KINGAZI BLOG: 03/15/17

HABARI KARIBU YAKO ZAIDI.

Breaking News
Loading...

Wednesday 15 March 2017

Ndege ya ‘wanawake pekee’ kutoka Malawi kutua Tanzania

HakiMALAWI AIRLINES / FACEBOOKImageNdege hiyo itakuwa chini ya Kapteni Yolanda Kaunda na Lusekelo Mwenifumbo

Shirika la ndege la Malawi, Malawi Airlines, limetangaza kwamba linapanga kufanya safari ya ndege itakayosimamiwa na wanawake pekee Alhamisi wiki hii.

Safari hiyo ya ndege, ambayo itakuwa na marubani na wasaidizi wa abiria kwenye ndege wote wakiwa wanawake, itakuwa ya kwanza kuandaliwa na shirika hilo.

Ndege hiyo itasafirisha abiria kutoka mji wa Blantyre hadi Dar-es-Salaam nchini Tanzania na itatua kwa muda Lilongwe kabla ya kuelekea Dar .

Taarifa kutoka kwa shirika hilo la ndege, lilisema lengo ni kufanikisha ulimwengu ambao "unakumbatia jinsia zote".

Ndege hiyo itakuwa chini ya Kapteni Yolanda Kaunda akisaidiwa na Lusekelo Mwenifumbo.

Bi Mwenifumbo, 24, alisomea taaluma ya uchukuzi wa ndege mjini Addis Ababa, Ethiopia.

ImageShirika la ndege la Malawi Airlines lilianzishwa Julai 2013 baada ya kuvunjwa kwa shirika la awali la Air Malawi Februari mwaka huo

"Lengo la hatua hii ni kuwahamasisha wasichana ambao wangependa kufanya kazi katika uchukuzi wa ndege lakini kwa njia moja au nyingine hufikiria ni vigumu au kwamba ni kazi ambayo wanawake hawaiwezi," taarifa ya Malawi Airlines ilisema.

Ndege hiyo aina ya Bombardier Q-400 itapaa kutoka Blantyre saa nne asubuhi Alhamisi.

Bunge la  lapiga Marufuku upigaji Punyeto




Mwanasiasa mmoja mwanamke anachukua hatua isio ya kawaida katika kile anachosema ni sheria kali za uavyaji mimba kwa kuwalenga wanaume wanaofanya punyeto.

Lengo la sheria hiyo yake anasema ni kuwalinda watoto ambao hawajazaliwa kila mahali.
Ndio sababu anataka mwanamume atakayemwaga mbegu zake za kiume nje ya uke wa mwanamke ama kutengezwa nje ya kituo cha matibabu kutozwa faini ya dola 100.

Iwapo mwanamume atapatikana na hatia kwa kumwaga mbegu hizo nje itachukuliwa kama kitendo dhidi ya mtoto ambaye hajazaliwa.

''Iwapo inaonekana kama hatua isio ya kawaida basi hivyo ndivyo inavyopaswa kuwa''alisema Farrar.
Jessica Farrar , ni mwanachama wa Democrat katika bunge la wawakilishi jimbo la Texas aliyewasilisha muswada huo nambari 4260 wiki iliopita.

Anajua hautaidhinishwa kuwa sheria.
Lakin anasema kuwa sio rahisi zaidi ya kuwawekea wanawake sheria kali za uavyaji mimba katika jimbo la Texas wakati mtu anapochagua kutaka kuavya mimba.

Hatua yake ya mwisho ilikuwa hivi karibuni kuhusu miswada kadhaa ya wanawake anayosema inapunguza haki za wanawake.

Sheria ya hivi karibuni ilikuwa ile inayowashinikiza wanawake kuchagua kuzika ama kuchoma mabaki ya viinitete kutokana na mimba iliotoka ama ile iliotolewa.

Wakati wa kusikizwa kwa muswada huo mnamo mwezi Agosti, Seneta wa jimbo hilo Don Huffines alisema: kwa muda mrefu sasa Texas imeruhusu viumbe visivyo na hatia kutupwa na uchafu.

Iwapo tunachukulia hatua hizi na umuhimu mkubwa kwa sababu ya maisha ,basi, hatuwezi kupoteza hata mbegu moja.

lakini wakosoaji wake hawakupendelea .
''Huu ni ujinga wa wazi'' mtu mmoja alituma ujumbe wake katika mtandao wa Twitter akisema kuwa ''ni yai lililorutubishwa pekee ambalo linahitaji kulindwa akiuliza iwapo angeweza kutumia sheria hiyo dhidi ya wanawake walio katika hedhi.

Jimbo la Texas lina sheria kali za uvanyaji mimba nchini Marekani ijapokuwa mahakama ya juu ilibatilisha marufuku ya uavvaji mimba uliosababishwa na dawa baada ya wiki saba mwaka uliopita.
Sheria hiyo inamaanisha kwamba kliniki zinazoavya mimba ni chache mno.

Kulingana na gazeti la Tribune katika jimbo hilo kulikuwa na kiliniki 19 za uavyaji mimba mnamo mwezi Juni 2016, nyingi zikifanya kazi katika maeneo ya mijini.

CCM Watangaza Kumshughulikia Makonda,Magazeti ya Tanzania Leo jumatano 15/3/2017.




WhatsApp kurudisha “status” za maneno..


Kuna tetesi kwamba WhatsApp ipo mbioni kurudisha status za maneno baada kuondoa huduma hiyo katika toleo lake la hivi karibuni, hii ni habari nzuri kwa watumiaji ambao hawakupendezwa na mfumo mpya ulioletwa mwezi uliopita.

Muonekano mpya wa WhatsApp baada ya mabadiliko ya status

Kulikuwa na maneno mengi baada ya WhatsApp kuleta mabadiliko makubwa katika mfumo wa status kwa kutambulisha namna ya kuweka status inayofanana na mfumo unaotumiwa na mtandao wa Snapchat, baadhi waliufurahia utaratibu huu lakini kulikuwa na wengi ambao waliona mabadiliko haya kama kosa kubwa kutoka kwa WhatsApp.

Nini chanzo cha tetesi hizi!?
Tetesi za kurudishwa kwa huduma ya status za maneno katika WhatsApp zinakuja baada ya toleo la WhatsApp beta kuletwa likiwa sio tu na mfumo mpya wa status lakini pia  mfumo wa status za maneno kama zamani. Hata hivyo bado watumiaji watalazimika kutumia app hii pendwa pamoja na vipengere vipya ambavyo vililetwa na mwezi uliopita.

Nini Kingine kipya kipo jikoni?
Kunatetesi kwamba Whatsapp pia ipo mbioni kuyaruhusu makampuni kuweza kuwatumia taarifa mbalimbali watumiaji wa mtandao huu, taarifa hizi zinahisiwa zitakuwa ni aina fulani ya matangazo ama taarifa kuhusu huduma fulani. Ingawa hatua hii inaweza kupata upinzani mkubwa kutoka kwa watumiaji lakini msukumo wa wawekezaji ni dhahiri ndio utakaokuwa uamuzi wa mwisho.

Mabadiliko haya  yatawafikia wakina nani?!
Ingawa sio kila kinachojaribiwa katika WhatsApp beta hufanikiwa kuingia katika soko lakini kuna nafasi kubwa huduma hizi zinazojadiliwa zikawafikia watumiaji wa kawaida siku za usoni.

 

Gallery

Popular Posts

About Us