KINGAZI BLOG: 04/16/17

HABARI KARIBU YAKO ZAIDI.

Breaking News
Loading...

Sunday 16 April 2017

kimenuka!! Majasusi wa Marekani Waanza Kuingia Korea Kaskazini Tayari kwa Vita..Siri Nzito za Silaha za Nyuklia za Korea Zaifichuliwa.


Hii habari ya majasusi wa USA, majasusi hawa wa America wenye Asili ya korea wamejipenyeza ndani ya korea kaskazi kuanzia December mwaka jana 

Na kwa taarifa zilizovuja Rais wa korea kaskazin ameamuru kusitisha Visa kwa raia wanaotoka nchi za magharibi kutokuingia North Korea kwa muda usiojulikana 

Pia ametoa wito kwa raia wazalendo wa korea kaskazin kutoa taarifa kwa mtu yeyote wanaemshukia hana maadili ya korea kaskazin 

Siku ya jumapili iliyopta wanajeshi watatu wamenyongwa korea kaskazin wakishutumiwa kuvujisha mipango ya jeshi Lao kwa jeshi la USA 

Pia Rais wa korea kaskazin jana alia muru kurushwa kwa kombora kwa siri kubwa ambalo badae lilifeli na mwana jeshi moja wa korea kaskazin anasemekana alituma kila kitu kilichofanyika makao mkuu pentagon 

Ndio maana Leo mkuu wa idara ya jeshi u pande wa peninsula alitangazaa kushindwa kwa kombora lililorushwa la North Korea kufeli vibaya 

Mike pence, makamu Rais wa USA Ambaye yupo njian kuelekea South Korea 

Inasemekana ameambatana na nyambizi zisizoonekana katika peninsula ya korea kaskazin 

Majasusi wa USA wamenasa mawaasiliano kati ya wazir wa mambo ya nje ya urusi, wakiwasiliana na wenzao wa China Pmj na uturuki na North Korea na iran 

Wakat huo huo makao Rais pence anawasiliana na Donald Trump akiwa njian kuelekea South Korea 

Wazir wa mambo ya nje wa uingereza amempigia simu wazir wa mambo ya kigeni wa USA kumhakikishia juu ya North Korea kurusha kombora lililofeli 

Na Inasemekana usiku mzima wa jana Rais Trump alikuwa kwenye mazungumzo mazito na waziri wa ulinzi wa USA pamoja na mkuu wa majeshi 

Wakuu ni baampa to baampa 

Mimi naomba USA asipagane Ase, maana madhara yake yatakuwa ni kwa dunia nzima 

Namwomba Mungu awaongoze washauri wa Trump wasimshauri kuvamia North Korea 

Wamshauri kuiwekea vikwazo tu 

We need peace and not war

IGP asema Tunawasaka Watu Wanaofurahia na Kukebehi Mitandaoni Baada ya Askari wetu Kuuwawa.


Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Ernest Mangu amesema jeshi hilo linawasaka watu wanaofurahia mitandaoni na kukebehi baada ya askari wake kuuawa.

IGP ameyasema hayo wakati Miili ya Askari nane wa Jeshi la Polisi ikiagwa leo Mkoani Pwani.

IGP Mangu amesema, tulitumue tukio hili kama changamoto, ili tupeane nguvu badala ya kukatishana tamaa. Kuna watu wameanza kukejeli kwenye mitandao baada ya hili tukio kutokea, mheshimiwa Waziri nakuhakikishia tutawasaka hao wanaoendeleza kejeli badala ya kutupa pole wanakejeli na wengine wanafurahia.

Na mtu wa namna hii anefurahia si mwingine isipokuwa ni mhalifu kama huyu aliyefanya tukio hili baya, nao tutawashughulikia kwa mujibu wa sheria tutakapowapata.

Ila tu niombe wananchi tutumie tukio hili kama changamoto na tutiane nguvu ili mwisho wa siku tuweze kushinda hii vita ya uhalifu kwa sababu hakuna mtu anayependa uhalifu na wote tunapenda amani.

KINGAZI BLOG TUNAWATAKIA HERI YA SIKUKUU YA PASAKA WADAU WETU WOTE



Kwa niaba ya Timu nzima ya Kingazi Media
ikishirikiana na Killertz blog Tundalako blog Mapenzichoice blog na kingazi blog Tunawatakia wote Heri ya sikukuu ya pasaka wote Tutaendelea kuwapa kila kinachojiri asanteni sana kwa support.Msherehekee kwa Amani. Mwenyezi Mungu awalinde na kuwatunza MBARIKIWE SANA

Salaam
Kutoka kwa

TITO EMMANUEL KINGAZI

MKURUGENZI WA KINGAZI MEDIA.


Imefichuka..kumbe Ufisadi Mzito Wagundulika Magari ya Mwendokasi.!! Hebu soma hapa


RIPOTI ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Prof. Mussa Assad kwa mwaka wa fedha 2015/16, imefichua udhaifu mkubwa katika mradi wa mabasi yaendayo kasi jijini Dar es Salaam.

Katika ripoti hiyo iliyowasilishwa bungeni mjini hapa juzi, CAG Assad anasema kuwa katika ukaguzi wake alioufanya kwenye mradi huo, amebaini Wakala wa Usafiri wa Mwendokasi Dar es Salaam (DART) una upungufu mwingi.

Anasema katika utoaji wa huduma ya usalama katika vituo vya DART na makao makuu ya wakala Jangwani, amebaini kuwa Mei 5, 2016 DART iliingia mkataba wa miezi 12 na M/S China Tanzania Security Company Ltd wa utoaji huduma ya ulinzi kwenye vituo vya DART na Jangwani kwa jumla Sh. milioni 178.652.

Hata hivyo, Prof. Assada anasema kuwa katika mapitio ya taratibu za manunuzi, imebainika matangazo na zabuni zilizotolewa hazikuwasilishwa PPRA, mkataba ulisainiwa baada ya tarehe ya kukamilisha mkataba kuisha kinyume cha Kanuni 370(1) cha Kanuni ya Manunuzi ya Umma ya Mwaka 2013 na pia nakala ya mkataba haikuwasilishwa kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) kwa ajili ya kupitia na kuhakikiwa (vetting) kinyume cha Kanuni 59(1) na (2) vya Kanuni ya Manunuzi ya Umma ya Mwaka 2013.

"Kutokana na mazingira hayo ni vigumu kuthibitisha kwamba taratibu sahihi za manunuzi zilifuatwa katika utoaji wa huduma za usalama, na iwapo matumizi ya Sh. milioni 178.652 yalikuwa matumizi sahihi ya fedha za umma," anasema.

CAG Assad anapendekeza kuwa menejimenti ya DART ifuate sheria na kanuni za usimamizi wa mikataba, na kuweka mikakati ya jinsi ya kutatua upungufu unaojitokeza, hivyo wahakikishe Wakala wa Serikali na taasisi nyingine wanaimarisha mifumo ya ndani ili kuhakikisha upungufu haujitokezi kwa baadaye.

CAG pia anasema kuwa katika ukaguzi wake wa mwaka wa fedha 2015/2016, amebaini kwamba DART ilinunua bidhaa na huduma za jumla ya Sh. milioni 332.653 nje ya mpango wa manunuzi kwa ajili ya kukodi sehemu ya ndani, nishati na mnara wa mawasiliano kwa Sh. milioni 154 na kutoa huduma ya usalama katika vituo vyake na kituo kikuu cha Jangwani kwa kiasi cha Sh. milioni 178.652.

Anasema manunuzi hayo ni kinyume cha Kanuni 69(3) ya Kanuni ya Manunuzi ya Umma ya Mwaka 2013 inayotaka taasisi inayofanya manunuzi kufanya makisio sahihi ya mahitaji ya bidhaa na huduma na kazi.

Anasema jumla ya mapato ya Sh. milioni 90.499 yaliyoonyeshwa kwenye taarifa za fedha yaliyotokana na matangazo katika miundombinu ya DART hayakuwa na uthibitisho zikiwamo nyaraka za manunuzi ya zabuni, jambo ambalo ni kinyume cha Kanuni 55(1) cha Kanuni ya Manunuzi ya Umma ya Mwaka 2013, hivyo ilishindikana kuthibitisha usahihi wa taratibu za manunuzi.

"Napendekeza kuwa wakala wa serikali wafuate taratibu za manunuzi na kuandaa mikataba kwa kila taasisi inayotumia miundombinu ya DART kufanya matangazo," anasema.

Prof. Assad anaongeza kuwa katika ukaguzi wake wa mwaka 2015/2016, amebaini Sh. milioni 372.6 zilitakiwa kulipwa na meneja wa mfuko wa ISP kwenda DART kama ada ya ISP kati ya Mei 16, 2016 na Juni 30, 2016, lakini hadi kufikia Juni 2016, kiasi cha Sh. milioni 85 kililipwa na kubaki kiasi cha Sh. milioni 287 ambazo hazijalipwa na ISP kupitia meneja wa mfuko DART, jambo ambalo anasema ni kinyume cha makubliano kati ya DART na UDART ya Mei 31, 2016 ambapo meneja wa mfuko alitakiwa kufanya malipo ya kila siku ya Sh. milioni 8.1 kwa wakala kama ada ya upatikanaji wa huduma.

"Na ikiwa siyo siku ya kazi, malipo yafanyike siku ya kazi inayofuata. Kutokulipa ada ya upatikanaji wa huduma kunaathiri ukwasi wa wakala, na hivyo kuchelewesha utekelezaji wa shughuli zilizopangwa," anasema CAG Assad.

Hivi karibuni wakati wa uzinduzi wa mradi huo, Rais John Magufuli aliwataka mawaziri mawili; Prof. Makame Mbarawa (Ujenzi) na George Simbachawene (Tamisemi) kueleza faida za awamu ya kwanza mradi huo unaotekelezwa kwa mkopo wa Benki ya Dunia (WB), agizo ambalo lilionekana kuwa gumu kwa Simbachawene huku waziri mwenzake akieleza kuwa jukumu lake katika mradi huo lilikuwa kusimamia ujenzi wa miundombinu na masuala ya faida za uendeshwaji wake yako Tamisemi.

Zitto Kabwe adai "Kila Wakipanga Kuniteka Wanakuta Mti wa Mrumba au Bwawa la Karosho au Ziwa Tanganyika..!!! "


“Mwaka jana niliambiwa kuwa wabunge tunaowindwa tupo watatu, mwanzoni mwa mkutano huu wakawa saba. Wakati huu wa Bunge la Bajeti nikajulishwa kuwa tumefikia saba. Sasa naona idadi iliyotangazwa na Mheshimiwa Bashe inasema ni wabunge kumi na moja wanaotakiwa kutekwa,” .
“Nadhani ni mambo ya kupeana hofu tu. Kwanza, sijafanya lolote la kusababisha nitekwe, kuteswa na kupotezwa. Hivyo habari hizi nazidharau kwa sababu sioni sababu kwanini nitekwe.”
“Wanaweza kupanga kuniteka wakanifuata wakakuta mti wa mrumba au Bwawa la Karosho au Ziwa Tanganyika. Wathubutu tu wataona.” 

Inasikitisha sana!! Kumbe Mmoja kati ya Askari waliouawa aacha mke anayetarajia kujifungua.

I

Dar es Salaam/Pwani. Ayoub Mwaikambo, askari aliyeuawa katika shambulio dhidi ya gari la Jeshi la Polisi wilayani Kibiti, ameacha mke ambaye anatarajiwa kujifungua mwezi mmoja ujao.

Hayo yamebainika katika hafla ya kuaga miili ya askari nane waliouawa katika shambulio lililotokea Alhamisi jioni, huku kukiwa na taarifa nyingine ya kushambuliwa kwa mapanga kwa mtoto wa mwenyekiti wa Kijiji cha Kitembo wilayani Kibiti ambako mauaji dhidi ya viongozi na askari yanazidi kuongezeka.

Mtoto huyo, Saidi Abdallah alijeruhiwa kwa mapanga baada ya kukataa kuwatajia watu waliovamia nyumba yao usiku wa kuamkia jana, sehemu aliyojificha baba yake ambaye ni mwenyekiti wa kijiji hicho.

Jana, wakati wa hafla ya kuaga miili ya askari hao iliyofanyika Kurasini Barracks, Francisco Mwaikambo, ambaye ni kaka wa askari huyo, alisema amempoteza mtu ambaye alikuwa akijadiliana naye mambo ya familia.

“Ah! Ayoub amekufa wakati nilikuwa nimepata mtu mwingine wa kujadiliana naye mambo ya familia baada ya kukua na kufahamu umuhimu wa familia,” alisema Francisco huku midomo ikimcheza mithili ya mtu anayejizuia kulia. “Amemuacha mtoto wake tumboni.”

Hili ndio gari jipya la Mbwana Samatta

 Mtanzania Mbwana Samatta anayeichezea KRC Genk ya Ubelgiji leo April 15 2017 amepost tofauti tofauti zikimuonesha akiwa na gari aina ya Mercedes Benz, Samatta ambaye kwa sasa anaishi Ubelgiji kutokana na kufanya kazi na KRC Genk nchini humo amepost picha gari hiyo bila maelezo mengi.

Inawezekana ikawa ni gari lake jipya ameamua kuliweka hadharani kupitia ukurasa wake wa instagram.



Pichaaa..Hebu ona Vannesa alivyotinga Mavazi Haya Yaliyomuacha Uchi Mbele ya Mashabiki Zake...




Kiama cha Bashite Chawadia..Rais Magufuli Asema Wote Walioghushi Vyeti Hawatapona..Habari Vichwa vya Magazeti ya Leo 16/4/2017..!!!

 

Gallery

Popular Posts

About Us