MAAJABU YA MWAKA HAYA ....Jamaa anayeatamia mayai ya kuku Ufaransa | KINGAZI BLOG

HABARI KARIBU YAKO ZAIDI.

Breaking News
Loading...

Monday 3 April 2017

MAAJABU YA MWAKA HAYA ....Jamaa anayeatamia mayai ya kuku Ufaransa

Msanii kutoka Ufaransa Abraham Poincheval anaendelea kuatamia mayai ya kuku akiwa na matumaini kwamba  yataangua vifaranga. Jamaa anatumia joto kutoka kwenye mwili wake kuatamia mayai hayo 10. Poincheval ambaye hufanya uigizaji wa kuigiza mambo ya ucheshi lakini ya hatari alishahi kuishi wiki mbili ndani ya dubu na mengine mengi ya kushangaza.

Jamaa atakuwa katika chumba maalum ambacho anatamia mayai ambapo watalii wanaweza kumtazama katika makumbusho ya Palais de Tokyo mjini Paris na anatarajia kuatamia mayai hayo kwa siku 21 hadi 26.

Badala ya kuatamia mayai hayo kwa kuchuchumaa juu yake moja kwa moja, anatumia kiti maalum ambacho kina mfuko eneo lake la kukalia, hapo ndipo mayai hayo yamewekwa.

Poincheval amejifunga blanketi kuzuia joto kupotea aidha anapanga kula vyakula vinavyoongeza sana joto mwilini, kama vile tangawizi. Wakati wa haja atatumia kijisanduku kidogo kilichomo mvunguni mwa kiti chake. Unaambiwa jamaa hatakiwi kuondoka zaidi ya dakika 30 kwa si

google+

linkedin

About Author
  • BLOG NAMBA MMOJA KWA MATANGAZO YA AJIRA NA NAFASI ZA KAZI TANZANIA. Soma zaidi

    0 comments:

    POST A COMMENT

     

    Gallery

    Popular Posts

    About Us