Makonda Amtaja Na Vee Money na Tunda Ishu ya Madawa ya Kulevya....Waliokaidi Agizo Lake Leo Kukamatwa | KINGAZI BLOG

HABARI KARIBU YAKO ZAIDI.

Breaking News
Loading...

Saturday 4 February 2017

Makonda Amtaja Na Vee Money na Tunda Ishu ya Madawa ya Kulevya....Waliokaidi Agizo Lake Leo Kukamatwa


Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam ameagiza kukamatwa kwa watu aliowataja jana kuhusika na dawa za kulevya ambao hawajajisalimisha kituo cha polisi leo, kama alivyoagiza

Makonda aliyefika katika Kituo Kikuu cha Polisi, amesema watu wao ambao hawajajisalimisha, wasakwe kokote waliko, na wawekwe ndani.

"Kuna watu tuliwaita, baadhi nimeambiwa hawajafika, ambao hawajafika nimeagiza wakachukuliwe wakae ndani mpaka siku ya Jumatatu" Amesema Makonda.

Amesema kati ya watu waliotajwa jana, ni wasanii watano pekee ndiyo wamejisalimisha siku ya leo katika kituo hicho wakiongozwa na aliyewahi kuwa Miss Tanzania Wema Sepetu, Nyandu Tozi (Hamidu), TID, Babuu wa Kitaa.

Pia kwa mujibu wa taarifa ya jeshi hilo, jumla ya polisi 7 wamekwisha kamatwa huku watatu wakiendelea kutafutwa na wengine wawili ambao hawako katika jiji la Dar es Salaam watakamatwa ndani ya muda mfupi ujao.  

 Katika hatua nyingine, Makonda ametaja orodha nyingine tofauti na aliyoitaja jana ya watu wanadaiwa kuhusika katika dawa za kulevya akiwemo msanii bongo fleva Vanessa Mdee, mwanamitindo anayefahamika kwa jina la Tunda.

Mbali na wasanii hao, makonda amewataja pia askari wengine watatu wa Jeshi la Polisi Tanzania ambapo amedai kuwa askari hao wanatuhumiwa kwa kupokea pesa kiasi cha shilingi bilioni 1 hivi karibuni kutokana na kuhusika na dawa za kulevya pamoja na kukamata dawa za kulevya kisha kuziuza tena.

Pia amemtaja anayejulikana kwa jina la Omari Sanga kuwa ni mmoja anayehusishwa na uletaji wa dawa ya kulevya na amesababisha asilimia 60 ya watanzania kufungwa katika magereza ya china.

Makonda amesema "Waliofika tutajadiliana nao kuona namna gani wanatupatia yale tunayoyataka kuyafanyia kazi kutokana na taarifa tulizo nazo. Vita hii ya dawa za kulevya haiishi leo, inaisha pale dawa zinapokuwa zimeisha"

Naye Kamanda Wa Polisi Mkoa wa Dar es Salaam kamishna Simon Sirro amesema kuwa Jeshi hilo limeunda tume ya kushughulika na mapambano dhidi ya dawa za kulevya mkoani humo


google+

linkedin

About Author
  • BLOG NAMBA MMOJA KWA MATANGAZO YA AJIRA NA NAFASI ZA KAZI TANZANIA. Soma zaidi

    0 comments:

    POST A COMMENT

     

    Gallery

    Popular Posts

    About Us