JOH Makini Afunguka Haya Baada ya Mashabiki Kumfananisha na Jay Z wa Marekani..!!! | KINGAZI BLOG

HABARI KARIBU YAKO ZAIDI.

Breaking News
Loading...

Tuesday 25 April 2017

JOH Makini Afunguka Haya Baada ya Mashabiki Kumfananisha na Jay Z wa Marekani..!!!


Msanii wa miondoko ya 'Hip hop' kutoka kampuni ya Weusi, Joh Makini amefunguka ya moyoni na kusema anajisikia faraja kwa mashabiki zake kumfananisha na msanii Jay Z.

Joh Makini amesema ufananisho huo uko wazi kwa kuwa kiwango cha muziki wake ni mkubwa kiasi ambacho watu wanaomzunguka na wapenzi wa kazi zake hawaoni mtu mwingine wa kumfananishia naye isipokuwa msanii huyo kutoka Ughaibuni.

"Jay Z ni 'role model' wangu...mimi naimba maisha ya sinoni daraja mbili na Tanzania na Jay Z anaimba maisha ya Brooklyn na Marekani, nafikiri nipo katika 'level' ambayo hawaoni mtu mwingine wa kunifananisha naye...Kwahiyo mimi naona poa kwa sababu kama unanifananisha na Jay z 'yeah i like it' kuliko ungenifananisha na mtu mwingine". Alisema Joh Makini

Kwa upande mwingine msanii huyo amedai changamoto na vikwazo anavyokutana navyo katika kufanya kazi zake za kila siku huwa ndiyo vinamfanya aweze kutengeneza mambo mazuri zaidi.

google+

linkedin

About Author
  • BLOG NAMBA MMOJA KWA MATANGAZO YA AJIRA NA NAFASI ZA KAZI TANZANIA. Soma zaidi

    0 comments:

    POST A COMMENT

     

    Gallery

    Popular Posts

    About Us