WAKATI Tukio la Ajali ya Arusha Halijapoa..Ajali Nyingine Imetokea Morogoro ..!!! | KINGAZI BLOG

HABARI KARIBU YAKO ZAIDI.

Breaking News
Loading...

Monday 8 May 2017

WAKATI Tukio la Ajali ya Arusha Halijapoa..Ajali Nyingine Imetokea Morogoro ..!!!


Watu 10 wamejeruhiwa na wamelazwa katika Hospitali ya Rufaa Morogoro, watatu kati yao wakiwa na hali mbaya baada ya basi la kampuni ya Karim walilokuwa wakisafiria kugongana uso kwa uso na lori.

Walikuwa wakitoka Turiani kwenda Morogoro ndipo basi hilo lilipogongana uso kwa uso na lori lililokuwa likitokea Morogoro kwenda nchini Rwanda.

Walioshuhudia ajali hiyo walisema ilitokea jana saa sita mchana eneo la Ranchi ya Dakawa wakati dereva wa lori alipojaribu kuyapita magari mawili bila ya kuchukua tahadhari.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Ulrich Matei alisema majeruhi walikuwa 24 na baada ya kufikishwa hospitali wengine walitibiwa na kuruhusiwa na waliolazwa ni 10, watatu wakiwa na hali mbaya.

Alisema dereva wa lori hilo anashikiliwa na polisi.

google+

linkedin

About Author
  • BLOG NAMBA MMOJA KWA MATANGAZO YA AJIRA NA NAFASI ZA KAZI TANZANIA. Soma zaidi

    0 comments:

    POST A COMMENT

     

    Gallery

    Popular Posts

    About Us