AZUNGUKA DUNIA MIAKA MIWILI KWA KUTUMIA PIKIPIKI YA VESPA | KINGAZI BLOG

HABARI KARIBU YAKO ZAIDI.

Breaking News
Loading...

Thursday 8 September 2016

AZUNGUKA DUNIA MIAKA MIWILI KWA KUTUMIA PIKIPIKI YA VESPA

Akiwa ameegesha pikipiki yake aina ya Vespa mjini Punjab. KULIA: Drew Milne akishangilia mwisho wa safari yake.Mwendesha pikipiki amemaliza miaka miwili ya kushangaza, safari ya maili 10,000 kutoka Australia hadi London akiendesha Vespa yake anayoipenda mno.Drew Milne, mhandisi wa programu ya kompyuta, alijipiga picha mwenyewe akiwa na pikipiki kwenye maeneo mbalimbali ya ajabu - kutoka Iran hadi India - wakati wa safari hiyo ya kipekee, ambayo ilianzia mji anaoishi wa Adelaide mnamo Machi 2011.
Milne, ambaye alikuwa na miaka 31 wakati safari hiyo ikianza, aliibatiza safari yake hiyo jina la 'Vescapade' na amepanga kuchapisha kitabu kuhusu alichojifunza kutokana na ziara hiyo.
Alipiga picha za sehemu mbalimbali alizopita katika safari yake na watu wa ajabu aliokutana nao njiani kwa kutumia kamera yake.
Drew anasema safari hiyo ilikuwa ni njia yake kuona ulimwengu katika njia ya kipekee. Alisema Vespa hiyo ilikuwa njia bora zaidi ya kukutana na watu wakati wa safari hiyo, huku ikiwavutia kwake kwa udadisi.
Miongoni mwa vidokezo katika safari yake hiyo ilikuwa safari kupitia Iran - ambako alipiga picha Vespa hiyo katika Persiopolis, na mbele ya alama za barabarani.Kivutio kingine kilikuwa picha aliyopiga na wanaume wawili wa kijijini pale aliposimama kwa mapumziko mjini Punjab, India.
Milne alijifunza kikamilifu mazingira mbalimbali ya uendeshaji wakati wa safari yake hiyo ndefu kwenda London, kuanzia joto kali kabisa hadi baridi inayofikia barafu nchini Italia.
Miongoni mwa nchi nyingine alizopita akiendesha Vespa yake hiyo zilikuwa Uturuki, Indonesia, Cambodia, Malaysia na Laos.
Alisherehekea mwisho wa safari hiyo kwa kusimama juu ya Vespa yake hiyo kwa ushindi mbele ya Trafalgar Square mjini London.
Vespa zilitengenezwa kwa mara ya kwanza na kampuni ya Italia ya Piaggio & Co katika miaka ya 1940.
Pikipiki hizo zilikuja kuwa alama kuu katika miaka ya 1960 - na zikawa nyenzo muhimu katika utamaduni mpya huko Uingereza na nchi nyinginezo.
Umaarufu wake umekuwa tena kwenye nchi nyingi katika miaka ya hivi karibuni kama sehemu ya kukumbukia enzi.

google+

linkedin

About Author
  • BLOG NAMBA MMOJA KWA MATANGAZO YA AJIRA NA NAFASI ZA KAZI TANZANIA. Soma zaidi

    0 comments:

    POST A COMMENT

     

    Gallery

    Popular Posts

    About Us