Nikki Mbishi Atoa Onyo Kwa Vyombo vya Habari Kwa Watakao Sambaza na Kupiga Wimbo wake wa "I am Sorry JK" | KINGAZI BLOG

HABARI KARIBU YAKO ZAIDI.

Breaking News
Loading...

Thursday 16 February 2017

Nikki Mbishi Atoa Onyo Kwa Vyombo vya Habari Kwa Watakao Sambaza na Kupiga Wimbo wake wa "I am Sorry JK"

Ikiwa ni saa zisizodi ishirini na nne (24) toka itoke taarifa ya MwanaHiphop Tanzania Nikki Mbishi kutoa taarifa ya kuitwa na Baraza la Sanaa Taifa (BASATA) kuhojiwa kuhusu wimbo wake unaomzungumzia Rais Mstaafu Jakaya Kikwete ‘I am sorry JK‘ Rapper huyo ameandika sentensi kadhaa.

“Salaam, baada ya salamu naomba niombe radhi kwa vyombo vyote vya habari kuwa sitoweza kuwapa ushirikiano wowote kuhusu wimbo wangu wa “I’M SORRY JK” uliositishwa na hii ni kwa usalama wao na wangu pia‘

Ameendelea kuandika kuwa

’Napokea simu nyingi sana zikihitaji maelezo juu ya suala hilo ila kiukweli kwa watakaohitaji taarifa kamili wanaweza kufika ofisi za BASATA, naomba nisiwe msemaji tena juu ya jambo hili‘

Nikki alitoa tahadhari pia

 ‘Kwa yeyote atakae endelea kuusambaza au kuucheza popote pale mimi sitohusika naye maana technology iko huru popote Duniani na siwezi kuzuia watu wasiupate kwa kuwa ulishasambaa, hivyo chukua tahadhari ili usijikute mikononi mwa sheria [​IMG] .

#Asanteni sana, naomba msubiri ujio wangu mpya wa #SINGELI na aina nyingine za muziki kama #NAIJA #MCHIRIKU n.k. MUZIKI NI AJIRA,MUZIKI NI KAZI YANGU #Mungu_Simama_Kweli_Idhihirike

Ni wako mtanzania mvumilivu:
Nikki Mbishi @2017
With no offence!

google+

linkedin

About Author
  • BLOG NAMBA MMOJA KWA MATANGAZO YA AJIRA NA NAFASI ZA KAZI TANZANIA. Soma zaidi

    0 comments:

    POST A COMMENT

     

    Gallery

    Popular Posts

    About Us