Inasikitisha Sana..Wamchoma Moto Hadi Kifo kwa Kisingizio cha Kumtoa Mapepo...!!! | KINGAZI BLOG

HABARI KARIBU YAKO ZAIDI.

Breaking News
Loading...

Thursday 2 March 2017

Inasikitisha Sana..Wamchoma Moto Hadi Kifo kwa Kisingizio cha Kumtoa Mapepo...!!!


MWANAMKE mkazi wa Managua, amekufa baada ya kufungwa kamba na kurushwa kwenye moto na watu wanaodhaniwa wafuasi wa dhehebu la dini kwa lengo la kuteketeza mapepo.

Watu wa familia yake wameviambia vyombo vya habari kuwa, Vilma Trujillo (25) alishambuliwa na watu wanne wakiongozwa na mtu aliyetajwa kuwa ni mhubiri.

Mhubiri huyo, Juan Rocha amekusha tuhuma za kumuua mwanamke huyo kwa kumchoma moto.

Amedai kuwa, Trujillo amekufa kwa kuwa pepo wabaya walimchukua mwanamke huyo na kumrusha motoni.

Mwili wa mwanamke huyo ulipatikana ukiwa na majeraha makubwa ya moto.

Maofisa wa polisi walimkamata Rocha na watu wengine wanaohusishwa na tukio hilo la kumchoma kwa moto Trujilo.

Mume wa mwanamke huyo, Reynaldo Perlata Rodriguez amesema mkewe alichukuliwa na kupelekwa kanisani wiki iliyopita wakati wafuasi wa kanisa hilo walipodai ana mapepo baada ya kujaribu kuwashambulia watu kwa panga.

"Hatuwezi kuwasamehe kwa kile walichotufanyia, alinukuliwa akisema. Walimuua mke wangu mama wa watoto wangu wawili. Nitawaambia nini watoto wangu?" amesema.

google+

linkedin

About Author
  • BLOG NAMBA MMOJA KWA MATANGAZO YA AJIRA NA NAFASI ZA KAZI TANZANIA. Soma zaidi

    0 comments:

    POST A COMMENT

     

    Gallery

    Popular Posts

    About Us