Ndege ya ‘wanawake pekee’ kutoka Malawi kutua Tanzania | KINGAZI BLOG

HABARI KARIBU YAKO ZAIDI.

Breaking News
Loading...

Wednesday 15 March 2017

Ndege ya ‘wanawake pekee’ kutoka Malawi kutua Tanzania

HakiMALAWI AIRLINES / FACEBOOKImageNdege hiyo itakuwa chini ya Kapteni Yolanda Kaunda na Lusekelo Mwenifumbo

Shirika la ndege la Malawi, Malawi Airlines, limetangaza kwamba linapanga kufanya safari ya ndege itakayosimamiwa na wanawake pekee Alhamisi wiki hii.

Safari hiyo ya ndege, ambayo itakuwa na marubani na wasaidizi wa abiria kwenye ndege wote wakiwa wanawake, itakuwa ya kwanza kuandaliwa na shirika hilo.

Ndege hiyo itasafirisha abiria kutoka mji wa Blantyre hadi Dar-es-Salaam nchini Tanzania na itatua kwa muda Lilongwe kabla ya kuelekea Dar .

Taarifa kutoka kwa shirika hilo la ndege, lilisema lengo ni kufanikisha ulimwengu ambao "unakumbatia jinsia zote".

Ndege hiyo itakuwa chini ya Kapteni Yolanda Kaunda akisaidiwa na Lusekelo Mwenifumbo.

Bi Mwenifumbo, 24, alisomea taaluma ya uchukuzi wa ndege mjini Addis Ababa, Ethiopia.

ImageShirika la ndege la Malawi Airlines lilianzishwa Julai 2013 baada ya kuvunjwa kwa shirika la awali la Air Malawi Februari mwaka huo

"Lengo la hatua hii ni kuwahamasisha wasichana ambao wangependa kufanya kazi katika uchukuzi wa ndege lakini kwa njia moja au nyingine hufikiria ni vigumu au kwamba ni kazi ambayo wanawake hawaiwezi," taarifa ya Malawi Airlines ilisema.

Ndege hiyo aina ya Bombardier Q-400 itapaa kutoka Blantyre saa nne asubuhi Alhamisi.

google+

linkedin

About Author
  • BLOG NAMBA MMOJA KWA MATANGAZO YA AJIRA NA NAFASI ZA KAZI TANZANIA. Soma zaidi

    0 comments:

    POST A COMMENT

     

    Gallery

    Popular Posts

    About Us