Imefichuka..kumbe Ufisadi Mzito Wagundulika Magari ya Mwendokasi.!! Hebu soma hapa | KINGAZI BLOG

HABARI KARIBU YAKO ZAIDI.

Breaking News
Loading...

Sunday 16 April 2017

Imefichuka..kumbe Ufisadi Mzito Wagundulika Magari ya Mwendokasi.!! Hebu soma hapa


RIPOTI ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Prof. Mussa Assad kwa mwaka wa fedha 2015/16, imefichua udhaifu mkubwa katika mradi wa mabasi yaendayo kasi jijini Dar es Salaam.

Katika ripoti hiyo iliyowasilishwa bungeni mjini hapa juzi, CAG Assad anasema kuwa katika ukaguzi wake alioufanya kwenye mradi huo, amebaini Wakala wa Usafiri wa Mwendokasi Dar es Salaam (DART) una upungufu mwingi.

Anasema katika utoaji wa huduma ya usalama katika vituo vya DART na makao makuu ya wakala Jangwani, amebaini kuwa Mei 5, 2016 DART iliingia mkataba wa miezi 12 na M/S China Tanzania Security Company Ltd wa utoaji huduma ya ulinzi kwenye vituo vya DART na Jangwani kwa jumla Sh. milioni 178.652.

Hata hivyo, Prof. Assada anasema kuwa katika mapitio ya taratibu za manunuzi, imebainika matangazo na zabuni zilizotolewa hazikuwasilishwa PPRA, mkataba ulisainiwa baada ya tarehe ya kukamilisha mkataba kuisha kinyume cha Kanuni 370(1) cha Kanuni ya Manunuzi ya Umma ya Mwaka 2013 na pia nakala ya mkataba haikuwasilishwa kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) kwa ajili ya kupitia na kuhakikiwa (vetting) kinyume cha Kanuni 59(1) na (2) vya Kanuni ya Manunuzi ya Umma ya Mwaka 2013.

"Kutokana na mazingira hayo ni vigumu kuthibitisha kwamba taratibu sahihi za manunuzi zilifuatwa katika utoaji wa huduma za usalama, na iwapo matumizi ya Sh. milioni 178.652 yalikuwa matumizi sahihi ya fedha za umma," anasema.

CAG Assad anapendekeza kuwa menejimenti ya DART ifuate sheria na kanuni za usimamizi wa mikataba, na kuweka mikakati ya jinsi ya kutatua upungufu unaojitokeza, hivyo wahakikishe Wakala wa Serikali na taasisi nyingine wanaimarisha mifumo ya ndani ili kuhakikisha upungufu haujitokezi kwa baadaye.

CAG pia anasema kuwa katika ukaguzi wake wa mwaka wa fedha 2015/2016, amebaini kwamba DART ilinunua bidhaa na huduma za jumla ya Sh. milioni 332.653 nje ya mpango wa manunuzi kwa ajili ya kukodi sehemu ya ndani, nishati na mnara wa mawasiliano kwa Sh. milioni 154 na kutoa huduma ya usalama katika vituo vyake na kituo kikuu cha Jangwani kwa kiasi cha Sh. milioni 178.652.

Anasema manunuzi hayo ni kinyume cha Kanuni 69(3) ya Kanuni ya Manunuzi ya Umma ya Mwaka 2013 inayotaka taasisi inayofanya manunuzi kufanya makisio sahihi ya mahitaji ya bidhaa na huduma na kazi.

Anasema jumla ya mapato ya Sh. milioni 90.499 yaliyoonyeshwa kwenye taarifa za fedha yaliyotokana na matangazo katika miundombinu ya DART hayakuwa na uthibitisho zikiwamo nyaraka za manunuzi ya zabuni, jambo ambalo ni kinyume cha Kanuni 55(1) cha Kanuni ya Manunuzi ya Umma ya Mwaka 2013, hivyo ilishindikana kuthibitisha usahihi wa taratibu za manunuzi.

"Napendekeza kuwa wakala wa serikali wafuate taratibu za manunuzi na kuandaa mikataba kwa kila taasisi inayotumia miundombinu ya DART kufanya matangazo," anasema.

Prof. Assad anaongeza kuwa katika ukaguzi wake wa mwaka 2015/2016, amebaini Sh. milioni 372.6 zilitakiwa kulipwa na meneja wa mfuko wa ISP kwenda DART kama ada ya ISP kati ya Mei 16, 2016 na Juni 30, 2016, lakini hadi kufikia Juni 2016, kiasi cha Sh. milioni 85 kililipwa na kubaki kiasi cha Sh. milioni 287 ambazo hazijalipwa na ISP kupitia meneja wa mfuko DART, jambo ambalo anasema ni kinyume cha makubliano kati ya DART na UDART ya Mei 31, 2016 ambapo meneja wa mfuko alitakiwa kufanya malipo ya kila siku ya Sh. milioni 8.1 kwa wakala kama ada ya upatikanaji wa huduma.

"Na ikiwa siyo siku ya kazi, malipo yafanyike siku ya kazi inayofuata. Kutokulipa ada ya upatikanaji wa huduma kunaathiri ukwasi wa wakala, na hivyo kuchelewesha utekelezaji wa shughuli zilizopangwa," anasema CAG Assad.

Hivi karibuni wakati wa uzinduzi wa mradi huo, Rais John Magufuli aliwataka mawaziri mawili; Prof. Makame Mbarawa (Ujenzi) na George Simbachawene (Tamisemi) kueleza faida za awamu ya kwanza mradi huo unaotekelezwa kwa mkopo wa Benki ya Dunia (WB), agizo ambalo lilionekana kuwa gumu kwa Simbachawene huku waziri mwenzake akieleza kuwa jukumu lake katika mradi huo lilikuwa kusimamia ujenzi wa miundombinu na masuala ya faida za uendeshwaji wake yako Tamisemi.

google+

linkedin

About Author
  • BLOG NAMBA MMOJA KWA MATANGAZO YA AJIRA NA NAFASI ZA KAZI TANZANIA. Soma zaidi

    0 comments:

    POST A COMMENT

     

    Gallery

    Popular Posts

    About Us