Picha 17: JAMAA ANAYEDAIWA KUFANYA MAPENZI NA WAKE ZA WATU KICHAWI SHINYANGA AKAMATWA,ASHUSHIWA KIPIGO | KINGAZI BLOG

HABARI KARIBU YAKO ZAIDI.

Breaking News
Loading...

Friday 9 September 2016

Picha 17: JAMAA ANAYEDAIWA KUFANYA MAPENZI NA WAKE ZA WATU KICHAWI SHINYANGA AKAMATWA,ASHUSHIWA KIPIGO


Wananchi wenye hasira kali katika kijiji cha Bugayambele kata ya Kizumbi katika manispaa ya Shinyanga wamemshushia kichapo jamaa anayedaiwa kuwaingilia wanawake nyakati za usiku kisha kufanya nao mapenzi kwa njia za kishirikina. 

Tukio hilo limetokea leo majira ya saa kumi jioni ambapo wakazi wa kitongoji cha Bugayambelele jirani na kijiji cha Nhelegani kilichokumbwa na taharuki ya kuwepo mtu anayefanya mapenzi na wake za watu kimazingara,walimshtukia jamaa huyo baada ya kuonekana akifanya vitendo walivyodai kuwa vya kishirikina katika familia mbili za kitongoji hicho. 

Malunde1 blog baada ya kupata taarifa za kuwepo kwa tukio hilo ilifika eneo la tukio haraka zaidi na kushuhudia umati mkubwa wa watu ukiwa umemzingira jamaa huyo huku askari polisi wakiwa eneo la tukio kuzuia wananchi wasiendelee kumshushia kipigo jamaa huyo. 

Wakazi wa eneo hilo walisema mtu huyo aliingia kwenye nyumba mbili(kaya mbili) bila kupiga hodi huku akidai kuwa alikuwa anatafuta mke wake, akidai kuwa ametoka kwa mganga wa kienyeji kaelekezwa kuwa mke wake yupo eneo hilo. 

Hata hivyo baada ya kumtilia mashaka jamaa huyo alianza kukimbia na kutupa simu zaidi ya tatu za mkononi alizokuwa nazo,wananchi wakafanikiwa kumkamata kisha kumpeleka kwenye mkutano wa sungusungu na walipompekua wakamkuta na dawa za kienyeji zinazodaiwa kuwa za mapenzi,zikisomoka kama ifuatavyo; 

“Imala yose -kuchoma kuomba mke wako roho yake irudi kwako akupende” na nyingine maandishi yakisomeka kuoga na kuchoma kuomba mkeo akupende na arudi kwako”.
Wakazi wa eneo hilo walisema kutokana na maelezo yake,pia kuingia katika familia moja bila hodi huku akidaiwa kupotea kimiujiza eneo hilo na kuibukia katika familia nyingine pamoja na dawa za kienyeji alizokuwa nazo walimhusisha moja kwa moja na tukio la ubakaji kwa njia za kishirikina.

Mwenyekiti wa kitongoji cha Bugayambelele Donald Francis alisema alipigiwa simu na kuelezwa kuwepo kwa mwanamme anayehusishwa na tukio la kubaka wanawake kishirikina katika kijiji jirani cha Nhelegani kata ya Kizumbi.
Alisema mwanamme huyo alikutwa na dawa za kienyeji huku akitoa maelezo yasiyoeleweka ikiwemo kudai amefika hapo kwa ajili ya kutafuta kazi ya kufyatua matofali,kutafuta mke wake na anatoka kwa mganga wake wa kienyeji aliyemnyweshwa dawa za ajabu.
Tutawaletea taarifa kamili hivi punde.... 

Mwanamme aliyejitambulisha kwa jina la Shaban Charles kutoka Kitangiri katika manispaa ya Shinyanga anayedaiwa kujihusisha na vitendo vya kubaka wanawake kishirikina nyakati za usiku-Picha na Kadama Malunde-Malunde1 blog

Polisi wakiwa eneo la tukio


Wananchi wakiwa eneo la tukio

Dawa za kienyeji alizokutwa nazo jamaa huyo

Dawa za kienyeji za jamaa pamoja simu yake

Dawa za kienyeji

Polisi na wananchi wakiwa wamemzunguka jamaa huyo

Mwandishi wa habari wa Radio Faraja Steve Kanyeph akifanya mahojiano na jamaa huyo

Wananchi wakiwa eneo la tukio

Wananchi wakiwa eneo la tukio

Gari la polisi likiwasili eneo la tukio


Jamaa akipanda kwenye gari la polisi

Baiskeli ya mtuhumiwa ikipandishwa kwenye gari la polisi


Polisi wakiondoka na mtuhumiwa

Wananchi wakiondoka eneo la tukio
Mwenyekiti wa kitongoji cha Bugayambelele Donald Francis akizungumza na waandishi wa habari ambapo alisema alipigiwa simu na kuelezwa kuwepo kwa mwanamme anayehusishwa na tukio la kubaka wanawake kishirikina katika kijiji jirani cha Nhelegani kata ya Kizumbi.

google+

linkedin

About Author
  • BLOG NAMBA MMOJA KWA MATANGAZO YA AJIRA NA NAFASI ZA KAZI TANZANIA. Soma zaidi

    0 comments:

    POST A COMMENT

     

    Gallery

    Popular Posts

    About Us