"SCORPION" MTOA MACHO AFUTIWA KESI ILIYOKUWA INAMKABILI. | KINGAZI BLOG

HABARI KARIBU YAKO ZAIDI.

Breaking News
Loading...

Wednesday 19 October 2016

"SCORPION" MTOA MACHO AFUTIWA KESI ILIYOKUWA INAMKABILI.


Mahakama ya Wilaya ya Ilala, imemfutia shtaka linalomkabili mshtakiwa Salumu Njwete baada ya upande wa mashtaka kuomba shtaka hilo liondolewe mahakamani kwa sababu hawana nia ya kuendelea na kesi hiyo.

Kutokana na maombi hayo, Hakimu Adelf Sachore amekubaliana na ombi hilo kwa kuzingatia kifungu namba 91 kifungu kidogo cha kwanza cha sheria ambacho kinampa Mamlaka Mkurugenzi Wa Mashtaka nchini (DPP) kuondoa shtaka mahakamani muda wowote ili mradi kama kesi hiyo haijatolewa hukumu.

Lakini kifungu hicho kinampa Mamlaka DPP kumshtaki mshtakiwa huyo endapo kama ana nia ya kuendesha shtaka hilo.

Njwete anakabiliwa na shtaka la unyang'anyi wa kutumia silaha na kumjeruhi Saidi Mrisho.

Lakini shtaka hili limefutwa hata hivyo anaweza kufunguliwa shtaka lingine

 afunguliwa mashtaka upya



Mahakama ya Wilaya ya Ilala, imemfungulia mashtaka mapya Salum Njwete (Scorpion).Amefunguliwa mashtaka mengine yanayofanana na ya awali ya unyang’anyanyi wa kutumia silaha.

Hata hivyo Njwete amekana shtaka na kurudishwa rumande,huku Hakimu Flora Haule anayesimamia kesi hiyo akizuia dhamana.

Awali Mahakama hiyo ilimfutia mashtaka yanayomkabili Scorpion baada ya upande wa mashtaka kuomba shtaka hilo liondolewe mahakamani kwa sababu hawana nia ya kuendelea na kesi hiyo nakutokana na maombi hayo, Hakimu Adelf Sachore alikubaliana na ombi hilo kwa kuzingatia kifungu namba 91 kifungu kidogo cha kwanza cha sheria ambacho kinampa Mamlaka Mkurugenzi Wa Mashtaka nchini (DPP) kuondoa shtaka mahakamani muda wowote ili mradi kama kesi hiyo haijatolewa hukumu.

Njwete anakabiliwa na shtaka la unyang'anyi wa kutumia silaha na kumjeruhi Saidi mrisho

google+

linkedin

About Author
  • BLOG NAMBA MMOJA KWA MATANGAZO YA AJIRA NA NAFASI ZA KAZI TANZANIA. Soma zaidi

    0 comments:

    POST A COMMENT

     

    Gallery

    Popular Posts

    About Us