MAMA ADAI WATOTO WAKE WANAZUNGUMZA NA WATU WALIOKUFA... | KINGAZI BLOG

HABARI KARIBU YAKO ZAIDI.

Breaking News
Loading...

Sunday 4 September 2016

MAMA ADAI WATOTO WAKE WANAZUNGUMZA NA WATU WALIOKUFA...

Billington (kulia) akiwa na watoto wake. Kutoka kushoto ni Lucy, Jadon na Hellen, ambaye yeye hakujaliwa uwezo walionao wadogo zake.

Wazazi wengi hupenda kujisifu kuhusu vipaji vya watoto wao, lakini unaweza kufikiri Pam Billington angebaki na uwezo wa kipekee wa familia yake mwenyewe.

Mama huyo mwenye umri wa miaka 38 anavutiwa watoto wake wawili wadogo Jadon mwenye miaka 10, na Lucy mwenye miaka minane, kuwa wanaweza kuongea na watu waliokufa.

Mama Billington, anayetokea Cheshire, anasema wamepata marafiki ambao ni mizimu zaidi ya kumi - akiwamo bibi yao - katika mwaka uliopita.

Anasema watoto hao wanaongea mno na marafiki zao wapya kiasi cha kuhisi kama ni sehemu ya familia yao hiyo.

"Hiyo ilianza miaka kadhaa iliyopita pale Jadon aliponieleza amekuwa akitembelewa na malaika wakati wa usiku," alisema Mama Billington.

"Mwanzoni nilipuuzia kama matokeo ya fikra zilizopitiliza. Lakini pale Lucy alipoanza kuongelea suala hilo pia nikaanza kusikiliza.

"Ni zawadi na pengine uipokee ama kuikataa. Sio mzaha, ninaamini kabisa watoto wangu wanaweza kuongea na mizimu."

Ziara za mizimu hiyo zilianza mwaka 2011 kwenye nyumba ya zamani ya familia hiyo mjini Manchester ambako, kwa mujibu wa watoto hao, mizimu hiyo iliishi kati yao na hata kwenye dari lao.

Machi mwaka huu, familia hiyo ikahamia kwenye nyumba yao mpya huko Sandback, mjini Cheshire, lakini watoto hao walidai mizimu hiyo ikawatafuta na kuwafuata.

Pam, mama wa nyumbani, anasema alikuja kuamini baada ya kushuhudia matukio mapya yeye mwenyewe.

Alisema: "Usiku mmoja nilikuwa nikitazama TV na nikamwambia Jadon kama kweli wapo hapa sasa amwambie mmoja wao avute mguu wa suruali yangu.

"Jadon akamwambia, kisha sekunde chache baadaye nikahisi kitu fulani kikigusa mguu wangu na nikaona kwa macho yangu mwenyewe suruali zangu zikisogea.

"Inashangaza. Sasa, wananigusa wakati wote. Wanaweza kunisukuma mkono na kunigusa kwenye mguu. Nimekuwa hata nikiguswa machoni na mzimu.

"Wanafanya pia televisheni kuwa timtimu pale Jadon anapoamuru mmoja kuthibitisha kwamba alikuwa mahali hapo.

"Unatakiwa kupitia haya kuweza kuelewa. Kila mara nimekuwa nikisoma vitu lakini sikuwahi kukubali kwa hakika hadi nilipovipitia nikiwa na watoto wangu."

Aliongeza: "Ninapenda kuwa na mizimu katika nyumba, nafikiri ni jambo muhimu.

"Nafikiri inaonesha kwamba kila kitu kinawezekana na inanipa matumaini wakati nitakapokufa. Ninafahamu kwamba huu sio mwisho na tunaendelea."

Kama mkanamungu, Mama Billington anasema hajawalea watoto wake kuamini mizimu na hana mashaka na uwezo wao wa kiakili kwa namna yoyote.

Lakini watoto hao, ambao wanasomea nyumbani, wanavutiwa.

Miongoni mwa wageni hao mizimu ni wawili wa Kimarekani wanaoitwa Sam na Simon Crease, ambao Jadon anaongea nao, sambamba na malaika anayeitwa Michael.

Lucy ameunda urafiki na msichana mdogo anayeitwa Rose.

Na, kwenye nyumba yake mpya huko Cheshire, anasema ameshawahi kumuona mzimu mwanamke kwenye bustani ya jirani, anayeaminika kuwa ni mzimu wa mwakamke mzee ambaye alifariki hivi karibuni mahali hapo.

Jadon alisema: "Nimekuwa na matatizo ya kulala sababu kila wakati nilihisi kama kuna mtu ananitazama.

"Nilikuwa naamka usiku na kukimbilia chumbani kwa mama na baba.

"Sasa ninapoona mizimu ninaongea nayo - na inanijibu. Ninaiona wakati wa mchana na usiku."

Aliongeza: "Mama na baba waliniuliza kama nilikuwa naiona kweli au la - hakika kuna mizimu ndani ya nyumba hiyo."

Ingawa Lucy bado anawasiliana na marafiki zake mizimu anakiri bado anatishika na vitendo vyao vya usiku wa manane.

Alisema: "Nimekuwa nikiogopa, Pale ninapowaona kwa mara ya kwanza nielewi kama ni mizimu au fikra zangu tu.

google+

linkedin

About Author
  • BLOG NAMBA MMOJA KWA MATANGAZO YA AJIRA NA NAFASI ZA KAZI TANZANIA. Soma zaidi

    0 comments:

    POST A COMMENT

     

    Gallery

    Popular Posts

    About Us