MPYA: HII HAPA TAARIFA MUHIMU TOKA TUME YA VYUO VIKUU TANZANIA (TCU) KUHUSU AWAMU YA TAU YA UDAHILI. | KINGAZI BLOG

HABARI KARIBU YAKO ZAIDI.

Breaking News
Loading...

Saturday 22 October 2016

MPYA: HII HAPA TAARIFA MUHIMU TOKA TUME YA VYUO VIKUU TANZANIA (TCU) KUHUSU AWAMU YA TAU YA UDAHILI.


tcu banner



                            
                               TCU - TANZANIA COMMISSION FOR UNIVERSITIES

          TAARIFA KWA UMMA 

Tume ya vyuo Vikuu Tanzania (TCU) inautangazia Umma kuwa baada ya kukamilisha mchakato wa maombi ya waombaji wa vyuo vikuu, vyuo Vikuu Vishiriki na Taasisi za elimu ya juu kwa awamu ya Kwanza, ya Pili na ya Tatu, na matokeo ya waombaji wote waliofanikiwa kupata nafasi vyuoni kukamilika, Tume ya vyuo Vikuu imebaini kuwa bado kuna waombaji takribani 5,301 ambao bado wako kwenye mfumo na hawajakamilisha maombi yao. 

Tume imebaini pia kuwepo kwa idadi kubwa ya waombaji hasa wenye Stashahada ambao hawakuomba kabisa kutokana na matokeo yao ya mitihani kuchelewa kufika Baraza la Elimu ya Ufundi (NACTE). Awamu hii itawahusu:

         • Waombaji ambao bado wako ndani ya mfumo ambao hawajachaguliwa; 
         • Waombaji wapya ambao hawakuwahi kuomba awali;
 na 
        • Waombaji walio na sifa linganifu ambao hawakukamilisha taratibu za uombaji hapo awali Kutokana na sababu tajwa hapo juu, Tume inautangazia Umma kuwa itafungua Mfumo (CAS) kwa siku tatu tu, kuanzia Jumatatu tarehe 24 hadi Jumatano tarehe 26 Oktoba 2016 ili kuruhusu Makundi tajwa hapo juu kuingia kwenye mfumo kutuma maombi. Waombaji wa Awamu ya Nne wanasisitizwa kuzingatia yafuatayo: 

    • Kuhakikisha wanaomba kozi walizo na sifa stahiki 
    • Kuhakikisha wanakamilisha maombi yao kiufasaha

     • kuhakikisha wanajiridhisha na nafasi zilizopo kwa kuzingatia viwango vyao vya ufaulu. Aidha Tume inapenda kuujulisha Umma kwamba kozi zote zisizoonekana kwenye mfumo kwa sasa kuwa zimejaa. Baada ya tarehe tajwa hapo juu Tume itafunga rasmi zoezi la udahili kwa mwaka 2016/17 ili kuruhusu mchakato mingine ya Bodi ya Mikopo na Vyuo kuendelea. 



Kaimu Katibu Mtendaji
Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania
21/10/2016


google+

linkedin

About Author
  • BLOG NAMBA MMOJA KWA MATANGAZO YA AJIRA NA NAFASI ZA KAZI TANZANIA. Soma zaidi

    0 comments:

    POST A COMMENT

     

    Gallery

    Popular Posts

    About Us