Picha na video!!! Rais Magufuli akiendesha basi la mwendokasi leo wakati wa sherehe za ufunguzi wa mradi mpya. | KINGAZI BLOG

HABARI KARIBU YAKO ZAIDI.

Breaking News
Loading...

Wednesday 25 January 2017

Picha na video!!! Rais Magufuli akiendesha basi la mwendokasi leo wakati wa sherehe za ufunguzi wa mradi mpya.


Rais wa Tanzania, Dk. John Magufuli, amesema serikali itajenga barabara za juu tatu za kuchepuka katika eneo la Ubungo ili kuupa maana Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka (BRT) ulioanzia Jijini Dar es Salaam 

Amesema lengo ni kuondokana tatizo la mabasi hayo kutumia muda mwingi kukatiza katika eneo hilo.

Rais Dk. Magufuli ametoa kauli hiyo leo Jijini Dar es Salaam wakati wa ufunguzi wa awamu ya kwanza ya mradi wa miundombinu ya utoaji huduma kwa mradi huo wa BRT uliogharimu shilingi bilioni 403, ambapo ametaka kuharakishwa kwa mchakato wa kukamilisha kuanza kwa ujenzi wa barabara hizo za juu za kuchepuka.

Rais Magufuli amesema awamu ya pili ya mradi mabasi yaendayo kasi itahusisha barabara ya urefu wa kilometa 19.3 inayotoka barabara ya Kilwa katikati ya jiji la Dar es Salaam hadi Mbagala rangi tatu, pamoja na ujenzi wa barabara ya juu katika makutano ya barabara ya Nyerere na Kawawa.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika Makhtar Diop wa kwanza kulia wavivuta kitambaa kuashiria ufunguzi rasmi wa Awamu ya Kwanza ya Miundombinu na Utoaji Huduma ya Mabasi yaendayo Haraka katika jiji la Dar es Salaam. Wengine katika picha ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais –TAMISEMI George Simbachawene pamoja na  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa.

Akitaja awamu nyingine amesema kuwa itahusisha barabara ya Nyerere hadi Gongolamboto yenye jumla ya urefu wa Kilometa 33.6 mradi, awamu ya nne ni barabara yenye kilomita 25.9 ikihusisha barabara ya Ali Hassan Mwinyi na Tegeta, yenye urefu wa Kilometa 22.8 awamu ya tano yenye urefu wa Kilometa 27.9 kwa awamu ya sita miradi yote hiyo itafadhiliwa na Benki ya Dunia.

Kwa upande wake Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa amesema wizara yake itatekeleza mikataba iliyowekwa na Banki ya Dunia ili kukamilisha miradi mingine ya maendeleo ikiwa ni pamoja na reli na umeme.

google+

linkedin

About Author
  • BLOG NAMBA MMOJA KWA MATANGAZO YA AJIRA NA NAFASI ZA KAZI TANZANIA. Soma zaidi

    0 comments:

    POST A COMMENT

     

    Gallery

    Popular Posts

    About Us