Chama cha Wamiliki wa Mabasi(TABOA) kimetangaza Mgomo kuanzia wiki ijayo. | KINGAZI BLOG

HABARI KARIBU YAKO ZAIDI.

Breaking News
Loading...

Sunday 2 April 2017

Chama cha Wamiliki wa Mabasi(TABOA) kimetangaza Mgomo kuanzia wiki ijayo.

 Image result for KITUO CHA  MABASI


Chama cha Wamiliki wa Mabasi(TABOA) kwa kushirikiana na Wamiliki wa Malori na Chama cha Wasafirishaji Mkoa wa Dar es Salaam kimetangaza mgomo wa usafirishaji abiria na mizigo nchi nzima kuanzia siku ya jumatatu ili kushinikiza serikali kutopitisha sheria ya usafirishaji inayotarajiwa kusomwa mara ya tatu na kupitishwa siku ya Jumanne wiki ijayo.

Akitoa maazimio hayo yaliyofikiwa katika mkutao mkuu maalumu wa chama cha wamiliki wa Mabasi, Malori, Daladala na Baji, katibu mkuu wa TABOA Bwana. Eneo Mrutu amesema sheria inaloyolenga kupitishwa haikuwashirikisha wadau na haitenganishi makosa ya dereva na mmiliki, hali inayosababisha kosa lililofanywa na dereva linasababisha mmiliki kufungwa jela.

Aidha amewaomba wabunge bila kujali itikadi za vyama vyao kutopisha sheria hiyo mpaka ifanyiwe marekebisho kwa kuwa inalenga kuharibu sekta ya usafirishaji nchini.

Chanzo: ITV

google+

linkedin

About Author
  • BLOG NAMBA MMOJA KWA MATANGAZO YA AJIRA NA NAFASI ZA KAZI TANZANIA. Soma zaidi

    0 comments:

    POST A COMMENT

     

    Gallery

    Popular Posts

    About Us