KINGAZI BLOG: 04/30/17

HABARI KARIBU YAKO ZAIDI.

Breaking News
Loading...

Sunday 30 April 2017

MAJINA YA WALIONA VYETI FEKI TANZANIA NZIMA HAYA HAPA NA WILAYA WANAZO TOKA.


Image result for VYETI FEKI


Baada ya Rais Magufuli kusema majina ya watumishi walioghushi vyeti yaanikwe; sasa yamewekwa hadharani.

Orodha ni hii hapa

Attached Files:

Ma'admin' wa makundi Whatsapp kukiona cha moto India


Kuwa msimamizi wa kundi katika whatsApp (WhatsApp Group Chat Admins) kwa wengi sio kitu kikubwa sana. Kimsingi ni kuwezesha kuongeza wanachama katika Kundi au kumuondoa yeyote katika kundi husika.

Hata hivyo nchini India ni zaidi ya hivyo, kuwa msimamizi wa kundi huko ni jambo linalomtaka msimamizi kuwa makini zaidi.

Kwa mujibu wa taarifa ya Economic Times serikali ya India na mahakama inataka kuwafanya wasimamizi wa makundi ya WhatsApp kuwa wasimamizi ambao watadhibiti taarifa za uongo zinazoenezwa na watu wengi kupitia whatsApp.

Kwa mujibu wa sheria mpya Msimamizi wa kundi anaweza kutupwa gerezani kama muhusika wa kusambaza habari za uongo endapo kama hakuchukua hatua ya kumtoa katika kundi lake na kumripoti Polisi.

Kama itatokea mtu ametoa habari ya uzushi katika Kundi basi msimamizi anatakiwa kumtoa (removed) katika kundi na kumripoti haraka zaidi Polisi ili hatua dhidi yake zifuate.

Kama habari ya uongo itazidi kuenea kwa kusambazwa kutokea kundi husika na msimamizi wa kundi hakufuata hatua hizo basi atachukuliwa hatua za kisheria kama aliyesaidia kupotosha umma.

Lengo la hatua hii ni kusaidia kukabiliana na kuenea kwa taarifa za uongo. Nchini India watu zaidi ya milioni 200 wamejisaJIli katika WhatsApp.

Wakati wa kampeni za uchaguzi wa Marekani kulikuwa na taarifa nyingi za uongo na uzushi kupitia makundi ya whatsapp.

Na hata hivi karibuni pia iliripotiwa kwamba Ufaransa ilikuwa na mafuriko ya habari za uongo zilizokuwa zinapikwa kutokea makundi ya WhatsApp katika kampeni za uchaguzi unaopigiwa kura leo.

Facebook nao wameanza mpango wa kupambana na taarifa za uongo kupitia mtandao wao.

Kwa sasa Dunia imekumbwa na wimbi la taarifa za uongo na uzushi kupitia mitandao ya kijamii. Kuanzia taarifa mpaka picha nyingi zimekuwa za uongo na uzushi.

Kwanini watumiaji wa mitandao ya kijamii wamekuwa wako mbele katika kuzusha na kusambaza habari za uongo? tatizo ni nini au msukumo wao ni upi?

NAMKUBALI DIAMOND KULIKO ALIKIBA -AMBER LULU

#AmberLulu kupita ukurasa wake Instagram alikuwa mubashara ameweza kuonesha ushabiki wake hadharani na mapenzi yake kwa #DiamondPlatnumz.

Akiwa mubashara kupitia kwenye akaunti yake ya Instagram amesema kuwa ajaona Msanii yoyote ambaye anaweza kumlinganisha na #Diamond kwani ni msanii mkubwa Afrika hata #AliKiba bado ajafika level za #DiamondPlatnumz

#Amberlulu👉“Diamond ni msanii mkubwa sana Afrika hata  Ali Kiba atii mguu hata kidogo hata ukiangalia katika timu yake Mond yuko vzuri na hata madensa wake wanaishi vizuri hata mtu anayemlinganisha Kiba na Chibu anakosea sana”Alisema
.
.
JE, KAULI YA AMBER_LULU INA UKWELI WOWOTE???

Pichaaz!! Anthony Joshua Amtwanga Wladimir Klitschko kwa TKO

Anthony Joshua ameonyesha kuwa yeye ndiye mfalme mpya wa ngumi za kulipwa kwa uzito wa juu baada ya kumshinda mkongwe Wladimir Klitschko kwa TKO katika raundi ya 11.

Pambano hilo la raundi 12 kwenye Uwanja wa Wembley jijini London, England lilikuwa kali na la kuvutia.








Inakuhusu hii..Upimaji wa Ukimwi wa Nyumba Hadi Nyumba Unaanza Rasmi Kesho..Jiandae Kikamilifu!!


UTAFITI wa viashiria na matokeo ya Ukimwi wa mwaka 2016 ambao unahusisha upimaji wa ugonjwa huo kaya kwa kaya kwa Mkoa wa Dar es Salaam, utaanza kufanyika Mei mwaka huu, ambapo jumla ya kata 31 kutoka wilaya tatu za mkoa huo ndizo zitakazoshiriki.

Utafiti huo pia utahusisha ukusanyaji wa taarifa zisizohusu maambukizi mapya ya Virusi Vya Ukimwi (VVU), kiwango cha VVU mwilini na kwa watu wanaoishi na ugonjwa huo, wastani wa maambukizi kwa watu wa rika zote na wingi wa chembechembe za kinga mwilini (CD4).

Hayo yalisemwa jana Dar es Salaam na Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema kwa niaba ya Mkuu wa mkoa huo, Paul Makonda wakati wa uzinduzi wa utafiti huo wa mwaka 2016/17 na kusema kuwa wakati wa utafiti huo, baadhi ya vipimo ambavyo wanakaya watapimwa, vitatolewa majibu papo hapo.

Utafiti huo umeanza kufanyika Oktoba mwaka jana na unatarajia kukamilika Julai mwaka huu ambao unashirikisha Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) na Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali Zanzibar, Shirika la ICAP la Chuo Kikuu cha Columbia na Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS).

Aidha, alisema utafiti huo ni wa nne kufanyika nchini, unaoangalia masuala ya afya ambapo utafiti wa kwanza ulifanyika mwaka 2003/2004, wa pili ulifanyika 2007/2008 na wa tatu ulifanyika mwaka 2011/12.

Alisema katika tafiti hizo zilikuwa zikiwahusisha wananchi wenye umri kati ya miaka 15 hadi 49 tofauti na utafiti huo ambao kwa mara ya kwanza utawahusisha wananchi wa rika zote katika kaya zilizochaguliwa.

Mjema alisema utafiti huo utaangazia viashiria vya usugu wa dawa, kiwango cha maambukizo ya kaswende na homa ya ini kwa watu wenye umri wa miaka 15 na zaidi. Sambamba na hayo, utafiti huo pia utakusanya taarifa za upatikanaji na utumiaji wa huduma zitolewazo katika kudhibiti maambukizi ya VVU na Ukimwi na viashiria vya tabia hatarishi zinazochangia maambukizi ya VVU.

HABARI KATIKA MAGAZETI YA LEO 29 / 4 / 2017





















Hizi hapa habari katika magazeti ya leo tar 29 / 4 / 2017





















 

Gallery

Popular Posts

About Us