stoo juu ya upotevu huo, licha ya kufahamu kuhusu upotevu wa vifaa hivyo. Vifaa vyenye thamani ya Sh milioni 991.4 havikutumika tangu kununuliwa kwake katika vipindi tofauti kuanzia Machi 2013 hadi Oktoba 2016.

Udanganyifu mwingine ulifanyika katika ushindanishi wa wazabuni katika ununuzi wa vifaa vya TEHAMA. Nida ilifanya manunuzi ya Ipad zenye thamani Sh milioni 63.4 zilizonunuliwa kutoka kwa M/s Elite computers baada ya kuonekana kukidhi vigezo vya ushindani na kupewa zabuni saba (7) tofauti. Lakini taarifa za wazabuni ambao waliainishwa kuwa washindani katika zabuni hii, M/s Prudent Enterprise na M/s Morex General Enterprise zilighushiwa; na wazabuni hawa hawakuhusishwa wala kutoa nukuu za bei.

Upangishaji nyumba Mamlaka ilitoa zabuni ya kuipangisha Ofisi ya Mamlaka kwa Mary Mwema kupitia barua ya maombi ya tarehe 06.05.2012 ambapo tangazo la zabuni husika ni la tarehe 25.05.2012 baada ya tarehe ya kuomba.

 “Zabuni husika haikupitia Kitengo cha Manunuzi na haikuwa imeidhinishwa na Bodi ya Zabuni,” inasema ripoti hiyo. 

Pia ripoti ilifafanua kuwa mzabuni wa upangishaji wa jengo la ofisi ya John Masenga haukujumuishwa kwenye mchakato wa tathmini ya kitaalamu licha ya kukidhi vigezo.

NYINGINE NI HII

Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) imebaini kasoro katika mambo matano baada ya kufanya ukaguzi wa hesabu za Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) kwa mwaka wa fedha 2015/2016.

Ripoti ya CAG imekuja wakati wakurugenzi sita, mameneja watano na mhandisi mmoja wakiwa wamesimamishwa kazi tangu Julai mwaka jana kupisha uchunguzi.
 
Ripoti hiyo iliwasilishwa bungeni Aprili 13 mwaka huu, ikiwa ni siku chache tangu CAG, Profesa Mussa Assad aikabidhi kwa Rais John Magufuli.
 
Kasoro zilizobainika katika mfuko huo ni kiwango cha chini cha ukaliwaji wa majengo, usimamizi na udhibiti wa mikopo ya vyama vya ushirika vya akiba na mikopo, udhaifu katika uwekezaji wa ardhi.
 
Ripoti hiyo inabainisha kasoro katika Shamba la Dungu na mradi wa uwekezaji Tuangoma na kasoro nyingine ni katika mkataba wa mshauri katika ununuaji wa Pan Africa Energy Limited kwa Sh551.61 milioni.
 
Ripoti inaonyesha kuwa NSSF imewekeza kwa kiasi kikubwa katika majengo ya kupangisha kwa wateja kama vile hoteli, kampuni, watu binafsi na kutumia sehemu nyingine ya majengo hayo kama ofisi zake.
 
Imegundulika kuwa, kiwango cha upangaji katika majengo tisa ya uwekezaji kilikuwa chini ya kusudio la kiwango cha soko cha asilimia 80. Ripoti inaonyesha kuwa kiwango cha upangaji kilikuwa kati ya asilimia 0 na 43.
 
Rasilimali hizo za uwekezaji katika majengo zinajumuisha hoteli ya Mwanza, Kigoma, jengo jipya la biashara la Old Moshi -Arusha, jengo jipya la biashara la Kaloleni (Arusha), jengo jipya (Kahama), Njiro (Arusha), jengo kubwa la kibiashara Kilimanjaro, Mafao House (Ilala) na jengo kubwa la kibiashara la Morogoro.
 
Mbali na hali hiyo CAG amebaini kuwa NSSF ilisimamisha kutoa mikopo kwa wanachama wa Chama cha Ushirika cha Akiba na Mikopo Juni, 2016 ili kuimarisha usimamizi na kuhakikisha kuwa kuna ukusanyaji wa marejesho ya mikopo.
 
Hata hivyo, mikopo iliyotolewa kabla ya kusimamisha utoaji, ilikuwa na mapungufu ikiwamo mikopo ya Sh1 bilioni iliyotolewa kwa Chama cha Ushirika cha Akiba na Mikopo zaidi ya kiwango cha ukomo.
 
Ripoti inaonyesha NSSF ilitoa Sh21.3 bilioni kwa Chama cha Ushirika cha Akiba na Mikopo cha Bunge (National Assembly Saccos) na Sh2.2 bilioni kwa Chama cha Ushirika cha Akiba na Mikopo cha Jumuiya ya Ndugumbi (Ndugumbi Community Saccos).
 
Utoaji huo wa mikopo ulizidi kiwango cha ukomo kwa Sh1 bilioni, lakini menejimenti ya NSSF ilieleza kwamba mikopo kwa wanachama wa Bunge ilitolewa kama mpango maalum wa kuvutia wanachama wapya kwenye mfuko.
 
Pia, kuna vyama vya ushirika vya akiba na mikopo vilivyopewa zaidi ya asilimia 50 ya mali zote ilizonazo.
 
Pia, CAG ameeleza kuwa ushuru wa stempu ulikuwa haujalipwa kwa vyama vinne vya ushirika ambavyo vilipewa mikopo.
 
Vyama hivyo ni Masoko Madogo Madogo ambacho hakijalipa Sh500 milioni, Ngima (Sh500 milioni), Mafanikio (Sh490 milioni) na Mount Meru (Sh260 milioni).
 
Udhaifu uliogundulika kwenye Uwekezaji wa Ardhi
Kwa mujibu wa CAG, taarifa za fedha za NSSF zilionyesha kuwa iliwekeza kwenye viwanja (Benki ya Ardhi) kwa thamani ya Sh97.2 bilioni, lakini imebainika kuwepo na mapungufu katika ununuaji na uwepo wa ardhi zilizonunuliwa.
 
Ripoti inaonyesha kulikuwa hakuna mipango na upembuzi yakinifu kuhalalisha sababu za kuwekeza katika rasilimali kinyume na aya ya 3.3 ya Sera ya Uwekezaji ya NSSF ya mwaka 2012 inayolitaka shirika hilo kuwekeza rasilimali zake katika miradi inayolipa zaidi ili kuweza kunufaisha wanachama wake.

“Sikuweza kupata hati ya umiliki ya viwanja/mashamba vinne kwa sababu vipo katika mzozo wa umiliki.  Viwanja hivi vilikuwa ni Nunge Beach kilichopo Bagamoyo chenye ukubwa ekari 67.35, kiwanja namba 146/4 Barabara ya Old Moshi kilichopo Halmashauri ya jiji Arusha, Clement Mabina Farm Bugando Magu na kiwanja namba 98 Barabara ya Nyerere (Pugu) Temeke chenye mita za mraba 8,825,” inaeleza ripoti ya CAG.
 
Ripoti hiyo inaeleza kuwa mfuko uliingia mkataba na Halmashauri ya jiji la Mwanza kwa ajili ya kununua viwanja 692 (viwanja 405 eneo la Kiseke na 287 Bugarika) kwa Sh1.89 bilioni.
 
Hata hivyo, ni viwanja 156 tu vilielekezwa Kiseke; wakati hakuna kilichoelekezwa upande wa Bugarika.
 
Pia, imesema kulikuwa na shamba namba 113 lililonunuliwa kwa Sh1.26 bilioni lililopo Mapinga, katika Manispaa ya Kinondoni lenye ukubwa wa hekta 127, lakini ni hekta 58 tu zilizokuwa zimetengwa na kufanyiwa kazi.
 
Ununuaji Pan Africa Energy
Dosari nyingine katika ripoti hiyo ni mkataba wa NSSF na Yakubu and Associates Chambers uliosainiwa Februari 12, 2016 kwa lengo la kutoa huduma ya ushauri ili kuwezesha kupatikana kwa mshirika Kampuni ya Pan Africa Energy Limited kwa ada ya utaalamu ya Sh551.61 milioni kwa ajili ya matumizi ya ziada na kodi za ndani.
 
Ripoti hiyo inaeleza mshauri huyo hakuwa na uzoefu uliohitajika kama ilivyoelekezwa kwenye hadidu za rejea iliyohitaji uzoefu wa mali zisizohamishika za ndani na mambo ya mazingira, ushauri wa kodi za ndani na nje na leseni na kanuni za mfumo wa hydrocarbon.
 
Pia, iligundulika kuwa Kampuni ya Yakubu and Associates Chamber ndiyo iliyokuwa imesajaliwa mwaka huohuo wa kukaribisha zabuni na hivyo washauri hawakuwa na uzoefu na mazingira ya ndani.
 
Mshauri alitakiwa kukagua taarifa ya uchunguzi iliyoandaliwa chini ya mkataba namba NSSF/CS/20/2014-2015 ulioingiwa Desemba 11, 2014 kwa ajili ya kutoa huduma ya ushauri katika ununuzi wa Kampuni ya Pan Africa Energy Limited. 
 
Kanuni iliyotumika ambayo ni namba 257(2)(a) ya Kanuni za Manunuzi ya Umma ya mwaka 2013 (PPR, 2013), haikuwa sahihi.
 
Mkataba ulikuwa umeisha muda wake tangu Aprili 26, 2016, lakini uliongezwa muda kupitia kanuni namba 111(1) ya Kanuni za Manunuzi ya Umma ya mwaka 2013 (PPR, 2013) inayomruhusu ofisa masuuli kuongeza muda wa mkataba na kuelezea sababu ya kufanya hivyo.
 
Ripoti ya CAG inasema mshauri aliwasilisha bili namba 01031604 ya Machi 1, 2016, lakini mpaka kufikia Oktoba 7, 2016 malipo yalikuwa hayajafanyika.
 
Kutokana na kasoro hizo, CAG ameeleza kuwa NSSF haikufuata vigezo vya kuchagua mshauri kama vilivyoainishwa kwenye Kanuni za Manunuzi ya Umma na Hadidu za Rejea (ToR) zilizoandaliwa na Bodi ya Wadhamini.
 
Pia, ameishauri menejimenti ya mfuko huo kuvunja au kusimamisha mkataba kwa kuwa mshauri hakuwa na uzoefu wa kutosha kufanya kazi hiyo.
 
Shamba la Dungu, Tuangoma 
Ripoti ya CAG inaeleza kuwa NSSF iliingia mikataba yenye thamani ya Sh165.4 bilioni kwa ajili ujenzi wa kijiji cha kisasa katika shamba la Dungu na Tuangoma Kigamboni katika Manispaa ya Temeke Dar es Salaam. Mfuko ulikuwa umeshaingia gharama ya Sh73.4 bilioni.
 
CAG anaeleza kuwa miradi ya mfuko huo ilitekelezwa bila kufanya upembuzi yakinifu ambao ungeipa menejimenti uhakika wa uwekezaji. Kwa sababu hiyo CAG ameshindwa kupata misingi na vigezo vilivyoshawishi maamuzi ya menejimenti kuwekeza, malengo ya uwekezaji na mipango ya kurudisha fedha zilizowekezwa.
 
Kutokana na hali hiyo, NSSF iligundua kuwa sehemu ya ardhi ya shamba la Dungu ilikuwa inamilikiwa na Shirika la Nyumba Taifa (NHC), hivyo baadhi ya ujenzi ulihamishiwa Tuangoma.
 
Hata hivyo, menejimenti haikuweza kutoa nyaraka za ununuzi wa viwanja vya Tuangoma na kama vilikuwa vina ukubwa sawa, vinauzika kwenye soko na kiwango cha kurudisha uwekezaji kama ilivyo kwa Dungu.

Kimenuka!!!Kikosi hatari cha US NAVY 'SEAL' chatua rasmi Korea Kasikazini tayari kwa Mapambano.


NI wazi kuwa jaribio lilifanywa na Korea Kaskazini la Makombora yake ya Nukria  limeshtua  Marekani ambapo sasa ni rasmi Kikosi hatari cha Makomandoo wa Kimarekani ambacho ndicho "The Most Feared Force" katika ulimwengu huu cha US NAVY SEAL inasemekana tayari kiko katika Peninsula ya Korea tangu Jana usiku kikitokea jimbo la Florida nchini Marekani.

Hiki ni kikosi hatari zaidi duniani ambacho kazi yake ni kufanya operations ambazo ni hatari zaidi mno na za mwisho. US Navy Seal ni mjumuisho wa makomandoo hatari zaidi wanaotumia ujuzi wa hali ya juu na wenye mafunzo ya kitaalamu zaidi kuliko makomandoo wengine wa majeshi yote ya kimarekani.

Makomandoo hawa ni wale tu wenye uzoefu wa hali ya juu wa kupambana popote pale iwe angani, ardhini au majini, na katika hali yoyote ile iwe barafu, mvua au jua. Na ndio maana ya neno SEAL ambayo kirefu chake ni Sea, Air and Land.

Ni Mara chache sana kutumika. Hawa ni tofauti na majeshi mengine kama US Army Rangers, US Delta Force na mengine. Katika utawala wa Obama, ametoa ruhusa MARA MOJA tu kwa US Navy Seal kutumika. Mara ya mwisho kilitumika usiku wa manane kwa takribani dakika 45 tu kumuangamiza Osama na ni askari mmoja tu alijeruhiwa kwa ajali ya helkopta zisizotoa sauti ambayo ilikosewa ikagonga ukuta wakati makomandoo wakidrop kwenye makazi ya Osama.

Na baada ya Operation Makomandoo hao waliilipua haraka helicopter yao iliyopata hitilafu ili maadui wasigundue teknolojia iliyotumika kutengenezea helicopter hiyo na baada ya kuilipua wakaondoka. Makomandoo wa Navy Seal waliotumika katika Operation hiyo ni 11 tu na Marubani Watatu ambao nao ni kutoka Navy Seal. Na ikumbukwe kuwa Operation hii ilikuwa ikitazamwa live (mubashara) kutoka White House ambapo Obama alikuwa akifuatilia (nilirusha tukio hili), kofia za makomandoo hawa zilikuwa na kamera mbele ambazo zilitumika kurekodi kila kitu kinachoonekana mbele na kurusha kwenye satelaiti had White House. Mkakati huu ulisimamiwa na Mwanamke hatari zaidi anayejulikana kama Alfreda Frances Bikosky ambaye ni Afisa mwandamizi wa CIA na jasusi aliyebobea na pia ni komandoo lakini si memba wa Navy Seal. Bibi Alfreda anajulikana zaidi katika jeshi la Marekani kama MALKIA WA MATESO. Serikali ya Marekani inajitahidi kudhibiti mitandao ya kijamii na google isisambaze picha za mama huyu hatari.

Kikosi hiki cha US Navy Seal hutumika baada ya makomandoo wengine wa majeshi tofauti ya marekani kusoma Jiografia ya sehem husika, ramani ya ngome za adui na silaha zake then Raisi wa Marekani hutoa ruhusa ya NAVY SEAL kutumika kumalizia Operation. Baadhi ya majukumu/kazi za Navy Seal ni Direct Operations (kama wanavyotaka kumfanyia North Korea), Strategic Special Missions (kama walivyofanya kwa Osama), Hostage Rescue (kama walivyofanya miaka ya nyuma kuwaokoa Ma-Intelligensia wa Kimarekani waliotekwa Iran) na Foreign Internal Defence.

Mpaka sasa Navy Seal ina jumla ya Makomandoo 8985 ambao ni hatari mno na wenye roho za kinyama. Makomandoo hawa huwa wapo kwenye mazoezi makali ya special operations na trainings ngumu muda wote huko Virginia, Marekani. Mara chache sana Navy Seal huwa Recruited kwenda CIA kufanya kazi za Kiintelligensia wanapotakiwa. Makamu wa Rais wa Marekani Bwana Pence yuko Korea Kusini na inasadikika ujio wake umeambatana na NAVY SEAL waliojichimbia katika Nyambizi zisizoonekana katika pwani ya Korea..

Habari ya Waziri Mwakyembe Yaliponza Gazeti la Mwanahalisi..Yadaiwa ilitungwa na Mwandishi !!

Katika toleo namba 387 la Jumatatu April 17-23, 2017 gazeti la MwanaHalisi katika ukurasa wake wa kwanza lina habari isemayo: “Mwakyembe: Maisha Yangu Yako Hatarini.”  

Habari hiyo inadai kuwa Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe ambaye ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo hayuko huru na maisha yake bado yapo hatarini, taarifa ambayo imemshtua na kumhuzunisha sana Waziri kwa uzushi, ulaghai na uzandiki uliopitiliza.

 

Mwandishi wa habari hiyo amedai kufanya mahojiano na Dkt. Mwakyembe nje ya viwanja vya Bunge mjini Dodoma Alhamisi iliyopita, na amenukuu kile anachodai ni Waziri kueleza wasiwasi kuhusu usalama wa maisha yake, kitu ambacho hakikutokea.

 

Tunapenda kuutaarifu umma kuwa, habari hiyo ni ya uongo na ya kutunga. Mhe. Dkt. Mwakyembe hajafanya mahojiano yoyote na mwandishi yeyote katika siku na mahali palipotajwa sembuse mwandishi husika wa gazeti la MwanaHalisi ambalo Mhe. Mwakyembe ana kesi nalo Mahakama Kuu kwa kumzushia habari za uongo alipokuwa Waziri wa Katiba na Sheria.

 

Wakati Serikali ikitafakari hatua za kuchukua kwa uandishi wa aina hii, tasnia ya habari inaendelea kukumbushwa kuzingatia weledi na maadili hasa wakati huu ambapo kwa mujibu wa Sheria ya Huduma za Habari Na. 12 ya 2016, tasnia ya habari imepewa hadhi ya kuwa taaluma kamili.




CAG: Mkataba wa Mlimani City na Chuo Kikuu cha UDSM ni Wizi Mtupu..!!!


RIPOTI ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), imeanika madudu ya mkataba wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kwenye mradi wa Mlimani City.

Madudu hayo yanaonyesha namna chuo hicho kinavyopoteza mamilioni ambako amependekeza mkataba huo ufanyiwe marekebisho.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo iliyowasilishwa bungeni hivi karibuni, ujenzi wa mradi wa Mlimani City ulianza Oktoba Mosi mwaka 2004, ukikadiriwa kukamilika Septemba Mosi mwaka 2016.

Hata hivyo, CAG ameshauri yafanyike marekebisho katika baadhi ya vifungu vya mkataba huo.

Ripoti hiyo inaonyesha kwamba moja ya sababu ya kukiukwa maeneo ya mkataba wa wabia hao wawili ni uzembe wa menejimenti ya chuo.

Ripoti inasema: “Tulibaini kwamba mradi mdogo wa hoteli ya nyota tatu (ambayo ina vyumba 100 kikiwemo chumba cha mikutano kinachochukua watu 1,000) na uboreshaji wa bustani ya botania, ikiwa ni sehemu ya mradi wa Mlimani City, haujakamilika kwa kipindi cha miaka 10 tangu tarehe ya makubaliano ya kumaliza mradi.

“Mtazamo wangu ni kuwa hakuna ufuatiliaji wa karibu, usimamizi na tathmini ya mkataba huo kwa uongozi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

“Kwa sababu hiyo kuna uwezekano wa kushidwa kumalizia kazi iliyobaki kwa sababu ya ongezeko kubwa ya gharama ya kumalizia mradi tangu kipindi kilichopangwa kupita.

“Menejimenti ya Chuo Kikuu inashauriwa kuuangalia upya mkataba iliouingia na Mlimani City Holding, kuharakisha umaliziaji wa miradi,” ilieleza ripoti hiyo ya CAG.

Ripoti hiyo pia inaainisha ukiukwaji wa ulipaji wa ada ambayo mwekezaji anatakiwa kuitoa kwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa kifungu cha 1.1(j) cha mkataba pamoja na kifungu 10.1 cha hati ya ukodishaji wa uwanja, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kinapaswa kipate asilimia 10 ya mapato ya kodi ghafi.

“Kinyume na kufungu tajwa hapo juu, Mlimani Holding Limited (MHL), hufanya hesabu za gawio la kodi ya Chuo Kikuu kwa kuzingatia asilimia 10 ya mapato ya kodi baada ya kutoa gharama za uendeshaji badala ya kujumuisha gharama za uendeshaji.

“Ukiukwaji huu unakifanya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kuwa katika hatari ya kupoteza kiasi kikubwa cha mapato kutoka katika mradi wa Mlimani City,” inasema ripoti hiyo.

CAG anaishauri menejimenti ya chuo hicho ifanye upya hesabu za gawio lake la asilimia 10 kutokana na mkataba na kuomba kulipwa na mpangaji kiasi kilichokuwa kimekosewa.

Pia alishauri kuwasiliana na mpangaji na kufikiria kubadilisha mkataba kuweka vifungu ambavyo vitaruhusu idara ya ukaguzi ya ndani ya chuo kuangalia mapato na gharama za uendeshaji za mradi.

Ripoti hiyo pia imeainisha udhaifu wa ufuatiliaji na usimamizi wa mapato kutoka kwa wapangaji wadogo kwenye mradi huo.

Inasema kifungu cha 11.2(l) cha hati ya makubaliano, mpangaji (MHL) anapaswa kutopangisha mtu yeyote ambaye hajathibitishwa na Mpangishaji (Chuu Kikuu cha Dar es Salaam), ikiwa ni njia ya kudhibiti mapato yake.

Kinyume na makubaliano ya hayo, ukaguzi wa CAG umebaini kwamba MHL amepangisha majengo kwa wapangaji wengine bila kupata kibali cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

“Kuna upungufu wa utekelezaji wa vipengele vya mkataba kwa upande wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam hivyo kusababisha Chuo kushindwa kujua kwa usahihi mapato ya kodi kutoka kwa wapangaji wote.

“Menejimenti ya Chuo Kikuu cha Dar-es-salaam inashauriwa kutekeleza vifungu na vipengele vyote vya hati ya makubalian ya upangaji kikiwamo kifungu 11.2 (l) cha hati ya makubaliano ambacho kinakitaka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kuwathibitisha wapangaji wadogo wadogo,” anashauri CAG.

Ripoti hiyo pia inaonyesha mapitio ya mkataba wa upangishaji wa ardhi kati ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Mlimani Holding Limited yamegundua kwamba mkataba haumpi mmiliki wa ardhi haki ya kukagua kazi zinazofanywa na mpangaji.

“Katika hali hii, mpangishaji, ambaye ni Chuo Kikuu cha Dar es Salaam hawezi kujua endapo mpangaji, Mlimani Holding Limited, anakiuka mkataba katika uendeshaji au kuna baadhi ya wapangaji wa nyumba hawawekwi wazi na mpangaji huyu,” inasema ripoti.

CAG anashauri Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kuwasiliana na Mlimani Holding Limited kupata haki ya kukagua shughuli za miradi kwa manufaa ya pande zote mbili.

Ripoti hiyo inasema pia kwamba mapitio ya mkataba yamegundua mkataba huo hauelezei hali halisi ya ugawanaji mali mkataba utakapoisha (miaka 50 au 85 kutokana na makubaliano ya pande mbili).

“Hakuna makubaliano yoyote yanayoelezea mgawanyo wa mali na miondombinu itakayokuwapo wakati mkataba unaisha.

“Kwa hali hii, kuna uwezekano wa kutokea mvutano wa sheria mwisho wa mkataba. Hali hii ikitokea, Chuo Kikuu kitakosa msaada wa sheria.

“Uongozi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, unashauriwa kuingia katika mazungumzo na Mlimani Holding Limited kuweka vifungu vitakavyoonyesha haki ya kila upande wakati wa mkataba utakapoisha,” anaeleza CAG.

Ripoti hiyo pia inasema Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ( kiliingia katika makubaliano na kampuni ya Ernest and Young kufanya ukaguzi maalumu kujua kiasi cha mapato ambacho kinaidai kampuni ya Mlimani Holding Limited katika kipindi cha Mei Mosi mwaka 2006 mpaka Juni 30 mwaka 2014 na kubaini kutolipwa dola za Marekani 57,607.

“Wakati wa ukaguzi niligundua kuwa kiasi cha Dola za Marekani 309,458 kilitakiwa kipokelewe na Chuo kutoka MHL, lakini usuluhisho wa hesabu ulionyesha MHL ililipa Dola za Marekani 213,850 kupitia uhamisho wa benki kwa njia ya eletroniki na kubakisha Dola za Marekani 57,607.

“Kuna ufuatiliaji duni kwa upande wa menejimenti ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam katika kukusanya deni hilo. Menejimenti ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam inashauriwa kuongeza nguvu katika kufuatilia na kukusanya deni wanalolidai MHL,” inasema ripoti hiyo.

Snura Ajipanga Kumuanika Mpenzi Wake

DAR ES SALAAM: Staa wa mduara Bongo, Snura Mushi ‘Snusexy’ amefunguka kuwa, baada ya ukimya wa muda mrefu na kuzushiwa kila mwanaume, sasa anajipanga kumuanika laazizi wake ili watu wamtambue kwani usumbufu umekuwa ‘too much’.

Snura aliliambia Wikienda kuwa, ishu ya kuambiwa mara anatoka na mtu fulani, mara na Mwarabu ni suala linalomsababishia usumbufu hivyo mashabiki wake wakae mkao wa kula kwani kuna kitu kikubwa anataka kukifanya katika kumtambulisha mwanaume anayetoka naye.


“Soon nitawatambulisha shemeji yao maana naona ni miaka miwili sasa nasingiziwa mambo mengi, mara yule mara huyu lakini wasiwe na wasi kwani kuna kitu kikubwa kinakuja,”  alisema Snura.


 

Gallery

Popular Posts

About Us