KINGAZI BLOG: 04/10/17

HABARI KARIBU YAKO ZAIDI.

Breaking News
Loading...

Monday 10 April 2017

Kauli ya Halima Mdee Baada ya Askofu Gwajima Kumtaka Amuombe Radhi Spika wa Bunge

Askofu Mkuu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Dr. Josephat Gwajima jana  alijitokeza hadharani mbele ya waumini wa kanisa lake na kumtaka Halima Mdee Mbunge wa CHADEMA kumuomba radhi Spika wa Bunge Job Ndugai kwa maelezo kuwa alimtukana. Gwajima alisema, kama hatafanya hivyo, basi ataitumia Jumapili Ijayo 'kumchapa' Hadharani

 Kutokana na madai hayo, Halima Mdee amejitokeza hadharani na kumjibu Gwajima

"Namuheshimu sana Mch. Gwajima,sitajibizana nae kwenye mitandao. Niweke rekodi sawa sijamtukana na wala sitarajii kumkosea heshima Spika.

"Hayo ya J2 namwachia yeye! Yangu na yaliyojiri Bungeni.. Najua jinsi ya kuyahandle. Yawezekana yalishamalizwa kabla ya Ibada yake LEO."


Gwajima Amchana Diamond..Amhusisha na Freemason..Habari Katika Magazeti ya Leo 10/4/2017..!!!






Wanaoniita shujaa watanigeuka - Nape Nnauye

Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye amedai wanaomuita shujaa leo ipo siku wanaweza kumgeuka kwa sababu kama binadamu bado ana safari ndefu na anaweza kujikwaa ndiyo maana hataki kulivaa jina hilo bali anahitaji watanzania waendelee kumuombea.

Akizugumza akiwa Mtama Mh. Nnauye amesema hawezi livaa jina hilo  bali amelipokea kwakuwa wananchi wameamua kumpatia jina hilo kwani hata sababu za kuitwa jina hilo zipo tofauti tofauti.

"Sikatai kuitwa Shujaa kwa sababu wao wenyewe ndiyo wameniita, lakini siyo jambo ambalo nitalivaa.  Hao hao wanaoniita shujaa siku nyingine wanaweza kunigeuka kwa sababu binadamu ukiwa hai unaweza kujikwaa safari bado ni ndefu nachotaka kuwaomba tu wananchi waendelee kuniombea. Hata hivyo sababu za kuitwa shujaa kila mtu ana sababu yake, mwingine atakuambia kwa sababu hujatetereka wengine wanasema umesimamia ukweli, kwa hiyo jina hilo siwezi kulivaa ila siwezi kulikataa". Alisema Nape.

Mh. Nnauye jana alipata nafasi ya kuzungumza na wananchi wa Mtama kwa mara ya kwanza baada ya kuvuliwa uwaziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Machi 22 mwaka huu.

Kimenuka!!! Hivi umeona alichokiandika Diamond kuhusu shetta?? SOMA HAPA


HEBU SOMA HAPA👇👇👇

NOMA SANA!!RC PAUL Makonda Aandika Ujumbe Huu Wenye Fumbo Ndani yake

RC wa Dar Ameandika ujumbe wa mafumbo kupitia ukurasa wake wa Instagram, Haijaeleweka na Nani analegwa hapo..Embu jisomee na wewe labda unaweza tegua mtego

By @paulmakonda 
"Hakuna kitu kibaya kama kudanganywa na mtu huku ukijua anakudanganya na wakati huo huo anaekudanganya hajui kama unajua anakudanganya. Basi kazi yako inakuwa nikucheka kimoyomoyo" 
.
TOA MAONI YAKO HAPA

Roma Mkatoliki Usiposema Ukweli Leo, Wakatoliki Halisi Tutausema Jumanne..!!!


Leo tunataka kusikia yafuatayo..wale watu wawili waliokuja kukuhoji kwanini walikuwa hawakujui je walielekezwa na nani kwako?..mlipoingia ndani ya ile noah kwanini nyote mlifungwa vitambaa vichwani na mkaja kufunguliwa mlipoingizwa katika nyumba ya kwanza mikocheni na siku mbili baadae mkahamishiwa katika nyumba iliyopo Oysterbay..

Kwanini kati yenu wote ni wewe tu ndiyo uliyepigwa sana na virungu magotini huku ukikanyagwa kila mara mbavuni mwako na kuna wakati ukawekewa bastola kichwani ndipo ukaanza kunywea..ni kiongozi gani ambaye juzi usiku alikuja katika hiyo nyumba na kuzungumza nanyi kisha akawatishieni nyote..yule dada aliyekuwa akiongoza mateso yenu huku akiwa anawahoji na kuwarekodi anatoka katika taasisi gani..

Kiongozi gani aliomba kuongea na wewe jana asubuhi kabla hamjaondoshwa hapo oysterbay na kupelekwa polisi?

ole wako usiseme huu ukweli .

SIO MAONI YETU NI HAYO NI MDAU WETU

SOURCE:JF

 

Gallery

Popular Posts

About Us