KINGAZI BLOG: 01/17/17

HABARI KARIBU YAKO ZAIDI.

Breaking News
Loading...

Tuesday 17 January 2017

Mbeya: Maiti Iliyozikwa Yakutwa Kwenye Godoro Chumbani



Wakazi wa Isanga Jijini Mbeya wamekumbwa na taharuki baada ya tukio lisilo la kawaida ambapo maiti iliyokwenda kuzikwa katika makaburi ya zamani ya Isanga ilikutwa ikiwa kwenye godoro ndani ya nyumba alimofia.

Taarifa yaJeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya inasema kuwa tukio lilitokea mnamo tarehe 16.01.2017 majira ya saa 4:30 asubuhi katika mtaa wa Igoma “A”, Kata ya Isanga, Jijini Mbeya.

Kufuatia taarifa hiyo Polisi walifuatilia na kubaini kuwa tarehe 16.01.2017 majira ya saa 1:00 asubuhi mtu mmoja aitwaye JAILO KYANDO na mke wake aitwaye ANNA ELIEZA wote wakazi wa mtaa wa Igoma “A” waliamka asubuhi na kukuta mtoto wao wa kwanza aitwaye HARUN JAILO KYANDO amefariki dunia akiwa amelala.

Taarifa za awali zinadai kuwa marehemu tangu utoto wake alikuwa na matatizo ya ugonjwa wa kifafa hali iliyopelekea kuishi nyumbani pasipo kusoma.

Kufuatia kifo hicho msiba uliendeshwa na taratibu za mazishi zilifanyika. Majira ya saa 6:00 mchana jeneza lililetwa msibani na kuwekwa sebuleni kando ya mwili wa marehemu ambao ulikuwa umeviringishwa na blanketi na kulazwa chini kwenye godoro, baada ya maombi yaliyoongozwa na walokole waitwao BONDE LA BARAKA vijana walibeba jeneza hadi makaburi ya zamani ya Isanga na kisha jeneza kuzikwa.

Waombolezaji waliporudi nyumbani walitaharuki kuona mwili wa marehemu mtoto HARUN JAILO KYANDO ukiwa chumbani umelazwa eneo ulipokuwa awali. 

Kutokana na hali hiyo taarifa zilifikishwa Polisi mara moja, askari Polisi walifika na kurejesha hali ya amani kwa kuuchukua mwili wa marehemu ambao kwa sasa umehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa Mbeya.

Taratibu nyingine za mazishi zitafanyika leo tarehe 17.01.2017. Mpaka sasa bado haijafahamika ni uzembe /bahati mbaya wafiwa kusahau kuweka mwili wa marehemu kwenye jeneza au kulikuwa na hujuma zozote.

Upelelezi unaendelea kuhusiana na tukio hili.

KAMA UNATATIZO LA KUNUKA MDOMO TIBA NI HII HAPA.


Afya ya mtu huanzia kwenye harufu ya mwili wake. Hakuna harufu inayoonyesha jinsi gani ulivyo msafi kama harufu ya kinywa. Je ulishawahi kuongea na mtu na ghafla ukajikuta unakosa hamu ya kuendelea sababu kinywa kinatoa harufu mbaya? Nafahamu kero hii inavyokuwa.

Kinywa ni muhimu kufanyiwa usafi wa hali ya juu ili kuhakikisha unapunguza harufu mbaya ya kukinaisha. Harufu ya kinywa, inakera na kuudhi. Kwa bahati mbaya huwa hatujui kama midoyo yetu inatoa harufu mbaya, bali wale tu wanaopata kuvuta hewa itokayo midomoni mwetu. Hii inakuwa ngumu kutatua tatizo sababu unaweza kudhani kila kitu kiko vizuri, kumbe unawapa watu wakati mgumu wakati wa mazungumzo. Harufu mbaya haifurahiwi, hasa ikiwa inatoka kwenye vinywa vyetu. Je nini kinasabisha vinywa kutoa harufu mbaya kiasi hiki? Hizi hapa sababu chache za kufanya kinywa kutoa harufu mbaya.

Kutosafisha vizuri kinywa vizuri

Kwa kawaida unatakiwa kusukutua kinywa chako angalau mara mbili kwa siku - asubuhi na usiku kabla ya kulala. Wakati wa kusafisha kinywa, hakikisha umesugua vizuri ulimi. Meno na fizi havina tatizo sana, bali ulimi ndio sehemu kubwa ambapo bakteria wanajijenga. Vilevile, ni ulimi unaosababisha kinywa kunuka. Ni vizuri kama utasafisha vizuri ulimi ili kuondoa harufu.

Ni vizuri kufahamu kuwa mswaki unatakiwa kubadilishwa kila baada ya muda - angalau kila mwezi. Usitumie mswaki kwa muda mrefu, maana hauwezi kusafisha kinywa chako kwa ufasaha kama inavyotakiwa maana wengine wanatumia mswaki kwa mwaka na zaidi. Je utaacha kunuka kinywa? 

Kutokula chakula vizuri

Harufu ya kinywa inaashiria kutokula chakula na kinywaji kwa muda mrefu. Kuwa na njaa husababisha mdomo kuwa mkavu. Mara nyingi harufu mbaya ya kinywa hupotea mara tu baada ya kula chakula kizuri na mdomo ukiwa una mate ya kutosha. Acha kutumia vyakula na vinywaji vinavyoongeza harufu kali mdomoni na kukupunguzia maji mwilini – mfano pombe, viungo kama kitunguu maji au kitunguu saumu.

Kinywa kikavu

Bakteria hushamiri kwenye kinywa kikavu. Kama hupendi kunywa maji mengi na kinywa chako kinakuwa kikavu mara nyingi basi jua kuwa kunuka kinywa kwako ni jambo la kawaida.

Jinsi ya kutatua tatizo

Hakikisha mdomo haukauki

Kwa kawaida mdomo mkavu hutoa harufu mbaya. Hii ndio sababu kuwa kinywa chako kinanuka sana asubuhi sababu mdomo wako unatengeneza mate machache sana ukiwa umelala. Mate ni adui wa harufu mbaya mdomoni siyo tu sababu inaondoa bakteria na masalia ya chakula, bali mate yana vimengenyo vinavyoua na kuzuia kuzaliana kwa vijidudu kwenye kinywa. Ili kuzuia kunuka, jaribu kufanya haya

Kunywa maji mengi ili kuondoa masalia ya chakula na bakteria Tafuna bazoka, sababu bazoka inasababisha mdomo kuwa na mate mengi. Kuwa makini katika kuchagua bazoka zisizo na sukari.  Sukari ni adui mkubwa wa kinywa chenye afya.

Piga mswaki kabla ya kulala

Kupiga mswaki ni muhimu, lakini wengi tunasahau kuwa mswaki ni lazima kupiga angalau mara mbili kwa siku haswa usiku naasubuhi.  Kupiga mswaki asubuhi ni muhimu ili kuondoa uchafu uliojijenga usiku kucha na hivyo harufu mbaya - lakini siku nzima mdomo unatengeneza mate na kuwa laini.  Hii ni tofauti na usiku. Usiku mdomo hubaki mkavu na mate kidogo, hivyo kuwa rahisi kwa vijidudu kuzaliana na kuharibu mazingira ya mdomoni kwako. Hivyo, ni afya zaidi kupiga mswaki usiku ili kuzuia kushamiri bakteria waharibifu wanaosababishwa na masalia ya bakteria kwenye kinywa chako.  Njia hii itasaidia kuzuia bakteria kuharibu meno na fizi, hivyo kutokuwa na harufu mbaya ya masalia wakati ukiamka.

Kula ndizi au apple

Ndizi au apple husaidia kuondoa harufu mbaya kinywani, lakini ni kwa muda mfupi sana. Ukiwa unahisi mdomo unanuka na unahitaji njia ya haraka, tafuta ndizi au apple, na hapo utakuwa umetatua tatizo kwa muda.

Kula Tango

Maji ya tango yana kemikali zinazozuia kukua kwa bakteria kwenye kinywa. Baada ya mlo mzuri wenye viungo vyenye harufu kali, kata kipande kidogo cha tango, kigandishe kwenye ukuta wa juu wa mdomo wako kwa sekunde 30 huku ukikandamiza na ulimi. Zoezi hili litasaidia kuua bakteria na kuacha kinywa chako kikiwa na afya na harufu nzuri.

Jenga Tabia ya Kupia Mabusu (Kissing)

Ni ukweli kuwa ukifanya kitu chochote kinachosababisha kutoa mate basi unazuia kunuka kinywa. Kissing ni mojawapo ya njia mbadala za kuzuia harufu mbaya mdomoni. Kiss mara nyingi uwezavyo ili kufanya mdomo wako uwe na mate mengi, na hivyo kuzuia kunuka kinywa.

Harufu ikizidi, kamuone daktari

Je harufu yako ya kinywa ni ugonjwa? Basi kamuone daktari. Wakati mwengine harufu ya kinywa hutokana na kuwa na matatizo mwilini na huwezi kuondoa kwa kutumia njia tulizozieleza hapo juu.


KAMA UNA MATATIZO YA MENO TIBA RAHISI NI HII HAPA

Meno ni muunganiko wa mfupa wa jino, Fizi na Mishipa. Maranyingi watu wengi huwa pale wanapoumwa na jino wanakimbilia kung’oa jino eti dawa ya jino kuling’oa jambo ambalo si kweli.

Tambua ndugu yangu kuwa unapokwenda kung’oa jino unang’oa Mfupa sio Fizi wala mishipa ambayo hakuna madhara kwa bakteria anaesababisha jino kuuma.

Tambua kuwa kwenye kinywa cha mwanadamu kuna bakteria wanaoishi mdomoni wanaitwa NORMAL FRALER. Bakteria hawa ndio wanaotengeneza ute wenye Acid unaolainisha chakula kwa haraka mdomoni. Na ndio kazi yao. Lakini wanasababisha ugonjwa unaoitwa GINGIVAITES, ugonjwa huu husababisha fizi kutoa damu haswa unapopiga mswaki, lakini ukiachwa ukawa sugu unasababisha ugonjwa wake kuwa sugu na hujulikana kama MACHODIFECE ugonjwa huu husababisha na hufanya meno kuoza, ama kutoboka kutokana na bakteria AFINOTOBALASAD ndio wanaosababisha na huwa wanaingia ndani kwenye fizi kwa ajili ya kula damu. Hapo ndipo mtu hupatwa na tatizo la  kuumwa na jino au meno.

 Ili kuondoa tatizo hili, ni lazima uwaue hao bakteria na si kong’oa jino kwani wadudu hao walivyo unapong’oa jino moja wao huwa wanahamia jino jingine.

Tiba rahisi ya jino au meno yanayouma bila kung'oa wala kutumia dawa za hospitali tumia mojawapo kati ya hizi hapa:

Tengeneza na kunywa juisi ya bilinganya (Bringal).Jino linalouma au fizi zilizovimba: Ponda ponda tangawizi mbichi kisha itie chumvi. Weka kwenye jino linalouma au fizi ilipovimba.Saga majani makavu ya mint kutengeneza unga wake, kisha tia chumvi na weka kwenye jino linalouma.Saga karafuu kuwa unga. Weka kiasi cha unga huo kwenye jino linalouma. Pia kama una mafuta ya karafuu, chukua nyuzi za pamba (cotton wool) chovya kwenye mafuta hayo na weka wool hiyo kwenye jino linalouma.Tiba hizi tunazo majumbani kwetu tunamoishi lakini tumekuwa hatujui kuwa ni tiba, badala yake huwa tunakimbilia kung'oa meno yanayouma! CHANGAMKA!



HUYU HAPA HARMONIZE NA WOLPER FEKI PICHAZ++

Msanii chipukizi wa Bongo Fleva anayefanana sana kwa sura na msanii kutoka WCB, Harmonize kiasi cha kubatizwa jina la ‘Pacha wa Harmonize’, Harmorapa, leo ametinga kwenye Ofisi za Global Publishers, Bamaga- Mwenge jijini Dar ambapo mbali na mambo mengine, amefungukia uhusiano wake wa kimapenzi na ‘Wolper’.

Harmorapa amesema kuwa kutokana na kufanana sana na Harmonize, aliamua kutafuta msichana anayefanana sana na mpenzi wa Harmonize, mwanadada Jacqueline Wolper ambaye naye kwa jinsi anavyofanana naye, ukikutana nao unaweza kudhani umekutana na Harmonize na Wolper ‘orijino’.

“Prodyuza wangu, Khalfan ndiye aliyenikutanisha na mwanadada huyu ambaye watu wanamuita Wolper kutokana na jinsi alivyofanana naye, alinikutanisha kwa lengo la kufanya naye kazi akiwa kama video queen, akatokea kuwa rafiki yangu sana na mara kwa mara nakuwa naye sehemu mbalimbali.

“Kiukweli uhusiano wetu ni wa kikazi tu tofauti na Harmonize na Wolper ambao ni wapenzi kweli.”

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumanne ya January 17




 

Gallery

Popular Posts

About Us