PICHAZ+++ MCHUNGAJI ANAYEOMBEA WATU NA KUWAPILIZIA DAWA YA MBU | KINGAZI BLOG

HABARI KARIBU YAKO ZAIDI.

Breaking News
Loading...

Tuesday 22 November 2016

PICHAZ+++ MCHUNGAJI ANAYEOMBEA WATU NA KUWAPILIZIA DAWA YA MBU



Nafahamu hii inaweza kukushtua sana, imetokea nchini Afrika Kusini kumuhusu mchungaji Lethebo Rabalago wa Kanisa la Mountzion General Assembly lililopo mji wa Limpopo, ambaye amekutwa akiwapulizia dawa ya kuua wadudu kwa madai kwamba itawaponya matatizo yao.

Mchungaji wa Limpopo Afrika Kusini awa gumzo, ni baada ya picha kusambaa akiombea watu kwa kuwapulizia dawa ya Mbu kanisani kwake Mount Zion



Mchungaji aliyezua gumzo kwa kuwaombea watu kwa kuwapulizia dawa ya Mbu South Africa aliwahi kusema chochote kinafaa kwa uponyaji akitamka.

Kupitia picha alizozishare kwenye ukurasa wake wa Facebook, ameonekana akiwapulizia dawa hizo waumini kwenye sehemu mbalimbali za mwili na kueleza kwamba yeye kwake kila kitu anaweza kukifanya kuwa baraka za uponyaji.

Sasa muda mfupi baada ya kusambaa kwa taarifa na picha za Mchungaji huyo akitumia dawa ya kuua wadudu kuwapulizia waumini kanisani kwake, Kampuni inayotengeneza dawa hizo iitwayo Doom imetoa tamko lake na kumuonya mchungaji huyo kuacha mara moja kutumia bidhaa zake kwa matumizi ya aina hiyo.


Nimekuwekea picha hapa chini.


 
 
 

google+

linkedin

About Author
  • BLOG NAMBA MMOJA KWA MATANGAZO YA AJIRA NA NAFASI ZA KAZI TANZANIA. Soma zaidi

    0 comments:

    POST A COMMENT

     

    Gallery

    Popular Posts

    About Us